Uchawi upo! Muendekeze Mungu ufe masikini

Uchawi upo! Muendekeze Mungu ufe masikini

Kwanza kabisa, Big Bang ni model.

Pili, kwa mujibu wa Einstein's Relativity, time is relative, there is no absolute time, time depends on the observers frame of reference. Sasa, ukiuliza kabla ya Big Bang, unauliza kabla ya Big Bang kutoka frame of reference gani?

From the Big Bang model, time and space started at the Big Bang, so in this framework, there is no time or space to call "before" the Big Bang. You need to reconcile Einstein's Relativity with Quantym Physics to find out how exactly did the Big Bang happen.

Asking what existed before the Big Bang is like asking what is north of the north pole.
Je kuna uwezekano wowote wa kufanya upatanisho wa Einstein's relativity na Quantum Physics?

Au hazipatani na hazi ingiliani?
 
Je kuna uwezekano wowote wa kufanya upatanisho wa Einstein's relativity na Quantum Physics?

Au hazipatani na hazi ingiliani?
Ugumu wa kujibu swali lako ni kwamba hatujui tusichokijua.

Inawezekana Relativity inaweza kupatanishwa na Quantum Physics, tukapata Quantum Gravity, ila hatujajua mahesabu ya kufanya upatanishi huo tu.

Ikiwa hivyo, tunaweza kufanya mahesabu kwa njia creative zaidi, tukatumia AI na Quantum Computers kutusaidia, tukaweza kupata upatanisho huo.

Inawezekana pia, hatuwezi kupatanisha Relativity na Quantum Physics, kwa sababu upatanisho huo hauwezekaniki, labda kuna fundamental barrier, some logical contradiction in the fabric of the universe inayosababisha hilo lisiwezekane.

Lakini kazi yetu ni kujaribu kuthibitisha, hata kama hili haliwezekani kabisa, inabidi tuthibitishe kwamba hili haliwezekani kabisa.
 
Ugumu wa kujibu swali lako ni kwamba hatujui tusichokijua.

Inawezekana Relativity inaweza kupatanishwa na Quantum Physics, tukapata Quantum Gravity, ila hatujajua mahesabu ya kufanya upatanishi huo tu.

Ikiwa hivyo, tunaweza kufanya mahesabu kwa njia creative zaidi, tukatumia AI na Quantum Computers kutusaidia, tukaweza kupata upatanisho huo.

Inawezekana pia, hatuwezi kupatanisha Relativity na Quantum Physics, kwa sababu upatanisho huo hauwezekaniki, labda kuna fundamental barrier, some logical contradiction in the fabric of the universe inayosababisha hilo lisiwezekane.

Lakini kazi yetu ni kujaribu kuthibitisha, hata kama hili haliwezekani kabisa, inabidi tuthibitishe kwamba hili haliwezekani kabisa.
Ahaa sawa nimekuelewa hapa.

Pia je, Kama time ni relative:

Aliye introduce theory ya "Bing Bang"
Ali itoa kwenye frame na reference ipi?
 
Hivi Mungu mwenye huruma, mpole mkaribu mwenye kusamehe.

Ndio huyu huyu anaewapa watu maradhi makubwa ya kutisha na ulemavu wa kudumu binadamu wake?

Amekuwa katiri kiasi kwamba haoni shida watu kufa kwa njaaa maradhi na mateso makubwa hapa duniani?

Mungu huyu huyu ndio husababisha ajali kubwa kuuwa watu na kuwaacha wakiteseka?

Mungu huyu huyu ndio anawapa pesa mashoga washirikina na wachawi alafu wachamungu wanaishi kama paka?

Mungu huyu huyu ndio hutoa umasikini wa kudumu kwa watu?

Mungu aliefanya yote hayo ndio anakupenda na wewe?
Wengine hawapendi?

Uchawi upo utumie vizuri baadae rudi kwa Mungu

Jifunze kuishi kwa technique.

Kosoeni masikini wanaomtegemea Mungu kuwa matajiri wakati wapo masikini wa kudumu wenye kudumu na ibada ila wanaishi mpaka aibu.
stupid!!
 
Ugumu wa kujibu swali lako ni kwamba hatujui tusichokijua.

Inawezekana Relativity inaweza kupatanishwa na Quantum Physics, tukapata Quantum Gravity, ila hatujajua mahesabu ya kufanya upatanishi huo tu.

