...Nadhani ni muafaka nikianza kwa nukuu ya Mwalimu Nyerere kutoka kwa kijitabu cha
TUJISAHIHISHE (1962, ukurasa wa 8):
Watu walio hatari ni wale ambao wanafikiri kuwa wanajua kila kitu, wala hawana haja ya kujifunza zaidi.
Inawezekana Mch. Gwajima hakuwahi kusoma kitabu hiki cha Mwalimu Nyerere (1962) na inawezekana Mch. Gwajima ana matatizo ya "ugonjwa" wa ubinafsi zaidi ya tunavyodhani! Nina sababu ya kudhani hivyo; na siwezi kuuma maneno juu yake, hoja zifuatazo zina kila sababu ya kujibu madai yake juu ya UCHIZI anaouona yeye (Mch. Gwajima). Hoja zangu ni hizi:
- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni zao la Mkataba wa Muungano (Articles of Union) baina ya nchi mbili;
- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliridhiwa Tanganyika na kupitishwa kwa Sheria Na. 22 ya mwaka 1964 inayotambua kwamba, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni "muungano" wa nchi MBILI (Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar)...rejea Kifungu cha 3 na 4 cha Sheria Na. 22, 1964...kwa jinsi hiyo, MUUNGANO wa Tanganyika na Zanzibar si muungano wa WATU isipokuwa ni muungano wa JAMHURI mbili (Tanganyika na Zaznibar).
Nadhani Mch. Gwajima anahitaji "aelewe" kwamba: ZILIZOUNGANA NI NCHI MBILI; NA SI WATU WA NCHI MBILI! Kwa kuwa nchi mbili (Tanganyika + Zanzibar) ndizo zilizoungana hakuna sababu yeyote kudhani kwamba kwa wingi wa WATU wa sehemu moja ya muungano ndivyo tunavyoweza kufanya maamuzi juu ya MUUNGANO ambao asili yake (kwa mujibu wa Articles of Union na Sheria Na. 22 ya 1964) ni mkataba wa kisheria baina ya NCHI MBILI HURU (NA ZILIZO SAWA MBELE YA SHERIA).
Hata kama kulikuwa na jitihada za makusudi za kupora UHURU wa nchi moja (Tanganyika) na kuipoteza kwenye ramani ya nchi za dunia kwa kisingizio cha MUUNGANO; bado sehemu ya wenye AKILI za upembuzi ulikuwa ukitafuta wakati wa kuliweka jambo hilo sawa na kulitafutia MUAFAKA (Zanzibar walipofanya Marekebisho ya Katiba 2010 waliamua kuandika wazi kwamba: Zanzibar ni NCHI inayounda MUUNGANO)...huu ndio mwanzo, na tamko (kauli) ya Mch, Gwajima inaonyesha wazi "agenda" iliyojificha nyuma ya tamko (kauli) lake/yake na hatuwezi kudhani kwamba amefanya hivyo akiwa na AKILI TIMAMU, au kama hajui kwamba MUUNGANO uliundwa kwa mujibu wa "makubaliano" yaliyoridhiwa na watu wawili (NYERERE na KARUME) kwa niaba ya NCHI MBILI (Tanganyika na Zanzibar).
Mwisho, kama Mch. Gwajima anadhani kwamba Watanganyika milioni 43 (sasa, kwa mujibu wa Matokeo ya Idadi ya Watu, 2012) wanaweza kuwameza Wazanzibari milioni 1+; hii ni dhana HASI (-) inayohitaji kukemewa kwa NGUVU (za UHURU, HAKI na USAWA) kwa kuwa Zanzibar ilikuwa NCHI na bado ni NCHI kama ilivyo TANGANYIKA. Kama dhana ya idadi ya watu ndio kigezo cha kufanya maamuzi ya kisiasa kuhusu MUUNGANO, basi Articles of Union (1964) na Sheria Na. 22 zingaliweka kipengele hicho kwenye nmuktadha wa sheria ili kwa sheria hiyo muafaka wa kisiasa baina ya watu wa Tanganyika na watu wa Zanzibar waamue justakabali wao kwa njia hiyo. Uchizi wa dhana hiyo unaweza kusomeka kwa mtu asiyehoji kisheria kwa MUUNGANO uliyofanywa kisheria; isipokuwa anataka (huyo mtu) kuhoji kwa utashi wa atakavyo yeye au kama anavyoona yeye pasipokuwa na hoja zenye mashiko ya kisheria na au rejea rasmi zilizokubaliwa na NCHI mbili (Tanganyika na Zanzbiar).
