Nguvu na maajabu ya uchawi

A43

JF-Expert Member
Nov 18, 2023
385
757
Tuanzie hapa. Sayansi ni nini? Ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli zilizo bainishwa pasi kuthibitishwa. Msingi wa sayansi ni vitendo.

Uchawi ni nini? Ni nguvu zinazotumiwa na watu wenye maarifa maalumu yasiyo ya kisayansi katika jamii nyingi duniani (zikiwemo za Afrika, Asia, Ulaya n.k.), ingawa kuna tofauti nyingi kulingana na mahali au utamaduni.

Binafsi nakiri kusema uchawi ni sayansi ambayo haitaki kuthibitishwa na kuhalalishwa kwa vitendo kwenye jamii lakini naamini kadri miaka inavyozidi kwenda kuna siku uchawi utakuwa halali nakufanywa kwa vitendo kwenye jamii nyingi duniani. Tunaona leo Wingereza wamefungua chuo rasmi cha mafunzo ya uchawi kwa vitendo, hapa tutaona jinsi gani sayansi ya uchawi inakwenda kuthibitishwa na kuhalalishwa.

Ebu leo tutizame miongoni mwa NGUVU NA MAAJABU YA UCHAWI ambayo binafsi nina hakika nayo, mimi sio mchawi lakini haya nayokupa ni 100% πi moja ya vitendo ambavyo uchawi unaweza kufanya pia kuna visa juu ya hizi simulizi za nguvu na maajabu yake.

1. Uchawi unaweza kuwasha umeme hata Tanesco wakizima.

2. Uchawi unaweza kubaini ni mtoto gani atazaliwa mf jinsia yake, ilihali hata kabla mtoto yule hajapandikizwa kwenye tumbo la mwanamke.

3. Uchawi unaweza kutoa mimba kwa mwanamke mwenye miezi 5 na akalelewa kwenye mifumo ya kichawi hadi kufika miezi 9, hii ni kama ile sayansi yakukuza watoto kwenye chupa, basi sayansi hii mchawi yuko nayo.

4. Uchawi wakuiba, mchawi anaweza kuiba bila kuonekana mf wachawi wamekuwa wakiiba sana sukari, nafaka, na vitu vingine kwenye maduka ya mahitaji ya nyumbani au shambani., hapa watu hula hasara kwenye maduka yao kishirikina kwani bidhaa zao wakati mwingine huibiwa kuchawi, na wale wakulima wenzangu wanafahamu jinsi mazao yanavyoibiwa mashambani kwa nguvu za kichawi.

5. Uchawi wakujibadirisha, au kujigawa, mf imewahi tokea dada mmoja alikuwa mchawi na kahaba kuna siku usiku mmoja alilala na wanaume wanne tofauti hadi asubuhi kwa wakati mmoja, ilikuwa hivi washkaji katika story zao mtaani mmoja alisema demu flani nimeichapa jana hadi asubuhi, mwingine akasema uongo huyo demu nimelala nae mimi hadi asubuhi kila mtu alibaki anahamaki inawezekanaje wakafanya utafiti / kuweka mtego ebana!... Demu mmoja amenunuliwa na washkaji wanne tofauti usiku mmoja na wote wakalala nao hadi asubuhi. haya ndio maajabu na nguvu ya uchawi.

6. Uchawi unaweza kufunga /vifungo usizae kana kwamba mtu anatumia mifumo ya uzazi wa mpango, huzai hadi utumie dawa au kutegua vifungo vya dawa uliyofungwa nayo hii iko wazi ndio maana dada zetu wanateseka sana leo na ishu za uzazi.

7. Uchawi unaweza kufanya uishi nje ya mwili, nadhani kuna ile elimu ya kuishi nje ya mwili, unaacha mwili umelala kitandani wewe huyooo unaondoka zako kana kwamba umekufa naukayaona mengi ya dunia ukiwa kwenye ulimwengu wa kiroho.

8. Uchawi, nguvu ya uchawi ni moja ya sababu za wana Sayansi wengi kubaini vitu na tabia za vitu flani mf tabia za wanyama na ndege, mf bundi, paka / nyau, mbwa n.k. Wana Sayansi wengi wamekuwa wagunduzi wa mambo hii ilisababishwa na NGUVU za kichawi n.k ila kwa bahati nzuri wakaleta makala za uthibitisho nakuhalalisha kuwa ni kweli lakini baadhi ya mambo tunaambiwa nakuyasoma kwenye Chemistry au biology lakini asili yake ni uchawi.

Ntaendelea....

