Uchambuzi: Uyahudi alizaa watoto wawili, mkubwa aliitwa Ukristo na mdogo akaitwa Uislam

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,895
Anaandika Robert Heriel,

Ukristo na Uislam ni watoto wa baba mmoja aitwaye Uyahudi.
Licha ya kuwa Ukristo ulitangulia kabla ya Uislam lakini Uislam kwenye ishu ya maadili upo makini zaidi kuliko Ukristo, na dini hizo zote mbili baba yao ni dini ya Kiyahudi (Judaism).

Ukisema Ukristo ni mtoto mtundu au mkaidi aliyegundua mavumbuzi mengi hautokuwa unakosea. Labda kwa vile ni mtoto wa kwanza. Uislam ni lastborn wa Uyahudi ambao umeendelea kushika baadhi ya Falsafa na principles za baba yake.

Dini ni maadili ambayo yamejengwa kwa msingi wa imani. Kuamini katika miungu, lakini lengo kuu la dini ni ishu ya maadili.

Ukristo na Uislam hauwezi kusimama wenyewe bila kutegemea Uyahudi, hiyo haiwezekaniki kwani huyo ndiye baba yao. Hata hivyo kama utatazama kwa jicho lisilo la makengeza, unaweza kuona bila ya shaka kuwa Ukristo unahangaika kujitegemea wenyewe pasipo kufuata misingi ya baba yake Uyahudi.

Licha ya kuwa lastborn Uislam anaonekana kuwa alimpinga na hamtaki baba yake Myahudi lakini ukiangalia mtazamo na falsafa zake bado zinajikita kwa baba yake. Wakati huo Ukristo yeye kwa vile ni firstborn ambaye kisheria ndiye mrithi kwa nje anaonekana kumkubali baba yake Myahudi lakini kimatendo na kifalsafa anampinga baba yake.

Baada ya watoto kukua wanahama na kwenda kuanzisha miji yao. Ukristo boma/mji wake aliuita KANISA
Uislam boma/mji wake akauita MSIKITI. Wakazaliwa watoto, Ukristo ukazaa Wakristo wakati Uislam ukazaa watoto Waislam ambaye babu yao ni Uyahudi.

Falsafa chache za baba Uyahudi ukilinganisha na watoto wake wawili:
1. Mungu ni mmoja,
Ukristo hauamini katika Mungu mmoja isipokuwa mmoja katika utatu Mtakatifu. Baba, mwana, na roho mtakatifu.

Uislam unaungana na Baba yake Uyahudi kuwa Mungu ni mmoja na wapekee asiye na mshirika. Yaani hakuna cha utatu wala upili. Katika falsafa hii Ukristo unapingana na baba yake huku Uislam ukiungana na Baba yake.

2. Mungu ni mtakatifu/msafi
Ukristo: Mtoto huyu anasema kwa mdomo jambo hilo lakini kivitendo anapingana nalo.
Ukristo huweza kumruhusu hata mtu aliyejinyea asimame madhabahuni, mtu mchafu wa mwili na mavazi.

Ukristo mtu huweza kwenda kanisani akaingia na viatu lakini akifika kwake akavua viatu.
Ukristo umejijenga zaidi katika kanuni ya kusafisha ndani zaidi kuliko nje. Lakini umesahau kuwa uchafu unatokea nje kwenda ndani.

Ukristo unaruhusu mtu kula jambo lolote kwa imani, siyo ajabu Ukristo mtu kula nguruwe au panya au mbwa kwa sababu ni kwa imani.

Uislam: Mtoto huyu anasema mdomoni na kutekeleza kwa vitendo. Falsafa na kanuni hizi amezitoa kwa baba yake aitwaye Uyahudi. Mungu ni msafi/mtakatifu na anataka watu wake wawe watakatifu/wasafi.

Uislam umeiga tabia ya baba yake kugawa vitu visafi na vichafu. Kipi chafaa kula na kipi hakifai. Uislam hauwezi kula uchafu.

