Wakuu Ogah na Pasco,
Sina matatizo na utendaji kazi wa John Pombe Magufuli kwa kipindi chote alichokuwa Waziri zama za BWM. Ni kweli kuna madudu alifanya kama ulivyotaja, swala la uuzaji nyumba za serikali.
Nina tatizo kubwa moja, unajua madudu mengi ya ufisadi yanayoibuka sasa yalifanyika zama Mkapa. Magufuli alikuwa ni pendekezo la Mkapa kwenye nafasi ya Waziri Mkuu mara baada ya uchaguzi wa 2005. JK aliweka mguu chini akalikataa hilo pendekezo la Mkapa na kuamua kumpa swahiba wake (EL).
Mtu yeyote ambaye ni chaguo la Mkapa ama ambaye anasema Mkapa ni mtu safi, mimi nimwogopa sana. Kama utakumbuka vyema, siku Pinda anachukua kiti cha u-PM, alimfagilia sana Mkapa kwamba alifanya kazi chini ya BWM pale Ikulu na akaendelea na kumfagilia EL. Few months down the road, Pinda huyo huyo akaja kumtetea Mkapa kwa makosa ambayo yako wazi, swala la Kiwira.
Ukisema tumchague mtu kama Magufuli, huu uchafu tulio nao (ufisadi) wote utafukiwa kwa kuwa ukizama ndani zaidi kwenye hizo kashfa utakuta kuna mikono wa Mkapa. CC na NEC tayari wameishasema kwamba Mkapa asiguswe, pamoja na huu uchafu wote uliopo ambao unamgusa yeye moja kwa moja.
Kiwira tayari imeishafunikwa, Radar imefukiwa, Ndege ya Rais ndo hiyo imetulia Terminal II, na hata hizi kesi za EPA ambazo hazijaenda mahakamani lazima kuna mikono ya CCM, Mkapa ama RA, ndiyo maana tunawaona watuhumiwa wanatesa mtaani. Ukiuliza utaambiwa kwamba hakuna ushahidi wa kutosha ama wamerudisha pesa zote. Je, waliopelekwa hawajarudisha? Ama waliopelekwa ushahidi wao ulipatikana wapi? Makosa ni yale yale, lakini hatuwa wanazochukuliwa watuhumiwa ziko tofauti.
Kwa maoni yangu, mtu yeyote ambaye alishawahi kuwa close na Mkapa ama ambaye anaona CCM ya sasa ni safi, huyo hatufai hata kidogo. Ninasema hatufai kwa kuwa ni CC na NEC ya CCM ndo wamekuwa kiwingu kikubwa sana kwenye agenda ya ufisadi. CC na NEC ndo wanaendesha kampeni za kuwasafisha baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi. SO, ukimchagua yeyote ambaye anaona CCM na Mkapa ni safi, hatuwezi kufika mahali, tutakuwa tunapiga mark-time, na kujikuta hatufiki popote. Sana sana atasaidia kufukia ushahidi wote uliopo ili Mkapa na baadhi ya viongozi wa CCM waonekane wako safi, na kumbe si kweli bali ndiyo wanaoongoza kwa ufisadi na kulindana wao wenyewe.
Kwa kuwa Magufuli ni mtu wa Mkapa, akiwekwa kwenye nafasi ya kumshughulikia Mkapa na madudu yake, hatuwezi kufika popote. Magufuli hana tofauti na akina JK, EL, Pinda na wengineo. Kinachomtofautisha ni kwamba yeye mwenyewe (Magufuli) ana madudu machache sana, sawa na jinsi alivyokuwa Pinda pia ni mchapa kazi mzuri sana, huwa hana siasa kwenye kazi. Lakini hayo madudu machache siyo warrant/guarantee kwamba akiwekwa kwenye nafasi hiyo atafuatilia mpaka mwisho ufisadi wote uliofanyika huko nyuma. Tunataka kiongozi atakayefuatilia hayo madudu ya nyuma ili kuweka msingi kwamba mtu akichaguliwa kuwa kiongozi ama akipewa uongozi basi asijihusishe na ufisadi. Akija kiongozi wa kufunika uchafu, tutakuwa hatufanyi kitu.
Kupata kiongozi safi ndani ya CCM ni kazi ngumu sana kwa kuwa mfumo wa kupata viongozi umetawaliwa na rushwa, ni mafisadi ndio wanaamua nani awe kiongozi kwa maslahi yao. Baadhi ya prominent figures ndani ya CCM ambazo tunaona kwamba zinafaa kupewa uongozi, hawakubaliki na "wenye chama" (mafisadi). Siku ikitokea hao tunaosema ni wasafi ndani ya CCM wakishika uongozi, basi ndiyo tutakuwa tumeizika CCM rasmi.
Magufuli atafaa iff atapewa condition kwamba agenda ya ufisadi inaanzia siku atakaposhika madaraka, lakini hawezi kurudi nyuma 15 yrs, maana atakuta mikono ya Mkapa na hawezi kumgusa.