Kwanza nakubaliana na wale wote wanaojaribu kujadili source ya matatizo ya Tanzania and principal problems ni UMASIKINI NA UJINGA(au ukosefu wa elimu). Inabidi kufahamu matatizo tuliyonayo kwanza kabla ya kutafuta kiongozi (RAIS) ambaye atatatua hayo matatizo.
Ni kutokana na UJINGA na UMASIKINI, ndiyo maana watanzania wanaendelea kuichagua CCM kila kukicha. Ukifanya utafiti utagundua kwamba waTanzania wengi wenye elimu ya angalau Chuo Kikuu (Genuine Degrees) si mashabiki au wanachama wa CCM kwa sababu wanaupeo wa kutosha kuelewa kwamba CCM na viongozi wake ndio chimbuko la matatizo ya Taifa letu.
Ni kutokana na UJINGA na UMASIKINI, ndiyo maana waTanzania wanashindwa kuungana kwa sauti moja na kudai KATIBA mpya ambayo ndiyo ingefungua milango ya kusimikwa institutions za uhakika za kulinda maslahi ya Taifa na kuzuia na kupambana na ufisadi na uharamia mwingine wowote ambao umekuwa ukifanywa na kulindwa na CCM.
Ni kutokana na UJINGA na UMASIKINI, ndiyo maana watu kama Rostam Aziz wanapata jeuri na kiburi cha kuifisadi Tanzania whenever they get an opportunity. Kama waTanzania tusingekuwa wajinga na maskini, tusingekubali kuhadaiwa na huyu m-burushi na kumpa nafasi ya kufanya uhaini anaoufanya ndani ya Tanzania.
Ni kutokana na UJINGA na UMASIKINI, ndiyo maana CCM kama chama bado kinaendelea kutetea maslahi ya CHAMA kabla ya maslahi ya TAIFA. Na inabidi kujiuliza, maslahi ya CHAMA kwa hakika ni maslahi ya nani? Rostam Aziz? Jakaya Mrisho Kikwete? Kwa hakika si maslahi ya WATANZANIA.
Kwa hiyo, ili kuondokana na UJINGA na UMASIKINI, inabidi tuondokane na CCM. Kwa kifupi, UJINGa na UMASIKINI wa waTanzania ndiyo mtaji mkubwa wa CCM na kwa maana hiyo CCM kama chama, hakiwezi kuondoa matatizo hayo mawili hata siku moja. Suluhisho la matatizo hayo mawili, ni kupata RAIS wa nchi kutoka kwenye vyama mbadala. Vyama ambavyo vinalenga kupambana na UJINGA na UMASIKINI. CHADEMA na CUF vinaweza kutoa uongozi unaoweza kupambana na matatizo hayo. NCCR-MAGEUZI, TLP, TADEA et al, ni extensions za CCM kwa hiyo sitegemei kupata mtu serious kutoka vyama hivyo.
Tuendelee na mjadala..........