Muungano umefanyiwa marekebisho mengi; na wasomi wa SHERIA wameandika sana juu yake, kwa hiyo namuomba Mch. Gwajima (na wenye mawazo kama yake) warejee rejea za kisomi juu ya sherehe (upembuzi na usanifu) wa tasnia ya MUUNGANO kwa mtazamo wa UHURU, HAKI na USAWA. Tusitengeneze wafuasi juu ya kuchukia jambo (au mambo) usiyoyajua...na kwa anayejiita "mtu wa mungu" kama Mch. Gwajima lazima atambue kwamba MUUNGANO wa Tanganyika na Zanzibar haukuwa "muungano wa watu" ulikuwa muungano wa kisheria baina ya NCHI MBILI HURU; na si kinyume chake - HUU NDIO UKWELI...kinyume chake Mch. Gwajima anataka atuaminishe UONGO (kwa maslahi yake).
Bakari..
asalaam
Bandiko lako umelinyima uhuru wako, kumbuka ulichobandika ni mawazo tu ya wazee tokea 1964, Na matamshi ya watanzania waliotutangulia lakini wewe Binafsi hujatoa maoni yako zaidi ya Kushutumu semi Kwa ghani Za kihistoria..
Embu funguka kifikra jaribu kujiuliza mwenyewe mbali Na hizo Article Za Muungano ambazo kwangumie ni Historia Na Historia haiwezi kunambia Leo kuna Nini. Embu jiulize ni lini Tanganyika Na Zanzibar ziliketi kuunda KATIBA TOKEA muungano???? Zaidi ya katiba hii ya Chief Adam Na Kombo JE kuna katiba ya Kimuungano??????? Kama waunganaji hawa hawajawahi kuketi kuunda mustakabali wao Sababu yake ni Nini ????
Unajua Hata ndoa zina 'instruction Manual' sasa iweje Nchi mbili ziungane Na zisiketi kutengeneza mstakabali wa maisha Yao?
Hembu acha uoga jaribu tu kuwaza Kwa sauti Kama from 1964 waunganaji hawa hawajaketi kujenga Katiba Lao Ndo waje walijenge 2012, inaingia akilini mwako BAKARIIII???
Tuache kulaumu historia embu tuje Kwenye uhalisia hii Tume ya Katiba inakusanya maoni ya nchi ngapi?, Muungano Gani?, na what shall be its compilation..
Tutapokuja Kwenye common fact, ok let's Vote.. What shall be the nature of votes .. Nchi hazipigi votes Bali wananchi, sasa 43:1 vote line unadhani kitu hiyo ipo.. Embu tuache kufumbia macho majanga, Wazanzibar wana interest zao Na kama kura Za watanzania 43:1 zitawafunika wana visiwa hao hujui tayari tumeshawakwida matakwa Yao ?????!!??
Twendeni Mbele mziki huu hauwezekani JAMANI, tafadhali tujadilini kwanza ni Muungano gani Watanzania tunautaka, kisha ichorwe mistari halisia ya wazi Kwenye Muungano kisha ndipo tuingie zoezi la kujenga mustakabali wa Nchi. Kama maamuzi ni Serikali Tatu, mbili, Moja Basi tujadili Kwa Uwazi hili.
Tungekuwa Na Muungano Leo usingesikia upuuzi Wa pande mbili au tatu.. Ingeundwa tume ya Jamhuri ya Muungano bila Kutaja pande Za ushiriki, ukishasema tu wajumbe 14 from Zanzibar haya wangine 14 from where???? Ukisema Tanzania Bara umeshavunja Muungano wewe, neno lenyewe Tanzania manaake (tanganyika + Zanzibar)
Unaposema unaunda tume ya katiba 14 members from Zanzibar hawa ni solid members from ZANZIBAR, but ukisema 14 from Tanzania Bara, this means 14 members from (Tanganyika Na Zanzibar walioko bara) hii unaiona Bado iko sawa BAKARI..?!!???
Ok tuje Kwenye kiinimacho kingine Unamwitamwitaje 'HUYU MZANZIBAR' 'HUYU MTANZANIA BARA' UNAMWITAMWITAJE?????, unatumia IDENTITY GANI, rangi?, lunga, Makazi?, Kuzaliwa ? Unatumia Nini Kama si viinimacho !?! Watanzania ni Watanzania tu, hatunaga ma Identity au Tatoo mwilini Kama alama Za Uzanzibari au uzanzibara wetu, ni total Confussion..
Mambo serikali inayoyafanya ni Kuvunja Muungano Na Kuleta roho Za kibaguzi mie Sijui akili hizi nani kawasaidia..??!! Wamrudishie akili zake walomwazima
BAKARI Haya unakubaliana nayo kweli..
Mie Binafsi Hoja yangu tuondoe uzanzibar Na utanganyika Tuunde katiba ya Tanzania.. Futeni ubaguzi Nchi zilishaungana Leo kuanza kuzibagua tena as if Ndo zinaungana ITAWACOST..