Ikiwa hivyo, tunaweza kufanya mahesabu kwa njia creative zaidi, tukatumia AI na Quantum Computers kutusaidia, tukaweza kupata upatanisho huo.

Inawezekana pia, hatuwezi kupatanisha Relativity na Quantum Physics, kwa sababu upatanisho huo hauwezekaniki, labda kuna fundamental barrier, some logical contradiction in the fabric of the universe inayosababisha hilo lisiwezekane.

Lakini kazi yetu ni kujaribu kuthibitisha, hata kama hili haliwezekani kabisa, inabidi tuthibitishe kwamba hili haliwezekani kabisa.
Unatapa tapa
 
Unatapa tapa
Umeshindwa hata kunikosoa kwa data, kwa hoja.

Kuonesha natapatapa wapi, kwa sababu gani, na ili nisitapetape niwe vipi.

Umetoa ad hominem attack, unamshambulia mtoa hoja, huwezi kupinga hoja kwa hoja.

Wewe ndiye unatapatapa.

Huna hata lugha ya kubishana nami.
 
Umeshindwa hata kunikosoa kwa data, kwa hoja.

Kuonesha natapatapa wapi, kwa sababu gani, na ili nisitapetape niwe vipi.

Umetoa ad hominem attack, unamshambulia mtoa hoja, huwezi kupinga hoja kwa hoja.

Wewe ndiye unatapatapa.

Huna hata lugha ya kubishana nami.
Mfa maji haishi kutapa tapa
 
Uwezo wetu wa akili si dhahabu ing'arayo juu ya mlima, la.. Ni uchafu wenye madhara yasiyo na tiba.

Nmekuwa nkikutilia umakini mkubwa sana tangu kale na hunifanya nisizungumze chochote nkiamini unatosha kabisa kutoa ukweli ulio thabiti kwa mpangilio unaofaa.

Ila nmeamini Imani haina tiba
Kuna kitu kinaitwa "anthropic bias".

Anthropic bias ni tabia ya kuchukua mambo kwa upeo fulani, ambao kikawaida ni finyu na unatokana na uwezo mdogo wa watu (hence anthropic, neno anthro ni mzizi wenye kumaanisha watu, as in anthropolgy, the study of humans). So anthropic bias, ni tabia ya kukaa na ku deduce mambo tu, kutokana na upeo wetu wa kiutu.

Ukienda kwa tabia hii, ni rahisi sana kubishana na mtu kumwambia kwamba dunia ni bapa na wala si mviringo, kwa sababu, ukiangalia mambo kwa juujuu, unaona dunia ni bapa tu, inabidi ufikiri sana ili kuona dunia ni mviringo.

Kufikiri kuhusu jinsi maisha yalivyoibuka mabilioni ya miaka, au kanuni za msingi za fizikia zinavyofanya kazi, au je, kuna Mungu au hakuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, inabidi ujivue hii anthropic bias.

Nitakupa mfano mmoja wa bwana mmoja aliuwa mvuvi. Yule bwana aliuwa na nyavu yake ya kuvulia, ile nyavu kila tobo lina ukubwa wa sentimeta 2 ya mraba. Sasa kaenda nayo kuvua, lakini pia alikuwa anataka kujua samaki mdogo kabisa anayeweza kumkamata. Basi akavua mchana kutwa, usiku kucha, akirudia hivyo mpaka siku tatu.

Alipomaiza kuvua, akaenda kuwapima wale samaki, akitaka kujua samaki gani ni mdogo kabisa katika bahari ile.

Akaja kugundua kwamba, katika samaki wake wote aliovua, hakuna samaki aliye na mdogo kuliko sentimeta mbili za mraba.

Akajiwekea kwamba kagundua kuwa, katika bahari ile inaonekana kuwa hakuna samaki mdogo zaidi ya sentimeta mbili za mraba, kwa kuwa hajakamata samaki mdogo hivyo na kakaa kweli baharini.

Lakini, mvuvi huyu kuna kitu kimoja kidogo tu hakukifikiria. Hakufikiria kwamba, nyavu yake aliyoitumia kuvua ilikuwa na matobo ya sentimeta 2 za mraba, na hivyo, samaki yeyote mdogo kuliko sentimeta mbili za mraba, aliweza kupenya kutoka kwenye ile nyavu, na hivyo samaki huyo mdogo hakushikwa na nyavu ile.

