Uchawi niliowahi kuushuhudia!

Uchawi niliowahi kuushuhudia!

Nilikuwa nasimamia Canteen pale halmashauri ya wilaya Korogwe,kazi ilikuwa inakwenda vizuri lakini ghafla ilitokea hali ya kigeni,chakula na na vinjwaji vilikuwa vinakwisha lakini nikija katika hesabu nakuta hatuna akiba na hata pesa ya kununua mahitaji haitoshelezi......kwa kuwa nilikuwa naweka akiba Benki,nilianza kuchukua pesa Benki kuziba mapengo,amini usiamini akiba niliimaliza ikawa sasa nimegonga ukuta, at the time nilikuwa bado mdogo ndio kwanza nimemaliza O level na pale nilikuwa nimewekwa na marehemu kaka yangu...kichwa kikawa kinaniuma nitaanza vp kumfahamisha kaka kwa kuwa pesa Benki nimemaliza na pale kazi inafanyika kama kawaida na sitoweza kulipa mishahara wala kwenda kuchukua stock ya kundeshea kazi.....Ikabidi nijisingizie ugonjwa.
Kiasi cha siku tatu nakumbuka marehemu kaka akaja nyumbani kuniuliza 'wewe pale unafanya vipi kazi?' nikamuuliza kwa nini? Akaniambia mbona mimi nikifunga kazi chakula hakibaki lakini nikitaka mahitaji mpaka niongeze pesa zangu nje ya kazi ile...ndio nikaona sasa hata nikimueleza ile hali atanielewa.

Nikamwambia A-Z mpaka sababu ya mimi kupumzika ni kwa kuwa nilikuwa naogopa nitaanza vipi kusema nafanya kazi lakini pesa hazionekani,nani ataniamini? Ndio wakahangaika jahazi likakaa sawa.

Sijaribu kuhalalisha au kulazimisha kuamini lakini huu ni UCHAWI NILIO WAHI KUUSHUHUDIA.

Hiyo ni chuma ulete na dawa yake ni ndogo tu, kama ukimjua mtu ambaye ni chuma ulete, na mara nyingi ni rahisi kumjua, kwani huja jioni kununua kitu cha bei rahisi halafu anakupa hela kubwa ili arudishiwe chenji, sasa ukishamshitukia ile hela yake usiichanganye na hela nyingine za biashara, na kwa kuwa lengo lake ni kutaka wewe uichanganye noti yake na fedha zako za biashara ili ziweze kuhamia kwenye mfuko wake, hataondoka akijaribu kukuangalia kwamba utafanya nini. wengine wanaweza kudiriki hata kukuliza kwamba kwanini unaitenge noti yake, wewe mpe kubwa na wala usimuogope mwambie kabisa wewe ni chuma ulete nimesha kushitukia, na hatakaa arudi tena na atakuogopa.

Lakini pia ipo njia nyingine, unaipokea ile hela kisha unaikunja mkononi kama vile umekunja ngumi halafu unapiga ngumi kwa upande wa nyuma wa mkono kwenye ardhi, hata uichanganye hiyo noti na fedha zako za biashara hapati kitu na akikuona anaweza kukulalamikia maana atajua umeshamjua.

Msishangae nilifundishwa mbinu hiyo na mjomba wangu.

Wakati mwingine nitawafundisha namna ya kumtega mchawi anase kwenye paa la nyumba au mlangoni.
 
aise zinduna inaonyesha we angalau una kauelewa na haya makitu,da hebu nisaidie basi my dear yani kuna mtu amenidhulumu mwaka huu ningetamani hata kesho nimu............sitanii kweli .. mahakamani naona nitapoteza muda nataka ki2 inayofanya kazi fasta ........nielekeze basi yule kiboko yao anapatikana wapi....km vp ni pm
 
Huyo kama kakudhulumu basi usipate taabu we nenda kwa mjomba angu hapo Kimbiji Dar es salaam anaitwa ustaadhi Sele, anaweza kuifanya hiyo kazi kama vile anakunywa kahawa.

