Stories of Change - 2023 Competition
Aug 24, 2022
10
18
Tanzania ni moja kati ya nchi nyingi barani Afrika ambazo, zina wimbi kubwa la vijana wasiokuwa na ajira hasa , wahitimu wa vyuo vya kati na vyuo vikuu. Jambo hili likionekana kuchochea sana vitendo vya kihalifu hasa, katika miji mikubwa kama Dodoma, Dar es salaam na Mwanza.

Sio kwamba serikali haijui, inajua na kumekuwa na mashauri mbalimbali kutoka kwa viongozi wakubwa wa nchi , wakihamasisha ujasiriamali kwa vijana wasio na ajira. Kwamba suluhisho la ukosefu wa ajira ni kujiajiri. Lakini hili pia limekua na ukakasi fulani kwani, vijana wengi hawana mitaji inayoweza kuwawezesha kujihusisha na ujasiriamali wenye tija. Badala yake kunakuwa na wajasiriamali wengi wanaofunga shughuli zao kila siku na kusumbuliwa na migambo bila kupatikana kwa faida katika pato la Taifa na vijana hao.

Ni sahihi sana kuhamasisha ujasiriamali hasa, kwa vijana. Lakini pia ni wazi kwamba serikali haina rasilimali za kutosha kuwasaidia wajasiriamali hao kuendelea zaidi. Mikopo itolewayo kwa wajasiriamali ni hafifu na wanufaika ni wachache . Na kwa hakika ni wale tu wenye taarifa kuihusu. Wajasiriamali wadogo wengi hawana taarifa juu ya mikopo hii. Na hata ikitolewa , warsha za kuwaelimisha wajasiriamali hao juu ya uwekezaji wenye tija ni chache na wakati mwingine hazipo kabisa.

Turudi sasa kwa wahitimu wa vyuo vikuu na vyuo vya kati. Vijana hawa wapo katika mfumo wa elimu unaolenga wao kuhitimu masomo yao na kuajiriwa katika sekta mbalimbali. Lakini wanaangukia kwenye wimbi la wahangaikaji wengine ambao, hata hawakusoma. Ni nini hasa kifanyike kuwatoa mamia ya vijana hawa kwenye wimbi la ukosefu wa ajira na umasikini? Jibu langu litakuwa ni elimu inayomuwezesha kijana wa kitanzania kuwa moja wa washindani katika soko la ajira duniani.

Katika ulimwengu huu ambao ni wa teknolojia ,mtu yeyote anaweza kufanya kazi mahali popote akiwa popote. Soko la ajira duniani haimaanishi kwamba vijana waende nchi za mbali tu, hapana. Ila wawe na uwezo kutumia elimu na vipaji vyao kutoa huduma mahali popote ulimwenguni.

Nchi ya India iliyopo bara la Asia ni mfano mzuri wa utawala wa soko la ajira duniani. Hasa katika kila jambo linalohusiana na teknolojia . Ikiwa ni kati ya nchi zenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani, ilifungua milango kwaajili ya vijana kuweza kushindana katika soko la ajira duniani. Na kwa sababu hiyo utakuta wahindi katika vitengo nyeti ,hasa katika nchi zilizoendelea mfano ,Marekani. Na kuwa wawekezaji wakubwa katika nchi zinazoendelea mfano, Tanzania.

Walitumia mbinu gani hasa? Au ni nini kifanyike ili kijana wa kitanzania aweze kushindana katika soko la ajira duniani?Zifuatazo ni baadhi ya njia ambazo zitamsaidia kijana wa kitanzania kuwa katika soko la ajira la dunia;

