Uchaguzi Serikali za Mitaa 2014: Matokeo kutoka nchi nzima (TZ Bara)

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kijiji cha Nyansurura Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara, kimechukua maamuzi magumu ya kuiadabisha CCM na vibaraka wao kupitia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka huu. Katika Uchaguzi huo uliogubikwa na mizengwe mingi toka kwa Viongozi waandamizi wa Serikali hasa wale waliokuwa na dhamana ya usimamizi wa Uchaguzi huo baada ya kusoma upepo wa kuangukia pua kwa CCM, hata ikapelekea kuahirishwa zoezi la Uchaguzi Tarehe 14/12/2014 hadi 16/12/2014. Siku ya Uchaguzi Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo: Mwenyekiti wa Kijiji:Francis Garatwa Muhingira (CHADEMA), Kitongoji cha Mto Mara:Mseti Mwikwabe Mseti (CHADEMA), Kitongoji cha Nyabichine:Werema Ngocho Ndera (CHADEMA), Kitongoji cha Matanka (CCM bila kupingwa). Wajumbe wote wa 12 Halmashauri ya Kijiji (CHADEMA), mmoja wa NCCR-Mageuzi na Wajumbe wote 8 wa Viti Maalum (CHADEMA). Maeneo mengine yaliyofanya vizuri ni:Kebancha, Sogoti, Machochwe, Gesarya, Rung'abure, Nyamerama, Nyamoko, Mugumu mjini n.k Piiiiipoooozz...

Chadema imefanya vizuri sana maeneo ya Bukoba Musoma Shinyanga Mwanza shinyanga,Manyara kuliko huko arusha na moshi haya ni mambo ya siasa sio ukabila . Kama wapizani wa ukawa watatumia dini na ukabila watashindwa vibaya maana hoja hiyo inajijibu yenyewe. Ni vizuri tukawaunganisha watanzania kuliko kuwagawa.Watanzania wanatofautina kiwango cha umasikini si tamaduni
 
Akiyataja maeneo ya Miji midogo ambayo CHADEMA imeshinda, Dr. Slaa amesema "1. Nkasi - Namanyere 2. Hai - Bomang'ombe. 3.Karatu - Karatu. 4. Arumeru Mashariki - Usa river. 5.Vunjo - Ukawa. 6. Mbeya vijijini - Mbalizi. 7. Mbozi Maghari - Tunduma. 8. Mbozi Mashariki - Mlowo. 9. Kyela - Kyela. 10. Lupa - Makongorosi. 11. Busanda - Katoro. 12. Geita - Geita. 13. Chato - Chato. 14. Kwimba - Ngudu. 15. Karagwe - Kayanga. 16. Bukombe - Ushirombo. 17. Sengerema - Sengerema. 18. Tarime - Tarime. 19. Tarime - Sirari mji mdogo. 20. Rorya - Shirati ( 7/2). 21. Bunda - Bunda. 22. Serengeti - Mugumu 10/10 ( CUF 3). 23. Kahama - Kahama. 24. Bariadi - Bariadi ( 49/43). 25. Kilombero - Ifakara. 26. Magu - Magu. 27. Mbozi - Vwawa. Sehemu zote hizo CCM ndio chama cha upinzani."
 
Kujichimbia? hivi hujuwi kulikuwa kuna uchaguzi na tumeshinda kwa kishindo? zaidi ya 80%.

Hiyo ni sawa na Kikwete alivyomshinda Mbowe mwaka 2005. Unakumbuka? Landslide victory.

Aaaaa wapi ccm hamjui hata hesabu za percentage, nani atakaa awaamini na data zenu za kupika. Ukawa imeshinda kwa kishindo kwakuipokonya ccm vijiji vingi, kata n.k sasa iv tunasubiri kucheza densi uwanja wa taifa, naomba siku hyo uje nicheze na wewe mtani hadi mornie kusherehekea mafanikio ya ukawa

Kutakuwa na mziki mnene, vinywaji na misosi yakufa mtu
 
Wewe leta zako ambazo mbichi. Kinakushinda nini?

Umebaki kubwabwaja na kuhororoja, bila mpango.

Krismasi unakula wapi?
 
