Uchawi niliowahi kuushuhudia!

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,379
1,500
0.jpg

Hawa ndio waathirika......

Kuna simulizi nyingi sana kuhusiana na mila zetu za Kiafrika na vijimambo vyake, hususana mambo ya kishirikina au uchawi. Kama utataka kuandika mada ya Uchawi au ushirikina hasa kwa sisi Waafrika, basi utajaza vitabu lukuki.

Katika kukua kwangu, nimekutana na mambo mengi sana na simulizi nyingi zinazohusiana na ushirikina au uchawi. Zipo nilizowahi kusimuliwa na nyingine nimewahi kushuhudia mwenyewe kwa macho yangu. Nisingependa kuzungumzia yale niliyowahi kuyashuhudia mwenyewe kwa undani kwa sababu yanaweza kuwagusa baadhi ya watu ambao kama wakisoma habari hii hawatajisikia vizuri na nisingependa kuwakera watu na kuwa sehemu ya tatizo.

Leo hii ningepeda kuzungumzia baadhi ya mambo ya kishirikina au uchawi kwa kuangalia baadhi ya mikoa ambayo nimewahi kuishi na kushuhudia au kusimuliwa.

Kwa Kule Tanga, kuna uchawi ambao huitwa Zongo ambapo walengwa wakubwa ni watoto wadogo wanaoazia uchanga hadi miaka kama sikosei kumi. Ingawa aina hii ya uchawi inahusishwa na macho mabaya yaani inavyosemekana ni kwamba kuna watu ambao wana macho yenye kudhuru kama ilivyo kwenye kauli. Kuna watu ambao wakitamka neno ni lazima litatokea na watu hawa wamekuwa wakihusishwa na uchawi wakati sio kweli, ingawa pia wapo watu ambao huwa ni wachawi kweli.

Nikirudi kwenye swala la macho mabaya yenye kudhuru, ni kwamba watu hawa inasemekana wanauwezo hata wa kusababisha mimba changa kutoka bila wao kukusudia, lakini kwa Mkoani Tanga huo ni uchawi kabisa ambao watu huununua na kuutumia kuwadhuru wengine, hususana watoto. Inasemekana kuwa watu wenye kutumia uchawi huo wa zongo huwatupia watoto ambapo mtoto anayetupiwa uchawi huo anaweza kuandamwa na homa kali na hata kutopata choo na tumbo kuuma sana.

Mtoto anayetupiwa uchawi huo hawezi kutibiwa kwa dawa za hospitali, na majaaliwa ya kupona kwake ni kupelekwa kwa mtaalamu wa mitishamba wa kutibu zongo. Lakini pia kwa wale wazee wa zamani wanajua tiba hiyo ambapo haihitaji sana kupelekwe kwa mtaalamu.

Kwa kutumia Tula au wengine huita Ndulele na ufagio ule wa kizamani na sio hii ya Shoprite au Mlimani City, unaweza kutibu hilo zongo. Simulizi hii niliwahi kusimuliwa na shoga yangu mwenyeji wa huko Handeni, na kama maelezo yangu hayako sahihi basi wenyeji wa mkoa huo wanaofahamu zaidi watanisahihisha.

Na kwa kule Moshi, nadhani na Arusha watu hao wenye macho mabaya huwa wanajijua na hata jamii inayowazunguka huwa inawajua. Nilisimuliwa kwamba, kwa mfano kama mtu mwnye macho hayo mabaya anakwenda kumtembelea mama aliyejifungua, kwa kule Moshi, mama mwenye macho mabaya hupewa kwanza kipande cha mgomba akipakate, mfano wa kama amepakata mtoto, kisha ndipo apewe mtoto halisi ampakate. Lengo ni kuhakikisha kuwa mtoto hadhuriwi na macho ya mtu huyo.

Wakati mwingine watu hao wenye macho mabaya hukiri kabisa kuwa wana macho mabaya ili watu waliomzunguka wafahamu hivyo, kuepusha lawama. Naomba Mzee Asprin ayaweke sawa maelezo yangu kama nitakuwa nimekosea.

