Uchawi niliowahi kuushuhudia!


Mkuu hiyo inatumika dua aliyofanya Bwana Yesu pale alipomaliza kuhubiri na makutano wamejaa na wana njaa ! Akauliza kuna chakula gani ? Akaambiwa kuna kipande cha samaki na mkate. Akavichukua, akaomba, kisha akaanza kuwagaiya makutano, walikula hadi na kusaza ! Ni hivyo tu hapo hamna uchawi ni duwa tu !
 
nyingi ni simulizi tu ambazo hazina uthibitisho. Tanga ni moja ya mikoa mbayo mungu ameibariki vitu vingi vzr... Panafaa kuishi kwani maisha ni rahisi, plan nzuri ya mji nk

Basi wewe huijui Tanga, Je unamkumbuka Sheikh Omari Vikapu?
Huyu alikuwa na shamba lake la minazi basi kuna vjana walikwenda kuiba nazi, shambani kwake. Akatangaza na kuwapa siku saba wezi wajisalimishe la sivyo atasoma hiyo Halal Badri, wezi wakakaidi. Basi Mzee Omari Vikapu akashusha dua ya Halal Badri, kilichotokea ilikuwa ni maafa, wale vijana wote walifariki isipokuwa mmoja alisalimika, punda waliobeba zile nazi waliangamia, minazi iliyotumika kufungwa wale punda ilikauka, vyuma vilivyotumika kufulia zile nazi vilivunjika vipande vipande. aliyesalimika ni kijana mmoja aliyekwenda kujisalimisha kwa huyo mzee na kuomba radhi, lakini aliambiwa ni too late dua ishasomwa. hata hivyo alimshika kichwani na kumuombea dua. alisalimika, lakini alioza pua na mdomo na baada kuhangaika sana akapona lakini alikuwa ameharibika sura kwani sehemu ya pua na mdomo ilikuwa imeondoka na hivyo kuacha kinywa wazi, alikuwa anafunga kigozi ili kuficha meno yasionekane. watu wakawa wanamwita Omari Kigozi na shughuli zake zilikuwa ni pale Soko la Ngamiani. Naamini waliowahi kuishi hapo miaka ya 80, watakuwa wanamkumbuka.
 
Mkuu hii ya vifaranga kiboko ! Daaaah ! Sasa vifaranga vinakuwaje ?
Ukifika hapo maeneo ya MSAMBIAZI unaweza kushangaa kukuta kuku kafungwa hirizi, kwani vifaranga wanweza kupigwa zongo visikue kabisa vinadumaa mpaka vinakufa...
Kuku anayetaga anaweza kupigwa zongo hadi atamie mwaka mzima, wewe achana na mkoa wa Tanga, na hapo hujaenda mahali panaitwa MARAMBA au MAGOMA, kuna wachawi hapo mwana ukome, unaweza kupigwa kitu ukajikuta uko Congo DRC wakati ulikuwa Tanga, wenyewe wanaita SAKIRIZI.

Ngoja nikipata muda nitasimulia ushuhuda kuhusu uchawi wa Tanga na vitongoji vyake.
 
nakuombea upate muda, yaani umefanya x-mass yangu kuwa njema!! bravo Zinduna. Merry x mass
Note; hivi uchawi wa radi ndo uko S'wanga tu? sijasikia hapa, au humu MMU hatuna wana s'wanga?
 

Juma Mgunda alikuwa anachezea Coastal Union BosS
 

si kumkumba tu, namfaham! Suala la kuijua Tanga si kwamba naijua tu nimezaliwa Bombo hospital na nimekulia usagara na sahare na kusoma kule up to O-level. Sikatai uchawi upo na c Tanga tu, hata hapo ulipo upo. Ninao mpaka rafiki zangu ambao walishaathirika na halal-badri, ipo ipo sikatai...but MENGINE NI SIMULIZI TU AMBAZO TUMEKUWA TUNAZISIKIA MPAKA TUMEONDOKA HUKO...hazina uthibitisho wowote
 



Wakati mwingine watu hao wenye macho mabaya hukiri kabisa kuwa wana macho mabaya ili watu waliomzunguka wafahamu hivyo, kuepusha lawama. Naomba Mzee Asprin ayaweke sawa maelezo yangu kama nitakuwa nimekosea.






nasema hiviiii Zinduna unikome. Tena nakuuliza unanitaka? Mie nliyemshiba Roho Mtakatifu na mambo ya kishirikina wapi na wapi?

Jongeeni kwenye Altare ya Bwana tumwimbie Bwana kwa Shangwe.

Mwokozi Kazaliwa Leo!!
 
Last edited by a moderator:
nasema hiviiii Zinduna unikome. Tena nakuuliza unanitaka? Mie nliyemshiba Roho Mtakatifu na mambo ya kishirikina wapi na wapi?

Jongeeni kwenye Altare ya Bwana tumwimbie Bwana kwa Shangwe.

Mwokozi Kazaliwa Leo!!
Leo unajifanya huzijui TUNGULI!
 
Hii wanadai dawa yake kumwaga
chumvi kidogo motoni kabla hujaanza upishi. Sijui inasaidia or not, sie
huwa tunaona hatuna cha kupoteza so tunajitupia chumvi motoni
tunaendelea. Au sijui bado hatujakutana na hilo jicho!

Kupika shughulini kumwaga chumvi kwenye moto muhimu vinginevyo utachochea mpaka vidole na msosi hauivi ng'o!
 

khaaaaaa tanga chiboko
 

nimependa ulivyomalizia
''jogoo linalomchubea mtetea'' watu8
 
Last edited by a moderator:
He! Hivi Asprin leo xmas badala ya kunywapo bia upo kwen mazongo huku?

Zinduna hebu ntupie zongo ili tupendane sisi tu hakuna kitu cha ivo?
 
Last edited by a moderator:

ebwanaeee,. Tena utakuta dogo kafungwa kamba kiunoni ina kibusta kama andazi vile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…