Uchaguzi 2010: Masilahi Ya Taifa Kwanza!

Uchaguzi 2010: Masilahi Ya Taifa Kwanza!

Dr Slaa hafai... Huko Upinzani tafuteni mtu mwingine.

Kibu, kwa vile hapa tunadadili tuu, hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kujadili, unapotoa dai, unalijengea hata japo kajihoja kadogo tuu hata ka neno moja. Mathalani unaposema Dr. Slaa hafai unatoa na sababu kwa vile ni mwiba kwa mafisadi, atampa wakati mgumu muungwana, au hafai, just hafai period.Watu wamemwaga data kuwa JK hatufai tena kwa 2010 kwa vile ni fisadi kisirisiri, aliingia madarakani kwa fungu la mafisadi, aliendesha kampeni chafu kwa udhamini wa mafisadi, ndio maana analea ufisadi kwa kuwaonea aibu mafisadi na anawajibika kwa mafisadi hao kama kulipa fadhila hivyo na yeye ni fisadi na hatufai kwa 2010. Bado tunawauliza nyinyi mliomo humo ndani, hivi kwenye nyumba yenu hakuna mwingine yoyote mwenye angalau afadhali, kama hakuna, ni tiketi nzuri ya kuwanadi kwa Watanzania, basi mpumzike kidogo tupumue fresh air.Sema basi kuhusu Dr. Slaa hafai kwa lipi?.
 
Sema basi kuhusu Dr. Slaa hafai kwa lipi?.
Dr. Slaa ni limbukeni wa siasa, kwa ulimbukeni huo hawezi kuongoza nchi. Ipo mifano mingi tu ya kuonyesha kuwa yeye ni limbukeni katika ulingo huo wa siasa.

Mfano wa karibu ni wakati alipokuwa akimtimua Kafilila huko Chadema, alidiriki bila ya aibu kumlinganisha na sisimzi, kauli ambayo nimeiona inatokana na ulimbukeni wake wa siasa.
 
Dr. Slaa ni limbukeni wa siasa, kwa ulimbukeni huo hawezi kuongoza nchi. Ipo mifano mingi tu ya kuonyesha kuwa yeye ni limbukeni katika ulingo huo wa siasa.

Mfano wa karibu ni wakati alipokuwa akimtimua Kafilila huko Chadema, alidiriki bila ya aibu kumlinganisha na sisimzi, kauli ambayo nimeiona inatokana na ulimbukeni wake wa siasa.

Shem siku zingine sijui unaamka nazo carlsberg!! Leo kwa mara ya kwanza umepumbalize! big time hahahahahah
 
Dr. Slaa ni limbukeni wa siasa, kwa ulimbukeni huo hawezi kuongoza nchi. Ipo mifano mingi tu ya kuonyesha kuwa yeye ni limbukeni katika ulingo huo wa siasa.

Mfano wa karibu ni wakati alipokuwa akimtimua Kafilila huko Chadema, alidiriki bila ya aibu kumlinganisha na sisimzi, kauli ambayo nimeiona inatokana na ulimbukeni wake wa siasa.

mkuu,

Naona kidogo upeo wako wa kuchambua mambo ni wakiwango cha chini ya wastani,hivi mtu akisema kwa mfano kuna mchwa wanokula hazina ya taifa pale BOT...wewe utachukulia hivyo hivyo?


Wewe ni limbukeni wa lugha,sasa hebu tuanzie hapo sasa kumjadili Dr.slaa!

Mfano mwingine tafadhali....
 
"Katika mfumo wa vyama vingi, Rais anaweza kutoka katika chama chochote cha siasa. Lakini Rais bora atatoka CCM" - Mwalimu Nyerere
 
Dr. Slaa ni limbukeni wa siasa, kwa ulimbukeni huo hawezi kuongoza nchi. Ipo mifano mingi tu ya kuonyesha kuwa yeye ni limbukeni katika ulingo huo wa siasa.

Mfano wa karibu ni wakati alipokuwa akimtimua Kafilila huko Chadema, alidiriki bila ya aibu kumlinganisha na sisimzi, kauli ambayo nimeiona inatokana na ulimbukeni wake wa siasa.

Nadhani lengo la Dr. kumuita kijana sisimizi, hallikuwa na nia ya kumtusi, bali kumdescribe position yake within set-up ya Chadema kwa kutumia tamathaki za semi, Chadema ni Tembo, Kijana Sisimizi. Hapo kuna kosa la kumkosesha urais kweli?
 
Join Date: Sat Nov 2009
Posts: 15
Thanks: 0
Thanked 2 Times in 1 Post
Rep Power: 0
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif





Una wiki moja humu mejuaje mambo ya JF



Inabidi achukue Kiswahili 101
.

Huo ni Umbumbu mkuu wangu.

