Kuelekea 2025 Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 bila Katiba mpya ni mwendelezo wa kuchafua uchaguzi kama 2019

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Apr 29, 2024
22
34
Wakuu habari za wakati.
Tunakumbuka yaliyotokea mwaka 2029 kwenye mchakato mzima wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji.

  1. Watendaji ngazi ya mitaa na vijiji walielekezwa kuweka vikwazo kwa wagombea wasiotokana na CC kwa nafasi zote.
  2. Wakurugenzi wa Halmashauri walishirikiana na wasimamizi wa uchaguzi ngazi zote kuhakikisha wanawawekea mapingamizi ya ndani na hali ilifikia kwamba kila fomu ya mgombea wa CCM iliporejeshwa ofisi nyingi za wasimamizi wa uchaguzi zikawa zimefungwa kuzuia wagombea wa upinzani kurejesha fomu kwa wakati
  3. Wagombea wengi walipita bila kupingwa kutokana na mapingamizi ya watendaji wa Mitaa ma vijiji kukwamisha fomu za wagombea wa upinzani.
  4. Sehemu ambapo chaguzi zilifanyika, kuliwekwa kura nyingi za maruhani na kuchezea uchaguzi kwa makusudi ili kukisaidia Chama Tawala
  5. Mapingamizi yote ya upinzani yalitupwa pembeni kwa makusudi ili kusaficha njia kwa wagombea wa CCM kushinda.
Leo, tunaishi kwenye matokeo hasi kabisa yatokanayo na kubaka uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019. Vijiji na mitaa mingi hakujafanyika mikutano ya kikatiba na hata ile ya mapato na matumizi haifanyiki kwa sababu ni utamaduni wa CCM kutopeleka mrejesho kwa wananchi na mila ya kutoheshimu mawazo ya wananchi ni hulka tukuka ya CCM.

Tupo kwenye mwaka wa uchaguzi ambapo mwaka huu 2024 kutafanika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuwachagua viongozi wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji. Lakini tunaingia kwenye mchakato wa uchaguzi bila dalili zozote za kurekebisha kasoro zilizojiri 2019. Tumesikia viongozi wakuu wa CCM Makamu Mwenyekiti Bara na Katibu Mkuu mara kwa mara wakisema kuwa Chaguzi zitakazofuata hazitakuwa nakasoro na makosa yaliyofanyika 2019/2020, lakini hawainishi ni makosa na kasoro zipi na yapi marekebisho yake. Kinachostusha ni kwamba CCM ndiyo inayotoa maelezo na majibu kana kwamba ndiyo mwenye sheria za uchaguzi.

Badili Mtazamo
Kuchelewa siko kukosa kufika.
  1. Katiba mpya inayotokana na Wananchi ndiyo muhimu zaidi ya chaguzi zote zilizo mbele yetu. Bila Katiba maridhawa ni kazi bure kuingia kwenye uchaguzi wowote
  2. Wizara ya TAMISEMI siyo sahihi kusimamia chaguzi za Serikali za Mitaa. Ilikuwa ni sahihi enzi za chama kimoja kwa sababu kila kitu kilitokana na Halmashauri Kuu ya CCM lakini sasa kila hatua ya kisiasa inapaswa kuwa ya Kikatiba na Kisheria zaidi. Kuuweka Uchaguzi wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji chini ya waziri ni kubaka Katiba na uchaguzi wenyewe.
  3. Serikali ije na road map ya Katiba Mpya ili kubariki michakato ya chaguzi zote zilizo mbele yetu
  4. Majeshi yetu yaheshimu Katiba ya nchi, wasijihusishe na siasa bali watoe uwanja sawa kwa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi.
Badili Mtazamo
 
Back
Top Bottom