Mwalimu wa Shule ya msingi Kahaazi Bukoba hatiani kwa kuomba na kupokea hongo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba imemhukumu NASWIRU MPENDEKELAKI, Mwalimu wa Shule ya Msingi Kahaazi na mmiliki wa Mpendekelaki stationary.

Mshitakiwa ametiwa hatiani na kuamriwa alipe faini ya shilingi 500,000/= au kwenda jela miaka 2 kwa kuomba na kupokea hongo ya shilingi 300,000/= kinyume na k/f 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329.

Hukumu hiyo dhidi ya Naswiru Mpendekelaki katika kesi ya Rushwa namba 7824/2024 imetolewa chini ya Andrew Kabuka, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bukoba, Machi 22, 2024.

Kwamba mshtakiwa akiwa mwalimu wa Shule ya Msingi Kahaazi na mmiliki wa Mpendekelaki Stationary, aliomba na kupokea rushwa ya shilingi 300,000 kutoka kwa John Bosco Balija ambaye ni raia wa Uganda ili aweze kumwombea cheti cha kuzaliwa na namba ya NIDA katika mamlaka husika.

Mshitakiwa amelipa faini na kuachiwa huru na Mahakama.
 
Mmh hi kazi ya ualimu ni kama laana tupu, mshahara ndo hivo hongo ndogo unakamatwa, wakati wa bunge wanajiongezea mshahara wa 5m ili walipwe 18m, kila mtu iko kimya loh........
 
Kukubali kulipa faini tayari amejifukuzisha kazi. Akate rufaaa.

Aloge wafuatao:-
Hakimu amkate sh 2,000,000
Waendesha mashitaka
 
Back
Top Bottom