Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,027
- 142,928
Tuma your real I'd na majina ya wazazi wako ya utotoni wote wawili, tuanze kazi ! Unamjua mchuzi wa nyoka ?!
Enzi hizo bwana kila kitu mzee ilikuwa ni Coastal Union tu kila siku lazima niende mazoezini kwao huko mzee wakali kama kina Mwameja,Carreca,Yasin Napili,Mgaza,Muhani,joseph razaro na kingslay marwilo walikuwa wanatisha ukja huku African Sports ndio unawakuta kina Juma Mgunda dah Tanga bwana ilikuwa inavutia sana enzi hizo.
Nitume wapi na kwa nani?
Na kwa nini hadi "real I'd"?
Kwani huyo mchawi hawezi kutumia hizo nguvu zake za kichawi kujua mimi ni nani?
Jina lako ndo password ya makombora kutumwa yaje moja kwa moja kwako, sasa unaogopa nini na umeamua kupima watu !? Tuma your real name tuwaambie wazee waanze advertising !
We kweli ni mshamba, kwani hujui wazungu waligunduaje BLUE TOOTH?
Ni kutokana na huo uchawi wa KOPEA na ndio wakagundua hiyo kitu inaitwa Blue tooth.
Niliwahi kusimuliwa kwamba kuna mzungu anaitwa Dawson Fitzgerald alikwenda huko Pangani Tanga kufanya utafiti wa Mbu waambukizao Malaria na siku moja wakati anakula kwenye mghahawa akachezewa huo mchezo wa Kopea, ikabidi aachane na utafiti wa Mbu na Malaria akahamishia utafiti wake kwenye huo uchawi wa KOPEA na ndipo akarudi kwao na hatimaye akaja na huo ugunduzi wa BLUE TOOTH.
African Sports waliwahi kuroga wakapitiliza ! Walifanya kufuru kwa kusoma "yasin" usiku kucha ! Masheikh walichukia sana kwani dua hiyo husomwa kama kuna vita au tishio la maangamizi ya kiasili, wao wakafanya kwa ajili ya mpira ! Ndo maana mpaka leo jamaa hawapandi daraja !
Halafu kulikuwa na gwiji wa NDUMBA mkoani TANGA almaarufu kwa jina la MANDONDO, nasikia alikuwa ni kiboko hasa, Je unazifahamu khabari zake Bwana Ally Kombo?
Hapa kwenye maangamizi ya asili umenikumbusha tukio la zamani sana nadhani mwishoni mwa miaka ya 70 liliwahi kutokea Tanga,kuna moto mkubwa uliwahi kuanzia nadhani barabara ya 10 na kufika mpaka Mabawa na ilipelekea kuja msaada wa gari za zima moto toka Mombasa....wakati watu wakiwa wametaharuki kila mtu akiwa hajui la kufanya Mungu amrehemu sheikh Mohamed Ally Mkanga alikuwa akisoma Quran na mzee wangu alikuwa busy akimwagia maji nyumba kwa kutumia pipe huku akisikitika kwa nini Sheikh hajishuhulishi na kumwagia nyumba yake maji ili kupunguza makali ya moto ukifika,kwa mshangao wa wengi nyumba ya marehemu Mohamed Ally Mkanga ilinusurika na janga lile la moto.
............It is a true stori, ndo maana Masheikh walichukia sana ! kuna Dua zingine Katika Uislaam hazisomwi ovyo, sasa jamaa kwa ajili ya ushabiki wa mpira wakasoma "yasin" elf mbili (2,000) !! (wako wataalaam wanajua mpaka dua aliyoomba Musa wakati anapusua Bahari, na wengine wanajua dua ya Yesu wakati anaomba aepushwe na kifo cha fedheha cha msalabani .... !!) Masheikh wanasema ingeweza kutokea balaa kubwa Tanga ! kwa hiyo walilaumu sana kitendo hicho, ndo maana African Sports mpaka jezi hawana sasa hivi !
hhahaha! Ali mapilau wa magomeni sio??
yaani kuna vitimbi dunian acha tu. sasa imagine mtu unapika halua badala ya pilau. ila ukweli msosi wa huyu bw n mtamu uspime ila huwez kula mwingi yaani kidogo tu unakinai.
hapo sasa!ndo anaponiacha hoi ali mapilau!
kuna siku niliwahi kumpeleka kwenye msiba home atupikie siku ya kuzika alifariki shangazi yangu!
sasa sijui tulikose mahesabu vipi bana au ndo alwatan wa marehemu si msosi nikauona mdogo,mwali akaniambia we tulia ukisikia ali mapilau ndo mimi!
mwali chakula kilitosha na kikabaki!
nikabakije mdomo wazi!
hawa watu sio wenyewe kabisa!
sasa hiyo ya kupika halua naona alikutana na wajanja wenzie!
sipati picha kile kitambi kilivocheza cheza!
hahahha!!umenikumbusha wakati nalipisha watu mishahara dirishani enzi hizo,kuna kitu pia inaitwa chuma ulete,fedha zinaisha halafu bado kuna watu kama 70 hivi hawajaisha,lol!pia wafanyabiashara ni wahanga wakubwa hii kitu!unapata presha eti,afadhali sasa zinapitia benki!hiyo zongo me nakaa na waarusha,wanazongo baya halafu wengine hawajijui,hiyo ndo mbaya zaidi,moja kati ya njia za wife kulinda kachanga chake ni kumpaka wanja,aisee mtoto ni wakiume lakini anakandikwa wanja mpk natamani kulia,hahahaaaaa but it works!!
Nilikuwa nasimamia Canteen pale halmashauri ya wilaya Korogwe,kazi ilikuwa inakwenda vizuri lakini ghafla ilitokea hali ya kigeni,chakula na na vinjwaji vilikuwa vinakwisha lakini nikija katika hesabu nakuta hatuna akiba na hata pesa ya kununua mahitaji haitoshelezi......kwa kuwa nilikuwa naweka akiba Benki,nilianza kuchukua pesa Benki kuziba mapengo,amini usiamini akiba niliimaliza ikawa sasa nimegonga ukuta, at the time nilikuwa bado mdogo ndio kwanza nimemaliza O level na pale nilikuwa nimewekwa na marehemu kaka yangu...kichwa kikawa kinaniuma nitaanza vp kumfahamisha kaka kwa kuwa pesa Benki nimemaliza na pale kazi inafanyika kama kawaida na sitoweza kulipa mishahara wala kwenda kuchukua stock ya kundeshea kazi.....Ikabidi nijisingizie ugonjwa.
Kiasi cha siku tatu nakumbuka marehemu kaka akaja nyumbani kuniuliza 'wewe pale unafanya vipi kazi?' nikamuuliza kwa nini? Akaniambia mbona mimi nikifunga kazi chakula hakibaki lakini nikitaka mahitaji mpaka niongeze pesa zangu nje ya kazi ile...ndio nikaona sasa hata nikimueleza ile hali atanielewa.
Nikamwambia A-Z mpaka sababu ya mimi kupumzika ni kwa kuwa nilikuwa naogopa nitaanza vipi kusema nafanya kazi lakini pesa hazionekani,nani ataniamini? Ndio wakahangaika jahazi likakaa sawa.
Sijaribu kuhalalisha au kulazimisha kuamini lakini huu ni UCHAWI NILIO WAHI KUUSHUHUDIA.