9. Mafanikio ya kiuchumi ni mamlaka ya pande zote nuru na giza, ukitaka kufanikiwa ni lazima utajihusisha na hasa upande wa huku ukiwa na baraka za nuru kwa hisari au kulazimisha, giza ni kama uchawi au ni uchawi wa namna flan ambao utakupa tips za kiuchumi, zenye uhalisia na bila kuzifata hizo kamwe huwezi kufanikiwa hata kama ukipewa Bilioni 10 leo kesho kutwa tutakukuta hauna hata 100, Pesa tu ina signs and symbols za kichawi, kuna mifumo ya kichawi kwenye mafanikio ya kiuchumi, ndio maana watu wenye mafanikio makubwa huwa na Power flan inaambatana nao zaidi tutakalia kuwaita Freemason / Illuminant n.k lakin ukwelu ni kwamba nguvu na maajabu ga uchawi

Lazima tukubaliane kukoswa maarifa ni kitu kibaya sana, mkoswa maarifa ni sawa na mtu mwenye kukimbia gizani, tafuta maarifa yatayokufaa sawa na hitaji lako, ITAKUSAIDIA

10. Uchawi unaweza kufanya gari mf bus kusafiri mwanza hafi arusha bila mafuta (Petrol) wala (Diesel) hakuna cha (Gas) wala nini, kuna Bus za matajiri haziendi Petrol Station wazee ni nguvu na maajabu ya uchawi, na watu wanatengeneza Pesa.

Naendelea kusema uchawi ni mzuri sana endapo utatumiwa kwenye mifumo ya kimaendeleo nasio kuumiza watu mf kwa kuwaroga wapate matatizo n.k

Uchawi ni sababu ya maendeleo makubwa sana Duniani kote kwani elimu kubwa ya dunua na ulimwengu imejificha huko, uchawi smart wa wavaa suti unaitwa UPAKO, MIUJIZA n.k (nacheka kwa dharau) umewekwa kwenye utakatifu kama miujiza aliyotenda Yesu. Anyway tukidumisha uchawi chanya itasaidia sana, uchawi wa miujiza au upako una matokeo mazuri kwani madhara yake si yakutisha kama ulivyo uchawi wakuharibu, kuangamiza, kujeruhi n.k

Leo tunaona England wamefungua rasmi chuo cha mafunzo ya uchawi hahaha hili wamelifanya kwa kipindi kirefu ki siri siri leo wanaliweka waza, bayana kabisa kila mtu ajue na ashiriki ujue kuna namna hapo.
 
Uchawi ni siri............

Ndio maana utajiri nao ni siri........na siri yenyewe ndio utajiri


Cha ajabu uchawi na uzinzi havipatani kabisa


Na uganga ni elimu ya juu ya uchawi inayoenda against na uchawi


Uchawi ni spiritual ( nafsi) ndio maana mtu anaweza kuwanga mchana kweupe we ukajua anacheza


Cha ajabu ukiwa msiri sana kwenye vitu vyako uchawi hauna nguvu
 
Kwann uchawi kimvuli kina nguvu kuliko object yenyewe....


Ili umdhuru mchawi ni lazma ukiattack kimvuli chake
Kwny elimu ya kchaw kvul huwa mwil halis na mwil halis huwa nothing....


Hivyo uki attack kvul umejeruh mwil wke moja kw moja na maumivu yke n zaid ya mwil sbb wanatumia kvul cha 3 ambcho kna nguvu sn kwny ulmwengu wa kroho au kichaw ( ulimwengu wao wa giza)
 
nyaya za umeme ziligoma kupitisha umeme huko mkoani iringa kijiji kimoja kinaitwa tanangozi kwenye kaburi la mzee kiyeyeu ila baada yazile nguzo kuchepushwa umeme uliendelea kuwaka kama kawaida nadhani waliosoma tosamaganga wanajua vizuri ishu iyo uyo mzee alikua mchawi kufuru uko iringa
Nina rafk angu .... 1 ya wazee wa tanangozi wachaw walioshindkana alikuwa babu yke ....

Wazee wa tanangozi walikuwa kufuru kw uchaw
 
Nina rafk angu .... 1 ya wazee wa tanangozi wachaw walioshindkana alikuwa babu yke ....

Wazee wa tanangozi walikuwa kufuru kw uchaw
Afu kuna mtu anakuja anakwambia uchaw hakuna....... England wameanzisha rasmi vyuo cha mafunzo ya uchawi. India n 1 ya nchi zimeanza rasmi mafunzo ya kichawi hususani kwenye tiba zilzoshndkana ambazo vifungo vyake vmefnyka kichaw il.watoe tiba au wategue kichaw mgonjwa apone ww n nan unabisha Grace glory ...acha ubishi dogo
 
Nataka mtu anifundishe dawa ya biashara ya kupata wateja wengi. Nitalipa
Ukifanikiwa nikumbuke
Mlipu, humbula, nyota nyeupe, kaka kuona, ndege huko mjini mnaita nyangenyange, kivumbasi,mchanga wa sehemu yenye mkusanyiko wa watu wengi, majani saba aina tofauti, damu ya ng'ombe mweupe, chungu, udi ule wa dua unafaa, asali.
Changanya mchanganyiko wako wote kwenye chungu kwa manuizi unayotaka baada ya hapo weka kwenye jua kali choma udi na ubani kwa manuizi jua likianza kuzama kabla ya giza saa 12 kamili peleka kwenye biashara yako kabla hujaiweka unaweza kusafisha kwa chumvi ile pure au chochote ambacho huwa unasafishia. Unaweza kuchimbia au kuweka juu ya duka lako. Kaa usubiri matokeo!
 
Back
Top Bottom