3. Ndoa na mahusiano.
Ukristo: Mtoto huyu amemuasi baba yake dhahiri shahiri. Uyahudi kuna sheria ya talaka lakini Ukristo kaamua kuiweka kapuni. Hii inafanya watu wawe watumwa kwenye mahusiano yasiyo na tija.

Ikiwa siyo lazima kuwa na mahusiano na Mungu iweje iwe lazima ukioa mke au kuolewa na mume muishi maisha yote? Ndoa ni mkataba wa hiyari kwasababu unahusu upendo. Upendo ni hiyari, kama watu watapishana waachane. Uyahudi unaeleza hivyo, Ukristo hautaki.

Ukristo huyu mtoto kapingana na baba yake. Uyahudi haukatazi mtu kuoa wake wengi, unaruhusu ndiyo maana kunasheria zinazohusu mtu atakayetaka kuoa wake wengi.
Ukristo hautaki na umepinga jambo hilo.

Uislam: Mtoto huyu licha ya kuonekana kama muasi kwa babaye lakini bado anatumia kanuni zilezile za baba yake.
Mtoto huyu anaruhusu Talaka kama kuna mambo yanaenda ndivyo alivyo. Pia mtoto huyu anaruhusu wake wengi ingawaje ameweka kikomo kuwa ni wake wanne.

4. Mavazi
Ukristo: Mtoto huyu anatumia u-firstborn wake vibaya. Ukristo unaruhusu mtu avae atakavyo kwani Mungu haangalii mavazi, anaangalia moyo wa mtu.
Siyo ajabu wafuasi wa Ukristo kuwaona wakivaa nguo zisizo na stara.

Hii ni tofauti na baba yake Uyahudi ambaye alikuwa na sheria za mavazi na kusisitiza watu wavae kwa adabu hasa wanawake wajistiri kutokana na maumbile yao kuwa na ushawishi.

Uislam: Mtoto huyu mwenye madeko ambaye yeye kila kitu lazima aone anaonewa, yeye anaungana na baba yake katika hilo. Uislam unazingatia maadili ya mavazi. Wafuasi wa mtoto huyo wamekuwa wastaarabu/waungwana sana katika hilo.

5. Mwanaume ndiye kuhani.
Ukristo: Ukristo kadiri siku zinavyoenda unazidi kuonyesha kupuyanga na kutumia urithi wa u-firstborn vibaya kama alivyofanya Esau. Ukristo unaruhusu mtu yeyote kuwa kuhani hata kama ni mwanamke. Wakati baba yake Uyahudi jambo hilo kwake kamwe lisingewezekana.

Nafasi ya mwanaume kwenye Ukristo huchukuliwa kuwa sawa na mwanaume. Wakati mzee Uyahudi hilo kwake lilikuwa ni ushetani.

Uislam: Ni kufuru kubwa kwa mtoto wa kike kusimama madhabahuni kuwahutubia wanaume. Hilo uislam alilichukua kama lilivyo na analitekeleza. Uislam umempa nafasi kubwa mwanaume kama ilivyo kwa baba yake Uyahudi.

6. Mungu hakuzaa wala hakuzaliwa.
Ukristo: Unatanabaisha kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, kupitia kwa Bikra Maria aliyepewa mimba kwa uwezo wa roho mtakatifu. Hoja hii ndiyo mzizi wa utatu mtakatifu na wengine hufikia hatua ya juu kabisa kufikiri au kusema Yesu ni Mungu, ilhali hilo kamwe hata kwa akili ya panzi haliwezekaniki.

Baba yao Uyahudi kama ungesikika ukisema maneno hayo, basi ilikuwa umeamua kutaka kuuawa kwa kupiga mawe kwani ungekuwa umekufuru na kufanya dhambi kubwa mno.

Uislam: Mtoto huyu yeye anabaki na msimamo wa baba yake kuwa Mungu hajazaa wala hajazaliwa. Na Hilo ni kosa kubwa la kukufuru.

7. Neema
Ukristo: Ukristo huu ndiyo msingi namba moja yaani huwezi tenganisha Ukristo na neema.
Kwamba mtu akifanya kosa basi anastahili kupewa nafasi ya pili, neema pasipo kuhukumiwa.
Wakati baba yake Uyahudi yeye kanuni yake ni haki. Kwamba mtu akikosea basi aadhibiwe, na mtu akipatia basi apewe zawadi yake (thawabu).

