Ufafanuzi juu ya Kanisa kufungisha ndoa ya Mjamzito

Ufafanuzi juu ya Kanisa kufungisha ndoa ya Mjamzito

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,454
Reaction score
872,084
Sikilizeni ninyi Wakristo, hasa mlio washiriki au communicants wa Roman Catholic, Anglikana, Moravian na Lutheran.

Kanisa hufungisha ndoa kwa Wakisto walio washiriki (communicants). Kanuni na taratibu za kushiriki mnazifahamu. Kama mtu alitengwa au alijitenga mwenyewe anaruhusiwa kushiriki baada ya kuondolewa kifungo hicho na Mchungaji/Kasisi/Padre au Askofu.

Tendo la kumruhusu mtu kushiriki ni la muda mfupi na linafuatia maungamo ya mtu mbele ya Mchungaji/Kasisi/Padri au Askofu. Ungamo linaweza kuwa la hadharani au la siri kutegemeana na mazingira ya kilichomfanya mhusika atengwe au ajitenge mwenyewe.

Kanisa halizuiwi kufungisha ndoa ya mjamzito kama aliungama. Mkiona ndoa inafungwa mjue kuwa ungamo lilifanyika mbele ya mtumishi wa Mungu. Ni vizuri watu wakaelewa kuwa Kanisa haliwezi kutangaza kila ungamo linalofanyika.

Yapo maungamo yanayotangazwa na pia yapo maungamo ambayo hayatangazwi. Kwa nini baadhi ya maungamo hutangazwa huku wakati mengine hayatangazwi, huo ndio Uchungaji wenyewe ambao Wakristo Walei hawaujui. Sio afya na haikubariki waumini wakaanza kuhoji mambo ya maungamo. Kwa ujumla masuala yanayohusu maungamo ni ya Mchungaji/Kasisi/Padri au Askofu.

Kama hata Askofu hawezi kuhoji maungamo yaliyofanywa na Mchungaji/Kasisi/Padri, basi hata Mkristo mshiriki hawezi kuhoji suala hilo. Mkiona mjamzito anafungishwa ndoa mjue kuwa ungamo lilishafanyika na mkiona Kanisa limekataa kufungisha ndoa ya mjamzito, basi mjue kuwa ungamo halikufanyika au ungamo bado halijamilika.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
 
Ila yule mjamzito anayesemwa anasali kwa mwamposa
Kama mtu alitengwa au alijitenga mwenyewe anaruhusiwa kushiriki baada ya kuondolewa kifungo hicho na Mchungaji/Kasisi/Padre au Askofu. Tendo la kumruhusu mtu kushiriki ni la muda mfupi na linafuatia maungamo ya mtu mbele ya Mchungaji/Kasisi/Padri au Askofu. Ungamo linaweza kuwa la hadharani au la siri kutegemeana na mazingira ya kilichomfanya mhusika atengwe au ajitenge mwenyewe.
 
Vipi kwa kijana anae vaa hereni
Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.
 
Nadhani vizuri angejifungua kabisa ila tumbo pale naona haileti maana kabisa swa na kuhalalisha uzinzi au mimba ingekuwa ndogo kabisa
Walipozidi kumwuliza, Yesu akainuka, akawaambia, “Mtu asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumpiga jiwe.”..

Usihukumu usije ukajukumiwa..!
 
Walipozidi kumwuliza, Yesu akainuka, akawaambia, “Mtu asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumpiga jiwe.”..

Usihukumu usije ukajukumiwa..!
Hapo mkuu unakosea pasingkuwa na mahakama za kuhukumu unakosea sana sisi waislamu tunaamini kufanya dhambi hadharani ni balaa zaidi kuliko anayefanya kwa Siri

Na ivyo ivyo kufanya matendo mema kwa Siri Kuna malipo makubwa kuliko kujionyesha

Kwa sababu kama nandy asingekuwa na tumbo kubwa au angeshajifungua hizi doubts mitandaoni zingepungua sana huoni
 
