Uchawi niliowahi kuushuhudia!

Uchawi niliowahi kuushuhudia!

Hata katika hotuba fulani ya Kambarage, nishawahi kumsikia jinsi walivyomfukia kwenye kaburi na matambiko mengine na wazee aliowaita wa Mzizima, hiyo ilikua ni kabla hajaenda Umoja wa Mataifa kudai Tanganyika huru.
 
Hivi hakuna mchawi humu anirushie hilo zongo nione linakuwaje? Hizi hbr za uchawi kila siku naishia kuziskia tu.
 
Uchawi na dini kimsingi havina tofauti maana vyote msingi wake mkuu ni imani. Labda tofauti iliyopo ni kwenye application tu ingawa hii nayo yaweza kuwa debatable.

Uchawi mtu unaweza kusema lengo lake ni ubaya wakati dini/imani kwa mungu lengo lake ni wema/ uzuri.

We nawe, sasa na ile Halal Badri ina wema au ubaya?
 
hahahha!!umenikumbusha wakati nalipisha watu mishahara dirishani enzi hizo,kuna kitu pia inaitwa chuma ulete,fedha zinaisha halafu bado kuna watu kama 70 hivi hawajaisha,lol!pia wafanyabiashara ni wahanga wakubwa hii kitu!unapata presha eti,afadhali sasa zinapitia benki!hiyo zongo me nakaa na waarusha,wanazongo baya halafu wengine hawajijui,hiyo ndo mbaya zaidi,moja kati ya njia za wife kulinda kachanga chake ni kumpaka wanja,aisee mtoto ni wakiume lakini anakandikwa wanja mpk natamani kulia,hahahaaaaa but it works!!
 
vipi na wale wazee wanaocheza bao kuanzia asubuhi mpaka jioni lakini huwaoni wakienda kujisaidia, ila sasa mtazamaji anayeangalia bao utaona kila baada ya muda anaenda haja kubwa au ndogo lakini wale wazee hawanyanyuki wanaendelea kucheza tu kumbe wanakupasia mizigo yao! Mimi ishanipata miaka ya nyuma pande za mwananyamala nilikuwa nazuga kwenye bao wakati namlia mingo dem flani, wewee si mchezo kila wakati wazee wananisakizia kupeleka mizigo yao, bahati kulikuwa na bar jirani nikawa najisevia kwenye toilet yao nilipokuja kushtukia mchezo washantesa sanaa! nikawa sikai tena nikawaacha wasakiziane mizigo yao wenyewe kwa wenyewe!

Hiyo kwa kule Morogoro inatumiwa na wazee wakati wakinywa pombe za matapu tapu maarufu kama Boha, Chimpumu au Ngedule, wakati wakinywa kama katika meza yao kuna mtu hajui hayo mambo, basi wanaambiana "kusanya, kusanya, kusanya" kisha jamaa anabebeshwa mikojo au haja kubwa na kila akirudi wanakusanya tena na kumsukumia huyo mgeni, ni mpaka ajitokeze mtu amnusuru kwa mumwambia kinachoendelea, la sivyo siku hiyo atatembea kwenda chooni mpaka akome
 
Kwa hiyo Pacha Zinduna na Shostito gfsonwin mnakiri kbs kuwa Tanga ndo kumejaa Uchawi???????????????

Tanga ni kiboko ya mambo weye, mie mwenyewe nina asili ya Tanga na huwezi kunidanganya kitu. Niliwahi kwenda Sumbawanga, na nilipowaeleza wenyeji kuwa mie ni mwenyeji wa Tanga walikuwa wananiogopa kama ukoma na walikuwa wanaambiana,"usikachezee kale kabinti, kametokea Tanga kale, ukikagusa tu, ukoo wenu wote utaangamia".
Kama mtu haamini aende Sumbawanga kisha aseme ametokea Tanga ataona atakavyoogopwa, tena ukitaka kuwatisha zaidi waambie umetokea Pemba, Mama weee, watatoka dima usipime
 
Nyani Ngabu kimsingi mambo ya uchawi hayawezi kuthibitishwa,lakini hii haimaanishi kuwa uchawi haupo.

Kwa nini kimsingi hayawezi kuthibitishwa? Sababu inayofanya yasiweze kuthibitishika ni nini? Maana kama kweli yapo sioni kwa nini yasiweze kuthibitishika.

Wazungu ni wachawi kuliko sisi,tena uchawi wao ni kiboko zaidi.

Duh! Ebana eeh we umejuaje kuwa Wazungu ni wachawi kuliko sisi na kwamba uchawi wao ni kiboko zaidi? Manake kwanza ushasema kimsingi mambo ya uchawi hayawezi kuthibitishwa. Sasa kama hayawezi kuthibitishwa wewe umejuaje kuwa uchawi wa Wazungu umeuzidi wa kwetu?

