Uchawi upo! Muendekeze Mungu ufe masikini

Ok jibu maswali yangu, hilo lilikuwa la mwisho we soma na uyajibu hayo maswali, nalusubiria
Nianze kukujibu swali kwa swali.

Unaweza kujua kwamba jibu fulani si sahihi, bila hata ya kujua jibu sahihi?

Kwa mfano, ikiwa wewe ni mwanamme wa miaka 30 leo, humjui mama yako mzazi, unamtafuta, na mtu akakuambia kuwa, mama yako mzazi ni binti mchanga wa miezi 6 leo, unaweza kujua kwamba huyu binti wa miezi 6 leo hawezi kuwa mama yako mzazi, kwa sababu huyu binti umemzidi karibu miaka 30, na mama yako mzazi ni lazima awe mkubwa kuliko wewe, hivyo, huyu binti wa miezi 6 leo hawezi kuwa mama yako mzazi, hata kama bado humjui mama yako mzazi, na unamtafuta?

Hapo unaweza kujua kuwa huyu binti mchanga wa miezi 6 si mama yako mzazi, hata kabla hujajua mama yako mzazi ni nani?
 
[emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]safi
Amemaanisha kua tajiri au masikini ni uchawi wako tu, sawa sawa na kumlisha Panya simenti iliyonakishiwa na Sukari au Chocolate alafu tumbo lake likawa ZEGE,
 
Nianze kukujibu swali kwa swali.

Unaweza kujua kwamba jibu fulani si sahihi, bila hata ya kujua jibu sahihi?

Kwa mfano, ikiwa wewe ni mwanamme wa miaka 30 leo, humjui mama yako mzazi, unamtafuta, na mtu akakuambia kuwa, mama yako mzazi ni binti mchanga wa miezi 6 leo, unaweza kujua kwamba huyu binti wa miezi 6 leo hawezi kuwa mama yako mzazi, kwa sababu huyu binti umemzidi karibu miaka 30, na mama yako mzazi ni lazima awe mkubwa kuliko wewe, hivyo, huyu binti wa miezi 6 leo hawezi kuwa mama yako mzazi, hata kama bado humjui mama yako mzazi, na unamtafuta?

Hapo unaweza kujua kuwa huyu binti mchanga wa miezi 6 si mama yako mzazi, hata kabla hujajua mama yako mzazi ni nani?
Binti wa miezi 6 hawezi kuwa mama wa mtu wa miaka 30 kiuhalisia na logically.
 
Sawa, kwa hiyo, hapo, kwa kufuata kanuni ya mantiki ya kuhusiana na timeline, kati ya mama mzazi na mtoto wake wa kumza nani anaanza kuzaliwa, umeweza kujua binti huyo wa miezi sita hawezi kuwa mama wa mtu mwenye miaka 30, hata kabla ya kujua mama wa huyo mtu mwenye miaka 30 ni nani.

Katika kutafuta jibu sahihi, kuna njia moja inaitwa "elimination method", unaangalia jibu fulani, unaliweka katika mtihani fulani wa kimantiki unaoweza kuthibitishika kama chujio la majibu sahihi na yasiyo sahihi, likishindwa kupita mtihani huo, unalitupa, unatafuta jibu sahihi.

Yani ukishajua tu kwamba, square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, mtu akikwambia tu kwamba square root ya 2 ni 10, wala huhitaji kujua square root ya 2 ni nini ili kujua kwamba 10 si square root ya 2, utaangalia tu, 10 ni kubwa kuliko 2, hivyo haiwezi kuwa square root ya 2, hata kabla ya kujua square root ya 2 ni ipi.

Kwa njia hii, unaweza kujua jibu fulani si sahihi, hata kabla hujajua jibu sahihi ni lipi.

Nikikwambia sheria zinazoongoza ulimwengu zinatoka wapi, nitakuwa nakudanganya, ningekuwa na jibu la swali hilo ningeshapata nishani ya Nobel ya Physics, sijui jibu la swali hilo.