Ni mtu maarufu sana hapo Kimbiji kwa shughuli hizo.
 
Ukishafanikiwa uje utoe ushuhuda hapa ili wale wanaume wakware waache kunifuatilia maana nikimwambia tu huyo mjomba wangu watafanyiwa kitu mbaya hata kama wako ughaibuni. yaani usisahau kuwasimulia hasa huyu Nyani Ngabu
 
Last edited by a moderator:
Ukishafanikiwa uje utoe ushuhuda hapa ili wale wanaume wakware waache kunifuatilia maana nikimwambia tu huyo mjomba wangu watafanyiwa kitu mbaya hata kama wako ughaibuni. yaani usisahau kuwasimulia hasa huyu Nyani Ngabu

Hivi hadi nifanye nini mpaka mniroge? Rukhsa nshawapa sasa mnasubiri nini tena? Nirogeni jamani.
 
Uchawi upo!! but evil eye (macho mabaya) siamin, hii ni hypothetic tu!! pili hearsay witness haukubaliki banah we vipi?
 
vipi na wale wazee wanaocheza bao kuanzia asubuhi mpaka jioni lakini huwaoni wakienda kujisaidia, ila sasa mtazamaji anayeangalia bao utaona kila baada ya muda anaenda haja kubwa au ndogo lakini wale wazee hawanyanyuki wanaendelea kucheza tu kumbe wanakupasia mizigo yao! Mimi ishanipata miaka ya nyuma pande za mwananyamala nilikuwa nazuga kwenye bao wakati namlia mingo dem flani, wewee si mchezo kila wakati wazee wananisakizia kupeleka mizigo yao, bahati kulikuwa na bar jirani nikawa najisevia kwenye toilet yao nilipokuja kushtukia mchezo washantesa sanaa! nikawa sikai tena nikawaacha wasakiziane mizigo yao wenyewe kwa wenyewe!

Yaani nimecheka mpaka machozi yanantoka, ama kweli dunian kuna mambo.
 
uchawi upo!! but evil eyes (macho mabaya) siamin, hiyo ni hypothetic tu!! pili hear say witness haukubaliki banah!!
 
hapo sasa!ndo anaponiacha hoi ali mapilau!
kuna siku niliwahi kumpeleka kwenye msiba home atupikie siku ya kuzika alifariki shangazi yangu!
sasa sijui tulikose mahesabu vipi bana au ndo alwatan wa marehemu si msosi nikauona mdogo,mwali akaniambia we tulia ukisikia ali mapilau ndo mimi!
mwali chakula kilitosha na kikabaki!
nikabakije mdomo wazi!
hawa watu sio wenyewe kabisa!
sasa hiyo ya kupika halua naona alikutana na wajanja wenzie!
sipati picha kile kitambi kilivocheza cheza!

Usipate shida, hata Yesu aligawa mkate mmoja na nusu samaki kwa mtaa makutano wote ! Ndo hiyo duwa inatumika kufanya chakula kitoshe !
 
Mmmmhhhh bibie.@v Umefikirianini leo mpaka ukaweka hii Thread?Kuhusu Uchawi kama kuna mtu anajuwa uchawi wakuwa mimi niwe Tajiri anifundishe mimi jamani.Sitaki uchawi wa kudhuru mimi ninataka Uchawi nijifunze wa kuweza kunipa Utajiri tu niwe Billionea mkubwa Kama Bill Gates. Kuhusu mambo ya Uchawi Tumuulize mtu mmoja yupo humu ndani anaitwa kwa jina MGANGA WA KIENYEJI yeye ndie atatujibu vizuri kama uchawi upo au hakuna?

