Mwalimu gfsonwin sasa kwenye mpira enzi zile za African Sports na Coastal Union,ilikuwa balaa,kuna mechi moja mwaka 89,Yasini Napili alipiga shuti mpira umempita kipa halafu ukapasuka vipande viwili na vile vipande havikuvuka goal line kuamanisha kwamba sio goli,na mechi hiyo hiyo kulikuwa kuna babu alikuwa amepelekwa ufukweni mwa bahari wakati maji yamekupwa, wakawa kama wamemzika kwa kusimama isipokuwa kichwa na shingo ,baada ya mpira kwisha matokeo yalikuwa nunge, basi watu wakasahau kwenda kumfukua kule ufukweni mpaka maji yakawa yanajaa bahati nzuri wavuvi wakasikaa kelele alizokuwa anapiga ndio wakaenda eneo la tukio ndio wakamfukua.Nilikuwa kambini usiku kabla ya mechi hii basi vitu vingine siwezi simulia kwani huwezi amini mambo yaliyokuwa yanafanyika.Mungu alinisaidia niliacha mpira msimu uliofuata kwani nilikuwa nimechaguliwa kwenda form five toka Usagara Secondary,oops isije id ika.........Sarikoki sikjui kama ulikuwa kishazaliwa..... ha ha ha