Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 12,911
- 11,405
Naomba niulize. Hivi hizo dissertation za UDSM ziko on-line?
Naona haya malumbano yanaendana na mada iliyopo hapa. Mimi ningeshauri kuwa wakati wakuu mkijiandaa kuandika vitabu kwa nini msifanye tafsiri ya vile vilivyopo wakati huo huo? Si muhimu kila wakati tuhangaikie kuvumbua gurudumu!
Fundi Mchundo:
Hiyo posti niiona na nilitaka kuileta hapa lakini mitambo hapa iligoma kufanya kazi.
Kabla ya kwenda chuo kwa nchi niliyosoma nilijiandaa kwa mwaka kujifunza lugha yao. Na nilitumia mieza saba kujifunza. Hii ilitokana na kwamba walimu walikuwa ni wataalamu wa kufundisha lugha ya pili.
Hivyo lugha yao nilijifunza kama tool ya kupatia knowledge. Kwa Tanzania lugha inakuwa sio tool ya kupatia knowledge inakuwa sehemu ya mafunzo.
Kuhusu kutumia vitabu vilivyopo tutalifanyia kazi bila kuvunja haki miliki. Na kwa somo kama hisabati tunaweza kutafsiri kitabu cha ki-china au kirusi bila wao kujua.
Kutafsriri ni moja ya mbinu bora za kusambaza elimu, sema sasa hawa wenzetu hakimiliki za kazi zao zinakuwa zinauzwa bei mbaya sana kwa nchi masikini sana kama zetu. Ila hakuna lisilowezekana.
Shida ya kutotumia lugha kama nyenzo ya kupatia maarifa nadhani ndiyo hasa inayokifanya Kiswahili kutokuwa na umaarufu sana. Labda tungeanza na kutatua hilo kwanza.
Nchi karibu zote za Skandinavia (nadhani na Ujerumani pia)wanasoma masomo yote hadi ngazi ya shahada kwa lugha zao za asili. Nadhani hata uelewa unakuwa mkubwa.
NILIKOSA KILICHOKUWA KINAENDELEA. SASA NINAKUBALIANA NANYI MIA KWA MIA. ILA SASA TUFANYE KWELI. SASA MIMI NIKO SHERIA, NA NYIE MNAANZA NA HESABU SI MCHANGO WANGU UNAWEZA KUWA LIMITED. NINASHAURI TUKISHA KUWA NA MEMBAZI WA KUTOSHA, BASI TUJIUNGE KWENYE GROUPS KADHAA, ILI WAKATI WENGINE WANADEAL NA HESABU, WENGINE SAYANSI, WENGINE VITABU VYA SANAA.
AU TUNAWEZA KUDEAL NA HIZO SAYANSI ILA WENGIGINE KAZI KUBWA IKAWA KATIKA KUYUMBULISHA MANENO, ILI KAZI IENDE HARAKA HARAKA.
KUNA RESEARCH REPORT "ACADEMIC REPORT" NINAIFANYA NA NINADHANI IKISHAKUWA TAYARI NITAIWEKA KWENYE KISWAHILI.
SHUKRANIA SANA KWA UAMUZI HUU.
Kutafsriri ni moja ya mbinu bora za kusambaza elimu, sema sasa hawa wenzetu hakimiliki za kazi zao zinakuwa zinauzwa bei mbaya sana kwa nchi masikini sana kama zetu. Ila hakuna lisilowezekana.
Shida ya kutotumia lugha kama nyenzo ya kupatia maarifa nadhani ndiyo hasa inayokifanya Kiswahili kutokuwa na umaarufu sana. Labda tungeanza na kutatua hilo kwanza.
Nchi karibu zote za Skandinavia (nadhani na Ujerumani pia)wanasoma masomo yote hadi ngazi ya shahada kwa lugha zao za asili. Nadhani hata uelewa unakuwa mkubwa.
Cha muhimu ni kuwa watanzania ni lazima tuwe Multi-Lingo. Masaa anayotumia mwanafunzi kujifunza kiingereza akiwa primary school yanatosha kabisa. Lakini ni lazima wanaofundisha wawe wataalamu wa kufundisha lugha ya pili.
Nadhani vyuo vya elimu ya juu vingeanzisha program za watu kuchukua digrii ya kufundisha kiingereza kama lugha ya pili.
Hizi programu zipo pale UDSM siku nyingi sana, katika kitengo cha "Foreign Languages and Linguistics" chini ya akina Michael Kadeghe na wenzake. Hapo kuna Kifaransa, Kiingereza n.k. na kuna watu kibao wamepikwa hapo na wanaendelea na majukumu uliyoyataja.
