Hujuma nzito bandarini

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,035
Imeridhika kuwapo mikakati ya wazi na siri ndani na nje ya nchi kuhujumu juhudi za Serilkali kuimarisha uchumi, RAIA MWEMA inataarifu.

Serikali, kupitia Mamlaka ya Usimamzi wa Bandari Tanzania (TPA), ina makati wa kuboresha ufanisi wa bandari ya Dares Salaam na mnyororo wa usafirishaji, lakini kuna wanaohujumu mpango huo kwa maslahi binafsi.

Uchunguzi uliofanywa kwa takriban mwezi mmoja sasa umebaini, kwamba wanaosuka mikakati hiyo wanalenga kuhakikisha muda uliowekwa kukamilisha majadiliano kati ya Serikali ya Tanzania na Ufalme wa Dubai kupitia IGA (Intergovernmental Agreement) unamalizika bila muafaka.

Oktoba mwaka jana, Tanzania ilingia makubaliano (IGA) na Serikali ya Dubai kuendeleza bandari ya Dares Salaam na maeneo mengine ya kiuchumi. Makubaliano hayo yanaelekeza TPA na Kampuni ya Bandari ya Dubai (DP World)
wazungumze na waingie Mkataba wa Nchi Mwenyeji (HGA) na ya uendeshaji itakayosimamia utekelezaji wa makubaliano hayo, kwa kuweka muda na masharti ya. utekelezaji wa mikataba itakayoingiwa.

Hata hivyo, kuna mjadala kutola kwa wanaohujumu wakidai kwamba DP World imepewa mamlaka makubwa kupitia IGA. bila kueleza kwamba. DP Worldna TPA bado wanajadillana kuhusu mkataba mahususi ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari. Muda wa majadiliano hayo kwa mujibu wa. IGA ni Oktoba 25 mwala huu, yaani takribani miezi mitatu ijayo

Nje ya nchi

Wakati hayo (hujuma) yakiendelea nchini, majirani zetu wanajiimarisha katika sekta ya usafirishaji, wakijipanga kutafuta bandari zerrye ufanisi zaidi," alisema Mkurugenzi Mkau wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (ICAA),
Hamza Johari

Hoja ya Johari ambaye ni mtaalamu wa uchumi na sheria inajikita katika ukweli, kwamba mataifa jirani ya Malawi na Zambia yanakamilisha mchakato wa kutumia ushoroba wa Lobito, Angola, kupitisha shehena yao na kuitelekeza bandari ya Dares Salaam. Hali hiyo inatokea wakati malumbano yakiendelea kuhusu DP World kupewa fursa ya uwekezaji nchini na kuimarisha usafirishaji hususani katika ushoroba wa kati.

Johari alisema: "Sasa ni kama vile tayari tumeshaipoteza Zambia kwa kupitia 'Lobito Corridor. Ni vizuri tukaelewa, kuwapo vita kali sana ya shoroba zetu dhidi ya shoroba shindani Kusini na Kaskazini."

Mashambulizi dhidi ya Tanzania kutoka Kusini yanahusisha Lobito, yenye uwezo wa kuunganisha usafirishaji na mataifa ya DRC, Zambia na Malawi. Kwa upande wa Kaskazini, mashambulizi hayo yanahusisha ushoroba wa Kenya unacunganisha bandari ya Lamu (Mombasa) na mataifa ya Uganda, Rwanda, DC na Sudani Kusini.

Johari ameliambia Raia Mwema kwamba Watanzania tunaendelea kulumbana juu ya DP World kupewa Uwekezaji tayari tumeishaipoteza Zambia kwa kupitia Ushoroba wa Lobito

"Ni vizuri tukaelewa kuna vita kali sana ya Shoroba zetu (Corridor battles) dhidi ya shoroda shindani (Campetting Corridors), kusini na kaskazini: Yaani Ushoroba huu wa Lobito kwa kusini, na Ushoroba wa Kenya kwa kaskazini. Ushoroba wa kati (central corridor) Ndio tupo sisi na uko weak na hatutaki umarike" anasema na kuongeza;
"Kama ulikuwa unataka kujua kwa nini njia ya kwenda DRC haiishi matatizo yanayokwamisha smooth flow ya Magari ya Mizigo kuanzia Tunduma right up to Kasumbalesa; jibu ni wazi sasa:Zambia wanataka Mizigo ya DRC (na hatimaye Burundi na Rwanda) ihamie Ushoroba huu wa Lobita