Uyahudi ulijikita kwenye mwili na roho. Wakati Ukristo unajikita katika roho pekee. Hii ni kumaanisha kinachopewa neema ni roho sio mwili. Yaani mtu akiomba neema ya msamaha, basi roho yake ndio ipewe second chance lakini mwili uadhibiwe.

Lakini wafuasi wa Ukristo wakalazimisha kuwa mwili na roho vyote vipewe neema😂😂. Huku wakishikilia kanuni isemayo usihukumu usije ukahukumiwa au samehe saba mara sabini. Wakisahau kuwa mwili ndio unafanya makosa wakati huo roho ndiyo hufanya dhambi😂😂. Mwili huadhibiwa na dunia kwa makosa yake wakati huohuo roho huadhibiwa na Mungu kwa dhambi zake.

Uislam: Mtoto huyo yeye kafuatisha kwa kiasi kikubwa kanuni na sheria na falsafa za baba yake. Mwenye makosa aadhibiwe kulingana na makosa yake na vile sheria zisemavyo.

Zingatia, binadamu hawezi kusamehe dhambi isipokuwa Mungu. Ila anasemehe makosa kwa sababu ya mwili ndiyo hufanya makosa na roho ndiyo itendayo dhambi. Kumaanisha, roho ndiyo inamuasi Mungu halafu mwili unamfanyia makosa binadamu mwenzako au kiumbe au mazingira yanayokuzunguka.

8. Hukumu
Ukristo: Mtoto huyu anajieleza kuwa atakayehukumu ulimwengu ni Kristo/Yesu.
Na Yesu ndiye atakuwa mtawala wa kila kitu. Hii ni tofauti na falsafa ya baba mtu Uyahudi. Yeye anajua Mungu ndiye mtawala na ndiye atakayehukumu viumbe vyake kwa haki. Zingatia neno viumbe inamaanisha vinavyoonekana na visivyoonekana. Hata Yesu pia ni kiumbe.

Uislam: Huyu mtoto anaungana na baba yake Uyahudi kwa kusema, hukumu atakayoitoa ni Mungu. Na kila kiumbe atahukumiwa kulingana na yale aliyoyafanya.

9. Urithi na mirathi
Ukristo: Umejikita zaidi katika mambo ya kiroho na kusahau mambo ya kimwili. Ukristo unajikita katika urithi wa Ufalme wa mbinguni pekee. Ilhali baba yake akijikita kwa yote mawili.
Uyahudi ilitoa utaratibu wa namna ya kurithisha mali kwa haki, na namna ya kutoa mirathi endapo mtu atakufa.

Ukristo jambo hilo limeachwa liamuliwe kidunia, hapohapo dunia kwa mujibu wa Ukristo inaongozwa na shetani😂😂. Unaona mambo hayo!

Uislam: Mtoto huyu kamuiga baba yake na kuongeza baadhi ya vitu. Kajikita kiroho na kimwili.
Urithi na mirathi kwa uislam imefafanuliwa namna itakavyogawiwa. Uislam haujaliacha jambo hilo liamuliwe na walimwengu kwani shetani ndiye mlimwengu mwenyewe.

Mpaka hapo sina la ziada, siyo kazi yangu kukuambia kipi chakuamini au kipi ni sahihi na kipi sio sahihi. Nilikuwa naeleza habari za watoto hao wawili wenye wafuasi wengi.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
Braza angu alinipa hadithi ya Yacobo na Yusuph nikiwa chalii tukisubiri gemu za Uefa nilimuelewa sana akasema hao ni ndugu na hata hapa unaona wanatofautiana sana ni kwa kuwa wengi hawana uelewa wa hizi dini zetu wamekaririshwa kuchukiana wakati ni ndugu moja...baadae nikafatilia kwenye Biblia nikakuta ni kitu kile kile hata mitume wengi ni wale wale...
 