Lakini, kwa kanuni zile zile za kuweza kujua jibu lisilo sahihi hata kabla sijajua jibu sahihi, naweza kusema jibu la Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote si jibu sahihi, na ninaweza kukuonesha jibu hili si sahihi kama ninavyoweza kukuonesha binti wa miezi 6 leo hawezi kuwa mama mzazi wa mwanamme mwenye miaka 30 leo, bila hata kumjua mama mzazi wa huyo mwanamme.

Tunachofanya hapa ni hiki.

Kiranga: Binti wa miezi 6 hawezi kuwa mama mzazi wa mwanamme wa miaka 30.
The Accuser: Kama huyo binti wa miezi 6 si mama wa mwanamme wa miaka 30, tuambie mama yake huyo mwanamme ni nani?
Kiranga: Swali hilo sina jibu lake, na wala sijawahi kusema namjua mama wa mwanamme huyu mwenye miaka 30 ni nani, tunaweza kumtafuta mpaka tukamjua, lakini ninachokuambia ni kwamba, binti wa miezi 6 leo hawezi kuwa mama mzazi wa mwanamme wa miaka 30, hii ni kinyume na mantiki za timeline zinazotaka mama mzazi wa mtu awe mkubwa kuliko huyo mtu, kwa hiyo, tunaweza kujua huyu binti wa miezi 6 si mama mzazi wa mwanamme wa miaka 30 hata bila ya kumjua mama mzazi wa huyo mwanamme wa miaka 30.

Kama unataka niuweke huu mfano kwenye muktadha wa maongezi yetu ya Mungu, naweza kuuweka, ikiwa itasaidia uelewe vizuri zaidi.

Umeelewa kwamba naweza kujua Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo na hivyo hakuumba sheria za ulimwengu huu, hata kabla sijajua sheria za ulimwengu huu zimetokeaje na kuwepo?
 
Ok, kwa kuwa huna uhakika na hizi sheria za ulimwengu zimetoka wapi, tuje kwenye mwili wa binadamu, tunafahamu mwili wa binadamu una ogani nyingi zinazotegemeana kuzifanya kuishi, tuje kwenye ogani ya ubongo ambao umegawanyika sehemu ya ubongo wa mbele, ubongo wa Kati na ubongo wa nyuma ambapo Kila Moja wapo Ina kazi zake zinazofanyika kama kumbukumbu, uwezo wa kufikiri, kuleta hisia kwa viungo mbalimbali za mwili namaanisha kupokea taarifa na kuzituma na viungo hivi huvitafsiri kama hisia. Unaona kabisa ubongo huu haiwezi kuwa ilifanyika hivihivi lazima kuna someone aliyedesign hii ubongo na hapa nimetaja part Moja kwa ufupi sijataka kuingia mbali zaidi mfano ubongo una Neva, ila Ina pia mirija ya damu inayopitisha nyutrienti kibao Ili kuipa ubongo nguvu ya kufanya kazi kwa ufanisi na pia ubongo huu wenye grey matter na white matter umelindwa vizuri na fuvu kiasi kwamba ukipigwa ngumi si rahisi hata kidogo uhisi mtikisiko wake ambao una matokeo mabaya zaidi kwenye saikolojia yako huko mbeleni, je huu ujuzi ulikujaga wenyewe from nowhere? Lazima awepo someone mwenye uwezo mkubwa wa akili kutengeneza system hii ya ulinzi na kufikiri wa binadamu.
 
Hatumpangi Mungu cha kufanya, tunasema habari za uwepo wake zinajipinga zenyewe kwa namna inayoonesha kuna mushkeli mkubwa sana, huenda hayupo kabisa.

Mfano, inakuwaje Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote apate hasira kwa sababu viumbe aliowaumba hawajafanya anavyotaka yeye?

Yeye kama Mungu mjuzi wa yote hakujua kwamba hilo litatokea?

Mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote anawezaje kupata hasira?

Hasira ni hisia za yule asiye na control, ambaye kapata matokeo asiyoyapenda, hakuyategemea, hakuyajua, sasa huyo Mungu anayejua kila kitu, anayeweza kila kitu, mwenye upendo wote, anaanzaje kupata hasira?

Tena anapata hasira na kuteketeza watu karibu dunia nzima.

Hapo huoni kwamba huyu Mungu katungwa na watu tu, tena kapea mpaka tabia za watu, anakasirika, anafurahi, ana wivu, ana upendeleo.

