UDOM wanakimbiza kwenye soko la ajira

bulabo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
620
759
Kwenye hizi nafasi za TRA zilizotoka vijana wengi wa UDOM wamepita.

Hii inaonesha jinsi gani udom wanadeliver katika ufundishaji hasa hasa Tehama.

Vijana wengi wa tehama kutoka udom wameiva me niliwahi kuwachukua vijana watatu intern wamenifanyia kitu kikubwa....Wakati wa kutengeneza mifumo yetu.

Kongole UDOM
 
Interview zenyewe zinafanyikia huko kwao unategemea nini? Yaani unaletewa chakula mdomoni bado ushindwe kula? Hicho sio chuo ni CHUO SHIKIZI
 
Kwenye mambo ya tehama hapa Tanzania Udom haina mpinzani.

Ila kwenye course zingine ni ujinga mtupu.
 
Unataka vita na watu wa UDSM ngoja wanakuja wameenda ku certify vyeti mahakamani.
 
Duh kwahiyo vijan hizi aptitude test ndio mnatumia kupima competency ya ufundishaji wa chuo husika, ?

Kuweni na heshima na walimu wenu…ubora wa product za chuo flani unapimwa kwenye skill set za mhitimu ku deliver kazi fulani, kufaulu interview ni kama kufaulu kweingine!
 
Kwenye mambo ya tehama hapa Tanzania Udom haina mpinzani.

Ila kwenye course zingine ni ujinga mtupu.
Hata education pia UDOM wako very systematic na course zao ni applicable wa ulimwengu wa sasa
 
Hivi zama za kutambua vyuo ulivyosoma bado zipo? Huo utoto na ujinga bado upo.
Maana hata zama za kutambiana vyeti ulivyotunukiwa zilishapitwa na wakati, sembuse chuo ulichosoma.

Uwe uliishia darasa la saba, form four, form six, Cheti, Diploma, Degree, Masters nk. kwa sasa wote tunakutana mitaani kupigwa na jua, kunyeshewa mvua, kula msoto, kubet. Wote tunapigika vilivyo. Kwa sasa kusoma ili kuja kuajiriwa ni sawa na kucheza tatu mzuka.
 
Back
Top Bottom