"Kama kweli sisi ni wataalamu wa Total/ Throughput Logistics with end to end port economics kwa upande mmoja, na wazalendo wa kweli kwa nchi yetu; tunapaswa kuheshimu Ukweli huu na kufanya maamuzi ya haraka sana iwezekanavyo.Nchi iko kwenye "Life and Death situation" kwenye Ports economics battle na tunatumiwa kujiangamiza wenyewe"

Akiongea kwa uchungu Hamza anaserna maamuzi magumu yanapaswa kufanyika kwa miradi yetu yote ya uboreshaji miundombinu yetu ya usafirishaji ikwemo bandari, Reli na barabara za kunganisha Tanzania na nchi za Maziwa makuu.

"Nusura yetu ni kuharalisha fursa hii iliyomo katika IGA tunayolumbania. Kinyume cha hivyo; itakula kwetu vibaya mno, kwani Bandari shindani zinapasha zikingojea IGA hi i-expire' ll wamvute DPW kwao Hii ya Zambia kutuacha na kujlunga Lobito Corridor ituamshe kwenye usingizi tunatumiwa bila kujijiua. Kari lendelee tuwawahi kabla hatujawahiwa sisi" anasema

Johari

RAIA MWEMA imeelezwa, kwamba vita hivi vinavyoshirikisha majasusi wa kimataifa wa kuchumi, ni sababu ya matatizo ya mara katika usafirishaji bidhaa za DRC kutoka Dar es Salaam kupitia Tunduma na Kulumbalesa

Folenil za mchoongo katika mpaka wa Tunduma ni kwa kuwa kuna Majasusi wanaotuhujumu ili shehena yote ya DRC, Burundi na Rwanda zipite Lobito

"Hapa panahitaji uzalendo na uamuzi makini na wa haraka kunusuru Taifa letu," mtaalamu wa usafirishaji shehena kimataifa alimwambia mwandishi wetu akisisitiza:

"Hali ilivyo sasa ni ya kufa au kupona. Ni vita ambavyo tukishindwa, tumekwisha kiuchumi na bahati mbaya tunatumiwa kujiangamiza."
Kenya waimezea mate DPWorld
Zipo taarifa za uhakika zinazodai kuwa Kenya, ambayo ni washindani wakubwa katika biashara baharini, inatamani kuingia mkataba kama wa Tanzania na DP World. Wataalamu kadhaa kutoka TPA wameliambia Gazeti hili, kwamba bandari za Lamu na Mombasa zinasubiri kumalizika kwa muda wa IGA, zianze mazungumzo na DP World.

"Wanataka wamvute (DP World) kwao. Hii ya Zambia kwenda Lobito itutoe usingizini. Tunatumiwa bila kujijua. Tunapaswa kuwawahi (Lamu na Mombasa) kabla hawajatuwahi," walisema wataalamu hao

Wafanyabiashara, wanasiasa
Nchini, hujuma zinazoendelea zinahusisha wanasiasa na wafanyabiashara kwa malengo tofauti. Wakati kauli za viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni za kibaguzi dhidi ya utaifa na Muungano wa Tanzania, zikilaaniwa na wapenda umoja wote, bado wanasiasa hao wanaendelea kulifanya suaia la uwekezaji kuwa kete yao kisiasa. Wafanyabiashara, hasa wamiliki wa bandari za nchi kavu (ICDs) wameingiwa na hofu, kwamba ujio wa DP World huenda ukawatoa 'sokoni.

"Hawa ni wanufaika wakubwa wa udhaifu na kukosekana kwa ufanisi bandarini. Ndio kwa miaka mingi wameihujumu bandari na kuifanya kichekesho mbele ya bandari ya Mombosa," alisema ofisa wa TPA.
Taarifa za kitakwimu zinaonesha, kwamba kampuni ya TICIS iliyokuwa ikitoa huduma ya makasha, huhudumia wastani wa makasha 79,000 kwa mwezi.