Tuendelee na mjadala wa kuandika vitabu vya kiada na ziada kwa Kiswahili.
Naomba niulize. Hivi hizo dissertation za UDSM ziko on-line?
Labda IDIM au BImkubwa wanaweza kutusaidia katika swali lako.
Kwenye mjadala wa vitabu, naona tuanze kuchukua hatua mpya. Weekend hii nita-set internet infrastructure ya communication.
Kitu kimoja ningeomba ni kuwa tuache tabia yetu ya kitanzania. Tunapoanzisha vitu tuna mbwembwe nyingi lakini baada ya muda si mrefu shughuli zinakufa bila kutoa mazao.
wewe tengeneza harafu tuangalie namna ya kutumia maneno
MzalendoHalisi:
Mabadiliko yoyote yanaleta CHAOS hata kama yana nia nzuri. Kitaaluma Nyerere was quite right kutumia kiswahili lakini kilichokwamisha ni resources.
Kuna siku nilikuwa kwenye mkutano na wana mapinduzi fulani. Na wao wakawa wanataka kutumia French Creole katika mashule huko Haiti. Niliwaambia kuwa nimetoka Tanzania na matokeo ya majaribio yetu sio mazuri. Wakaniona mimi ni msaliti mkubwa wa PAN Africanism na wakanipa mifano ya Lugha ya Ki-Hebrew kutumika tena.
Kwa bahati nimeishi na nina marafiki wayahudi. Wahayahudi wengi walikuwa ni wataalamu wa fani mbalimbali. Hivyo walipohamua kurudi Israel na kutumia lugha yao ya zamani walijua wanafanya nini.
Kwa upande wa Tanzania tulianzisha matumizi ya kiswahili lakini hatukuwa na wataalamu ambao wangeweza kuandika mambo yao katika kiswahili. Na bado tulitegemea wataalamu wa kigeni ambao hawakuwa tayari kujifunza kiswahili.
Kuna jamaa alimaliza Phd ya Physics na sasa anafanya kazi ya kuwasaidia wajapan wanapoandika research papers zao.
Hivyo hata Tanzania, tukiacha roho mbaya. Watu wanaweza kufanya research paper kwa lugha walizozoea na wengine wakawa wanawasaidia kuziweka katika kiingereza safi.
Mwanafunzi Chuo Kikuu Dar ajiua kwa kunyimwa shahadaNa Kizitto Noya
MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Nilla Makingu amejiua kwa kunywa sumu baada ya uongozi wa chuo hicho kugoma kumtunuku shahada yake.
Habari zilizolifikia gazeti hili miezi kadhaa baada ya kifo cha mwanafunzi huyo na baadaye kuthibitishwa na ndugu wa marehemu zinasema kuwa mwanafunzi huyo aliyekuwa anasomea shahada ya uhandisi, alijiua baada ya kushindwa kuwasilisha utafiti wake kwa wakati na chuo kukataa kuipokea.
Hata hivyo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala ametupilia mbali mdai hayo na kufafanua kuwa kifo cha mwanafunzi huyo si tukio la kuhusishwa na kushindwa kwake mitihani kwani alikuwa na njia mbadala ya kukamilisha masomo yake.
Kabla ya kifo chake mwanafunzi huyo aliyekuwa anahitimu mwaka wa nne katika Kitivo cha Uhandisi Julai 16 mwaka jana, aliandika kwa mkono ujumbe unaowalaumu maprofesa kadhaa wa chuo hicho (majina tunayo) kuwa wamemwonea kwa kukataa wake aliowasilisha kwa kuchelewa kutokana na ugonjwa.
"Nilishindwa kuwasilisha ripoti yangu kutokana na ugonjwa, pamoja na kutoa taarifa hiyo kwa uongozi wa chuo, bado hawakutaka kunielewa. Nimeona nichukue hatua hii ngumu kwa sababu ni wazi kwamba nimeshindwa kufikia matarajio yangu," sehemu ya ujumbe wa marehemu inasomeka na kuongeza:
?Ninasikitika kwa uamuzi huu ambao utamhuzunisha mpenzi na ndugu zangu lakini naamini mtanisamehe na kusahau muda mfupi ujao. Mnisamehe pia kwa kuwa tegemezi kwenu kwa muda mwingi lakini sikuwa na namna wala njia yoyote ya kuwasaidia.
