UDSM: Utumiaji wa teknolojia kidijitali sio sababu ya Watanzania kukosa ajira bandarini

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Katika utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kuhusiana na mkataba wa makubaliano ya uendeshaji na uboreshaji wa bandari kati ya Tanzania na Dubai, imebainika kuwa kuwepo kwa teknolojia ya kisasa, hakutaondoa ajira za Watanzania bandarini hapo.


Akizungumza na waandishi wa habari Juni 26, 2023 Mhadhiri wa chuo hicho David Rwehikiza amesisitiza kuwa haoni sababu ya Watanzania kuwa na wasiwasi wa kukosa ajira.

"Wakati kompyuta zinaanza kuingia, watu wengi walisema tunapoteza ajira, kuna hofu kubwa sana watu kukimbia teknolojia…katika vitu ambavyo tumeingia navyo makubaliano ni kwamba Serikali ya Dubai itaanza kuwafundisha Watanzania wanaofanya kazi bandarini ili waendane na teknologia ya kisasa," amesema.

Credit: Mwananchi​
 
Back
Top Bottom