Braza angu alinipa hadithi ya Yacobo na Yusuph nikiwa chalii tukisubiri gemu za Uefa nilimuelewa sana akasema hao ni ndugu na hata hapa unaona wanatofautiana sana ni kwa kuwa wengi hawana uelewa wa hizi dini zetu wamekaririshwa kuchukiana wakati ni ndugu moja...baadae nikafatilia kwenye Biblia nikakuta ni kitu kile kile hata mitume wengi ni wale wale...
Uongo! Hapo Yakobo na Yusuf ni nani Muislim? Unamaanisha Yusuf yupi?
 
2. Mungu ni mtakatifu/Msafi
Ukristo; mtoto huyu anasema Kwa mdomo
Jambo Hilo lakini kivitendo anapingana nalo.
Ukristo huweza kumruhusu hata mtu aliyejinyea asimame madhabahuni, mtu mchafu WA mwili na mavazi,
Ukristo mtu huweza kwenda kanisani akaingia na viatu lakini akifika kwake akavua viatu.
Kama Mungu angekuwa anaangalia usafi wa mavazi huko kanisani tungetoboa wengi kweli kweli....kibaya Zaid Mungu huyo huyo anasema anasema anaangalia umebeba Nini Moyoni mwako.
#Mnatuchanganya na tafsiri zenu
 
Na wengine hufikia hatua ya juu kabisa kufikiri au kusema Yesu ni Mungu ilhali Hilo kamwe hata Kwa akili ya Panzi haliwezekaniki
Roho zidanganyazo zimekupata. Nadhani utakuwa umetembelewa na jibril. Uwe makini maana jibril alimkaba muhammad kule mapangoni hadi akarudi kwa Khadija akiomba afunikwe na mablanketi.

Jibril alikuwa anamlazimisha asome kitabu. Alikuwa hajui kama Muhammad alikuwa illiterate? Hicho kitabu ni kipi hasa wakati quran haikuwepo?

Yesu Kristo ndiye Mungu wa milele, muumba wa mbingu na nchi na vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.
 
Kama Mungu angekuwa anaangalia usafi wa mavazi huko kanisani tungetoboa wengi kweli kweli....kibaya Zaid Mungu huyo huyo anasema anasema anaangalia umebeba Nini Moyoni mwako.
#Mnatuchanganya na tafsiri zenu


Mungu anaangalia kila resources aliyokupatia😂😂
Mwili, akili, hisia, roho, Mali, n.k.

Ni mtu mjinga pekee anayeweza kufikiri kuwa Mungu anaangalia roho pekee yake.
 
UCHAMBUZI; UYAHUDI ULIZAA WATOTO WAWILI; MKUBWA ALIITWA UKRISTO, ALAFU YULE MDOGO AKAITWA UISLAM.

Anaandika, Robert Heriel

Ukristo na uislam ni watoto wa Baba mmoja aitwaye Uyahudi.
Licha ya kuwa Ukristo ulitangulia kabla ya Uislam lakini Uislam kwenye ishu ya maadili upo makini zaidi kuliko Ukristo. na dini hizo zote mbili Baba Yao ni Dini ya Kiyahudi (Judaism).

Ukisema Ukristo ni mtoto mtundu au mkaidi aliyegundua mavumbuzi mengi hautokuwa unakosea. Labda Kwa vile ni mtoto wa Kwanza.
Uislam ni Lastborn wa Uyahudi ambao umeendelea kushika baadhi ya Falsafa na principles za Baba yake.
Dini ni maadili ambayo yamejengwa Kwa msingi wa Imani. Kuamini katika miungu.
Lakini lengo kuu la dini ni ishu ya maadili.

Ukristo na uislam hauwezi kusimama wenyewe bila kutegemea Uyahudi hiyo haiwezekaniki kwani huyo ndiye Baba Yao. Hata hivyo Kama utatazama Kwa jicho lisilo la makengeza unaweza kuona bila ya Shaka kuwa Ukristo unahangaika kujitegemea wenyewe pasipo kufuata misingi ya Baba yake Uyahudi.

