Mushobozi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2007
- 543
- 103
Hili sio suala la dini. Na kama lawama za Nyerere zinakuja, zije kwa siasa zake katika masuala ya elimu.
Shule zilizotaifishwa nyingi zilikuwa za dini lakini sehemu kubwa ya funding ilikuwa inatoka serikalini. Hivyo Nyerere alifanya vizuri kutaifisha shule. Nyerere alisomeshwa kwa schoolarship ya serikali lakini kazi alipangiwa katika shule ya dini. Na haya yalikuwa mapungufu makubwa ya serikali ya mkoloni.
Pamoja na kutaifisha hizo shule na kuzifanya kuwa za taifa, sera zake za kuendeleza elimu zilikuwa mbovu sana. Mpango wa UPE ambao ulikuza literacy rates ulikuwa ni mbovu. Wataalamu wa mambo ya elimu walitoa mapendekezo yao kuwa ili UPE iwe na mafanikio bila kupunguza kiwango cha elimu, ni lazime mpango uwe wa miaka 20 (long term). Mapendekezo hayo aliyakataa na kusema UPE inaweza kufanyika kwa mpango wa miaka 7 tu. Na katika mpango wake huo akatumia walimu wasio na mafunzo. Na matokeo mabovu ya mfumo mzima yalianza kuonekana kabla ya yeye kuondoka madarakani. Na kama mipango yake ingekuwa mizuri katika UPE, serikali ya Mkapa isingerudia kufanya mpango uliofanana na UPE miaka michache iliyopita.
Pamoja na kuongeza shule nyingi wakati wa mpango wa UPE bajeti ya elimu haikuongezeka kukidhi mahitaji ya wizara hiyo. Hivyo kuwa na sera na kutotoa pesa za kusaidia sera hizo ni sawa na kutokuwa na sera zenyewe.
Pia alikuwa nyuma sana katika sera za elimu ya juu. Model yake ilikuwa kwa watu wengi kuwa na elimu ya darasa la saba. Baada ya kundi hilo kuwe na kundi watu waliomaliza vyuo vya kati ambao watakuwa kama viranja. Na baada ya kundi hilo liwepo kundi la wachache wenye elimu ya juu watakaongoza wenzao.
Mfumo huu ulizungumzwa kwanza na William Edward Burghardt DuBois (mmoja wa waanzilishi wa Pan Africanism). Yeye alisema kuwa hili watu weusi waendelee ni lazima wawe na talented ten (asilimia kumi ya wenye vipaji).
Matalajio yalikuwa ni kutoa watu wenye vipaji kuendeleza jumuia zao. Siku za mwisho wa maisha ya DuBois alisema hawa talented ten wamekuwa ni dissapointment kwa jumuia za watu weusi. Badala ya kutumikia jumuia zao wamekuwa Bourgeoisie na mchango wao ni mdogo katika maendeleo ya mtu mweusi.
Watanzania wengi wanapoteza muda katika vyuo vya kati. Kwa maoni yangu vyuo vya kati vifanyiwe marekebisho hili viwe vyuo vinavyotoa digrii. Na wataalamu wa ngazi za kati (Viranja) wawe ni watu wenye digrii na sio diploma. Wahitimu wenye digrii wafanye kazi kama viranja katika miaka mitatu mpaka mitano ya mwanzo (Entry and Junior level). Na baada ya miaka hiyo waweze kushika senior position, lakini hizo senior position zitegemee performance yao ya miaka iliyopita.
Ukiajiri wanafunzi kutoka shule na darasa moja, bado kutakuwa na tofauti kati yao. Ukichukua wanafunzi kutoka shule moja campus tofauti, bado kutakuwa na tofauti. Na vile vile tofauti kati ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali ni kitu cha kutegemewa lakini sio cha kufanya chuo moja kuwa bora zaidi ya kingine. Mwajiri anapotoa ajira kwa wahitimu wapya ni lazima kutoa mafundisho ya utamaduni wa sehemu yake ya kazi, matarajio ya mwajiri na baadaye atumie angalau mwaka kuona ni jinsi gani mwajiriwa anafanya kazi yake vizuri.
Mpaka sasa utasikia wanasiasa wetu au wenye elimu ya juu Tanzania wanasema kutoa digrii kwa watu wengi kutawafanya wahitimu kuwa madreva wa taksi kama ilivyo Nigeria au Ghana. Kwa maoni yangu msimamo huu ni PURE CRAP. Watu wasinyimwe elimu kwa sababu ya ukosefu wa kazi. Mwenye digrii akiwa dreva wa taksi anafanya kazi hiyo kama stepping stone na lazima atakuwa na shughuli zingine za kuendeleza maisha. Mwenye elimu ndogo akiwa dreva wa taksi atafanya kazi hiyo kama way of life.
Mkuu Zomba,
Bado nasisitiza kwamba hujatenda haki kuleta malumbano ya kidini katika mada hii. Utatuhaibia mtiririko!
Unajua nilicheka pale wasomi wetu na Walimu wao, walipopelekwa DIAMOND JUBILEE wakavaa sale za CCM, na kuanza kuimba kidumu chama cha mapinduzi. waliporudi kwenye account zao wakakuta hela hamna na wakaanza kuandamana haikuchelewa wakatimuliwa mkuku. huku walimu wao walioenda nao wakiwatetea. nilipomuuliza jamaa mmoja aliyekuwepo kwenye DIAMOND kwa nini alienda akaambiwa alidhani wangeongezewa hela. nilimwambia haki inadaiwa na haibembelezwi. tuendelee kukata shule.