Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,900
- 944
UFAFANUZI KUHUSU NYUMBA YA MWALIMU WA SHULE YA MSINGI MAWENI, IGUNGA INAYOSAMBAA MITANDAONI
Tarehe 20 Septemba 2021 nikiwa naendelea na Ziara ya Kijiji kwa Kijiji kwenye Jimbo la Igunga, Nikiwa na Wasaidizi wa Ofisi ya Mbunge na Waandishi wa Habari, tulifika Shule ya Msingi Maweni iliyopo Kijiji cha Mwamshoma Kata ya Nguvumoja.
Waandishi wa Habari walivutiwa na stori ya "Mazingira magumu ya nyumba ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Maweni". Mwandishi wa ITV kutoka Singida Bw. Elisante Mkumbo alituma kwenye chombo chake (ITV) picha ambazo zimekuwa zikirudiwa rudiwa kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii siku za karibuni. Baadhi ya "Waungwana" wamekuwa wakitumia picha iyo kufanya kejeli kwa Viongozi wa Nchi au Chama chetu.
Binafsi nimeona nitoe ufafanuzi na hatua iliyofikia mpaka sasa ili kuweka kumbukumbu sawa.
Baada ya kufanya Ziara ya kikazi, niliamua tupeleke Fedha za Mfuko wa Jimbo Kukamilisha ujenzi wa Boma la Nyumba ya Mwalimu iliyokuwa imeanza kujengwa. Mpaka Sasa tumeshapau Nyumba ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Maweni, tumefika hatua ya kupiga lipu, sakafu, kupaka rangi na kuweka madirisha ya aluminum ili Mwalimu Mkuu aweze kukaa na familia yake kwenye mazingira bora.
Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Walimu wetu wanaishi mazingira bora, kwa sasa Halmashauri inaendelea na programu ya kukamilisha maboma ya Nyumba za Walimu ikiwa jitihada za kuboresha mazingira ya utoaji wa Elimu. Picha ya Nyumba ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Maweni imeambatanishwa ili kujua tulipotoka na tulipofikia katika kufanya jitihada ya kuboresha mazingira ya makazi.
Nicholaus George Ngassa
Mbunge wa Jimbo la Igunga