Wiki ya AZAKI: Tusichukulie Teknolojia kama tisho kwenye ajira za watu, binadamu ana uwezo mkubwa wa kuendana na mazingira yake

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Wiki ya AZAKI (Asasi Za Kiraia) 2023 imeanza leo: Kaulimbiu ni Teknolojia na Jamii Yetu “Tech x Society: Then, Now and Beyond”

Huu ni msimu wa tano wa kusanyiko kubwa zaidi la Asasi za Kiraia nchini Tanzania mwaka huu ikiangazia umuhimu wa maendeleo ya kiteknolojia katika jamii na athari zake kwa asasi za kiraia.

Wiki ya AZAKI 2023: Kijana Abuubakar Ally, kutoka kampuni ya Apple Inc. (California) atatoa hotuba ya ufunguzi itakayoangazia Mustakabali wa Teknolojia kwenye sekta mbalimbali kama Afya, Elimu na Kilimo kama mifano ya kusisitiza umuhimu wa teknolojia kwenye jamii yetu inayokua.

=====

Screenshot 2023-10-28 013355.png

Balozi Didier Chassot (Uswisi)

Ni matumaini yangu kwamba katika siku hizi 5, AZAKI zilizopo hapa zitajadili changamoto na fursa zinazoletwa na maendeleo ya Teknolojia na pia mbinu za kutatua changamoto zake.

Vilevile, ninatumaini kuwa maono mapya yataletwa katika mijadala ili kila mmoja aondoke hapa akiwa na maarifa mapya ya kukabiliana na changamoto za ulimwengu wa Teknolojia.

Jambo jingine ambalo ni muhimu tuligusie ni Mgawanyiko wa Kidijitali (Digital Divide).

Wakati Teknolojia inakua sana duniani kote, bado kuna watu wasioweza kufikia huduma za kiteknolojia. Natumaini Mijadala ya Wiki hii itaangalia ni namna gani hakuna anayeachwa nyuma.

20231023_105515.jpg

Mahojiano na Aboubakari Ally: Mzungumzaji mkuu Wiki ya CSO

Amesoma Havard University, na amaeishi Marekani kwa miaka 15. Anafanyakazi Apple inc. Wasilisho lake ni kuhusu Africa's Technological Horizons. Wasilisho linafanywa kwa mfumo wa majadiliano ambapo anahojiwa na Aidan Eyakuze.

Swali: Unafanya nini kwenye Teknolojia?

JIBU: Ninachofanya ni kutengeneza semi conductors chip ambazo ni kama ubongo wa hivi vifaa tofauti tofauti tunavyotumia. Mfano kwenye Iphone 15 promax kuna chip ambayo nimeshiriki kuitengeneza.

Swali: Kwa hiyo kwenye iMac, iPod, iPhone kuna akili zako mule ndani?

JIBU: Ndio.

Swali: Hadi sasa umetengeneza chip ngapi?

JIBU: Kama milioni mia nne.

Swali: Kwa hiyo mchakato wa chip huwa unakuwaje?

JIBU: Chip huwa inatokana na uhitaji wa wateja ambapo wanaanza watu wa marketing kwa kusema kuwa tunataka chip ya namna hii au ile kisha tunatengeneza. Mfano watu wa marketing wanaweza sema wanataka chip inayoweza kutengeneza camera inayopiga 3-D.

20231023_105515.jpg

Aboubakar azungumzia masuala ya teknolojia ilipofikia ambapo kwasasa teknolojia ya virtual reality ni pamoja na mtu kuweza kushika vitu vilivyopo katika computer. Katika hili, Aboubakar ameshiriki katika uundaji wa chip ya kitu hiko.

Teknolojia ya Hololense
Hii ni teknolojia ambayo inamfanya mtu afanye kitu kwa vitendo kama yupo kwenye mazingira halisi. Mfano mtu unataka kumfundisha mtu kutengeneza gari, mtoto akitumia teknolojia hii anavaa hololence na anaweza kushika tairi, na kila kitu ambapo atakuwa kama anafanya kwa vitendo.

Akitolea mfano wa Apple Watch ambayo amesema amempa bibi yake anaweza kujua bibi yake ametembea kwa muda gani na umbali gani. Bibi yake amekuwa akitumia Apple Watch kujua ametembea hatua ngapi na kujua mapigo yake ya moyo.

Swali: Teknolojia inatusaidiaje kutambua dawa feki ambalo ni tatizo hapa nchini (Tanzania)?

JIBU: Teknolojia inaweza kuthibitisha uhalali wa dawa. Kwasasa ipo application inayotumika zaidi Afrika Magharibi. Application hiyo unapiga picha unawatumia ambapo wanaiprocess na kukwambia kama dawa hiyo ni sahihi au ni feki kwa kuangalia mtengenezaji wake na tarehe zake za kuharibika.

Swali: Kuhusu Autonomous cars (gari zisizo na dereva), zinafanyaje kazi?