Licha ya kuwa Lastborn Uislam anaonekana kuwa alimpinga na hamtaki Baba yake Myahudi lakini ukiangalia mtazamo na falsafa zake bado zinajikita Kwa Baba yake.
Wakati huo Ukristo yeye Kwa vile ni Firstborn ambaye kisheria ndiye mrithi Kwa nje anaonekana kumkubali Baba yake Myahudi lakini kimatendo na kifalsafa anampinga Baba yake.

Baada ya watoto kukua wanahama na kwenda kuanzisha miji Yao.
Ukristo Boma/mji wake aliuita KANISA
Uislam Boma/ mji wake akauita MSIKITI
Wakazaliwa watoto, Ukristo ukazaa Wakristo wakati Uislam ukazaa watoto Waislam ambaye Babu Yao ni Uyahudi.

Falsafa chache za Baba Uyahudi; ukilinganisha na watoto wake wawili,
1. Mungu ni mmoja,
Ukristo hauamini katika Mungu mmoja isipokuwa Mmoja katika utatu Mtakatifu. Baba, mwana, na roho mtakatifu.

Uislam unaungana na Baba yake uyahudi kuwa Mungu ni mmoja na wapekee asiye na mshirika. Yaani hakuna cha utatu wala upili.
Katika falsafa hii Ukristo unapingana na Baba yake huku Uislam ukiungana na Baba yake.

2. Mungu ni mtakatifu/Msafi
Ukristo; mtoto huyu anasema Kwa mdomo
Jambo Hilo lakini kivitendo anapingana nalo.
Ukristo huweza kumruhusu hata mtu aliyejinyea asimame madhabahuni, mtu mchafu WA mwili na mavazi,
Ukristo mtu huweza kwenda kanisani akaingia na viatu lakini akifika kwake akavua viatu.
Ukristo umejijenga zaidi katika kanuni ya Kusafisha ndani zaidi kuliko nje. Lakini umesahau kuwa uchafu unatokea nje kwenda ndani.

Ukristo unaruhusu mtu Kula Jambo lolote Kwa Imani, sio ajabu Ukristo mtu Kula nguruwe au panya au Mbwa Kwa sababu ni Kwa Imani.

Uislam; mtoto huyu anasema mdomoni na kutekeleza Kwa vitendo.
Falsafa na kanuni hizi amezitoa Kwa Baba yake aitwaye Uyahudi.
Mungu ni Msafi/mtakatifu na anataka watu wake wawe watakatifu/wasafi.

Uislam umeiga tabia ya Baba yake kugawa vitu visafi na vichafu. Kipi chafaa Kula na kipi hakifai. Uislam hauwezi Kula uchafu.

3. Ndoa na mahusiano.
Ukristo; Mtoto huyu amemuasi Baba yake dhahiri shahiri. Uyahudi kuna sheria ya Talaka lakini Ukristo kaamua kuiweka kapuni. Hii inafanya Watu wawe watumwa kwenye mahusiano yasiyo na tija.
Ikiwa sio lazima kuwa na mahusiano na Mungu iweje iwe lazima ukioa mke au kuolewa na mume muishi maisha yote. Ndoa ni mkataba WA hiyari Kwa sababu unahusu Upendo. Upendo ni hiyari. Kama watu watapishana waachane. Uyahudi inaeleza hivyo.
Ukristo hautaki.

Ukristo huyu mtoto kapingana na Baba yake. Uyahudi haukatazi mtu kuoa wake wengi, unaruhusu ndio maana kunasheria zinazohusu mtu atakayetaka kuoa wake wengi.
Ukristo hautaki na umepinga Jambo hilo.

Uislam; mtoto huyu licha ya kuonekana Kama muasi Kwa Babaye lakini bado anatumia kanuni zilezile za Baba yake.
Mtoto huyu anaruhusu Talaka Kama kuna mambo yanaenda ndivyo alivyo.
Pia mtoto huyu anaruhusu Wake wengi ingawaje ameweka kikomo kuwa ni Wake wanne.