Huoni huyu Mungu katungwa na watu tu, na kapewa tabia za watu?
Damn!! Even the blind man, could see truth to this post.
 
Ok, kwa kuwa huna uhakika na hizi sheria za ulimwengu zimetoka wapi, tuje kwenye mwili wa binadamu, tunafahamu mwili wa binadamu una ogani nyingi zinazotegemeana kuzifanya kuishi, tuje kwenye ogani ya ubongo ambao umegawanyika sehemu ya ubongo wa mbele, ubongo wa Kati na ubongo wa nyuma ambapo Kila Moja wapo Ina kazi zake zinazofanyika kama kumbukumbu, uwezo wa kufikiri, kuleta hisia kwa viungo mbalimbali za mwili namaanisha kupokea taarifa na kuzituma na viungo hivi huvitafsiri kama hisia. Unaona kabisa ubongo huu haiwezi kuwa ilifanyika hivihivi lazima kuna someone aliyedesign hii ubongo na hapa nimetaja part Moja kwa ufupi sijataka kuingia mbali zaidi mfano ubongo una Neva, ila Ina pia mirija ya damu inayopitisha nyutrienti kibao Ili kuipa ubongo nguvu ya kufanya kazi kwa ufanisi na pia ubongo huu wenye grey matter na white matter umelindwa vizuri na fuvu kiasi kwamba ukipigwa ngumi si rahisi hata kidogo uhisi mtikisiko wake ambao una matokeo mabaya zaidi kwenye saikolojia yako huko mbeleni, je huu ujuzi ulikujaga wenyewe from nowhere? Lazima awepo someone mwenye uwezo mkubwa wa akili kutengeneza system hii ya ulinzi na kufikiri wa binadamu.
Kuna kitu kinaitwa "anthropic bias".

Anthropic bias ni tabia ya kuchukua mambo kwa upeo fulani, ambao kikawaida ni finyu na unatokana na uwezo mdogo wa watu (hence anthropic, neno anthro ni mzizi wenye kumaanisha watu, as in anthropolgy, the study of humans). So anthropic bias, ni tabia ya kukaa na ku deduce mambo tu, kutokana na upeo wetu wa kiutu.

Ukienda kwa tabia hii, ni rahisi sana kubishana na mtu kumwambia kwamba dunia ni bapa na wala si mviringo, kwa sababu, ukiangalia mambo kwa juujuu, unaona dunia ni bapa tu, inabidi ufikiri sana ili kuona dunia ni mviringo.

Kufikiri kuhusu jinsi maisha yalivyoibuka mabilioni ya miaka, au kanuni za msingi za fizikia zinavyofanya kazi, au je, kuna Mungu au hakuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, inabidi ujivue hii anthropic bias.

Nitakupa mfano mmoja wa bwana mmoja aliuwa mvuvi. Yule bwana alikuwa na nyavu yake ya kuvulia, ile nyavu kila tobo lina ukubwa wa sentimeta 2 za mraba. Sasa kaenda nayo kuvua, lakini pia alikuwa anataka kujua samaki mdogo kabisa anayeweza kumkamata. Basi akavua mchana kutwa, usiku kucha, akirudia hivyo mpaka siku tatu.

Alipomaiza kuvua, akaenda kuwapima wale samaki, akitaka kujua samaki gani ni mdogo kabisa katika bahari ile.

Akaja kugundua kwamba, katika samaki wake wote aliovua, hakuna samaki aliye na mdogo kuliko sentimeta mbili za mraba.

Akajiwekea kwamba kagundua kuwa, katika bahari ile inaonekana kuwa hakuna samaki mdogo zaidi ya sentimeta mbili za mraba, kwa kuwa hajakamata samaki mdogo hivyo na kakaa kweli baharini.

Lakini, mvuvi huyu kuna kitu kimoja kidogo tu hakukifikiria. Hakufikiria kwamba, nyavu yake aliyoitumia kuvua ilikuwa na matobo ya sentimeta 2 za mraba, na hivyo, samaki yeyote mdogo kuliko sentimeta mbili za mraba, aliweza kupenya kutoka kwenye ile nyavu, na hivyo samaki huyo mdogo hakushikwa na nyavu ile.

