Ufafanuzi juu ya Kanisa kufungisha ndoa ya Mjamzito

Ufafanuzi juu ya Kanisa kufungisha ndoa ya Mjamzito

Hapo mkuu unakosea pasingkuwa na mahakama za kuhukumu unakosea sana sisi waislamu tunaamini kufanya dhambi hadharani ni balaa zaidi kuliko anayefanya kwa Siri

Na ivyo ivyo kufanya matendo mema kwa Siri Kuna malipo makubwa kuliko kujionyesha

Kwa sababu kama nandy asingekuwa na tumbo kubwa au angeshajifungua hizi doubts mitandaoni zingepungua sana huoni
Accumen Mo naomba uzingatie hili andiko mwanzoni kabisa mwa mada..kwakuwa umesema hivi..[emoji1485]waislamu tunaamini kufanya dhambi hadharani ni balaa zaidi kuliko anayefanya kwa Siri


Sikilizeni ninyi Wakristo, hasa mlio washiriki au communicants wa Roman Catholic, Anglikana, Moravian na Lutheran. ...
 
Sikilizeni ninyi Wakristo, hasa mlio washiriki au communicants wa Roman Catholic, Anglikana, Moravian na Lutheran.

Kanisa hufungisha ndoa kwa Wakisto walio washiriki (communicants). Kanuni na taratibu za kushiriki mnazifahamu. Kama mtu alitengwa au alijitenga mwenyewe anaruhusiwa kushiriki baada ya kuondolewa kifungo hicho na Mchungaji/Kasisi/Padre au Askofu.

Tendo la kumruhusu mtu kushiriki ni la muda mfupi na linafuatia maungamo ya mtu mbele ya Mchungaji/Kasisi/Padri au Askofu. Ungamo linaweza kuwa la hadharani au la siri kutegemeana na mazingira ya kilichomfanya mhusika atengwe au ajitenge mwenyewe.

Kanisa halizuiwi kufungisha ndoa ya mjamzito kama aliungama. Mkiona ndoa inafungwa mjue kuwa ungamo lilifanyika mbele ya mtumishi wa Mungu. Ni vizuri watu wakaelewa kuwa Kanisa haliwezi kutangaza kila ungamo linalofanyika.

Yapo maungamo yanayotangazwa na pia yapo maungamo ambayo hayatangazwi. Kwa nini baadhi ya maungamo hutangazwa huku wakati mengine hayatangazwi, huo ndio Uchungaji wenyewe ambao Wakristo Walei hawaujui. Sio afya na haikubariki waumini wakaanza kuhoji mambo ya maungamo. Kwa ujumla masuala yanayohusu maungamo ni ya Mchungaji/Kasisi/Padri au Askofu.

Kama hata Askofu hawezi kuhoji maungamo yaliyofanywa na Mchungaji/Kasisi/Padri, basi hata Mkristo mshiriki hawezi kuhoji suala hilo. Mkiona mjamzito anafungishwa ndoa mjue kuwa ungamo lilishafanyika na mkiona Kanisa limekataa kufungisha ndoa ya mjamzito, basi mjue kuwa ungamo halikufanyika au ungamo bado halijamilika.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
Kwani kuna nini!??
 
Walipozidi kumwuliza, Yesu akainuka, akawaambia, “Mtu asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumpiga jiwe.”..

Usihukumu usije ukajukumiwa..!
Hivyo hivyo aliyeoa bila kuonja au aliye na mchumba na hajamuonja miongoni mwenu na awe wa kwanza kufuta comment yake. Utakuta uzi una comment yangu pekee.
 
Huwa mnalikimbilia sana hili neno mkikosolewa madhambi yenu
Wanameremetaaa....[emoji7]
Zawadi ya kamati 168,000,000
Coaster mpyaa
FB_IMG_1658043895998.jpg
 
Hivyo hivyo aliyeoa bila kuonja au aliye na mchumba na hajamuonja miongoni mwenu na awe wa kwanza kufuta comment yake. Utakuta uzi una comment yangu pekee.
Utakuta uzi una comment yangu pekee.[emoji23]
 
Kwkuwa wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.. Hivyo yatupasa kuwa watu wa toba nyakati zote
Na ni furaha mwenye dhambi mmoja akitubu...!
Sawa Sawa, utaratibu umeeleweka sasa,ni mimba kisha toba kisha ndoa kanisani.

Tumepungukiwa na utukufu wa Mungu 🤣🤣🤣

Tumsifu Yesu Kristo🤣😆😆🏃🏃🏃🏃🏃
 
Kwakuwa WOTE tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.. Chini ya jua hakuna MKAMILIFU la HATA MMOJA
🤣🤣🤣🤣Tujifiche kwenye hayo maneno hakuna namna sasa.

Chini ya jua hakuna mkamilifu hata mmoja,Tumepungukiwa utukufu 🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom