Hivi hakuna mchawi humu anirushie hilo zongo nione linakuwaje? Hizi hbr za uchawi kila siku naishia kuziskia tu.
ahahahahhaaa!?!?Tanga,tanga!! inaitwa Tanga na Tangata bwana,Tanga ya sasa sio ile ya mwaka 47,hadi vibibi vizee sasa vimebanwa vinafanya ukahaba,ila dadangu Zinduna wewe nashindwa kukupata kuna siku uliwahi kunitishia kunisomea ahl badr dah!!,nakumbuka tanga ilikuwa tanga enzi hizo miaka ya 80 na 90 siyyo sasa nakumbuka enzi hizo majestik sinema na mapicha ya kihindi duh!!enzi hizo coasstal union na affrican sports kina mwameja,razaq carecca na kina juma mgaza na juma mgunda tanga ilikuwa noma.mi niikuwa na kaa karibu na hapo uwanja wa gym khana enzi hizo huo mtaa wa shule ya bombo basi nakumbuka kuna dada mmoja jilani etu alikuwa form 2 alipita asubuhi anawahi shule njia a makaburini ya shule ya msingi bombo asubuhi peke ake si akakanyaga jini bwana alilotegeshewa mwingine likamwingia likadai binti awe mganga mara atake kaniki mara pete mara kile liliwasumbua...,nakumbuka ukitaka kwenda kota za NASACO kuna ukuta pale uko wazi basi ikifika killa saa 8 usiku ukipita hapo lazima watu waliobeba mienge wawatimue mbio!!!ni kweli haya jamani,nakumbuka enzi hizo tukienda beach karibu na mkonge hotel dah si majini hayo jamani yapo kama watu ukiwatongoza tu utakoma labda wakukubali wenyewe,kwa vihoja tanga utapapenda yaani vinatisha mbaka basi,ukioa binti wa kitanga so siri hata kama utamwona mstaarabu na alietulia kiasi gani ujiandae kutengenezwa!!nakumbuka enzi hizo wa2 wanatngoza majini tanga bila kujijua ila kwa sisi tuliokulia pale mjni tulikuwa tuna hafadhali kidogo kucompare na waliokuwa wakiishi mbali na town,nakumbuka mbabe wa Tanga enzi hizo alikuwa anaitwa Pama alikuwa mwizi balaa halafu alikuwa mwembamba ila nguvu sijui alikuwa anazitolea wapi mana alikuwa anapiga,nusura anipore baiskeli angu aina a shangshang enzi hizo sifa ake alikuwa akikupiga kibao lazima upoteze fahamu!!maneno a chumba geni hayo baba si majini hayo huko yaani kunatisha si mchezo,ndio mana mi hata sasa nkirudi tanga hata nikitaka kuchukua malaya usiku huwa nipo makini nao sana.
Kuna mwenzio alibebeshwa mimba miezi tisa alipopelekwa hospitali kujifungua akatoa ushuzi na tumbo likanywea, kumbe haikuwa mimba bali alipigwa Zongo
hahahha!!umenikumbusha wakati nalipisha watu mishahara dirishani enzi hizo,kuna kitu pia inaitwa chuma ulete,fedha zinaisha halafu bado kuna watu kama 70 hivi hawajaisha,lol!pia wafanyabiashara ni wahanga wakubwa hii kitu!unapata presha eti,afadhali sasa zinapitia benki!hiyo zongo me nakaa na waarusha,wanazongo baya halafu wengine hawajijui,hiyo ndo mbaya zaidi,moja kati ya njia za wife kulinda kachanga chake ni kumpaka wanja,aisee mtoto ni wakiume lakini anakandikwa wanja mpk natamani kulia,hahahaaaaa but it works!!
Umetukana bibi zetu na umesema uongo,kwanza Coastal kulikuwa na Rubern Mgaza na Sio Juma Mgaza...Jambo la pili Pama hakuwa mwizi bali mtemi na miaka hiyo ya 80/90 Tanga ku-pump na mchezo wa ngumi ilikuwa ndio fashion na huyu Pama ambaye ni marehemu 'alifariki Italy mwaka jana nadhani' Mwenyezi Mungu alimbariki ubavu na ngumi alikuwa anazijua.