Hapo utaona jinsi kipimo chako kinavyoweza kukufanya upate majibu yasiyo sahihi.

Wewe una "anthropic bias", una nyavu unayoitumia kuvua 9mawazo yako, utu wako, elimu yako ambayo haijui vizuri mambo mengi kama particle physics, quantum mechanics, evolution etc), nyavu hii ina ukubwa fulani, na ukubw ahuo unaathiri hata kufikiri kwako.

Kwa kutumia nyavu hii, utaweza kuvua samaki wa aina fulani tu, wadogo zaidi ya nyavu yako watakuponyoka tu, halafu ukitaka kujua samaki mdogo zaidi kwa kuangalia samaki uliovua kwa nyavu hiyo, utaweza kupata jibu lisilo sahihi kirahisi tu.

Hoja yako kwamba vitu vinaonekana kama vimeumbwa, order must come out of deliberate design, na kuhitimisha Mungu yupo, ina matatizo mengi.

Nitayaorodhesha hapa.

1. Kwanza kabisa, nakupa immanent critique. Immanent critique maana yake ni kwamba, hata nikikubaliana nawe unavyoanza, conclusion yako bado si sawa. Hata nikikubaliana nawe kwamba inaonekana vitu vina design, si lazima design hii itoke kwa Mungu muumba yote, mwenye ujuzi wote na upendo wote. This is a logoical non sequitur. Yani ni hivi, hata kama tukikubaliana kwamba wewe ni lazima uwe na mama aliyekuzaa, ukweli kwamba wewe una mama aliyekuzaa haumaanishi kwamba mama yako ni Samia Suluhu Hassan, rais wa Tanzania. Ukisema Samia Suluhu Hassan ni mama yako mzazi, inabidi utuhakikishie hilo. Hutakiwi kusema "Mimi Mama yangu mzazi ni Samia Suluhu Hassan, rais wa Tanzania" halafu watu wakikuuliza "Kwa nini unasema hivyo?", ujibu "Aaah, si lazima niwe na mama, lazima niwe na mama, unafikiri nimejizaa mwenyewe, lazima niwe na mama, na kama lazima niwe na mama, basi mama yangu ni Samia Suluhu Hassan, rais wa Tanzania".

Kwa hivyo, hoja ya kwanza, hata kama ni lazima vitu vyenye order viwe vimeumbwa kwa makusudi, hilo halimaanishi vimeumbwa na Mungu. Unatakiwa kuthibitisha kwamba vimeumbwa na Mungu.

2. Lakini pia, kwenye asili kuna uthibitisho kwamba si lazima vitu vyenye complexity/ order vitokee kwa kuumbwa kwa makusudi. Hii ni dhana ya kidini ambayo ilikuja kutaka kuelezea vitu ambavyo hatuvielewi tu. Kuna mifano mingi ya vitu vinavyotoka kuwa simple na kuwa complex, evolution inatupa mifano mingi ya natural selection by survival of the fittest. Hapa tunaongelea mabilioni ya miaka, hivyo kunaweza kutokea mabadiliko makubwa sana kuliko yanayoweza kueleweka kwa uzoefu wetu wa kawaida wa kuishi miaka michache.

3. Uiweka hoja kwamba, vilivyo complex/ vyenye order kubwa, ni lazima viwe vimeumbwa kwa design maalum, na mwenye order/ complexity kubwa zaidi, haviwezi kutokea vyenyewe vikiwa na order/ complexity kubwa au kuanzia na complexity/ order ndogo vika evolve mpaka kuja kuwa na order/ complexity kubwa, kimsingi unajenga hoja ya kukataa uwepo wa Mungu bila kujijua.

Unaweza kuona unatetea uwepo wa Mungu, kwa sababu unamuweka Mungu kama mwenye order/ complexity kubwa zaidi, akawa muumba, lakini kama tunashikilia kanuni yako ya kwamba order/ complexity haiwezi kutokea tu, ni lazima iwe designed kwa nia maalum, basi utajikuta unapata tabu kujibu swali dogo tu.