4. Mavazi
Ukristo; mtoto huyu anatumia U-Firstborn wake vibaya.
Ukristo unaruhusu mtu Avae atakavyo kwani Mungu haangalii mavazi anaangalia moyo wa mtu.
Sio ajabu wafuasi WA Ukristo kuwaona wakivaa nguo zisizo na stara.
Hii ni tofauti na Baba yake Uyahudi ambaye alikuwa na sheria za mavazi na kusisitiza watu wavae Kwa adabu hasa wanawake wajistiri kutokana na maumbile Yao kuwa na ushawishi.

Uislam; mtoto huyu mwenye madeko ambaye yeye kila kitu lazima aone anaonewa, yeye anaungana na Baba yake katika Hilo. Uislam unazingatia maadili ya mavazi. Wafuasi wa mtoto huyo wamekuwa wastaarabu/waungwana Sana katika Hilo.

5. Mwanaume ndiye Kuhani.
Ukristo; Ukristo kadiri siku zinavyoenda unazidi kuonyesha kupuyanga na kutumia Urithi wa U-Firstborn vibaya Kama alivyofanya Esau.
Ukristo unaruhusu mtu yeyote kuwa Kuhani hata Kama ni Mwanamke.
Wakati Baba yake Uyahudi Jambo hilo kwake kamwe lisingewezekana.

Nafasi ya mwanaume kwenye Ukristo huchukuliwa kuwa Sawa n mwanaume. Wakati Mzee Uyahudi Hilo kwake lilikuwa ni ushetani.

Uislam; ni kufuru kubwa Kwa mtoto wa kike kusimama madhabahuni kuwahutubia Wanaume. Hilo uislam alilichukua Kam lilivyo na analitekeleza.
Uislam Umempa nafasi kubwa Mwanaume Kama ilivyo Kwa Baba yake Uyahudi.

6. Mungu hakuzaa wala hakuzaliwa.
Ukristo; unatanabaisha kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, kupitia Kwa Bikra Maria aliyepewa mimba Kwa uwezo wa roho mtakatifu.
Hoja hii ndio mzizi wa Utatu mtakatifu.
Na wengine hufikia hatua ya juu kabisa kufikiri au kusema Yesu ni Mungu ilhali Hilo kamwe hata Kwa akili ya Panzi haliwezekaniki.
Baba Yao Uyahudi kama ungesikika ukisema maneno hayo, basi ilikuwa umeamua kutaka kuuawa Kwa kupiga Mawe kwani ungekuwa umekufuru na kufanya dhambi kubwa mno.

Uislam; mtoto huyu yeye anabaki na msimamo wa Baba yake kuwa Mungu hajazaa wala hajazaliwa. Na Hilo ni kosa kubwa la kukufuru.

7. NEEMA.
Ukristo; Ukristo huu ndio msingi namba moja yaani huwezi tenganisha Ukristo na Neema.
Kwamba mtu akifanya kosa basi anastahili kupewa Nafasi ya pili, neema pasipo kuhukumiwa.
Wakati Baba yake Uyahudi yeye kanuni yake ni HAKI. Kwamba mtu akikosea basi aadhibiwe, na mtu akipatia basi apewe zawadi yake(Thawabu).
Uyahudi ulijikita kwenye Mwili na roho. Wakati Ukristo unajikita katika Roho pekee.
Hii ni kumaanisha kinachopewa Neema ni Roho sio Mwili.
Yaani mtu akiomba neema ya Msamaha, basi Roho yake ndio ipewe Second chance lakini mwili uadhibiwe.
Lakini Wafuasi WA Ukristo Wakalazimisha kuwa mwili na roho vyote vipewe neema. Huku wakishikilia kanuni isemayo Usihukumu usije ukahukumiwa au samehe Saba mara sabini. Wakisahau kuwa mwili ndio unafanya makosa wakati huo roho ndio hufanya dhambi
Mwili huadhibiwa na Dunia Kwa makosa yake wakati huohuo roho huadhibiwa na Mungu Kwa dhambi zake.

Uislam; mtoto huyo yeye kafuatisha Kwa kiasi kikubwa kanuni na sheria na falsafa za Baba yake. Mwenye makosa aadhibiwe kulingana na makosa yake na vile sheria zisemavyo.