JIBU: Hii teknolojia ni kama bolt hapa kwetu, ambapo mtu anarequest gari itakuja lakini haina dereva na atapanda, itamkumbusha vitu muhimu kama kufunga mkanda nk, kisha safari itaendelea hadi sehemu uliyoandika utafika. Taxi hii inapokuja inakuwa na sensor kuwa ni wewe. Mfumo huu ni bei rahisi zaidi kuliko taxi za kawaida.

Swali: Vipi kuhusu application ya afya ambayo unajipima mwenyewe kabla ya kwenda kwa daktari?

JIBU: Kwenye application hii unaitajia dalili zako zote na yenyewe itasearch kwenye database, kisha itakuambia ukapime vitu gani ili kubaini maradhi uliyonayo. Pia itakuuliza kama unahitaji kumuona daktari.

Hii inaweza kusense hata mtu akianguka na akianguka itamuuliza kama ni kosa limefanyika au iwasiliane na emergence kwa ajili ya msaada.

Swali: Wewe ni mkulima, je unafanyaje kilimo cha dijitali?

JIBU: Boston ni mji wenye baridi ambapo sehemu kubwa ya chakula ina import, lakini zamani watu walikuwa wanazalisha vizuri katika hali hii hii iliyopo hivi sasa. Hivyo tulifikiria namna ya kuzalisha chakula ndani ya Boston ikiwa na gharama nafuu. Sasa, tukatengeneza power plant ikiwa ni pamoja na kuwasha taa, kwa kuwa wakati mwingine jua linatoka muda mdogo ambapo ukitegemea jua hautaweza kuzalisha. Hivyo tunazalisha mwanga, joto na carbondioxide kwa mbogamboga tunayoizalisha.

Screenshot 2023-10-28 013502.png

Project ya kilimo ya Aboubakari inaendelea. Bado hawajapanda lakini tayari supermarket kadhaa zimeshanunua mazao yote. Ushauri wa Aboubakar Ally kwa vijana wa Tanzania ni utayari wa kuwekeza muda wako, skills zako na kila unachoweza na kukabiliana nacho.

Swali: Je, Teknolojia ni tishio la ajira za watu?
Mshiriki aliuliza swali kuhusu ajira za watu kwa kuzingatia suala la Autonomous cars ambazo hazina dereva.

JIBU
Aboubakari ambaye ni Mzungumzaji Mkuu wa Wiki ya CSO amesema tusiuchukulie poa uwezo wa mwanadamu kuendana na mazingira yake.

Hata zilipogunduliwa gari, watu waliokuwa wanaendesha farasi waliona kama ajira zao zinaenda kuchukuliwa, na kila ugunduzi mpya huwa na maswali kuwa nafasi yetu itakuwa ni nini katika teknolojia husika. Hata hivyo mwanadamu ana uwezo mkubwa wa kwenda sawa na mazingira yake.
 

Attachments

  • 20231023_112725.jpg
    20231023_112725.jpg
    955.7 KB · Views: 3
Sijaona cha maana. Kutengeneza kwake hizo chip kunatusaidia nini sisi kama watanzania?
Nunua hizo bidhaa utakuwa umesaidika...!

Wanao tumia bidhaa za Apple wamesaidika kwa alicho kifanya au changia ku patikana kwa bidhaa ambayo imeenda kutumiwa na watu wengi duniani pamoja na bibi yake😂

Wewe subiri serikali tukuletee maji na umeme ili useme serikali imenisaidia Au tukununulie mahindi kg moja🤣
 
Waafrika inferiority complex inawasumbua. Kwa hio mnajihisi na nyinyi tayari mnaijua technolojia.
Kiufupi mtu yeyote aliesoma sayansi anaweza kuwa trained kufanya kazi kwenye kiwanda cha chip au electronics. Ni ku operate machine, very softcated machine ambazo zinaratibu mambo mengi zenyewe.
Ningeona kuwa yeye ni mwamba kama anaweza kuwa na start up ya chip company.
Mnashobokea kuwa vijakazi vya wazungu.
Pumbavu zenu.
Hana msaada wowote kwa TZ na Afrika.
Jifunzeni kwa wachina na wajapani hawashobokei kuwa vijakazi bali kuanzisha technolijia mikononi mwao.
Mnaosema nna muonea wivu nawashangaa. Kwanza hata simjui na hana faida yoyote kwangu labda nyie mna fsada nae.
Sishobokei vijakazi walio west wakitumikishwa na wazungu hata awe nani, hawana faida yoyote kwa uchumi wa mtanzania na Afrika.
Hivi nishobokee kwa lipi hasa na kwa nini ulazimishe matakwa yako ya kushobokea watu wa ulaya.
Acheni tabia ya kitumwa tumwa.
Zamani mtu akitoka ulaya anapewa na micheo mikubwa mikubwa siku hizi serikali na watu kama mimi tulisha shituka, wakija wajipambanie. Hawana lolote ndio maana hawana hata vikampuni uchwara halafu niwashobokee.
POVU RUKSA NYIE MSIOKUWA NA HOJA, MNAULIZWA MASWALI MNAANZA KU REACT NEGATIVELY.
 
Back
Top Bottom