Obama na Hillary ni wachawi sana.

Are you serious?

Uchawi wao ni black Magic ambao una asili ya Kabalah.Usidhani huko haupo.

Na wa kwetu ni nini? Green magic?

Hata kuipata nafasi ya kuwa mgombea uraisi wa Marekani achilia mbali kuwa raisi,ni lazima uwe mchawi na unashiriki uchawi.

I'm starting to think you aren't serious with what you are contending.

Tatizo tumeaminishwa Ulaya na Marekani hakuna uchawi na uchawi upo Africa tu,kuamini hivi ni jambo la ajabu sana.Hakuna jamii isiyokua na uchawi.Na uchawi ukifanyika kokote ni uchawi tu!

Imani za kishirikina shirikina hata Ulaya na Marekani zipo kwani zisingekuwepo basi hata misamiati inayohusu mambo hayo isingekuwepo kwenye lugha zao. Ila kwa maoni yangu nadhani sisi Afrika tumezidi sana.
 
Hahahahahahahahahaha
Zinduna hapo kwenye kula alaf ana shiba mwingine umeniacha hoi sana!

We kweli ni mshamba, kwani hujui wazungu waligunduaje BLUE TOOTH?
Ni kutokana na huo uchawi wa KOPEA na ndio wakagundua hiyo kitu inaitwa Blue tooth.

Niliwahi kusimuliwa kwamba kuna mzungu anaitwa Dawson Fitzgerald alikwenda huko Pangani Tanga kufanya utafiti wa Mbu waambukizao Malaria na siku moja wakati anakula kwenye mghahawa akachezewa huo mchezo wa Kopea, ikabidi aachane na utafiti wa Mbu na Malaria akahamishia utafiti wake kwenye huo uchawi wa KOPEA na ndipo akarudi kwao na hatimaye akaja na huo ugunduzi wa BLUE TOOTH.
 
Mmmmhhhh bibie.@v Umefikirianini leo mpaka ukaweka hii Thread?Kuhusu Uchawi kama kuna mtu anajuwa uchawi wakuwa mimi niwe Tajiri anifundishe mimi jamani.Sitaki uchawi wa kudhuru mimi ninataka Uchawi nijifunze wa kuweza kunipa Utajiri tu niwe Billionea mkubwa Kama Bill Gates. Kuhusu mambo ya Uchawi Tumuulize mtu mmoja yupo humu ndani anaitwa kwa jina MGANGA WA KIENYEJI yeye ndie atatujibu vizuri kama uchawi upo au hakuna?
 
Last edited by a moderator:
By the time unahisi utashuhudia, unajikuta hata hizo guts za kushuhudia huna tena maana wataalam washafanya ya kufanya!

ila sasa ntajuaje kama ndio washanifanyia mambo?
 
ila sasa ntajuaje kama ndio washanifanyia mambo?

Kuna mwenzio alibebeshwa mimba miezi tisa alipopelekwa hospitali kujifungua akatoa ushuzi na tumbo likanywea, kumbe haikuwa mimba bali alipigwa Zongo
 
Hivi hakuna mchawi humu anirushie hilo zongo nione linakuwaje? Hizi hbr za uchawi kila siku naishia kuziskia tu.

wakati ule nakua nilipata simuliwa kwamba mwanamama mmoja alichaguliwa kuwa mkuu wa wilaya magu. alipofika huko aliwapiga mkwala wenyeji kwamba anasikia wao ni "wachawi" lakini kwake ni breki kwani haamini mambo hayo. asubuhi alipoamka akajikuta amelala nje ya nyumba akiwa mtupu! mama akamwomba jk (mwalimu) amhamishe haraka. mama huyu alikuja kuwa waziri awamu ya 2 na 3 kama sikosei. yupo bado mtafute atakuelekeza wapi ukakutane na wakukurushia zongo 🙂
 
Mwalimu gfsonwin sasa kwenye mpira enzi zile za African Sports na Coastal Union,ilikuwa balaa,kuna mechi moja mwaka 89,Yasini Napili alipiga shuti mpira umempita kipa halafu ukapasuka vipande viwili na vile vipande havikuvuka goal line kuamanisha kwamba sio goli,na mechi hiyo hiyo kulikuwa kuna babu alikuwa amepelekwa ufukweni mwa bahari wakati maji yamekupwa, wakawa kama wamemzika kwa kusimama isipokuwa kichwa na shingo ,baada ya mpira kwisha matokeo yalikuwa nunge, basi watu wakasahau kwenda kumfukua kule ufukweni mpaka maji yakawa yanajaa bahati nzuri wavuvi wakasikaa kelele alizokuwa anapiga ndio wakaenda eneo la tukio ndio wakamfukua.Nilikuwa kambini usiku kabla ya mechi hii basi vitu vingine siwezi simulia kwani huwezi amini mambo yaliyokuwa yanafanyika.Mungu alinisaidia niliacha mpira msimu uliofuata kwani nilikuwa nimechaguliwa kwenda form five toka Usagara Secondary,oops isije id ika.........Sarikoki sikjui kama ulikuwa kishazaliwa..... ha ha ha