Ushirikiano kati ya TICIS na wamiliki wa ICDs unatajwa kuwa miongoni mwa sababu za kuongezeka kwa gharama ya usafirishaji wa kasha moja kuia nchini. "Kasha moja kutoka China kwenda Mombasa hutozwa dola 1300 lakini kwa kuwa meli zinazokuja Tanzania, gharama huwa kubwa, kwa madai kuwa meli huchelewa kushusha mzigo hadi siku 20," alisema mfanyakazi wa zamani wa TICTS.

Takwimu zinaonesha, kuwa kasha likienda kuhifadhiwa ICD, hutozwa dola 1,200 mbali na dola 80 na tozo zingine ndogondogo na wharfage ya kuchelewa kushusha mzigo.

Ukweli wa mambo
Wakati Watanzania wakiaminishwa, kuwa bandari inauzwa, ukweli ni kwamba wanaosema hivyo, wanalenga kuwachochea hasira wakati wao wakinufaika.

'Wanaopinga mkataba kwa vitisho, ukiangalia historia zao ziko wazi juu ya nani aliwasomesha, wamekuwa wakipata nini na sasa wanataka nini kiendelee," alinukuliwa mwanasheria akisema. Taarifa zinaonesha kuwa wanufaika wa mdororo wa ufanisi bandarini unagusa hata vigogo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Vigogo hao wanadaiwa kutumia nguvu kubwa kuikataa DP World, wakifahamu kwamba biashara iliyokuwa ikiwapa mamilioni kama si mabilioni ya fedha, inakaribia kufa.

"Wanafahamu kuwa gharama ya kusafirisha kasha moja litashuka DP World wakiingiza teknolojia mpya, ambapo mteja atalipia gharama za kasha lake na itafikia hatua ya kasha kutoka kwenye meli na kupakiwa kwenye treni au lori la mteja, kwenda dukani kwake moja kwa moja. "Hapa maana yake mrija wa ICD utakuwa umekatika," anasema.

Hatua zaanza kuchukuliwa

Wakati ikisalia miezi mitatu na siku kadhaa kabla ya IGA kumaliza muda wake, Jeshi la Polisi nchini lilimtaka mmoja kati ya wakosoaji wakubwa wa majadiliano hayo, Dk Rugemeleza Nshala, kuripoti kituoni kwa mahojiana. Kwa mujibu wa barua ya mwito wa Polisi ilivotolewa Julai 10 mwaka huu, DkNshala alitakiwa kuripoti jana bila kukosa katika Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dares Salaam.

"Ofisi inafanya uchunguzi kuhusu kauli ulizotoa Julai3, 2023 na kusambaza katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu mkataba wa uwekezati wa bandari ya Dares Salaam," inasomeka sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na ACP Joseph Mfungomara kwa niaba ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini. Msisitizo wa Serikali Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wiki iliyopita amekaririwa akisema DP World watapewa mkataba unaofanana na waliokuwa nao TICTS, kwa nia ya kuongeza ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam, kukuza ajira na kuongeza mapato ya nchi yatokanayo na bandari.

Akizungumzia matumizi mabaya ya fursa ya kujieleza iliyopo nchini kwa sasa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alisema: "Tutaendelea kupokea ushauri, maoni na mawazo, lakini bahati mbaya sana kuna baadhi ya Watanzania wenzetu wamekuwa wakitaka kutumia uhuru huo vibaya, kiasi cha kutoa kauli zinazolenga kuhatarisha usalama wa nchi yetu, kuvunia sheria za nchi na kupasua Taifa.

"Kauli hizi haziwezi kukubalika, haiwezekani tutumie kisingizio cha uhuru wa kutoa maoni kavunja sheria za nchi, sheria hizi zitaendelea kubaki kuwa sheria, na tuna wajibu wa kuhakikisha tunasimamia sheria zilizotungwa kwa maslahi ya watu wa nchi hii.

"Nataka nichukue fursa hii, kwanza kutoa mwito kwa wananchi kujiepusha kutumia uhuru huu uliotolewa, kuvunia sheria za nchi. "Lakini nataka nielekeze Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama, kuhakikisha hawafumbii macho mtu yeyote au kikundi kitakachosababisha ama kwa vitendo au kwa kauli, kuvunja sheria za nchi yetu na hatimaye kuhatarisha usalama wa nchi.

