Uchaguzi Serikali za Mitaa 2014: Matokeo kutoka nchi nzima (TZ Bara)

Nimegundua hawa watu wa Tamisemi wahuni sana,wanaongea in general kiasi kwamba mtu wa kawaida ataona CCM wameshinda sana na kwa kila sehemu mfano ni matokeo ya Muleba,wameona wakitangaza kwa Tiba peke yake (kus) itaonekana wamekula mweleka ndo wakaona bora wachanganye ya (kus+kas) ili ionekane wameshinda sana,kwahiyo walitangaza ya jumla ya wilaya nzima ila si kwa majimbo moja moja kama ilivyo.Binafsi,nashauri kurugenzi ya habari ihitishe press ili nayo ifanye marekebisho kwa kutangaza upya matokeo huku wakionesha wazi maeneo kama ni mtaa,kitongoji ama kijiji ambako Cdm/Ukawa wameshinda.Mfano matokeo ya Tamisemi hayaoneshi kama Lissu kashinda kitu ambacho watu wanatakiwa kupewa ukweli harisi ili Cdm/Ukawa itendewe haki yake.cc:Kurugenzi ya Habari
 
Mara nyingi nimekuwea nikiangalia meza za magazeti na kuangalia gazeti gani linabaki kwa muda mrefu naona mawio ni mojawapo ya gazeti ambalo haliuziki. Jana nimegundua sababu kuu ya kwa nini haliuziki..Kwa sababu linaandika uongo mtupu..Limeandika CCM aibu tupu ati wapinzani wameata asilimia 38. lakini wasimamizi wa uchaguzi kila wilaya wanasema ccm imeshinda kwa zaidi ya asilimia 70 sasa ukifanya wastani tu utaona bado ccm imepata ushindi mnono lakini kwa kuwa mawio wanataka kuwalisha watu uongo wameamua kufanya propaganda hizo ambazo kwa kiwango kikubwa zinaua soko la gazeti lao

Hongera,kama umeweza kupitia meza za magazeti Tanzania nzima na kufanya hitimisho lako hilo,umetisha.
CCM inamuhitaji aliyekua msemaji wa Serikali ya Sadam Hussein awasaidie.
 
Hongera,kama umeweza kupitia meza za magazeti Tanzania nzima na kufanya hitimisho lako hilo,umetisha.
CCM inamuhitaji aliyekua msemaji wa Serikali ya Sadam Hussein awasaidie.

Ungenunua gazeti ukasoma ungalipata kilichoandikwa ki ufasaha . Maisha bora haya unashindwaje kununua gazeti?
 
Mbona walikuwa wanamsifu sana ndovu na vuvulela kuwa wamejenga sana chama?afadhali wangemwacha mzee mkama
 
nilijua lazima canimito atajibu. Msemaji tunaye na anaitwa Nape. Aliyekua msemaji wa sadam hussein alikuwa muong kama mawio hivyo hatumhitaji. Tunataka wale wasema kweli na kweli tupu bila kuegemea upande wowote..lakini ninyi mawio kwa hili mmeegemea chadema..au mmeahidiwa uwaziri wa habari kama sahaf
Hongera,kama umeweza kupitia meza za magazeti Tanzania nzima na kufanya hitimisho lako hilo,umetisha.
CCM inamuhitaji aliyekua msemaji wa Serikali ya Sadam Hussein awasaidie.
 
haikuwa propaganda yeye alizungumza ukweli ninyi mmezungumza uongo tofauti na wakurugenzi wanaotoa matokeo rasmi.
Na Nape aliyetoa matokeo kuwa ccm wamepata 85% hata kabla vituo vingine havijahesabu kura, haikuwa propaganda?
 
tembelea tovuti ya tamisemi tafuta chaguzi za serikali za mitaa halafu bofya matokeo ya jumla utayapata
hebu tupe ukweli wa matokeo yote nchi nzima maana nape alisema ni 84% hapo wewe umesema zaidi ya asilimia 70 nisaidie kujua ukweli maana mawio wamesema wapinzani wameshinda asilimia 38 wewe umepinga.
 
kibwaso jimboni kwa lissu hakuna tofauti na jimboni kwa dewji hukohuko singida.tofauti ni kuwa kwa lissu ccm tumeweza kupenya na kupata imani ya watu lakini singida mjini chadema hawakufurukuta
kama hata jimboni kwa lissu au kilombero wasimamizi wamesema ccm imepata asilimia 70 basi wanaogopa kufukuzwa kama wenzao
 
hata tukienda kwenye real votes bado tumewabwaga kwa mbali sana. na unachofanya kwa upogo wako kwanza umenilisha maneno ambayo mimi sikusema kuwa nimechukua matokeo ya pingamizi lakini pili ni wazi kuwa hata ukiletewa jedwali la matokeo bado hutakubali. Ila ifike mahali tuiite beleshi kwa jina lake tusiweke ushabiki wa chadema mbele. Kubalini kuwa bado hamjakomaa na mnatakiwa mjipange hasa.
Tafsiri ya matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa inategemea utashi wa mtu. Mfano wewe umeamua kuchukua Yale matokeo yenye pingamizi pamoja na kupita bila kupingwa, ambayo kwa ufasaa sio matokeo ya uchaguzi kwa kuwa uchaguzi haukufanyika. Ila ukijitoa upogo Wako na kuangalia matokeo halisi yaani kura zilizopigwa, real votes, utagundua kuwa ccm ilipata chini ya asilimia sitini. Ila kama mnataka kujifariji na matokeo ya nje ya sanduku la kura mkidhani hata mwakani mtapata, uwanja ni wenu.
 
bila ubishi ccm wenyewe wamekili kua sasa tsunami inakuja japo wamefanya mizengwe na fitina kupita kiasi ila nchi wataiachia tu tukomae jamani
 
Safi sana watani zang wasukuma, sisi wagogo nasi ndio mwaka huu tumeanza kuamka usingizini i hope tutawafuata huko msitutusi jaman haya mambo yanahtaji kauelewa kadogo ambako nasi tumeanza kukapata siku hz kupitia vjana wetu
Wapi hasa mme anza kuamka?
 
116 Reactions
Reply
Back
Top Bottom