Zingatia, Binadamu hawezi kusamehe Dhambi isipokuwa Mungu. Ila anasemehe makosa Kwa sababu ya Mwili ndio hufanya makosa na roho ndiyo itendayo dhambi. Kumaanisha Roho ndio inamuasi Mungu alafu mwili unamfanyia makosa binadamu mwenzako au kiumbe au Mazingira yanayokuzunguka.


8. Hukumu
Ukristo; mtoto huyu anajieleza kuwa atakayehukumu ulimwengu ni Kristo/Yesu.
Na Yesu ndiye atakuwa Mtawala wa kila kitu. Hii ni tofauti na Falsafa ya Baba mtu Uyahudi yeye anajua Mungu ndiye Mtawala na ndiye atakayehukumu viumbe vyake Kwa haki. Zingatia neno viumbe inamaanisha vinavyoonekana na visivyoonekana. Hata Yesu pia ni Kiumbe.

Uislam; huyu mtoto anaungana na Baba yake Uyahudi Kwa kusema Hukumu atakayoitoa ni Mungu. Na kila kiumbe atahukumiwa kulingana na Yale aliyoyafanya.

9. Urithi na mirathi.
Ukristo; umejikita zaidi katika mambo ya kiroho na kusahau mambo ya kimwili. Ukristo unajikita katika Urithi wa ufalme wa mbinguni pekee. Ilhali Baba yake akijikita Kwa yote mawili.
Uyahudi ilitoa utaratibu wa namna ya kurithisha Mali Kwa haki, na namna ya kutoa mirathi endapo mtu atakufa.
Ukristo Jambo hilo limeachwa liamuliwe kidunia, hapohapo dunia Kwa mujibu wa Ukristo inaongozwa na Shetani. Unaona mambo hayo.

Uislam; mtoto huyu kamuiga Baba yake na kuongeza baadhi ya vitu. Kajikita kiroho na kimwili.
Urithi na mirathi Kwa uislam imefafanuliwa namna itakavyogawiwa. Uislam haujaliacha Jambo Hilo liamuliwe na walimwengu kwani Shetani ndiye Mlimwengu Mwenyewe.

Mpaka hapo sina la ziada, sio kazi yangu kukuambia kipi chakuamini au kipi ni sahihi na kipi sio sahihi.
Nilikuwa naeleza habari watoto hao wawili wenye wafuasi wengi.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Chapisho lako linatafakarisha, kwa maana nyingine First born kamuasi Baba yake (kapotea)
 
Roho zidanganyazo zimekupata. Nadhani utakuwa umetembelewa na jibril. Uwe makini maana jibril alimkaba muhammad kule mapangoni hadi akarudi kwa Khadija akiomba afunikwe na mablanketi.

Jibril alikuwa anamlazimisha asome kitabu. Alikuwa hajui kama Muhammad alikuwa illiterate? Hicho kitabu ni kipi hasa wakati quran haikuwepo?

Yesu Kristo ndiye Mungu wa milele, muumba wa mbingu na nchi na vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.

Usikufuru.
Vitu Kama huvielewi omba Muongozo.
Akili ndio upo mahususi Kwa ajili ya kutafakari na kuelewa. Weka hisia na ushabiki pembeni
 
Huyo Robert sio mkristo, ni jamaa fulani anayejipendekeza kwenye ukristo.
Wewe majamaa kumbe mfia dini kiasi hiki kivipi umtoe Taikon ROBERT HERIEL kwenye ukiristo ?wakati huyu mwamba anaboshana sana na Kisai katika kutetea ukiristo vilevile ana nyuzi kibao ambazo positive kuhusu ukiristo kuna Moja alisema "Bila ukiristo Dunia ingekuwa kitu cha upuuzi " humo ndani kapamba ukiristo na influence za ukiristo duniani mpaka kapitiliza.

Kwako Maghayo una kauli ipi baada ya champions kumtoa Taikon kwenye ukiristo kisa kupinga YESU SIO MUNGU ?

Kwako DJ mlete Maghayo mlete Maghayo ..
 
Back
Top Bottom