Kuwa na ujuzi wa fani mbalimbali ambazo zitaongeza thamani ya elimu aliyoipata. Mfano tehama ,lugha ,uandishi na uwasilishaji wa mawazo kwa uma. Soko la ajira la dunia halihitaji sana mtu amejifunza nini ,badala yake , ni nini mtu huyu anaweza kuchangia na kufanya bora katika kampuni fulani au shirika fulani la dunia. Uwezo wa kijana kuzungumza lugha fulani ya kimataifa kwa ufasaha mfano, kiingereza, unamuongezea thamani na kumtofautisha na vijana wengine wenye kiwango cha elimu kama chake. Au uwezo wa kuzungumza lugha zaidi ya moja inamfanya kijana huyu kuvuta fursa nyingi zaidi za ajira. Tasnia nyingi zinahitaji ujuzi wa tehama hasa, sanaa. Pia kuweza kuwasilisha mawazo kwa njia ya uandishi wa kimataifa ni muhimu, kwasababu kila mtu huandika lakini si wote huandika kwa namna inayotakiwa. Hivi ndivyo utofauti unajengeka baina ya watafuta ajira katika soko la dunia. Unaweza kuona pia ni mambo ambayo kijana wa kitanzania anaweza kujifunza na akapata fursa ndani na nje ya nchi.

Kuwa na uchu wa kupata taarifa kuhusiana na nafasi za ajira katika soko la dunia. Moja kati ya vitu vinavyowakwamisha sana na kuwanyima fursa vijana wa kitanzania ni kutokuwa na taarifa. Mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi , hutoa nafasi za ajira kwa vijana . Mfano shirika la afya duniani( WHO) ,shirika la chakula duniani(FAO) na mengine mengi. Lakini ni vijana wachache sana hufatilia kujua zaidi au kuomba nafasi katika mashirika hayo. Pengine ni kwasababu vijana wengi wameelemea katika matumizi ya mitandao kwa lengo la kuburudishwa,hali inayowapelekea kukosa na taarifa muhimu kuhusu ajira.

Kuwa na mfumo wa elimu unaomuwezesha kijana kuwa na ujuzi wa mambo na sio elimu tu ya mambo hayo. Elimu ya kitanzania inalenga sana kumpa mwanafunzi taarifa juu ya kitu alichochagua kusoma na sio kumpa ujuzi. Kujifunza kwa vitendo ni kwa kiasi kidogo sana na wakati mwingine hakuna kabisa .Jambo linalopelekea vijana hawa kutoweza kushindana katika soko la ajira la dunia kwani wapo vijana wengine wengi wenye ujuzi wa vitendo na sio taarifa tu. Japo kuna juhudi zimewekwa katika sekta ya elimu lakini bado kuna mapengo mengi ambayo yakizibwa, kijana wa kitanzania atagombaniwa katika soko la ajira duniani.

Kumjengea kijana wa kitanzania ujasiri wa kushindana katika soko la ajira duniani, elimu ya kitanzania haimjengei mtoto au kijana uwezo wa kusimama na kujiamini ukilinganisha na elimu ya mitaala mingine kama vile Cambridge . Vijana wadogo wenye umri sawa wanaotumia mitaala ya NECTA na Cambridge huwa tofauti kabisa kwa namna ya kufikiri , kujiamini na kupambanua mambo. Hii inaonesha kuna nafasi ambayo sekta ya elimu hasa katika shule za msingi na sekondari inaweza kufanya ili kukuza vijana wenye kujiamini. Vijana watakaoweza kusimama kwenye majukwaa makubwa ya dunia na kuzungumza kwa manufaa ya nchi yetu.

Na mwisho kabisa kwa kujitangaza; zama hizi si kama zama za zamani ambapo mtu mwenye ujuzi au kipaji fulani alisakwa kokote aliko na kusaidiwa. Sasa inampasa kila kijana kuweza kuonyesha kila anachofanya au anachoweza kufanya ili dunia ione . Lakini pia vijana wengi hukosea na kukosa fursa pale wanapotangaza sanaa zao na kazi zao katika majukwaa ambayo si sahihi . Kujua namna sahihi ya kujitangaza ni muhimu sana ,mfano linkedln ni sehemu nzuri ya kuanzia katika safari ya kuliteka soko la ajira la dunia.

Kama iliyoainishwa ni halisi kwamba, kijana mwenyewe ndiye mwenye nafasi ya kujiongezea thamani yake. Wapo vijana wa kitanzania wanaofanya kazi kimataifa na hii ni uthibitisho kwamba ipo nafasi kwa kila mwenye uthubutu kuweza kujiongezea thamani ili aweze kuteka soko la ajira la dunia na kupata mafaniko chanya.
 
Point nzuri ila sasa kwa Hawa vijana ambao hawana ajira tunawasaidiaje? Maana umeishauri Serikali kufikiria kutengeneza future plan kwa ajili ya kizazi kijacho.