Uchawi upo, Majini yapo na Mashetani yapo. Ila ni mada pana saana. Unaweza kua utakavyo kwa kujua kuutumia uchawi vizuri, bila hata kumkufuru Mwenyezi Mungu. Lakini kujua uchwawi ni sawa na kumiliki BOMU ndani ya nyumba. Hatari saana, kwa wewe Mwenyewe, familia yako na jamii kwa ujumla usipokua makini.
 
Posted Jumatano,Januari9 2013 saa 13:20 PM (MWANANCHI)
Kwa ufupi
“Mawe yanapigwa na yanadondoka chini mchana, sijui nifanyeje au ni huu umeme wa jua nilioweka kuna watu wananionea wivu,”

FAMILIA moja katika Kitongoji cha Matakani, Kata ya Bushiri, wilayani Pangani, imelazimika kuhama nyumba yao na kujihifadhi kwa majirani.

Hatua hiyo imetokana na nyumba hiyo kupigwa mawe juu ya bati usiku na mchana huku wanaopiga mawe hayo wakiwa hawaonekani.

Mmiliki wa nyumba hiyo, Boka Jack alisema tukio hilo ambalo analihusisha na nguvu za ushirikina, lilianza saa 6.01 usiku wa mkesha wa Mwaka Mpya.

Jack alisema ilianza kama mzaha usiku huo na walifikiri mawe hayo ni kwa ajili ya watu wanaosherehekea mwaka mpya kwa sababu kitongoji hicho hakina umeme na yeye anatumia umeme wa jua.

Alisema aliamua kutoa kioo juu ya paa usiku huo, lakini mawe hayo yaliendelea kupigwa hadi asubuhi.

“Mawe yanapigwa na yanadondoka chini mchana, sijui nifanyeje au ni huu umeme wa jua nilioweka kuna watu wananionea wivu,” alisema Boka.
Wakati mwandishi wa habari hizi akiwa kwenye mahojiano na Jack, mawe yalikuwa yakiendelea kupigwa juu ya bati huku milio ikisikika.

Kwa mujibu wa Boka, tangu siku hiyo wanalazimika kulala kwa majirani na kufunga duka lake, kwani kila anapojaribu kuingia ndani mawe yana zidi kupigwa hasa anapoingia dukani kuhudumia wateja.

Alisema tukio hilo analihusisha na imani za ushirikina na kuomba kama kuna mtu yeyote bila kujali imani, anaweza kumsaidia ampe msaada ili kuondokana na hali hiyo.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Athuman Mbilinyi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba, haijawahi kutokea kijijini hapo.

Mbilinyi alisema licha ya jitihada za kuunda kikosi cha doria kuzunguka nyumba hiyo kuwatafuta wanaopiga mawe, mmoja alijaribu kupanda juu ya paa lakini alikoswa kupigwa jiwe la kichwa.
Alisema suala lililowashangaza hata mchana nyumba hiyo inapigwa mawe, hivyo kulazimika kuamini kwamba tukio hilo linahusiana na imani za ushirikina, ambazo zinalenga kuua maendeleo.
 
Duh hii ilinipita maana nimesoma nikajikuta nikisheka peke yangu....
 
Zinduna nilipooanza kazi tanga nilijionea mengi chumba geni. yaani huko ukipiga kifuu tu cha sema. kuhusu zongo usiseme ila nilichokuja kujua kuna wengine hawajui kabisa kwamba wana macho mabaya.

yaani sijui niwaite misfortune ama nn watu wa aina hii yaani hata kama ni msosi unapika kama akiangalia tu hakiivi.
Vipi Mwembe Basha ulishajikinga na kivuli chake?
 
Usinikumbushe Ali Mapilau, yeye yalimkuta alifanyiwa vitimbwi na mwenzake akapika halua badala ya pilau, chezea ZONGO weye
Yaani Magufuli ana kazi nzito,kama watu akli zenu ziko hivi,basi tegemeeni ufukara tuuuuuuuuuuuuuuuuu.
 
Back
Top Bottom