Hili tukio la Yasin Abuu Napil kupiga mpira na kupasuka ni la kweli ingawa sio kama ulivyo elezea....Nakumbuka Coastal walikuwa wanaelekeza mashambulizi upande wa kaskazini,Napil alijaribu kupiga shuti la mbali kwa mshango wa wengi mpira ukapasuka,na kwa kuwa mechi ya Coastal vs African Sports ilikuwa ikiandamana na vituko vingi vya kishirikina watu walipelekea huko.

Na hatidhi ya kuzikwa mtu ufukweni ni ya siku nyingi kwa waliowahi kuishi Tanga, na imasemekana marehemu Hamisi Mduruma ambaye alikuwa ndio muongoza ushangiliaji wa Coastal ndiye aliye sahauliwa pwani.
 
Zinduna nishaona mengi ila hilo la mimi niagize msosi wewe ushibe iko kazi. No wonder Tanzania wako mstari wa mbele ki-uchawa! Ee Mungu niepushe.
 
Last edited by a moderator:
ahahahahhaaa!?!?Tanga,tanga!! inaitwa Tanga na Tangata bwana,Tanga ya sasa sio ile ya mwaka 47,hadi vibibi vizee sasa vimebanwa vinafanya ukahaba,ila dadangu Zinduna wewe nashindwa kukupata kuna siku uliwahi kunitishia kunisomea ahl badr dah!!,nakumbuka tanga ilikuwa tanga enzi hizo miaka ya 80 na 90 siyyo sasa bwana viwanda vilikuwa kila kona mji umenawili tanga ilipendeza tazama sasa jinsi ilivo tanga,imechakaa huwezi kuamini kuwa ndio mji huu huu uliozaa tanganyika na uliokuwa makao yake makuu ya kwanza mahoteli yalikuwa yamejaa nenda sasa yote yamebaki magofu tu!!??!!,SHAME ON THE GUYS WHO LED TO ZE DESTRUCTION OF TANGA INDUSTRIES!!nakumbuka enzi hizo majestik sinema na mapicha ya kihindi na kzungu wakati Tanzana nzima ipo gizani sisi tulikuwa tunaona vitu hadimu toka marekani na india duh!!enzi hizo coasstal union na affrican sports kina mwameja,razaq carecca na kina juma mgaza na juma mgunda tanga ilikuwa noma.mi niikuwa na kaa karibu na hapo uwanja wa gym khana enzi hizo huo mtaa wa shule ya bombo basi nakumbuka kuna dada mmoja jilani etu alikuwa form 2 alipita asubuhi anawahi shule njia a makaburini ya shule ya msingi bombo asubuhi peke ake si akakanyaga jini bwana alilotegeshewa mwingine likamwingia likadai binti awe mganga mara atake kaniki mara pete mara kile liliwasumbua...,nakumbuka ukitaka kwenda kota za NASACO kuna ukuta pale uko wazi basi ikifika killa saa 8 usiku ukipita hapo lazima watu waliobeba mienge wawatimue mbio!!!ni kweli haya jamani,nakumbuka enzi hizo tukienda beach karibu na mkonge hotel dah si majini hayo jamani yapo kama watu ukiwatongoza tu utakoma labda wakukubali wenyewe,kwa vihoja tanga utapapenda yaani vinatisha mbaka basi,ukioa binti wa kitanga so siri hata kama utamwona mstaarabu na alietulia kiasi gani ujiandae kutengenezwa!!nakumbuka enzi hizo wa2 wanatngoza majini tanga bila kujijua ila kwa sisi tuliokulia pale mjni tulikuwa tuna hafadhali kidogo kucompare na waliokuwa wakiishi mbali na town,nakumbuka mbabe wa Tanga enzi hizo alikuwa anaitwa Pama alikuwa mwizi balaa halafu alikuwa mwembamba ila nguvu sijui alikuwa anazitolea wapi mana alikuwa anapiga,nusura anipore baiskeli angu aina a shangshang enzi hizo sifa ake alikuwa akikupiga kibao lazima upoteze fahamu!!maneno a chumba geni hayo baba si majini hayo huko yaani kunatisha si mchezo,ndio mana mi hata sasa nkirudi tanga hata nikitaka kuchukua malaya usiku huwa nipo makini nao sana.
 
Back
Top Bottom