Prof. Nombo: Mtaala mpya wa Elimu una Viwango vya Kimataifa

Prof. Nombo: Mtaala mpya wa Elimu una Viwango vya Kimataifa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,161
Reaction score
17,621

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema Mtaala ulioboreshwa ulioanza kutekelezwa Januari 2024 una ulinganifu wa viwango vya kimataifa, hivyo kuwataka walimu kwenda kufundisha somo la biashara ili kuwasaidia wanafunzi kupata mahiri za kimataifa.

Soma pia: Mhadhiri wa UDSM Dkt Ibrahimu Nzima: Kidato cha 6 wanaojiunga vyuo uwezo wao wa kuchambua mambo umeshuka

Hayo yamesemwa Julai 27, 2026 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Tkenolojia , Prof. Carolyne Nombo wakati akifungua mafunzo ya walimu wa ajira mpya wa somo la Elimu ya Biashara yanayofanyika katika chuo cha Ualimu Morogoro.

"Naomba niwaambie Mitaala tulionayo sasa ni yakimataifa, yaani inaulinganifu na Mitaala mingine ya kimataifa, kwahiyo ni imani yetu kwamba ninyi mtaofundisha somo hili la Biashara mtasaidia wanafunzi wa somo hilo kipata mahiri za kimataifa" Amesema Prof. Nombo

Ameendelea kusema, Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan imewezezesha maboresho ya Sera ya Elimu ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023 yaliyopelekea maboresho ya Mitaala yaliyokidhi ubora wa kimataifa na kuzalisha somo hilo la biashara.

Aidha, Prof. Nombo amesema, Serikali inatambua kazi kubwa na nzuri inayofanywa na walimu nchini katika kumjenga mtoto kuanzia ngazi zote ndani na nje ya shule na kuwataka kuiona kazi hiyo ni ya heshima kuifanya.

Pia, ametoa wito kwa walimu wote nchini kuhakikisha wanajiunga katika jumuia za ujifunzaji ili kupata maarifa zaidi yatakayowasaidia kurahisha katika eneo la ufundiushaji ambapo amesema watumie mifumo kama Learning management sytem (LMS) ambayo itawasaidia katika kujiboresha kwenye kazi yao ya ufundishaji.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba ameeleza kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwa walimu wa ajira mpya kuweza kupata maarifa yatakayowasaidia katika eneo la ufundishaji na kuwa litasaidia sana kwa walimu hao kupata ujuzi na maarifa watakayowapa wanafunzi shuleni ambapo wataweza kuhitimu na baadae kuweza kuajiriwa na kujiajiri wenyewe kupitia somo hilo la biashara.
 
Swala ni utekelezaji unaweza uka copy na ku-paste mtaala wa Norway au Singapore bila shida yoyote… kipengele kinakuja kwenye implementation
 
Watoto wao wanasoma huo mtaala wa kimataifa 😂
 
Back
Top Bottom