Uchawi upo! Muendekeze Mungu ufe masikini

Mm mungu namuomba ila uchawi usiohusisha kuabudu miungu.kutoa kafara au kumumiza mwingine sifanyi.
Ila niashindwe hata kutambika kwa babu zangu?? Nishindwe toa kafara ya wanyama kwenye kuita mazao?? Mtoto kachizika niache kwenda kwenye kuagua ? Na kunywa dawa za miti na kuoga chumvi tu .mfano kusafisha mikosi unaweka glas za maji safi ya Bomba au kisima kila kona ya nyumba Kisha unaomba yanakaa usiku 2 Kisha unaenda yamwaga mbal hapo nimememkosea nn muumba
 
Kuna jamaa alimwendekeza Mungu kwa kila kitu, mtoto wake alifaulu la saba enzi hizo miaka ya 80. Kwa kuwa hakuamini uchawi, mtoto wake sasa anaokota majalalani. Walioamini uchawi watoto wao wanapeta.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Mm mungu namuomba ila uchawi usiohusisha kuabudu miungu.kutoa kafara au kumumiza mwingine sifanyi.
Ila niashindwe hata kutambika kwa babu zangu?? Nishindwe toa kafara ya wanyama kwenye kuita mazao?? Mtoto kachizika niache kwenda kwenye kuagua ? Na kunywa dawa za miti na kuoga chumvi tu .mfano kusafisha mikosi unaweka glas za maji safi ya Bomba au kisima kila kona ya nyumba Kisha unaomba yanakaa usiku 2 Kisha unaenda yamwaga mbal hapo nimememkosea nn muumba
Nicheki PM tafadhali
 
Mtoa mada hueanda una depression na maisha sio bure, Mungu ana terms zake ili akubariki,hauna budi u comply kumbukumbu LA torati 28:1 maana neno linasena nchi na vyote vijazavyo ni Mali yake,alafu neno hilo hilo linasema siku sita Fanya kazi utende mambo yako yote alafu siku ya saba upumzike,tatizo vijana mnafanya kazi siku moja alafu mnataka mpuzike siku sita.Jambo kingine LA kuzingatia Dar inawenyewe ambao wali wahi ,nenda mikoani na nchi jirani,kutafuta mpunga ,mafanikio yatakufuata.
 
Hivi Mungu mwenye huruma, mpole mkaribu mwenye kusamehe.

Ndio huyu huyu anaewapa watu maradhi makubwa ya kutisha na ulemavu wa kudumu binadamu wake?

Amekuwa katiri kiasi kwamba haoni shida watu kufa kwa njaaa maradhi na mateso makubwa hapa duniani?

Mungu huyu huyu ndio husababisha ajali kubwa kuuwa watu na kuwaacha wakiteseka?

Mungu huyu huyu ndio anawapa pesa mashoga washirikina na wachawi alafu wachamungu wanaishi kama paka?

Mungu huyu huyu ndio hutoa umasikini wa kudumu kwa watu?

Mungu aliefanya yote hayo ndio anakupenda na wewe?
Wengine hawapendi?

Uchawi upo utumie vizuri baadae rudi kwa Mungu

Jifunze kuishi kwa technique.

Kosoeni masikini wanaomtegemea Mungu kuwa matajiri wakati wapo masikini wa kudumu wenye kudumu na ibada ila wanaishi mpaka aibu.
Mungu atakuokoa na utamtunikia
Siku Moja
Mungu aliwabadilisha wengi
Nawe Kuna siku utamuabudu
 
Usifanye attack kwa mtoa mada, JIBU HOJA.

Na wale watoto wachanga na Mifugo wanaokufa kwenye Majanga, NAO WAMEPEWA MITIHANI?

#YNWA
Kwa imani yangu mimi Muislam kifo,vita,khofu,maradhi,njaa mitetemeko ya ardhi na Majngaa mengine yote hayo ni mitihani ya Mwenyeezi Mungu aliyotupa sisi viumbe wake tunachotakiwa tusubiri kwa hiyo mitihani na turejee kwake muumba tulete toba juu makosa yetu tunayo mkosea Mungu atatusamehe na kutondolea hayo Mabalaa yote.

Qur'an Sura Al-Baqara 2: 155. Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri,

156. Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea

157. Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Nao ndio wenye kuongoka

Tafsiri yake . 155. Subira ni ngao na silaha ya Muumini ambayo kwayo hushindia kila shida na mashaka. Na nyinyi zitakuja kupateni shida nyingi. Tutakujaribuni na kukufanyieni mitihani kwa vitisho vya maadui, kwa njaa, na uchache wa vifaa, na kupungukiwa mali, na watu kufa, na kupotea mazao. Na hapana la kukulindeni katika mtihani huu mkali ila Subira. Basi Ewe Nabii! Wape bishara nzuri wanao subiri kwa moyo na ulimi

156. Wale ambao kwamba yanapo wateremkia machungu ya kuwaumiza wanaamini ya kuwa hakika kheri yote na shari inatokana na mwenyewe Mwenyezi Mungu, na ya kwamba amri yote ni ya Mwenyezi Mungu. Hao husema: Sisi ni milki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na sisi ni wenye kurejea kwake Yeye. Sisi hatuna letu jambo lolote. Na Yeye ni mwenye kustahiki kushukuriwa kwa anacho toa, na juu yetu kusubiri wakati wa kujaribiwa, na kwake Yeye ndiyo zipo thawabu na malipo.

157. Basi hao wenye kusubiri, wenye kumuamini Mwenyezi Mungu, wanapewa bishara njema kuwa watapata msamaha na ihsani ya Mwenyezi Mungu, na wao ndio wenye kuongoka njia ya kheri na uwongozi mwema.
 
[emoji706][emoji1787]
 
Basi Waafrika wangekuwa matajiri sana.Watu wanaloga sana lakini mafanikio hola
 
Back
Top Bottom