Nabii Suguye: Kufunga ndoa kanisani ni upagani

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,195
Reaction score
27,806
Sitaki kuwachosha, hebu twende kwenye mada moja kwa moja. Nabii na mtume mkuu wa kanisa la WRC amewaambia wafuasi wake na jamii kwamba kufunga ndoa kanisani ni upagani.

Mtume huyo, ambaye ni maarufu kwenye kauli tata, amesema hayo wakati akiwahubiria waumini wake huko Matembele, Kata ya Kivule, na mahubiri hayo yamesambaa nchi nzima hadi kwa raia wa kawaida. Wengi wa wananchi niliowashirikisha hii video, wamesema mtume yupo sahihi kwa mujibu wa maandiko matakatifu. Siongezi neno. Hebu msikilize wewe mwenyewe hapo chini mkuu:

MAONI YANGU
Ijapokuwa sikubaliani na huyu nabii katika mambo mengi, kwa hili la ndoa, namuunga mkono 💯%. Kama kufunga ndoa kanisani ndiyo deal, basi hata Mungu angewafungisha Adam na Hawa ndoa ya kanisani. Vinginevyo, ufungishaji ndoa unaosisitizwa na viongozi wa dini na kuvalishana mipete mbele ya mchungaji au askofu, ni ubatili na uopagani mtupu. Hawa viongozi wanalazimisha kufungisha ndoa kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

Nawasilisha.​
 
Mkiishi pamoja ndio ndoa tayari. Hizi ndoa zetu zimekaa kimaonesho tu, kushindana harusi ya nani ilipendeza zaidi au ilikuwa kubwa zaidi.

Ndoa ni sherehe za ulimwengu ambazo Mungu hazitambui.

Narudia tena, maana ya ndoa ni muunganiko wa mtu mke na mtu mume wanapoamua kusihi pamoja, kama ilivyokuwa kwa Adamu na Hawa bustani ya Eden.

Kwanza hata hayo madhehebu, hakuna kati yetu anayejua Yesu Kristu alikuwa dhehebu gani.
 
Uwe hai
Yesu yu hai

Mm ni mfuatiliaji wa mahubiri yake kupitia WRM TV
MM NI MUANGLIKANA, LAKINI HUYU NABII KANIZINDUA MAMBO MENGI SANA.
Nabii kaongea mambo ya msingi sana. Kama mtu hataki kumsikiliza na kufuata mafundisho, hilo ni tatizo lake binafsi.
 
Mkiishi pamoja ndio ndoa tayari. Hizi ndoa zetu zimekaa kimaonesho tu, kushindana harusi ya nani ilipendeza zaidi au ilikuwa kubwa zaidi.

Ndoa ni sherehe za ulimwengu ambazo Mungu hazitambui.

Narudia tena, maana ya ndoa ni muunganiko wa mtu mke na mtu mume wanapoamua kusihi pamoja, kama ilivyokuwa kwa Adamu na Hawa bustani ya Eden.

Kwanza hata hayo madhehebu, hakuna kati yetu anayejua Yesu Kristu alikuwa dhehebu gani.
Mkuu, umemaliza kila kitu. Tusubiri wabishi waje kubisha bila hoja.
 
Huyu jamaa tangu azuiliwe kuwa padri kwa vile alizaliwa nje ya ndoa bado ana kinyongo
Jamaa yupi mkuu? Kwani kaongea uwongo? Amesema ukweli tupu mkuu.
 
Sitaki kuwachosha, hebu twende kwenye mada moja kwa moja. Nabii na mtume mkuu wa kanisa la WRC amewaambia wafuasi wake na jamii kwamba kufunga ndoa kanisani ni upagani.

Mtume huyo, ambaye ni maarufu kwenye kauli tata, amesema hayo wakati akiwahubiria waumini wake huko Matembele, Kata ya Kivule, na mahubiri hayo yamesambaa nchi nzima hadi kwa raia wa kawaida. Wengi wa wananchi niliowashirikisha hii video, wamesema mtume yupo sahihi kwa mujibu wa maandiko matakatifu. Siongezi neno. Hebu msikilize wewe mwenyewe hapo chini mkuu:

View attachment 3592197

MAONI YANGU
Ijapokuwa sikubaliani na huyu nabii katika mambo mengi, kwa hili la ndoa, namuunga mkono 💯%. Kama kufunga ndoa kanisani ndiyo deal, basi hata Mungu angewafungisha Adam na Hawa ndoa ya kanisani. Vinginevyo, ufungishaji ndoa unaosisitizwa na viongozi wa dini na kuvalishana mipete mbele ya mchungaji au askofu, ni ubatili na uopagani mtupu. Hawa viongozi wanalazimisha kufungisha ndoa kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

Nawasilisha.​
Ningekuwa mimi ndiyo Rais wa nchi, ningetengeneza sheria ya kuhakikisha watu wa aina hii wanakuwa na elimu ya shahada ya Teolojia na Falsafa kutoka vyuo vinavyo tambulika kama ilivyo kwa Mapadre wa Katoliki! Baada ya hapo sasa ndiyo wapate sifa ya kuanzisha makanisa yao.
 
Nakuunga mkono mkuu. Lakini ameongea ukweli 💯%.
 
Ni upagani kulingana na dini ya Ukristo kwa sababu sio fundisho lililo kwenye biblia, yuko sahihi.

Ukristo kwa asilimia tisini ni upagani kwa sababu unafuata mafundisho yasiyo ya kibiblia nikupe mifano;

1. Sadaka na zaka ni zawalawi na makuhani.
Wakristo sadaka wanawapa wachungaji.
Wachungaji wengi hawana sifa za ukuhani.

2. Siku ya ibada ni Sabato jumamosi. Lakini Wakristo wanaabudu jumapili.

3. Biblia inatuhusu talaka. Wakristo wanakataza talaka.

4. Biblia inaruhusu kuoa wake wengi. Wakristo wanakatazwa kuoa Wake wengi.

5. Biblia inakataza Kula nguruwe na baadhi ya wanyama. Wakristo karibu madhehebu yote wanaruhusiwa Kula Nguruwe.

6. Biblia inamzuia mwanamke mwenye Siku zake asiende kuabudu kanisani au hekaluni.
Wakristo hiyo Sheria hawaifuati.

7. Biblia inatambua Mungu ni mmoja.
Wakristo wanaamini Miungu(Mungu mmoja katika nafsi tatu) ambalo ni fundisho la kikafiri/kipagani

Yapo mengi
 
Back
Top Bottom