Hapo utaona jinsi kipimo chako kinavyoweza kukufanya upate majibu yasiyo sahihi.

Wewe una "anthropic bias", una nyavu unayoitumia kuvua 9mawazo yako, utu wako, elimu yako ambayo haijui vizuri mambo mengi kama particle physics, quantum mechanics, evolution etc), nyavu hii ina ukubwa fulani, na ukubw ahuo unaathiri hata kufikiri kwako.

Kwa kutumia nyavu hii, utaweza kuvua samaki wa aina fulani tu, wadogo zaidi ya nyavu yako watakuponyoka tu, halafu ukitaka kujua samaki mdogo zaidi kwa kuangalia samaki uliovua kwa nyavu hiyo, utaweza kupata jibu lisilo sahihi kirahisi tu.

Hoja yako kwamba vitu vinaonekana kama vimeumbwa, order must come out of deliberate design, na kuhitimisha Mungu yupo, ina matatizo mengi.

Nitayaorodhesha hapa.

1. Kwanza kabisa, nakupa immanent critique. Immanent critique maana yake ni kwamba, hata nikikubaliana nawe unavyoanza, conclusion yako bado si sawa. Hata nikikubaliana nawe kwamba inaonekana vitu vina design, si lazima design hii itoke kwa Mungu muumba yote, mwenye ujuzi wote na upendo wote. This is a logoical non sequitur. Yani ni hivi, hata kama tukikubaliana kwamba wewe ni lazima uwe na mama aliyekuzaa, ukweli kwamba wewe una mama aliyekuzaa haumaanishi kwamba mama yako ni Samia Suluhu Hassan, rais wa Tanzania. Ukisema Samia Suluhu Hassan ni mama yako mzazi, inabidi utuhakikishie hilo. Hutakiwi kusema "Mimi Mama yangu mzazi ni Samia Suluhu Hassan, rais wa Tanzania" halafu watu wakikuuliza "Kwa nini unasema hivyo?", ujibu "Aaah, si lazima niwe na mama, lazima niwe na mama, unafikiri nimejizaa mwenyewe, lazima niwe na mama, na kama lazima niwe na mama, basi mama yangu ni Samia Suluhu Hassan, rais wa Tanzania".

Kwa hivyo, hoja ya kwanza, hata kama ni lazima vitu vyenye order viwe vimeumbwa kwa makusudi, hilo halimaanishi vimeumbwa na Mungu. Unatakiwa kuthibitisha kwamba vimeumbwa na Mungu.

2. Lakini pia, kwenye asili kuna uthibitisho kwamba si lazima vitu vyenye complexity/ order vitokee kwa kuumbwa kwa makusudi. Hii ni dhana ya kidini ambayo ilikuja kutaka kuelezea vitu ambavyo hatuvielewi tu. Kuna mifano mingi ya vitu vinavyotoka kuwa simple na kuwa complex, evolution inatupa mifano mingi ya natural selection by survival of the fittest. Hapa tunaongelea mabilioni ya miaka, hivyo kunaweza kutokea mabadiliko makubwa sana kuliko yanayoweza kueleweka kwa uzoefu wetu wa kawaida wa kuishi miaka michache.

3. Uiweka hoja kwamba, vilivyo complex/ vyenye order kubwa, ni lazima viwe vimeumbwa kwa design maalum, na mwenye order/ complexity kubwa zaidi, haviwezi kutokea vyenyewe vikiwa na order/ complexity kubwa au kuanzia na complexity/ order ndogo vika evolve mpaka kuja kuwa na order/ complexity kubwa, kimsingi unajenga hoja ya kukataa uwepo wa Mungu bila kujijua.

Unaweza kuona unatetea uwepo wa Mungu, kwa sababu unamuweka Mungu kama mwenye order/ complexity kubwa zaidi, akawa muumba, lakini kama tunashikilia kanuni yako ya kwamba order/ complexity haiwezi kutokea tu, ni lazima iwe designed kwa nia maalum, basi utajikuta unapata tabu kujibu swali dogo tu.

Kama kweli order/ complexity haiwezi kutokea tu, ni lazima iumbwe na order complexity kubwa zaidi, huyo Mungu katokeaje? Utajikuta inakubidi umuelezee Mungu kama kaumbwa na Mungu wake na yeye, na Mungu wake kaumbwa na Mungu wake, ad infinitum, ad nauseam. Kifupi, umemfanya Mungu kuwa ki sehemu kidogo tu cha mashine kubwa isiyo na mwisho, na kwa msingi huu, Mungu huyu aliyeumbwa, anapoteza uungu wake.

Kwa hivyo, hoja yako, ya kusema kitu chenye order/ complexity kubwa hakiwezi kutokea chenyewe, ni lazima kimeumbwa, ukiiangalia kwa juu juu, unaweza kuona inatetea uwepo wa Mungu, lakini, ukichambua kwa kina, utakuja kugundua kumbe hoja hii, ukiishikilia barabara, inatuonesha Mungu hawezi kuwapo.

Kuna mengi ya kuchambua kwa kina zaidi, lakini nisiandike gazeti, nikuachie na wewe upate nafasi ya kusoma vizuri hoja zangu, kuzichambua, na kunijibu.
 
Uwezo wetu wa akili si dhahabu ing'arayo juu ya mlima, la.. Ni uchafu wenye madhara yasiyo na tiba.

Nmekuwa nkikutilia umakini mkubwa sana tangu kale na hunifanya nisizungumze chochote nkiamini unatosha kabisa kutoa ukweli ulio thabiti kwa mpangilio unaofaa.

Ila nmeamini Imani haina tiba
Asante sana mkuu.

Wiki hii wewe ni mtu wa pili unaniambia unanifuatilia kwa ukaribu hivyo. Ninafarijika kusikia hivyo.

Maana mara nyingne napingana na watu hapa mpaka nashangaa inakuwaje hawaoni mambo ya wazi kabisa.
 
Kuna atheist anaitwa David Wood amekuwa atheist kwa muda mrefu na kuwapinga theist ila baadaye akaona hizi beliefs ni za kijinga akampa maisha yake Yesu Kristo, sasa hivi yeye ana convert atheists na Muslims wale washika dini na wasomi wakubwa wa Holy Qur'an kama Nabeel Qureshi (Mungu ampumzishe kwa amani) na amefanikiwa sana.
David Wood aliona baadaye ni ujinga kuamini kuwa Mungu hayupo.
Kwa hiyo upeo wako umeishia kwenye fikra za Wood? Fikirisha akili yako zaidi. Nimeamua kutafakari zaidi kuhusu imani hizi kama zina nguvu mbele ya mantiki
 
Shida hujui purposes ya wewe kuweko duniani, laiti ukija kujua huta kuwa na akili na maono uliyonayo sasa. Cha maana saiz nikupe Pole tu.
Ulitakiwa umfafanilie afahamu hicho unachoshani hajui. Sasa wewe badala ya kumwongezea maarifa umeshia kumtisha tu
 
Hatumpangii Mungu cha kufanya, tunasema habari za uwepo wake zinajipinga zenyewe kwa namna inayoonesha kuna mushkeli mkubwa sana, huenda hayupo kabisa.

Mfano, inakuwaje Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote apate hasira kwa sababu viumbe aliowaumba hawajafanya anavyotaka yeye?

Yeye kama Mungu mjuzi wa yote hakujua kwamba hilo litatokea?

Mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote anawezaje kupata hasira?

Hasira ni hisia za yule asiye na control, ambaye kapata matokeo asiyoyapenda, hakuyategemea, hakuyajua, sasa huyo Mungu anayejua kila kitu, anayeweza kila kitu, mwenye upendo wote, anaanzaje kupata hasira?

Tena anapata hasira na kuteketeza watu karibu dunia nzima.

Hapo huoni kwamba huyu Mungu katungwa na watu tu, tena kapewa mpaka tabia za watu, anakasirika, anafurahi, ana wivu, ana upendeleo.

Huoni huyu Mungu katungwa na watu tu, na kapewa tabia za watu?
Mkuu unaelezea kwa namna rahisi sana kieleweka. Mifano yako ni kama kunywa maji urahisi wake.
 
Frame of reference ya kuwa ndani ya ulimwengu uliokuja baada ya Big Bang kutokea.
Mkuu bado najiuliza hapa, Kama ulivyo kwisha sema kabla kwamba:

"Hatuwezi kujua tusicho kijua"

Inatokeaje Mtu Anajua Asicho kijua.

Mfano aliye introduce "Bing Bang theory" na kusema ilitokea alijuaje na alifahamu vipi?

Au kabla ya Einstein's relativity, Albert Einstein alitafakari tu kimawazo na kugundua theory yake hii?

Au kuna frame na reference alitumia?
 
Shetani ndiye mtawala wa ulimwengu huu na ndiye chanzo cha mambo yote mabaya.

Ni maskini duniani ila kwa Yehova sisi ni matajiri.
Hazina zetu tunaweka mbinguni huko mchwa, nondo hawawezi kiziharibu. Hata wezi hawawezi kutuibia...
Hoja hujibiwa kwa hoja! Shetani ndie mtawala wa dunia wakati huo huo biblia inasema tawala zote zilizopo duniani zimewekwa na Mungu. Kwahiyo Mungu ndie aliemuweka Shetani atawale??
Walokole wengi wao ni masikini kwa sababu ya kutumika na wachungaji wao kama mitaji.
Pia ni watu wenye majibu mepesi sana kwenye hoja nyepesi na ngumu.
 
Mkuu bado najiuliza hapa, Kama ulivyo kwisha sema kabla kwamba:

"Hatuwezi kujua tusicho kijua"

Inatokeaje Mtu Anajua Asicho kijua.

Mfano aliye introduce "Bing Bang theory" na kusema ilitokea alijuaje na alifahamu vipi?

Au kabla ya Einstein's relativity, Albert Einstein alitafakari tu kimawazo na kugundua theory yake hii?

Au kuna frame na reference alitumia?
Hatuwezi kujua tusicho kijua, lakini, tunaweza kupunguza tusichokijua kwa kujielimisha.

Haya mambo si kwamba mtu alikaa mara moja tu akagundua, ni maelfu na maelfu ya miaka ya watu kusoma, kuvumbua, kuchambua, kuandika na kurithishana vizazi na vizazi.

Einstein alikuwa mdadisi tangu mtoto. Alipewa compass, dira, na baba yake, akawa anajiuliza kwa nini ile needle ya compass inaelekea upande mmoja tu kokote anapoenda? Alijenga udadisi huo mpaka ukubwani, akafanya thought experiments, akasoma mambo ya sayansi ya wengine, akatupa kitu alichoongeza yeye, Relativity, special na general.

Umeuliza kama Einstein alifanya thought experiments tu, au alifanya nini? Alianza kwa thought experiment, akiangalia frame of reference tofauti, mtu aliye kwenye treni na aliyesimama kituoni, jinsi muda unavyokuwa tofauti, watu walio katika elevator (lift) wanavyoweza ku simulate gravity. Ni udadisi tu. Lakini, hizo thought experiments zake ziliangaliwa kimahesabu zikakutwa sawa, zimethibitishwa, aliweza mpaka kufanya utabiri. Mfano, katika solar eclipse ya mwaka 1919, hesabu za Newton zilitabiri kwamba nyota fulani za zilizotakiwa kuwa zinaonekana pembeni ya jua zitakuwa pahali fulani, hesabu za Einstein zikatabiri kwamba, kutokana na gravity ya jua, nyota hizo zitaonekana pembeni kidogo ya zilipotabiriwa na Newton, Arthur Eddington akafanya experiment na kuona hesabu za Einstein ziko sahihi, mwaka 1919.

Kuanzia hapo, Einstein amethibitishwa mara nyingi sana katika muktadha wa Relativity. Hata GPS system inatumia kanuni za Einstein za Relativity, ukitumia Newtonian math kuendesha GPS utatengeneza ajali dunia nzima. Ukiangalaia TV inayotumia matangazo ya satellite, unatumia Relativity. Mambo mengi sana yanayotaka high accuracy in time yanatumia hesabu za Relativity.

Hiyo Big Bang Theory watu hawakugundua mara moja. Ukisoma historia za kina George Lemaitre na Edwin Hubble utaona kwamba hizi habari za ugunduzi zina safari ndefu sana ya uchunguzi, na mpaka leo watu wanachunguza na kuhakiki bado. Mimi hizi habari nazifuatilia tangu form one angalau, na ugunduzi mwingine kama wa Cosmic Microwave Background au Higgs Boson unafanyika mimi nilikuwa nausubiri kwa miaka mingi.

Ttatizo jamii yetu watu wengi hawafuatilii mambo haya kwa karibu, hivyo yanaonekana kama uchawi tu.
 
Back
Top Bottom