Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 61,023
- 36,888
Kampeni za kumgeuzia kibao Rais Kikwete zaanza
Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye watu wake wa karibu wanadaiwa kumgeuka n a kuanza kumfanyanyia kampeni za kumchafua.
*Baadhi ya wabunge watumika kufanya kampeni
*Wana CCM wahoji ukimya wa Kikwete
Na Mwandishi wetu
KAMPENI za kusafisha watuhumiwa wa kashfa mbalimbali za ufisadi nchini sasa zimechukua sura mpya baada ya kikundi cha baadhi ya wabunge na watu wengine kufanya kampeni za chini chini za kumgeuzia kibao Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.
Habari zilizopatikana mjini Dodoma, zinaeleza kuwa kampeni hiyo inafanywa na baadhi ya watu na wabunge waliopo karibu na watu wanaotuhumiwa kwa kashfa za ufisadi nchini kwa kuwafuata wabunge wenye ushawishi mkubwa.
Mbunge mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake aliiambia Mwananchi Jumapili kuwa hivi karibuni alifuatwa na mmoja wa wabunge wenzake akimshawishi ajiunge katika harakati za kusafisha mtuhumiwa mmoja wa kashfa ya kampuni ya kuzalisha umeme wa Dharura ya Richmond.
Alimweleza kwamba kimsingi watu wanaotajwa katika kashfa hiyo hawahusiki na kwamba walitolewa kafara kumlinda Rais Kikwete.
Alipomwuliza kwa nini rais aingizwe katika kashfa hiyo alisema kwamba alijua utaratibu mzima na kwamba kuwawajibisha mawaziri pekee haitoshi lazima watu wote waende na maji.
Mbunge huyo alisema alimwambia wazi kwamba hawezi kujiunga katika harakati hizo kwa sababu anajua rais hakuhusika kwa lolote na suala hilo na kwamba walioaguka kutokana na kashfa hiyo wamewajibika kutokana na nafasi zao.
"Nchi hii inaelekea kubaya kuanza kufanya kampeni za kusafisha viongozi kwa kutumia njia za kutaka kumchafua rais ni hatari sana," alisema.
Alisema kama serikali na Rais Kikwete hawasimama kuhakikisha kuwa watuhumiwa ufisadi wanachukuliwa hatua ipo hatari kwa vikundi hivi vinavyoibuka nchini kufanya kampeni chafu zikaivuruga nchini.
Mbunge mwingine alidokeza Mwananchi Jumapili kampeni hizi za kuwasafisha baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi zinaendelea na kwamba sasa zinafanyika chini chini baada ya hapo awali kufanyika kwa njia ya wazi kabla ya kupigiwa kelele na wananchi.
Alisema baada ya watu hawa kushindwa kujitokeza wazi bungeni kuwatetea watuhumiwa wa ufisadi kutokana na kuogopa macho ya wapigakura wao, sasa wanamfuata mbunge mmoja mmoja kumshawishi kujiunga na kambi yao.
Mbunge huyo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) alisema kitendo cha Rais Kikwete kushindwa kutumia vikao vya juu vya chama kuwadhibiti mafisadi, kimetoa mwanya kwa watu hao kuanza kumgeuzia kibao kuwa hawezi kuwafanyia kitu.
"Unajua kama baadhi ya makada wanaoendesha kampeni za kumchafua rais wana uwezo wa kuzungumza naye kwa simu na kumtumia message akajibu, lakini hivi sasa wanamsliti, ni hatari sana lazima awe mkali sasa rais wetu watammaliza," alionya.
Baadhi ya watu nchini walipoulizwa maoni yao kuhusiana na kampeni hizo, walisema Rais Kikwete hana njia nyingine zaidi ya kuwabana ndani ya CCM na serikalini na kwamba watakaobainika wachukuliwe hatua kali.
Kwa upande wake Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema mjadala wowote kuhusu suala la Richmond kuendelea kufanyika sasa hauna maana kwani suala hilo limefungwa baada ya kufanyiwa kazi na kumalizika.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Kapteni George Mkuchika aliliambia gazeti hili jana kuwa chama hakuna maelezo yoyote ya ziada kuhusu suala hilo kwani kinaamini kuwa limefungwa na kinachosubiriwa sasa ni utekelezaji wa kazi iliyofanyika.
"Bwana kuhusu Richmond suala limemalizika na kazi imefanyika sina maelezo ya ziada na mjadala wowote sasa hauna maana," alisema Mkuchika.
Mbunge wa Njombe Kaskazini, Jackson Makweta alisema viongozi lazima waelewe kwamba hii ni nchi yetu sote lazima tuonyeshe mapenzi.
Alisema viongozi ni sawa na gari ambalo kama tutazembea tutalifanya liache njia na kunguka na kuua watu wasoiokuwa na hatia.
Makweta alisema uchambuzi wa kina kuhusu mafisadi lazima ufanyike ili ukweli wa mambo ufahamike .