SoC02 Uchawi na Ushirikiana unavyoathiri maendeleo ya taifa

Stories of Change - 2022 Competition

Nasibu hemedi

Member
Aug 27, 2022
11
4
Kwa majina naitwa ramadhani selemani ramadhani ni kijana wa kitanzania. Leo nimependa kuzungumzia maswala ya imani ya kishirikina na uchawi zinavyo athiri maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Katika mchi kuna makabila mbalimbali zaidi ya 150 kila kabila lina utamaduni wake na imani zake. Katika utamaduni wa kila kabila kuna utamaduni mzuri na mbaya hivyo leo nataka nizungumzie utamaduni unavyo leta ushirikina na kuathiri maendeleo katika jamii kwa ujumla.


Jinsi uchawi unavyo athiri maendeleo ya jamii na nchi.

Katika jamii zetu za tanzania huwa zinaamini kwa asilimia kubwa japo sio wote, unakuta mtu anaumwa au kupata matatizo fulani katika jamii badala wampelete hospitalini kabla hajazidiwa wao huanza kumpeleka kwa wa kienyeji wakiamini huenda atakuwa amelogwa kumbe huenda mgonjwa anaupungufu wa damu na kupelekea umauti na kupoteza nguvu kazi ya taifa kwa ujumla.

Baadhi ya jamii huwa zinawauwa vilema yani walemavu wakiamini ni njia nzuri na mojawapo ya kupata utajiri na mafanikio katika maisha. Kumbe ni imani potofu inayopelekea kupotea kwa nguvu kazi nchini.

Wengine huenda kwa waganga ili walate vyeo maofisini ila wanapofika kwa waganga hupewa masharti magumu mfano kuwauwa watoto wao kuwauwa wake zao na wazazi wao ili wapate vyeo jambo ambalo sio kweli na nikinyume cha sheria ni upotevu wa nguvu ya taifa.

Baadhi ya watumishi wa uma mfano madokta na mahakimu huogopa kutenda haki huku wakiamini huenda moja ya watuhumiwa au wagonjwa ni wachawi huenda akitenda haki au kufuata utaratibu atalogwa jambo ambalo hupoteza haki ya kila mtu.

Kuna baadhi ya jamii kunapotokea misiba huamini huenda marehemu atakuwa amelogwa kwa kuchukuliwa msukule kiushirikina.

Wanapo amini hivyo hupelekea migogoro kwa kuwa kila moja huhisi labda mwenzake au jirani yake ndio alio muuwa kwa uchawi hii hupelekea utengano na migogoro katika jami.

Baadhi ya jamii ukizaa mtoto mlemavu unatakiwa umtoe sadaka usipo fanya hivyo unauwawa au unatengwa na jamii yako hali hii inathiri watu kwakuwa kwenye jamii zetu tuna welemavu nao wanahaki ya kuishi kama wengine na wanamchango mkubwa sana katika jamii zetu na wanaleta maendeleo ya mchi.

Katika imani zetu za kidini zimezungumzia sana maswala ya ushirikina na uchawi kuwa upo tangu enzi za zamani ila kuna jamii zinatumia vibaya imani hii ya uchawi na kufanya vitendo vya ukatili na unyanyasaji katika jamii zetu.

Hivyo serikali inatakiwa izidi kuunda zaidi ya kuweza kutokomeza wimbi hili mana lina zoofisha maendeleo ya mchi kwa ujumla.


Nini kinapelekea imani za kishirikina?

(a) Ugumu wa maisha; jamii zetu nyingi ni maskini hivyo kupitia imani za kishirikina wanaamini huenda watafanikiwa katika maisha kumbe sio kweli ni imani potofu.

(b) Utamaduni zaifu, kwakuwa kuna jamii huamini kuwa ulemavu ni ugonjwa na ni laana hivyo hupelekea huuwa nguvu kazi.

(c) Ukosefu wa elimu kwa baadthi ya wana jamii. Kuna baadhi ya jamii haina elimu juu ya imani potofu huwa bado haijawafikia kwa ukaribu huenda kutokana na ubovu wa miundombini ya baadhi ya maeneo ya nchi yetu.

(d) Tabia ya kurithi.kuna baadhi ya watu wasomi kabisa na wanaelimu ya kutosha ila bado imani hii inawasumbua kutokana na utamaduni wa kurithi kutoka kwa mababu zao au kwenye koo zao.

Je, Serikali inachangia kuongezeka kwa kudidimiza elimu za kishirikina?
Hili swali kila mtu ataitaji kujua kuwa je ni kivipi serikali inadidimiza elimu yakutokomeza elimu ya kishirikina. Kwa sababu zifuatazo

(a) Serikali ni watu na watu ndio wenye imani ibakuwaje serikali idai haiamino uchawi wakati serikali ni watu nandio hao hao wenye imani hio alafu serikali eti haiamini na haioneshi nguvu kubwa katika jambo hili la kukomesha uchawi kwakuwa srikali haiamini kuwa uchawi upo.

Hata unapofika mahakamani ukishitaki mtu fulani kaniloga huwa kesi haisikilizwi kwakua kiserikali haitambui uchawi. Haliakuwa huyo hakimu mwenyewe bafahamu fika kuwa uchawi upo nae huenda alisha wahi kwenda kwa mganga.

(b) Ndani ya serikali kuna viongozi ni waganga wengine huenda niwachawi lakini hao hao wakikaa kwwnye baraza wanakuambia uchawi hakuna na serikali haiamini imani hio ya ushirikina na ndio mana hawaoneshi sapoti kubwa katika kutatua hili tatizo katika jamii

Je, kwenye jamii zetu kuna mtu hafahamu kuwa uchawi upo?
Mimi kama mimi siamini kama dunia ya leo ya utanda wazi kuna mtu hafahamu na hajui kuwa uchawi upo.

Kwa hio kwa 90% watu wote wanafahamu juu ya swala la ushirikina.
Ukipita maeneo ya mjini utakuta mabango ya waganga ya kienyeji yamebandikwa hakuna asiyo fahamu hilo hata ukipita mtandaoni unakuta matangazo ya waganga yapo.


Hasara za imani za kishirikina.

(a) Kuongeza wimbi la umaskini katika jamii kwa ujumla kutokana na vijana tulio wengi tunaacha kufanya kazi na kutafuta utajiri kwa njia ya ushirikina na mwisho wa siku hatufanikiwi tunapoteza muda wetu.

(b) Kupunguza nguvu kazi katika jamii mfano kuwauwa walemavuu kama albino. Hii hupunguza nguvu kazi kwakuwa watu hawa husaidia serikali kupata maendeleo na kujenga taifa la kesho.

(c) Kuua vipaji ; vijana wengi wamefariki kutokana na imani za kishirikina huenda wangekuwepo wangekuwa moja ya wasanii wa taifa letu.

Mimi kama kijana nilioguswa na swala hili nimemua hufikisha nakala hii mbeleyenu tusaidiane kutatua changamoto hii katika jamii zetu kwa pamoja tupaze sauti kwa njia tofauti tofauti tuokoe wenzetu wanao angamia.

Nina imani kwa pamoja tutafanikiwa.
 
Back
Top Bottom