Uchaguzi Serikali za Mitaa 2014: Matokeo kutoka nchi nzima (TZ Bara)

Wadau kwa matokeo yanayoendelea kutangazwa ya serikali za mitaa,vijiji,na vitongoji inanipa picha kwamba suala la upinzani kwa Watanzania bado halijawaingia kabisa.kwani Pamoja na mazonge yoote yaliyoikumba serikali ya CCM hivi karibuni hasa hili suala la ESCROW nilitegemea kwa uchaguzi huu mdogo tu, Wananchi wangekuwa nahasira na CCM na Serikali yake, lakini kwa matokeo haya inaonekana wapinzani Hasa Chadema kuna mahali wanakosea, na wasipoangalia kuingia madarakani itakuwa ni sawa na jua kuchomoza Magharibi na kuzama Mashariki. na naimani 2015 Hali kwa upinzani itakuwa ngumu sana kama hawatabadilika toka walipo sasa kwani kuna vitu muhimu wanakosa.Niko mkoani Morogoro Mitaa,vijiji na Vitongoji vyote Wamechukua chama Tawala CCM.nahitimisha kwa kusema wapinzani Badirikenikama mnatakamfike mnakotakana sasa muende kwa raia na Hoja zenye Mashiko.
Labda kitongojini kwako. Sehemu nyingi chadema wamechukua. Kilakala chadema, bigwa chadema Bong`ola chadema ccm imeshinda wapi?
 
Mleta mada Magazetini hebu weka updates hapo juu...

Mengi ya yanayowekwa humu si matokeo rasmi, maana mtu akipita mtaani na kukuta wanachama wa cdm au ccm wakishangilia anasema kuwa wameshinda. Nadhani matokeo ya kuwekwa hapo juu ni yale yatakayotangazwa na mamlaka husika
 
Last edited by a moderator:
CCM 8, ACT 8, CHADEMA 2 and ADC 1 ndio matokeo ya Mji Mdogo wa Mwandiga. Ili kupata Meya inabidi CHADEMA na ADC waunge mkono ACT. Je CHADEMA watapiga kura na ACT?

Mzee huu ni uchaguzi wa serikali za mitaa, swala la umeya wa mji ni mwakani wakati wa uchaguzi mkuu ambapo madiwani pia watachaguliwa!


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Ifakara kati ya vitongoji 35.CCM imepata vitongoji3 CHADEMA vitongoji 31 kituo kimoja matokeo bado.
 
Kitongoji Nyakashansha B, Kijiji Bushasha, Kata Kishanje (Bukoba Vijijini) ....Chadema/UKAWA imeshinda
Nyakashansha A...CCM imeshida...kunauwezekano UKAWA wakaongeza vitongoji vingine mchuano ulikuwa mkali...huko Kabitego na Buyumba
 
Mzee huu ni uchaguzi wa serikali za mitaa, swala la umeya wa mji ni mwakani wakati wa uchaguzi mkuu ambapo madiwani pia watachaguliwa!


Sent from my iPad using JamiiForums

Hahahaah,,,,,huyo anayeleta habari za umeya sasa katokea wapi???
 
Back
Top Bottom