Akiyataja maeneo ya Miji midogo ambayo CHADEMA imeshinda, Dr. Slaa amesema " 9. Kyela - Kyela."

Kyela ni Jimbo la bure la CHADEMA hata CCM wanajua haya!Dr Mwakyembe anazomewa hadi kijijini kwake Ikolo!

Ona juzi picha hizi wapiga kura wanamuambia wazi kabisa kuwa "Dr Mwakurmbe akagombee Ilala aliyo wapa tren au Temeke aliko inarisha bandari yao au Dodoma aliyo wapa usafiri wa gari moshi*
 
Attachments

  • 1419028608093.jpg
    1419028608093.jpg
    111.6 KB · Views: 153
  • 1419028645313.jpg
    1419028645313.jpg
    96.5 KB · Views: 137
Hata huku Magu ni nyumbani kwa wachaga? Ccm inapumua kwa msaada wa mashine hapa magu

Hapo polisi wameitwa kuja kumuondoa Dr Mwakyembe baada ya wapiga kura waliokuwa wanambeba mwaka 2010 sasa kumuambia wazi kuwa 2015 wala asijihangaishe kugombea!
 
Attachments

  • 1419028738865.jpg
    1419028738865.jpg
    113 KB · Views: 207
Mara nyingi nimekuwea nikiangalia meza za magazeti na kuangalia gazeti gani linabaki kwa muda mrefu naona mawio ni mojawapo ya gazeti ambalo haliuziki. Jana nimegundua sababu kuu ya kwa nini haliuziki..Kwa sababu linaandika uongo mtupu..Limeandika CCM aibu tupu ati wapinzani wameata asilimia 38. lakini wasimamizi wa uchaguzi kila wilaya wanasema ccm imeshinda kwa zaidi ya asilimia 70 sasa ukifanya wastani tu utaona bado ccm imepata ushindi mnono lakini kwa kuwa mawio wanataka kuwalisha watu uongo wameamua kufanya propaganda hizo ambazo kwa kiwango kikubwa zinaua soko la gazeti lao
 
Tafsiri ya matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa inategemea utashi wa mtu. Mfano wewe umeamua kuchukua Yale matokeo yenye pingamizi pamoja na kupita bila kupingwa, ambayo kwa ufasaa sio matokeo ya uchaguzi kwa kuwa uchaguzi haukufanyika. Ila ukijitoa upogo Wako na kuangalia matokeo halisi yaani kura zilizopigwa, real votes, utagundua kuwa ccm ilipata chini ya asilimia sitini. Ila kama mnataka kujifariji na matokeo ya nje ya sanduku la kura mkidhani hata mwakani mtapata, uwanja ni wenu.
 
Kiujumla ni ngumu sana kuamini takwimu za tamisemi pekee. Ukiangalia kwa makini kimahesabu sio kweli kama ccm imeshinda kwa 80.5%, Kwa sababu bado maeneo mengine uchaguzi haujafanyika. Pia kuna mapingamizi. Tamisemi wanajaribu kutoa taarifa za kupotosha umma zaidi!
 
hivi Mawio ni gazeti la kusoma watu wenye akili? Gazeti liandikwe na taahira kubenea halafu wasome werevu?
 
Mara nyingi nimekuwea nikiangalia meza za magazeti na kuangalia gazeti gani linabaki kwa muda mrefu naona mawio ni mojawapo ya gazeti ambalo haliuziki. Jana nimegundua sababu kuu ya kwa nini haliuziki..Kwa sababu linaandika uongo mtupu..Limeandika CCM aibu tupu ati wapinzani wameata asilimia 38. lakini wasimamizi wa uchaguzi kila wilaya wanasema ccm imeshinda kwa zaidi ya asilimia 70 sasa ukifanya wastani tu utaona bado ccm imepata ushindi mnono lakini kwa kuwa mawio wanataka kuwalisha watu uongo wameamua kufanya propaganda hizo ambazo kwa kiwango kikubwa zinaua soko la gazeti lao

kama hata jimboni kwa lissu au kilombero wasimamizi wamesema ccm imepata asilimia 70 basi wanaogopa kufukuzwa kama wenzao
 
Back
Top Bottom