Sikilizeni ninyi Wakristo, hasa mlio washiriki au communicants wa Roman Catholic, Anglikana, Moravian na Lutheran. Kanisa hufungisha ndoa kwa Wakisto walio washiriki (communicants). Kanuni na taratibu za kushiriki mnazifahamu. Kama mtu alitengwa au alijitenga mwenyewe anaruhusiwa kushiriki baada ya kuondolewa kifungo hicho na Mchungaji/Kasisi/Padre au Askofu. Tendo la kumruhusu mtu kushiriki ni la muda mfupi na linafuatia maungamo ya mtu mbele ya Mchungaji/Kasisi/Padri au Askofu. Ungamo linaweza kuwa la hadharani au la siri kutegemeana na mazingira ya kilichomfanya mhusika atengwe au ajitenge mwenyewe.

Kanisa halizuiwi kufungisha ndoa ya mjamzito kama aliungama. Mkiona ndoa inafungwa mjue kuwa ungamo lilifanyika mbele ya mtumishi wa Mungu. Ni vizuri watu wakaelewa kuwa Kanisa haliwezi kutangaza kila ungamo linalofanyika. Yapo maungamo yanayotangazwa na pia yapo maungamo ambayo hayatangazwi. Kwa nini baadhi ya maungamo hutangazwa huku wakati mengine hayatangazwi, huo ndio Uchungaji wenyewe ambao Wakristo Walei hawaujui. Sio afya na haikubariki waumini wakaanza kuhoji mambo ya maungamo. Kwa ujumla masuala yanayohusu maungamo ni ya Mchungaji/Kasisi/Padri au Askofu.

Kama hata Askofu hawezi kuhoji maungamo yaliyofanywa na Mchungaji/Kasisi/Padri, basi hata Mkristo mshiriki hawezi kuhoji suala hilo. Mkiona mjamzito anafungishwa ndoa mjue kuwa ungamo lilishafanyika na mkiona Kanisa limekataa kufungisha ndoa ya mjamzito, basi mjue kuwa ungamo halikufanyika au ungamo bado halijamilika.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
Kwa hio huo ndio utakua utaratibu kwa vijana kuanzia sasa

Mtu anapigwa mimba,alafu anaungama kwa paroko ndoa ifungwe.

Watu wanazinzika kwanza kisha mimba kisha ndoa

Maparoko,mapadre,matowashi na makasisi wategemee kufunga ndoa nyingi za aina hii,maana wao wenyewe wameshazihalalisha hakuna namna sasa 😆

kwishaa😆😆
 
Kwa hio huo ndio utakua utaratibu kwa vijana kuanzia sasa

Mtu anapigwa mimba,alafu anaungama kwa paroko ndoa ifungwe.

Maparoko,matowashi na makasisi wategemee kufunga ndoa nyingi za aina hii,maana wao wenyewe wameshazihalalisha

kwishaa😆😆
Wiki iliyopita Kuna ya jamaa mmoja na mkewe wamatiana mimba kubwa Tena eti wanaenda kufungua ndoa ushakuwa utaratibu rasmi
 
Wiki iliyopita Kuna ya jamaa mmoja na mkewe wamatiana mimba kubwa Tena eti wanaenda kufungua ndoa ushakuwa utaratibu rasmi
😆😆😆Huu ndio utakua utamaduni mpya wa haya makanisa kwa kua wao wenyewe wamebariki,wasianze tena kutupa lawama kwa watu

Wangekua wapo serious wangekomaa a BIG NO.

watu wangeogopa kwa kua wameshalegea huu ndio utakua utaratibu mpya sasa kwenye haya makanisa.
 
Kwa hio huo ndio utakua utaratibu kwa vijana kuanzia sasa

Mtu anapigwa mimba,alafu anaungama kwa paroko ndoa ifungwe.

Watu wanazinzika kwanza kisha mimba kisha ndoa

Maparoko,mapadre,matowashi na makasisi wategemee kufunga ndoa nyingi za aina hii,maana wao wenyewe wameshazihalalisha hakuna namna sasa [emoji38]

kwishaa[emoji38][emoji38]
Kwkuwa wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.. Hivyo yatupasa kuwa watu wa toba nyakati zote
Na ni furaha mwenye dhambi mmoja akitubu...!
 
Back
Top Bottom