Kule Pangani napo pamoja na uchawi wa zongo ambao nadhani karibu Mkoa wa Tanga wote unafanyika, pia niliwahi kukutana na uchawi maarufu kama Kopea. Uchawi huu ukoje? Inasemekana watu wanaotumia uchawi huu ni vijana na wazee na uchawi wenyewe unahusiana na chakula.

Inakuwaje? Ni hivi, kwa mfano unaweza kwenda kwenye mghahawa na kuagiza chakula, basi anaweza akatokea mtu akaja na kukaa jirani na wewe akawa anakuangalia unavyokula kwa jicho la wizi. Utakapomaliza na kulipa ukishatoka nje ya mghahawa huo unajisikia njaa kama vile hujala kitu.

Hiyo ina maana kwamba, umekula wewe lakini aliyeshiba ni mwingine, yaani yule mtu aliyekaa jirani na wewe wakati unakula ambaye aliyekuwa anakuangalia kwa jicho la wizi.

Kwa Pangani huo uchawi unachukuliwa kama mchezo tu ambao wenyeji huufanya kwa mazoea, ingawa haudhuru. Kwa wale wenye mighahawa mjini Pangani wanawajua watu wenye tabia hizo na mara nyingi wakiwaona huwatoa nje kwa sababu ya kuepuka kupotezewa wateja.

Mpaka hapo nadhani utakuwa umepata picha juu ya swala zima la ushirikina na vijimambo vyake.

Nikipata muda nitawaletea uchawi na vijimambo vya Wa-Commoro.

Unaweza kusoma na hii link hapa chini:
https://www.jamiiforums.com/mahusia...bu-ona-wachawi-wa-london-na-vibweka-vyao.html


CC: cacico, gfsonwin, AshaDii, Lisa, nivea, Remmy, Asprin, Bishanga, Erickb52, Arushaone, Mungi, marejesho, Preta, snowhite, Madame B, MadameX, watu8, Ruttashobolwa, Fidel80, King'asti, Husninyo, fabinyo, Angel Msoffe, flora msoffe, MwanajamiiOne, BADILI TABIA, nyumba kubwa, Zion Daughter, Paloma, manoah, Bujibuji, Nyani Ngabu, Kaunga, Kiranga, lara 1, SnowBall na wadau wengine wa MMU
 

Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
56,734
2,000
Mmh! Zinduna umeenda Tokomwile au Mwakizaro kwa bibi nini?
Tanga hapo kuna eneo moja karibu na Kwa Minchi kulikua na kimsitu flani hivi kinaitwa "Mtupie"....maana yake kila anayepita mtupie uchawi. Hilo eneo lilikua halikauki mauzauza, ulipita eneo hilo lazima nywele zisimame kama kama mkia wa jogoo linalomchobea mtetee!
 
Last edited by a moderator:

Erickb52

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
18,515
2,000
Zinduna umenikumbusha TULA.
Pia nimekuwa nikiona eti wanawapaka watoto wadogo WANJA ili hata wakiangaliwa na wenye macho mabaya wasiathirike....huwa najiuliza connection nakosa ila ndio hivyo sasa!
 
Last edited by a moderator:

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,379
1,500
Mmh! Zinduna umeenda Tokomwile au Mwakizaro kwa bibi nini?
Tanga hapo kuna eneo moja karibu na Kwa Minchi kulikua na kimsitu flani hivi kinaitwa "Mtupie"....maana yake kila anayepita mtupie uchawi. Hilo eneo lilikua halikauki mauzauza, ulipita eneo hilo lazima nywele zisimame kama kama mkia wa jogoo linalomchobea mtetee!
Achana na hapo Mtupie, kama ukitoka Segera kuelekea Tanga, baada ya kupita kijiji cha Msanga kam a sikosei kuna muembe uko kando ya barabara hapo mahali panaitwa MWEMBE BASHA, kama mnsafiri mkifika hapo mnapata tamaa ya kupumzika, na mkija shituka mshaliwa tigo zamaaani, mara nyingi katika eneo hilo huzuka ugomvi kati ya utingo na dereva kila mmoja akimtuhumua mwenzake.