?Nimejiua mwenyewe na kutaka taifa linizike hapa Dar es Salaam kwani hakuna sababu za kutumia gharama nyingi kunisafirisha kwenda Matongo - Bariadi. Nitupeni popote ili mradi tu nirudi kwenye udongo na asilaumiwe mtu. Ni mimi Nilla," uliendelea kusema ujumbe wake ambao nakala yake halisi ilipelekwa kituo cha polisi Stakishari, Ukonga, Dar es Salaam.
Ndugu wa Marehemu katika taarifa yao waliulaumu uongozi wa chuo hicho wakisema kuwa isingewezekana mtoto wao anyimwe shshsda kwa kushindwa somo moja wakati masomo mengine yote amefaulu vizuri.
Wameonyesha wasiwasi juu ya mfumo wa vyuo vikuu wakidai kuwa ni wa kirasimu, unyanyasaji na ukandamizaji huku wakihusisha rushwa kuwa ni jambo lililokuwa likilalamikiwa na marehemu katika kushindwa kwake kumaliza masomo.
"Pia kulikuwa na mazingira ya rushwa, kujuana, ukabila na kunyanyasana huku wasionacho wakikosa haki zao," ilisema sehemu ya taarifa yao kwa vyombo vya habari.
Wazazi hao wameiomba serikali kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na suala hilo ili kubaini ukweli wake na kufanya mabadiliko ya mfumo wa uongozi katika chuo hicho.
"Wazazi wangependa kuona suala hili linachunguzwa kwa kina na serikali na mhusika, wahusika wanachukuliwa hatua za kisheria kwani inaonekana ?madokta? na maprofesa ni miungu watu na mfumo wa uendeshaji wa chuo hicho ni mbovu na unahitaji marekebisho makubwa," ilisema taarifa yao.
Mdogo wa marehemu Nhandi Makingu aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kushindwa kupata shahada yake, marehemu alikuwa anafundisha shule ya chekechea iliyoko Gongo la Mboto Dar es Salaam.
Alisema awali baada ya rufaa yake kukataliwa, marehemu alikuwa amekata tamaa ya kuishi na kuanza kuwakimbikia ndugu na rafiki zake kabla ya kuamua kufundisha katika shule hiyo ya awali.
Akifafanua zaidi Mukandala alisema mwanafunzi anayeshindwa kutimiza masharti ya kipindi, pamoja na kupewa alama ya kufeli, anapewa muda wa kurudia mtihani au anaweza kuendelea na masomo huku anarudia mtihani aliofeli au kurudia mwaka wa masomo jambo ambalo Nilla hakutaka kulifanya.
Kuhusu tuhuma za rushwa, Profesa Mukandara alisema haamini kwamba kuna wahadhiri wanaoweza kumdai mwanafunzi fedha ili wamfaulishe mitihani ingawa anaamini pia kuwa wahadhiri wa vyuo vikuu si malaika. "Mimi siamini kwamba kuna Profesa anayeweza kumwomba mwanafunzi fedha ingawa pia wao si malaika. Lakini katika hali ya kawaida mwanafunzi ana hela gani ya kumhonga Profesa?" alihoji Profesa Mukandara.
Ngoja niongeze chumvi kwenye huu mjadala.. Hii ni kutoka gazeti la Mwananchi la March 1 2008
http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=4781
Kwa kuanza nime-install engine ya wikipedia. Hivyo mnaweza kutembelea www.elimupedia.com . Nafanya custumization ya lugha. Kwa hiyo naomba michango yenu katika kutafsiri link na navigation button. Tutaendelea kutumia JF kama forum.
Sisi tunatumia elimu ya Chuo Kikuu kama filtration system ambayo ina-discourage progress na hivyo kuishia kuwa na idafi finyu ya watu walioelimika na kuweza kutuongezea wataalamu na wabunifu. Tumefikia kuzalisha tabaka kubwa la Wanaohitimu kwa kufaulu mitihani na kushindwa kutumia elimu yao kwa jamii.
Nakumbuka sifa za Muhimbili, Kitivo cha Uhandisi na hata Sheria vilivyokuwa vikisifika kwa ku-disko watu na hata Waalimu kujisifu kwa kusema "mwaka huu nimewakomoa wanafunzi walikuja 100 nitahakikisha 10 tuu ndio wanafaulu!"
Hii si dhana endelezefu bali ni dhana dumazi! No wonder hata UDSM wanakuwa wagumu kukubali kuwa kuna taasisi nyingine ambazo zinaweza kuwa na uwezo wa kuwa vyuo.