Nelson Jacob Kagame
JF-Expert Member
- Dec 26, 2022
- 9,591
- 13,645
Baada ya kupotea mda mrefu nimerudi tena ndugu zangu.
Mniwie radhi kwa simulizi nilizoshindwa kuzimalizia.... sababu zilikua nje ya uwezo wangu.
Leo ningependa niwaulize watu ambao mnajiita kua mna ubini wa Adamu. Mnamjua Mungu aliyeumba au mnakariri hadithi na mapokeo. Mungu yupo ila asilimia 97 ya binadamu hamna uelewa kuhusu yeye. Mungu yupo na kuna sehemu anakaa na ana utaratibu wake. Kuna makundi machache ya watu wanaomjua Mungu:
1 : Wachawi wa Hiyari
2 : Watu wa Dini ya Damu (Walokole)
3 : Viumbe vya Rohoni
Tuanze na Wachawi wa Hiyari
1 : Wachawi wa Hiyari
Kwanza tujiulize uchawi ni nini??? Mtaniwia radhi, Wachawi, uchawi ni taaluma isiyokua ya kibinadamu...ambayo binadamu anajifunza kupitia viumbe vya rohoni. Uchawi una kanuni zake ambazo zinakinzana na kanuni mkuu wa utashi. Naposema Mkuu wa Utashi, namaanisha Mkuu wa Universe asiye na mpinzani. Wachawi ni binadamu na wanajifunza hiyo taaluma.
Kwanini wanaitwa Wachawi wa Hiyari? Ni kwa sababu wanajua wanachokifanya. Mnaweza mkauliza nimejuaje ila msijali, tutafika tu. Ukiwa mchawi unakua na uwezo wa kuona vitu ambavyo binadamu wa kawaida hawezi. Utaona viumbe vya rohoni, utashirikiana na viumbe vya rohoni, utaona ukuu wa Mkuu wa Utashi ambaye ana viumbe wake na kanuni zake tofauti kabisa na uchawi. Ila uchawi umefungwa na viapo vya kiroho na siri, hivyo huwezi kutoa siri.
Sasa kwanini nimesema wachawi wanamjua Mungu Mkuu wa Utashi anayekinzana na wachawi? Katika harakati zao za kila siku kuna upinzani wanakutana nao...wa nguvu inayowapinga na inayowatetea wanayoitumainia...hasa wale watu wa dini ya damu mnawaita Walokole. Wachawi wanajiuliza hii nguvu inatoka wapi na kwanini inawalinda hawa watu wa dini ya damu??? Wanaamua kufuatilia na wanagundua kua hii nguvu ipo pote na inawakilishwa na viumbe vyenye mfano wa wanadamu kimuonekano, ila kuna utofauti wa urefu na vipimo. Ila asilimia 97 wanafanana na binadamu. Hata huyo Mkuu wa Utashi, namaanisha Mkuu wa Anga Zote, wanafanana na binadamu, inavyoonyesha binadamu wamekopi kwake asili yao.
Baada ya kufuatilia, wachawi wanagundua kua huyo ndio kiumbe wa kiroho anayeitwa Mungu Mkuu au Bwana wa Miale ya Mioto. Haongeagi sana sababu macho yake tu yanamulika anga lote, na ana umbo la kibinadamu kimuonekano, ambaye hakuna kiumbe wa kiroho anayweza kumsogelea au kumchunguza mpaka atake yeye. Viumbe vya rohoni vilivyo kinyume nae vinamuogopa. Wanagundua katika masomo yao kua binadamu wana miungu mingi, ila huyo Mungu Mkuu yupo tofauti kabisa. Na ni mwiko kwao kushirikiana nae, sababu hakubaliani na mambo yao. Ila wanajua kabisa huyo ndio Mungu Mkuu anayezungumziwa na binadamu. Ila kwa kua uchawi ni siri na viapo vya kiroho, basi wanaamua kukaa kimya, kama moja ya masharti yao waliopewa na wakufunzi wao ambao ni viumbe vya kiroho pia.
Ukiwauliza wachawi watakuambia huyu Mkuu wa Utashi ndiye Mungu Mkuu ambaye binadamu wanamtaaja, ambao wachawi wameshinda kuiba hazina zake kuu za malighafi, mjengeo wa ulimwengu wa juu na chini. Waulize wachawi watakuambia ukweli huu.
2 : Watu wa Dini ya Damu (Walokole)
Katika maisha yangu sijawahi kuona watu wabishi kama hawa watu wa dini ya damu, mnawaita Walokole. Kwanza, wao wana nguvu ambayo inawalinda, afu hawajui. Unakuta binadamu mtu wa dini ya damu anaomba kwa kusema naafunga anga kwa minyororo na damu ya mwana wa kondoo. Yeye anachukulia masikhara, hajui, ila anga lote linafungwa. Kabla sijaanendelea, niwaambie kidogo kuhusu mwana kondoo wa damu.