"Tuwambie kabisa kwa kasi va mandeleo na mafanikio makubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita, katika muda mfupi imetokana na nia ya dhati ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua anazochukua.

"Ndiyo maana leo hi tukiwa tumeshuhudia mchango mkubwa wa sekta binafsi, uwekezaji umeongezeka katika chi, biashara zimeimarika zaidi, uhusiano wa kimataifa umeimarika kiasi cha kuchangia kupata fedha nyingi zenye masharti nafuu, kwenye mandeleo ya Tanzania yote.

"Kwa faida ya mafanikio haya ya Watanzania, tushirikiane kudumisha amani yetu, ili matunda haya ya kazi nzuri inayofanywa na Serikali iweze kutunufaisha kwa masiahi yetu sisi na Tanzania."

1689164311586.png

Raia Mwema
 
kwa uelewa nilionao na elimu yangu ya ngumbaru std 7 + exposure kubwa niliyonayo kwenye dunia ya kimafia na giza kuna mahala nagundua watu wetu wana uelewa mdogo sana.

huyu Bwana Johari sijui anazungumzia kuipoteza Zambia na Lobito yakina Angola nk leo wakati bandari tunayo toka uhuru na tumeshindwa kuperform just kwasababu ya poor management ya watawala wa CCM yeye haoni baadala yake akili imejikita kwenye DP world na sio kusema ukweli kwamba watawala wa CCM wameshindwa kila mahala sio bandari tu na solution sio kubindafsisha bandari maana wameshabinafsisha vingi na bado vimeleta shida tu baadala yake ni CCM kuondoka madarakani tu na kutoa wigo mpana kwa watanzania mbalimbali wenye akili na exposure kuchukua usukani.

Tunyooshe maneno, shida sio ufanisi bali shida ni watawala wa CCM kushindwa kusimamia vyema rasimali za nchi na kuwaletea watanzania maendeleo.
 
Kwahiyo bwana mkubwa johari,wewe unaona tukichelewa tutawakosa Zambia,congo na Malawi!! Kenya wanashubiri muda uishe waite dpw!!

Tatizo sio kushindwa (ufanisi) Tatizo ni kushindwa kwa serikali.Ikiwa Kuna wizi bandarini Ina maana hatuwezi Kama taifa kuzuia?

Ikiwa ufanisi ni lazima tukubali masharti kandamizi yaliyopo katika mkataba wetu?

Watanzania watakuelewa Kama ungejaribu kueleza mambo yanayowatatiza watz ktk mkataba wetu.

Wasomi mnatufelisha.
 
R

View attachment 2685831

Raia Mwema

Raia mwema kweli hiyo, kama ni kweli basi Generali Yuko likizo
 
Tatizo sio muwekezaji tatizo mkataba umekaa kimangungo, hauna expiration date, do world wamejiwekea nyama zote Sisi mifupa
 
kwa uelewa nilionao na elimu yangu ya ngumbaru std 7 + exposure kubwa niliyonayo kwenye dunia ya kimafia na giza kuna mahala nagundua watu wetu wana uelewa mdogo sana.

huyu Bwana Johari sijui anazungumzia kuipoteza Zambia na Lobito yakina Angola nk leo wakati bandari tunayo toka uhuru na tumeshindwa kuperform just kwasababu ya poor management ya watawala wa CCM yeye haoni baadala yake akili imejikita kwenye DP world na sio kusema ukweli kwamba watawala wa CCM wameshindwa kila mahala sio bandari tu na solution sio kubindafsisha bandari maana wameshabinafsisha vingi na bado vimeleta shida tu baadala yake ni CCM kuondoka madarakani tu na kutoa wigo mpana kwa watanzania mbalimbali wenye akili na exposure kuchukua usukani.

Tunyooshe maneno, shida sio ufanisi bali shida ni watawala wa CCM kushindwa kusimamia vyema rasimali za nchi na kuwaletea watanzania maendeleo.
Hizi ni propaganda za kipumbavu kweli kweli za kutaka kuwapumbaza wajinga wasiojielewa kuunga mkono huu uuzwaji wa bandari kwa waarabu wa mama Samia. Hell big NO! Hatumtaki mwarabu hata kwa dakika moja.
 
Back
Top Bottom