Mie Bwana watu8, nimeishi viunga vya MWANZANGE na RASKAZONI hapo jijini TANGA
 
Last edited by a moderator:

gfsonwin

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
18,263
2,000
Zinduna nilipooanza kazi tanga nilijionea mengi chumba geni. yaani huko ukipiga kifuu tu cha sema. kuhusu zongo usiseme ila nilichokuja kujua kuna wengine hawajui kabisa kwamba wana macho mabaya.

yaani sijui niwaite misfortune ama nn watu wa aina hii yaani hata kama ni msosi unapika kama akiangalia tu hakiivi.
 
Last edited by a moderator:

SnowBall

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
3,054
1,750
Haya mageni kwangu aisee..Hivi Pangani nako vipi Zinduna ?
Nasikia kuna vibabu hata vikitaka kusafiri, vinatuma tu mtu kutoa taarifa kwa wenye mabasi, haviji stendi wala nini..mwafanya kuvifuata nyumbani..Ole wenu mviache??.......................
 
Last edited by a moderator:

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,379
1,500
Zinduna umenikumbusha TULA.
Pia nimekuwa nikiona eti wanawapaka watoto wadogo WANJA ili hata wakiangaliwa na wenye macho mabaya wasiathirike....huwa najiuliza connection nakosa ila ndio hivyo sasa!


Je yale mahirizi yanayochomelewa na mabati kwa mafundi vibatari ili mtoto akikogeshwa hirizi isilowane.
Unajua kilichomo humo ndani ya hizo hirizi?

Nitakuja kusimulia hapa siku nyingine kwa ID nyengine maana hii kuna mkuda anaijua, akisoma atamwambia nyanya yake anizulie balaa
 

gfsonwin

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
18,263
2,000
umenikumbusha msiba mmoja niliwah kwenda manzese. basi ilibingwa kura ya upish pish la pilau lilimwangukia mtu tofauti kumbe yule mma alotaka apike ule msosi hakupenda. basi kila pilaua likikolezwa viungo aaah wappy halitokelezei mmh! tukajiuliza jamani kunanii hapa??

mama mmoja ambaye alikuwa ni mwenyeji wa eneo lile akasema hebu jamani mwiten mama fulan aje atusaidie ni mpish mzuri basi yule mama kuja tu alishika ukuni akasogeza jikoni. pilau likatokelezea......... nilichoka mie na haya mambo lol!
mpaka leo nikienda msibani sipiki vyakula vya watu najikalia pembeni bingwa wa kuleta maji na kukata vitunguu ila ukoroga mwiko hunikamati lol!
 

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,379
1,500
Zinduna nilipooanza kazi tanga nilijionea mengi chumba geni. yaani huko ukipiga kifuu tu cha sema. kuhusu zongo usiseme ila nilichokuja kujua kuna wengine hawajui kabisa kwamba wana macho mabaya.

yaani sijui niwaite misfortune ama nn watu wa aina hii yaani hata kama ni msosi unapika kama akiangalia tu hakiivi.

Hao ndio wale hata huko kwa wazungu wapo na wanajulikana kwa jila la evil eye

Evil eye - Wikipedia, the free encyclopedia
 

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,379
1,500
Haya mageni kwangu aisee..Hivi Pangani nako vipi Zinduna ?
Nasikia kuna vibabu hata vikitaka kusafiri, vinatuma tu mtu kutoa taarifa kwa wenye mabasi, haviji stendi wala nini..mwafanya kuvifuata nyumbani..Ole wenu mviache??.......................

hiyo ni huko Bagamoyo bana, Pangani vile vibabu vigagula vinajulikana kama Invisible (samahani mkuu simaanishi jina lako). Kizee kinaweza kupanda basi na kisilipe nauli, kila konda akipita kuchukua nauli hakionekani na kinaweza hata kushika nauli mkononi na kisiulizwe mpaka mwisho.
 
