Uchaguzi Serikali za Mitaa 2014: Matokeo kutoka nchi nzima (TZ Bara)

Safi sana watani zang wasukuma, sisi wagogo nasi ndio mwaka huu tumeanza kuamka usingizini i hope tutawafuata huko msitutusi jaman haya mambo yanahtaji kauelewa kadogo ambako nasi tumeanza kukapata siku hz kupitia vjana wetu
 
Wana Bodi
nahitaji kufahamishwa matokeo ya uchaguzi wa s/mitaa upande wa Ubungo-mwisho hadi Kimara
 
Mtu mwenye akili timamu zama hizi za magumashi huwezi kusoma MZALENDO NA UHURU na mkono wa pili huwezi kusoma TANZANIA DAIMA na MAWIO.Tusome magazeti huru.
 
Matokeo serikali za mitaa Arumeru Mashariki 2014.

MAMLAKA YA MJI MDOGO USARIVER(JUMLA YA MITAA 9) CHADEMA 5 CCM 4.

Jumla ya vijiji 89,halali Uchaguzi ni 75,venye pingamizi na utata wa matokeo 14,CDM 34 na CCM 41.

Vitongoji jumla 308 vilivyofanya uchaguzi halali ni 268,venye pingamizi na utata wa matokeo 40,CDM 112, CCM 156.

Ikumbukwe kabla ya uchaguzi huu vijiji vyote vilikuwa ni Vya CCM na vitongoji chadema tulikuwa na 7 tu.
Vilevile jimbo hili madiwani wote 23 ni wa ccm. Hakuna hata mmoja wa upinzani.

Pia watia nia wa ubunge kupitia ccm wote waliongoza kampeni.
Hivyo ccm ilikuwa na timu ya kutosha ya kampeni tofauti na chadema iliyoongozwa na Mbunge Nassari pekee.

Katibu wa chadema meru.



DONDOO MUHIMU.

Kijiji cha Samaria Anakotoka katibu wa ccm Wilaya ya Meru Ndg Langael Akyoo CHADEMA imeshinda kijiji na vitongoji vyote.

Kata ya na Kijiji anakotoka katibu mwenezi wa ccm Wilaya ya Meru Ndg Aenea Kitomari CHADEMA imeshinda vijiji vyote vitatu an vitongoji vyote.

Kata ya maji ya chai anakotoka katibu wa fedha na uchumi wa ccm Wilaya Wakili Dr Daniel Pallangyo CHADEMA imeshinda vijiji vyote 7, kata hii Ina madiwani watatu wa ccm (diwani wa kata Ndg Loti Nnko, Frida Kaaya na Mambisse) na hapa pia anatoka Makamu mwenyekiti was halmashauri ya Meru Frida Kaaya.
Diwani wa kata hii pia aligombea uenyekiti wa kijiji cha Ngongongare na CHADEMA ikashinda kwa kishindo.

Kata ya Songoro anakotoka Mbunge wa Jimbo Mhe Joshua Nassari CHADEMA imeshinda vijiji vinne na ccm viwili.
 
kama hata jimboni kwa lissu au kilombero wasimamizi wamesema ccm imepata asilimia 70 basi wanaogopa kufukuzwa kama wenzao
haa haa, hao watendaji wanamfurahisha mfalme huku amekaa uchi. Nimeamini ccm inaangushwa na watendaji kama hao!
 
Hakuna gazeti linalouza kama Mawio kwa sasa. Wanatoa copy nyingi na zinaisha kabla ya mzungiko. Ni gazeti la week nzima Kumbuka. Serikali za mitaa tukija kupiga Mahesabu vizuri utakuta CHADEMA wana 60% vs 40% za CCM. Ila kwa sababu wao ndo wasemaji wanatulisha matango. Ukweli tunao vichwani na CCM wamebaki na propaganda tu hawana lingine la kushawishi wananchi. Sasa huu ni mwanzo. Mtadanganya sana. Mara tunaongea na wazee, mara Jumatatu. Kwishne. Rudisheni na hela zetu kwanza.
haa haa mkuu nimegundua Tamisemi wanapika data. Usishangae wakasema kwamba kule kwa lissu ccm imeshinda kwa kishindo.
 
Huo ni ukweli usiopingika. Naomba walio na matokeo watupe idadi ya kura za CCM na za Ukawa/Chadema ukiacha sehemu ambazo CCM wamejipitisha bila kupingwa.
 
mkuu. ngurati naomba unieleweshe kuhusu haya mapingamizi.
_nijuavyo mimi kama nilivyoona kwenye ubunge mgombea akiwekewa pingamizi huwa linaamuliwa kabla ya siku ya kupiga kura,je haya utaratibu ulikuweje maana nchi nzima waliowekewa pingamizi ni wa ukawa tu na sikusikia ukawa wakiwekea wa ccm?
ninasubiri jibu
 
Last edited by a moderator:
Mangamba pole yao sana. Mimi naamini kitu kimija tu kama maisha ya kiumbe hai yanamwisho iweje chama tu na tena CCM kisiwe na mwisho Tz???

Tatizo la hawa wa Tz wenzetu wa mangamba ni wanakiburi sana na hiyo yote ni kwa sababu ya wao kujiaminisha kuwa hakuna akiye juu yao. Hope for this watakuwa wamejifunza kitu

ccm hawajui kujifunza na hawawezi kujifunza ndio maana wakina nape wanabishana na facts kitu ambacho sio logical kwa chama kama ccm,wanapenda kujiona wazima hata kama ni mahuthuti.
 
Hongera sasa ndogo janja Mhe. Joshua Nassari kazi yako imeonekana dhahiri. Usibweteke na huu ushindi, huu uwe mwanzo wa maandalizi ya uchaguzi mkuu, tunataka 2015 madiwani wote wa Halmashauri ya Arumeru Mashariki watoke CDM.

Tumeanza na Mungu tutamaliza na Mungu, IshaAllah
 
Huu uzi kama kina Laki si Pesa, Msalani na magamba wengine watatia timu, Nawaruhusu kina Modes mnipige ban.
 
Kwa mujibu wa takwimu za matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa zilizotangazwa na TAMISEMI kupitia TBC1 eti CCM wameshinda kwa 70% ya matokeo yaliyokuwa tayari hadi siku ya jumanne kwa IKUNGI huko Singida.
 
Back
Top Bottom