Kama kweli order/ complexity haiwezi kutokea tu, ni lazima iumbwe na order complexity kubwa zaidi, huyo Mungu katokeaje? Utajikuta inakubidi umuelezee Mungu kama kaumbwa na Mungu wake na yeye, na Mungu wake kaumbwa na Mungu wake, ad infinitum, ad nauseam. Kifupi, umemfanya Mungu kuwa ki sehemu kidogo tu cha mashine kubwa isiyo na mwisho, na kwa msingi huu, Mungu huyu aliyeumbwa, anapoteza uungu wake.

Kwa hivyo, hoja yako, ya kusema kitu chenye order/ complexity kubwa hakiwezi kutokea chenyewe, ni lazima kimeumbwa, ukiiangalia kwa juu juu, unaweza kuona inatetea uwepo wa Mungu, lakini, ukichambua kwa kina, utakuja kugundua kumbe hoja hii, ukiishikilia barabara, inatuonesha Mungu hawezi kuwapo.

Kuna mengi ya kuchambua kwa kina zaidi, lakini nisiandike gazeti, nikuachie na wewe upate nafasi ya kusoma vizuri hoja zangu, kuzichambua, na kunijibu.
 
Mungu aliweka Kanuni katika kila jambo.
Pili Mungu alimuumba mwanadamu akiwa na mawazo chaguzi, huku akimuonya kuwa akienda against na yeye Kuna matokeo hasi.
Kwanini alifanya hivyo?
Kwa kuwa yeye ndo aliumba na ndo mwenye maamuzi.
Tatu hatujui mpaka sasa Siri za Mungu huyu so hakuna haja ya kutengeneza hoja wakati yeye hajataja kufungua sababu ya mambo yote haya.
Unaposema "Mungu aliweka kanuni katika kila jambo" unaweza hata kuthibitisha kwamba huyo Mungu yupo kwanza?

Unaweza hata kutatua Epicurean Paradox kuhusu dhana ya uwepo wa huyo Mungu?

Ukishajiona unajibu swali la "kwa nini" kwa jibu la "kwa kuwa yeye ndiye muumba" kimsingi umesema hujui jibu, humjui Mungu wako. Na mimi nakwambia huwezi kumjua, kwa sababu hayupo.

Ona hii flow hapa chini, halafu tatua contradiction katika dhana ya kuwapo Mungu huyu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.

epicurean_paradox.jpg
 
Hivi Mungu mwenye huruma, mpole mkaribu mwenye kusamehe.

Ndio huyu huyu anaewapa watu maradhi makubwa ya kutisha na ulemavu wa kudumu binadamu wake?

Amekuwa katiri kiasi kwamba haoni shida watu kufa kwa njaaa maradhi na mateso makubwa hapa duniani?

Mungu huyu huyu ndio husababisha ajali kubwa kuuwa watu na kuwaacha wakiteseka?

Mungu huyu huyu ndio anawapa pesa mashoga washirikina na wachawi alafu wachamungu wanaishi kama paka?

Mungu huyu huyu ndio hutoa umasikini wa kudumu kwa watu?

Mungu aliefanya yote hayo ndio anakupenda na wewe?
Wengine hawapendi?

Uchawi upo utumie vizuri baadae rudi kwa Mungu

Jifunze kuishi kwa technique.

Kosoeni masikini wanaomtegemea Mungu kuwa matajiri wakati wapo masikini wa kudumu wenye kudumu na ibada ila wanaishi mpaka aibu.
Hakunap nguvu iliyo juu ya nguvu ya Mungu
 
Kajifunze kuandika kwanza ndo uje kumkosoa Mungu.

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Unaposema "Mungu aliweka kanuni katika kila jambo" unaweza hata kuthibitisha kwamba huyo Mungu yupo kwanza?

Unaweza hata kutatua Epicurean Paradox kuhusu dhana ya uwepo wa huyo Mungu?

Ukishajiona unajibu swali la "kwa nini" kwa jibu la "kwa kuwa yeye ndiye muumba" kimsingi umesema hujui jibu, humjui Mungu wako. Na mimi nakwambia huwezi kumjua, kwa sababu hayupo.

Ona hii flow hapa chini, halafu tatua contradiction katika dhana ya kuwapo Mungu huyu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.