Kama hujaona uchawi ukifanya kazi utaendelea kubisha uwepo wake,lakini kwa tuliowahi kushuhudia tunajua ukweli!
Nyani Ngabu nimesema nimeona uchawi ukifanya kazi maana yake nimeona matokeo yake
Uchawi ni nguvu kama vile umeme,huwezi kuuona bali unaona matokeo yake kwakuwa hauna mwili.
Unachoweza kukiona ni kile chenye mwili tu nje ya hapo huwezi.
Sina haja kukuambia kwa kuwa binadamu wengi tunaamini kwa kuona au kugusa,hivi nikikuambia nimeshuhudia mtu anaruka na ungo itakusaidiaje?Si utaniambi muongo?Au utataka ushuhudie?
Tunadhani kuwa hakuna maisha nje ya kugusa na kuona.Sayansi isingesema na kuleta ushahidi wa sayari halafu ukaambiwa kuna sayari angani ungemuona kama amechanganyikiwa,sababu tu hauzioni.
Vile ambavyo hatuvioni au kuvithibitisha haimanishi havipo,inatakiwa tuendelee kuvifanyia utafiti ili tuvijue
Hivi hakuna mchawi humu anirushie hilo zongo nione linakuwaje? Hizi hbr za uchawi kila siku naishia kuziskia tu.
Umetukana bibi zetu na umesema uongo,kwanza Coastal kulikuwa na Rubern Mgaza na Sio Juma Mgaza...Jambo la pili Pama hakuwa mwizi bali mtemi na miaka hiyo ya 80/90 Tanga ku-pump na mchezo wa ngumi ilikuwa ndio fashion na huyu Pama ambaye ni marehemu 'alifariki Italy mwaka jana nadhani' Mwenyezi Mungu alimbariki ubavu na ngumi alikuwa anazijua.
wakati ule nakua nilipata simuliwa kwamba mwanamama mmoja alichaguliwa kuwa mkuu wa wilaya magu. alipofika huko aliwapiga mkwala wenyeji kwamba anasikia wao ni "wachawi" lakini kwake ni breki kwani haamini mambo hayo. asubuhi alipoamka akajikuta amelala nje ya nyumba akiwa mtupu! mama akamwomba jk (mwalimu) amhamishe haraka. mama huyu alikuja kuwa waziri awamu ya 2 na 3 kama sikosei. yupo bado mtafute atakuelekeza wapi ukakutane na wakukurushia zongo 🙂
Hili tukio la Yasin Abuu Napil kupiga mpira na kupasuka ni la kweli ingawa sio kama ulivyo elezea....Nakumbuka Coastal walikuwa wanaelekeza mashambulizi upande wa kaskazini,Napil alijaribu kupiga shuti la mbali kwa mshango wa wengi mpira ukapasuka,na kwa kuwa mechi ya Coastal vs African Sports ilikuwa ikiandamana na vituko vingi vya kishirikina watu walipelekea huko.
Na hatidhi ya kuzikwa mtu ufukweni ni ya siku nyingi kwa waliowahi kuishi Tanga, na imasemekana marehemu Hamisi Mduruma ambaye alikuwa ndio muongoza ushangiliaji wa Coastal ndiye aliye sahauliwa pwani.
Njoo nikupeleke kijiji kinaitwa Mnyuzi, hapo Korogwe kwa akina maji Marefu. Wao wame advance katika taalum ya "zongo" hivyo zongo hapigwi mtu ili kuepuka lawama. Zongo linapigwa kitanda, shuka, au nguo uliyoianika katika kamba. Ukilalia kitanda tu, una malaria kali sana ya kuwekewa drip za quinine ! Ila ukinyanyuka tu kitandani umepona. Ukitokea zongo limepigwa kwenye shati, basi utashinda na homa mpaka ulivue ! Kabla hujaenda Hospital au Zahanati hakikisha umehakikiwa na vipimo vyote vya zongo !
Tangan kwa uchawi bwana kunatisha nakumbuka ilikuwa ikifika jioni enzi hizo tulikuwa hatupiti ile njia a makaburini nyuma ya shule ya msingi bombo jinsi kulivyokuwa noma ila nimekaa miji mingi sana ila hakuna hata mmoja nnaoupenda zaidi ya Tanga,