Hivi hiyo pic ni ya kwako?
 
Point nzuri ila sasa kwa Hawa vijana ambao hawana ajira tunawasaidiaje? Maana umeishauri Serikali kufikiria kutengeneza future plan kwa ajili ya kizazi kijacho.

Hivi hiyo pic ni ya kwako?
Zipo njia nyingi sana wanaweza wakajifunza na kufanya kama chanzo cha ajira. Mfano nimejifunza graphics na designing mtandaoni na kuwauliza wanaojua katika mazingira yangu.

Lakini pia najifunza kiingereza international cha kuongea na kuandika , hii inaongeza nafasi za chochote nitakachotaka kufanya kama ni mashairi ninayofanya, vitu ninavyoandika ,biashara ninazofanya na masomo ninayosoma.

Kuna kitu kila mtu anaweza kufanya, cha kwanza ni kujua anaweza kufanya nini ndipo akiongezee thamani kimlipe.
 
Tanzania ni moja kati ya nchi nyingi barani Afrika ambazo, zina wimbi kubwa la vijana wasiokuwa na ajira hasa , wahitimu wa vyuo vya kati na vyuo vikuu. Jambo hili likionekana kuchochea sana vitendo vya kihalifu hasa, katika miji mikubwa kama Dodoma, Dar es salaam na Mwanza.

Sio kwamba serikali haijui, inajua na kumekuwa na mashauri mbalimbali kutoka kwa viongozi wakubwa wa nchi , wakihamasisha ujasiriamali kwa vijana wasio na ajira. Kwamba suluhisho la ukosefu wa ajira ni kujiajiri. Lakini hili pia limekua na ukakasi fulani kwani, vijana wengi hawana mitaji inayoweza kuwawezesha kujihusisha na ujasiriamali wenye tija. Badala yake kunakuwa na wajasiriamali wengi wanaofunga shughuli zao kila siku na kusumbuliwa na migambo bila kupatikana kwa faida katika pato la Taifa na vijana hao.

Ni sahihi sana kuhamasisha ujasiriamali hasa, kwa vijana. Lakini pia ni wazi kwamba serikali haina rasilimali za kutosha kuwasaidia wajasiriamali hao kuendelea zaidi. Mikopo itolewayo kwa wajasiriamali ni hafifu na wanufaika ni wachache . Na kwa hakika ni wale tu wenye taarifa kuihusu. Wajasiriamali wadogo wengi hawana taarifa juu ya mikopo hii. Na hata ikitolewa , warsha za kuwaelimisha wajasiriamali hao juu ya uwekezaji wenye tija ni chache na wakati mwingine hazipo kabisa.

Turudi sasa kwa wahitimu wa vyuo vikuu na vyuo vya kati. Vijana hawa wapo katika mfumo wa elimu unaolenga wao kuhitimu masomo yao na kuajiriwa katika sekta mbalimbali. Lakini wanaangukia kwenye wimbi la wahangaikaji wengine ambao, hata hawakusoma. Ni nini hasa kifanyike kuwatoa mamia ya vijana hawa kwenye wimbi la ukosefu wa ajira na umasikini? Jibu langu litakuwa ni elimu inayomuwezesha kijana wa kitanzania kuwa moja wa washindani katika soko la ajira duniani.

Katika ulimwengu huu ambao ni wa teknolojia ,mtu yeyote anaweza kufanya kazi mahali popote akiwa popote. Soko la ajira duniani haimaanishi kwamba vijana waende nchi za mbali tu, hapana. Ila wawe na uwezo kutumia elimu na vipaji vyao kutoa huduma mahali popote ulimwenguni.

Nchi ya India iliyopo bara la Asia ni mfano mzuri wa utawala wa soko la ajira duniani. Hasa katika kila jambo linalohusiana na teknolojia . Ikiwa ni kati ya nchi zenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani, ilifungua milango kwaajili ya vijana kuweza kushindana katika soko la ajira duniani. Na kwa sababu hiyo utakuta wahindi katika vitengo nyeti ,hasa katika nchi zilizoendelea mfano ,Marekani. Na kuwa wawekezaji wakubwa katika nchi
Well said Jackie.
 
Back
Top Bottom