Last edited by a moderator:

gfsonwin

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
18,263
2,000
Usinikumbushe Ali Mapilau, yeye yalimkuta alifanyiwa vitimbwi na mwenzake akapika halua badala ya pilau, chezea ZONGO weye

hhahaha! Ali mapilau wa magomeni sio??

yaani kuna vitimbi dunian acha tu. sasa imagine mtu unapika halua badala ya pilau. ila ukweli msosi wa huyu bw n mtamu uspime ila huwez kula mwingi yaani kidogo tu unakinai.
 

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,379
1,500
hhahaha! Ali mapilau wa magomeni sio??

yaani kuna vitimbi dunian acha tu. sasa imagine mtu unapika halua badala ya pilau. ila ukweli msosi wa huyu bw n mtamu uspime ila huwez kula mwingi yaani kidogo tu unakinai.

Yeah, huyo huyo, wakati huo nakaa viunga vya Ilala kwa mjomba wangu, si unajua Ilala kwa shughuli, basi kila shughuli ni lazima Ali Mapilau apewe tenda, kumbe kuna wenzake inawauma, wakamfanyizia, hadi Pilau likamshinda
 

gfsonwin

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
18,263
2,000
ngoja kwanza nikupe stori ya kweli kwenye shughuli za watu.

mie naish uswaz nusu sasa huku shughuli ni almost kila wiki. kuna katabia kale ka watu kusoma dua kwenye menu ya sherehe like wengi wanaopenda mambo ya ushirikina wanatafuta mganga wa vitabu anasoma dua kwenye vyakula kabla havija pikwa na kuandika dua nyingine kwenye maji.

sasa bana hata kama ni watu mia mbili ukapika kg 20 zinaenea kabisa manake mtu akipewa upawa mmoja tu hawez kula tena yaani vinakinaisha usipime halafu unaviona vitam mno. kumbe vimesomewa ma dua ya kiganga nyie mnakinai mnapokula.

binafsi huwa kula kwenye shughuli ni kitu cha mwisho kwangu.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,353
2,000
Eti kuna uliyoona na uliyosikia, halafu unataka kuandika uliyosikia.

Mpaka hapo ushashindwa tayari.

Matokeo yake mtu ana epileptic bouts mnasema kalogwa!

Sijawahi kuona a convincing case for uchawi, some mumbo jumbo and abracadabra mind games maybe, actual witchcraft, no.
 

gfsonwin

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
18,263
2,000
Yeah, huyo huyo, wakati huo nakaa viunga vya Ilala kwa mjomba wangu, si unajua Ilala kwa shughuli, basi kila shughuli ni lazima Ali Mapilau apewe tenda, kumbe kuna wenzake inawauma, wakamfanyizia, hadi Pilau likamshinda

ila na yeye ni mkali uspime.
manake na ule mwiko wake wa chuma anasimamia kistool sio mchezo atii.
basi huwaga anasomeaga dua menu yake lazima muione tamu tu taka ustake lol!
 

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,379
1,500
Eti kuna uliyoona na uliyosikia, halafu unataka kuandika uliyosikia.

Mpaka hapo ushashindwa tayari.

Matokeo yake mtu ana epileptic bouts mnasema kalogwa!
Kiranga nilijua hutakosa la kusema na ndio maana nilikuita.
Yaani laiti ningepeta mume kama wewe, maisha yangu ya ndoa yangekuwa burdaaaani, huwa napenda sana challenge
 
Last edited by a moderator:

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,379
1,500
ila na yeye ni mkali uspime.
manake na ule mwiko wake wa chuma anasimamia kistool sio mchezo atii.
basi huwaga anasomeaga dua menu yake lazima muione tamu tu taka ustake lol!

Mtu wa Rufiji yule, lakini akakutana na wa Bagamoyo alikomaje
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom