Asante. Key word ni mantiki. Kwa kweli ukifuata mantiki kubishana nami kwenye hizi mada za Mungu/dini/uchawi/supernatural powers ni vigumu.
Maana, hizi si hoja zangu tu, ni hoja za siku nyingi zenye mantiki yenye kina kirefu na historia kubwa.
Tatizo linakuja watu wengi, mara nyingi, hawajui au wanakataa mantiki, wakifikiri kwamba, kwa kukataa mantiki wanaweza kupinga hoja zangu kirahisi zaidi.
Huku wakishindwa kuelewa kwamba hoja zangu zina msingi thabiti sana, kiasi kwamba, wakikubali mantiki zinashinda, kwa sababu zimejengwa katika mantiki, lakini pia, wakikataa mantiki, wanajiondolea hata wao wenyewe hoja za kunipinga, kwa sababu, ili kupinga hoja kikamilifu, inabidi utumie mantiki.
Tatizo ni kwamba, watu wengi hawawezi au hawataki kufikiri kwa kina, wanaridhika na kufikiri kijuujuu, wanakariri tu na kwenda na hadithi za mapokeo, wanajiridhisha kwa wanasaikolojia wanachokiita "cognitive dissonance", wanaishia kwenye imani tu, ambayo haina haja ya kupasi mitihani ya uthibitisho, wengine wananinyanyapaa kwa ad hominem attacks ( kumshambulia mtu yeye binafsi, badala ya kujibu hoja zake) kwa sababu nasema wasichopenda tu.
Wengine wanabishana kwa "identity politics" tu.Mtu anatetea dini yake, imani yake, kwa sababu ni yake tu.Ni kama ule ushabiki wa mpira ambao mtu anaitetea timu yake, hata kama timu mbovu anaitetea tu, kwa sababu ni yake.
Ila, nikipata hata mtu mmoja anayeweza kusema kama wewe, kwamba, zamani nilikuwa sikuelewi, lakini sasa nakuelewa, napata faraja sana, kwamba, the situation is not that hopeless, kuna watu angalau wachache wanafunguka macho kwa majadiliano tunayofanya hapa JF.
Shukurani nyingi sana kwa kufuatilia kwa makini mazungumzo haya ambayo si mepesi na mara nyingine yanaweza kukera watu.