View attachment 2600955

Sawa hakuna Mungu,Lakini unakubali kuna kitu kina nguvu ya asili inayokuzidi wewe?unaamini kuna Nguvu ya uumbaji ambayo ndio wewe ulipotokea?
 
Hatumpangii Mungu cha kufanya, tunasema habari za uwepo wake zinajipinga zenyewe kwa namna inayoonesha kuna mushkeli mkubwa sana, huenda hayupo kabisa.

Mfano, inakuwaje Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote apate hasira kwa sababu viumbe aliowaumba hawajafanya anavyotaka yeye?

Yeye kama Mungu mjuzi wa yote hakujua kwamba hilo litatokea?

Mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote anawezaje kupata hasira?

Hasira ni hisia za yule asiye na control, ambaye kapata matokeo asiyoyapenda, hakuyategemea, hakuyajua, sasa huyo Mungu anayejua kila kitu, anayeweza kila kitu, mwenye upendo wote, anaanzaje kupata hasira?

Tena anapata hasira na kuteketeza watu karibu dunia nzima.

Hapo huoni kwamba huyu Mungu katungwa na watu tu, tena kapewa mpaka tabia za watu, anakasirika, anafurahi, ana wivu, ana upendeleo.

Huoni huyu Mungu katungwa na watu tu, na kapewa tabia za watu?

I definitely agree with you,huyu Mungu ni fiction imetengenezwa na watu wachache wajanja na wamefanikiwa
Naamini kuna nguvu iliotuumba ambayo haihitaji kuabudiwa wala kusujudiwa,jinsi ilivyo ni kamilifu haihitaji chochote kutoka kwetu
Kazi yetu kuu sisi ni kuishi maisha basi
 
So if there is no God
Where did natural and physical laws that governs the universe came from?
Because within those laws, there are mathematics phenomenon inside it, and it has been proven over and over again, it's just like jamiiforums, created by someone who coded this website with a mathematical algorithms supporting this website formation, so then where did the laws come from?
Don't say it's nature, for we will ask you, who is nature?

Mimi naamini kuna Mungu(ambae ndio huyo mnajichanganya mara alete magonjwa kwa watu innocent au mabalaa mara ni Mungu mwenye upendo etc yani complexity ya vitu vingi),kuna shetani ambae nae ana mambo yake you can say negative energies na kuna Nguvu ya asili iliotuumba hii haihitaji chochote kutoka kwetu yenyewe ni kamilifu,imetuumba ili tuishi

However naheshimu kila imani ya mtu na siwezi kumshangaa yeyote kati yetu
 
Hivi Mungu mwenye huruma, mpole mkaribu mwenye kusamehe.

Ndio huyu huyu anaewapa watu maradhi makubwa ya kutisha na ulemavu wa kudumu binadamu wake?

Amekuwa katiri kiasi kwamba haoni shida watu kufa kwa njaaa maradhi na mateso makubwa hapa duniani?

Mungu huyu huyu ndio husababisha ajali kubwa kuuwa watu na kuwaacha wakiteseka?

Mungu huyu huyu ndio anawapa pesa mashoga washirikina na wachawi alafu wachamungu wanaishi kama paka?

Mungu huyu huyu ndio hutoa umasikini wa kudumu kwa watu?

Mungu aliefanya yote hayo ndio anakupenda na wewe?
Wengine hawapendi?

Uchawi upo utumie vizuri baadae rudi kwa Mungu

Jifunze kuishi kwa technique.

Kosoeni masikini wanaomtegemea Mungu kuwa matajiri wakati wapo masikini wa kudumu wenye kudumu na ibada ila wanaishi mpaka aibu.
Unajitoa akili he subili siku akiichukua roho yako kisha ukafukiwa na kifusi cha tani 10 ndipo utakapo amini kuwa mchawi hana uwezo
 
Hahahaha hehehhehhe hohoho
Yehova[emoji23]
Una uhakika gani kama utamkuta Mungu huko mbinguni, kuna mtu amewai kurudi akakuambia??
Toa fact acha utoto
Kwa sasa unaweza kusema hutakavio lakini siku roho ikikutoka ukafukiwa na kifusi cha tani 10 siku hiyo utaamini kuwa hiyo elimu yako inayo kufanya kuwa mshenzi aina maana
 
Back
Top Bottom