Ufafanuzi juu ya Kanisa kufungisha ndoa ya Mjamzito

Ufafanuzi juu ya Kanisa kufungisha ndoa ya Mjamzito

Sawa Sawa, utaratibu umeeleweka sasa,ni mimba kisha toba kisha ndoa kanisani.

Tumepungukiwa na utukufu wa Mungu [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Tumsifu Yesu Kristo[emoji1787][emoji38][emoji38][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
Milele amina.. Barikiwa
Screenshot_20220717-124226.jpg
 
Wiki iliyopita Kuna ya jamaa mmoja na mkewe wamatiana mimba kubwa Tena eti wanaenda kufungua ndoa ushakuwa utaratibu rasmi
sio umeisha kuwa bali ulikuwa ni utaratibu toka zaman wa wakwepa kuuliwa kisa uzinzi kumbuka ata Maria (mama yake yesu) aliolewa akiwa mjamzito tena mkubwa kiasi cha kumfanya mwanaume kuugundua najua utauliza nimejuaje?

Jibu ni kuwa Yusuph alimshutukia kuwa Maria ana ujauzito wakati yupo kwenye process za kumchumbia akataka kumpotezea (had kuona mwanaume ana fikia hatua ya kugundua ujauzito Kwa mwanamke kwa kumuangalia tu jua hio mimba ni kubwa) alimuoa baada ya kuoteshwa ndoto.
 
😆😆😆Huu ndio utakua utamaduni mpya wa haya makanisa kwa kua wao wenyewe wamebariki,wasianze tena kutupa lawama kwa watu

Wangekua wapo serious wangekomaa a BIG NO.

watu wangeogopa kwa kua wameshalegea huu ndio utakua utaratibu mpya sasa kwenye haya makanisa.
Utaratibu uliharibika toka watu walipoanza kuoana wakiwa hawana bikra.
Mda mnakesea hii tabia kumbukeni kukemea na tabia ya kusema unatest kama yaliyomo yamo (uwezi oa dem ambayo ujamgonga ata mara moja)
 
sio umeisha kuwa bali ulikuwa ni utaratibu toka zaman wa wakwepa kuuliwa kisa uzinzi kumbuka ata Maria (mama yake yesu) aliolewa hakiwa mjamzito tena mkubwa kiasi cha kumfanya mwanaume kuugundua najua utauliza nimejuaje? Jibu ni kuwa Yusuph alimshutukia kuwa Maria ana ujauzi wakati yupo kwenye process za kumchumbia akata kumpotezea (had kuona mwanaume ana fikia hatua ya kugundua ujauzito Kwa mwanamke kwa kwa kumuangalia tu jua hio mimba ni kubwa) alimuoa baada ya kuoteshwa ndoto.
Weledi na maarifa[emoji1545][emoji1545]
 
Na wakati huo hakukuwepo na hizi taratibu za kurudishwa kundini
 
😆😆😆Huu ndio utakua utamaduni mpya wa haya makanisa kwa kua wao wenyewe wamebariki,wasianze tena kutupa lawama kwa watu

Wangekua wapo serious wangekomaa a BIG NO.

watu wangeogopa kwa kua wameshalegea huu ndio utakua utaratibu mpya sasa kwenye haya makanisa.
Pesa pesa pesa... Inawafanya wabadili sheria za Mungu wao...
 
Sikilizeni ninyi Wakristo, hasa mlio washiriki au communicants wa Roman Catholic, Anglikana, Moravian na Lutheran.

Kanisa hufungisha ndoa kwa Wakisto walio washiriki (communicants). Kanuni na taratibu za kushiriki mnazifahamu. Kama mtu alitengwa au alijitenga mwenyewe anaruhusiwa kushiriki baada ya kuondolewa kifungo hicho na Mchungaji/Kasisi/Padre au Askofu.

Tendo la kumruhusu mtu kushiriki ni la muda mfupi na linafuatia maungamo ya mtu mbele ya Mchungaji/Kasisi/Padri au Askofu. Ungamo linaweza kuwa la hadharani au la siri kutegemeana na mazingira ya kilichomfanya mhusika atengwe au ajitenge mwenyewe.

Kanisa halizuiwi kufungisha ndoa ya mjamzito kama aliungama. Mkiona ndoa inafungwa mjue kuwa ungamo lilifanyika mbele ya mtumishi wa Mungu. Ni vizuri watu wakaelewa kuwa Kanisa haliwezi kutangaza kila ungamo linalofanyika.

Yapo maungamo yanayotangazwa na pia yapo maungamo ambayo hayatangazwi. Kwa nini baadhi ya maungamo hutangazwa huku wakati mengine hayatangazwi, huo ndio Uchungaji wenyewe ambao Wakristo Walei hawaujui. Sio afya na haikubariki waumini wakaanza kuhoji mambo ya maungamo. Kwa ujumla masuala yanayohusu maungamo ni ya Mchungaji/Kasisi/Padri au Askofu.

Kama hata Askofu hawezi kuhoji maungamo yaliyofanywa na Mchungaji/Kasisi/Padri, basi hata Mkristo mshiriki hawezi kuhoji suala hilo. Mkiona mjamzito anafungishwa ndoa mjue kuwa ungamo lilishafanyika na mkiona Kanisa limekataa kufungisha ndoa ya mjamzito, basi mjue kuwa ungamo halikufanyika au ungamo bado halijamilika.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
Heheheheh
 
Hivyo hivyo aliyeoa bila kuonja au aliye na mchumba na hajamuonja miongoni mwenu na awe wa kwanza kufuta comment yake. Utakuta uzi una comment yangu pekee.
Nakumbuka zamani ndugu zetu Walokole walikua wanawacheka wakatoliki,waanglikana ,walutheri n.k kwanini eti wanafungisha ndoa kwa mtu ambaye ni mjamzito au kashazaa tayari ila siku nao walewale tu mchungaji wa kilokole anafungisha ndoa huku mwanamke ana mimba pembeni yupo na kibakuli cha kutemea mate😂😂😂
 
Ila hana sehemu ya kuwatunza au kuweka kumbukumbu zozote, zaidi kufanya fellowship na kutawanyika.
Hivi wapo watu ambao ni waumini wa kudumu kwenye lile kanisa?
 
Yapo maungamo yanayotangazwa na pia yapo maungamo ambayo hayatangazwi. Kwa nini baadhi ya maungamo hutangazwa huku wakati mengine hayatangazwi, huo ndio Uchungaji wenyewe ambao Wakristo Walei hawaujui. Sio afya na haikubariki waumini wakaanza kuhoji mambo ya maungamo. Kwa ujumla masuala yanayohusu maungamo ni ya Mchungaji/Kasisi/Padri au Askofu.
Kukuna mtu humu alikwenda kuungama, kesho yake akaamkia kwenye bangili za polisi
 
Back
Top Bottom