Jina mwana kondoo wa damu katika ulimwengu wa kiroho limetokana na chanzo cha kiumbe wa kiroho anayeitwa Mwana wa Mmilikii, ambaye ametokana na yule Mungu niliyemzungumzia mwanzo...Mungu wa Utashi, mmiliki wa hazina za mbingu ya juu na chini, ambaye watu wa dini ya damu wanamuita Baba yao. Kumbuka, huyu Mungu anaabudiwa tu na watu wa dini ya damu.
Sasa huyu Mwana Kondoo ni sehemu ya Utashi wake, na inasemekana kwa mujibu wa simulizi za kiroho, huyu Mwana Kondoo alimwaga damu yake, ambayo watu wa dini ya damu wanaitumia kufanya mambo yao kiroho na kimwili. Wao jambo lolote bila kutaja jina la Mwana Kondoo na damu yake, mambo hayaendi. Huyo Mwana Kondoo ana wasaidizi wake ambao ndio wanahusika kuwahudumia watu wa dini ya damu, nyinyi mnawaita Walokole. Hao wasaidizi wake kwenye ulimwengu wa kiroho wanaitwa Wana wa Mungu wa Utashi.
Na Mwana wa Kondoo kwenye ulimwengu wa kiroho au Mwana wa Mmilikii... sasa hawa watu wa dini ya damu Walokole wanamjua huyu Mungu wa kweli, na katika ulimwengu wa kiroho hakuna mtu au kiumbe wa kiroho anayekuwa kukinazana nao. Mungu wao ni wa ngazi nyingine kabisa, na ndio maana anaitwa Mungu wa kweli au Mtashi Mkuu asiye na mawaa ya kiutendaji pande zote za anga kuu.
Ukibisha...toka nje ya mwili, afu uingie kwenye kumi na nane zake au uingie kwenye kumi na nane za wafuasi wake wa kibinadamu, utaniambia. Kwanini tunamuita Mungu wa kweli? Ni kwamba mpaka sasa hakuna mpinzani katika ulimwengu wa kiroho anayekuwa kukinazana nae, sababu yeye ndiye anaemiliki siri kuu ya uhai. Sasa watu wa dini ya damu Walokole ndio waga, wanamuomba huyu, na huyu ndiye anaemiliki siri kuu ya uhai na Mkuu wa Utashi.
Ukitaka kujua Mungu wa ukweli, ingia kiroho, afu watafute watu wa dini ya damu Walokole. Wakifunga anga, wamefungwa, wakisema moto...ni moto kweli, wakilia na kuomba. Anga lote linajaa Wana wa Mungu. Kali zaidi, wana ushirika wa kiroho na kimwili, na yule kiongozi wa Wana wa Mungu aitwae Mwana wa Mmilikii.
3 : Viumbe vya Rohoni
Hapa kwenye viumbe vya rohoni kuna makundi machache hayazidi matano:
1 : Mwana wa Mmilikii
2 : Wasaidizi wa Mwana wa Mmilikii
3 : Viumbe vya kwenye maji / Wakufunzi wa Wachawi
1 : Huyu Mwana wa Mmilikii ni kiumbe wa kiroho anajishughulisha mno na wanadamu, maana wamechukua mfano wake. Ulimwengu wote wa kiroho unajua nguvu aliyonayo. Huyu anajua kuhusu Mungu wa kweli ambaye ni babake. Ukifanikiwa kukutana nae, atakupa majibu kuhusu Mungu wa kweli.
2 : Wasaidizi wa Mwana wa Mmilikii hawa kwenye ulimwengu wa kiroho wanajulikana kama watumishi wa Mungu wa kweli, ambaye Wachawi wameshinda kuiba hazina zake kuu za malighafi, mjengeo wa ulimwengu wa kiroho. Mungu wao ndio Mungu Mkuu wa Utashi ambaye ana ushirika na watu wa dini ya damu Walokole. Ukipata nafasi ya kuzungumza nao watakueleza ukweli.
3 : Viumbe vya kwenye maji wanajulikana kiroho kama Wakufunzi wa Wachawi. Hawa pia wanamjua Mungu Mkuu wa Utashi, namaanisha Mkuu wa Universe asiye na mawaa. Hawa viumbe wana upinzani wa asili na Mungu wa Utashi. Inaonekana hapo zama za kale waligombana nae kwa sababu za kimaslahi na ujeuri, ila walikua washirika pamoja. Hawa viumbe pua wanajiita miungu kupitia dini tofauti tofauti ulimwengu wa kibinadamu. Ukipata nafasi ya kuzungumza nao watakueleza ukweli kuhusu Mungu mwenye nguvu kuliko wote.
Sasa binadamu yoyote ambaye anataka kujua ukweli kuhusu Mungu afanye uchunguzi kupitia risala hii. Maarifa ya kiroho yanatafutwa, ila sio kupitia hadithi za kukaririshwa.
NB: Ulimwengu wa kiroho ni siri. Tafuta maarifa, ujue siri.
Tutaendelea.