Kujiunga week moja iliyopita maana yake nilikuwa sisomi hata post za wan JF?
 
Uchaguzi 2010 ni kweli lazima maslahi ya taifa yatangulizwe.

Maslahi ya taifa ni yapi hayo?

Ni pamoja na kupunguza matumizi ya fwedha za walipa kodi, kupunguza mishahara ya wabunge na kuwalipa walimu mishahara mizuri ili waweze kuboresha bongo za watoto wa shule.

Mengine ni kulinda na kutunza rasilimali zote za taifa yakiwemo madini, mbuga za wanyama, na mali asili.

Mambo haya yakilindwa na kutumiwa kwa ajili ya maslahi ya taifa nchi yetu itapiga hatua sana kimaendeleo kwani viwanda vitafufuliwa au kuendelezwa maana chini ya utawala wa awamu ya kwanza viwanda vyote vya Tanganyika Meat, Mwatex, SunguraTex, Urafiki, Gapex, General Tyre, SIDO na kampuni kama MECCO viwanda hivi vilikuwa vinajikongoja na baadae kumalizwa kabisa na walafi kama si kuuzwa.

Sasa tunahitaji mtu mwingine mwenye vision ya kuona hata wapi pana UFISADI na RUSHWA na ambae yupo tayari kudhibiti hali hio na kuhakikisha demokrasia inafanya kazi yake katika maeneo yote hasa majimboni na mtu huyo ni Dr Wilbroad Slaa.

Kwamba Dr Slaa ataweza kusimama peke yake jibu ni kwamba ni vigumu, yeye anahitaji wapinzani wote waungane na CHADEMA na asimamishwe kugombea uraisi kwa tiketi ya upinzani.

Jambo hili litakuwa gumu sana endapo mambo ya ubinafsi katika kambi ya upinzani yatatawala na kuwapa nafasi CCM kuendelea kushinda.

Watanzania tunataka mabadiliko na wapinzani wote ni lazima watambue hilo. Ufisadi upo hata kwenye nchi zilizoendela lakini umekuwa minimized na ukigundulika unajitema mwenyewe bila kungaja kuambiwa.

Ni hayo tu.
 
9534_179942535338_747855338_4355325_7952301_n.jpg


Uchaguzi unafanyika wenye kucheza rafu wanapita kimezengwe alafu haoooooo Dar wanavimbiana matumbo huko vijijini wanawaacha walio waweka madarakani wakitaabika watoto wao wanaketi chini hakuna kinacho endelea zaidi ya ubinafsi tu badilikeni wanatushinda Rwanda jamani!
 
- Wakuu heshima mbele, kabla hatujaendelea na majimbo mengine kuna hoja moja inaonekana kukubalika na wengi nayo ni DR. Slaa for President, I like it lakini nina wasi wasi kwamba wengi hatumjui vizuri sana na hasa record yake ingawa ya vita na ufisadi iko wazi, mnaoijua vizuri record yake iwekeni hapa maana Urais wa Dr. Slaa unajadilika,

- Halafu vipi wakuu kweli Dr. Slaaa anaweza kuwa Rais bila muungano wa wapinzani halafu wakamsimika kuwa mgombea wao?

Respect and Later!

FMEs!
To be honest to my fellow country man and women,
Dr. Slaa hafai kuwa rais wa Tanzania kwasababu zifuatazo:-
1. Ni MUASI:-
a)Aliasi kanisa katoliki alipoacha u-padre akaja kwenye uraia kwakuwa tunajua kwamba kuwa padre unaapa kumtumikia Mungu milele..sasa mtu aliyemuasi mungu wake atashindwa kutuasi sisi kama taifa..no trust this guy whatsoever..
b) Aliasi CCM baada ya kutochaguliwa kwenye chama chake akakimbilia Chadema ambako ndipo alipo sasa..anaendeleza utaratibu wa kuasi nafikiri ni hulka yake..I don't trust this fellow...
2. Hatari ya kuvunja umoja wa kitaifa na Amani
a) Huyu bwana aliwahi kuwa katibu wa Wakatoliki je ameacha kutumikia kanisa? je hamuoni kwamba atakuwa bias sana kwa jamii ya kiislamu ya Tanzania? kwasababu ya historical backround sioni kama ana mvuta kwa pande zote za jamii zetu kwa hivyo ni hatari kwa umoja wetu..!!!
b) Kama katibu mkuu wa chadema hawana hata mwenyekiti wa kijiji huko zenj...na sioni kama kuna juhudi zozote za kufanya hivyo..damn nionavyo mimi hana interest na zenj kwasababu ya malezi ya kikanisa??does it make sense??? kuwa rais wa Jamhuri NO NO.
3. Ni Mbabe na Mjeuri..
Mimi namuona kama mtu ambaye hakuwezi kutengeneza relations na watu wanaofanya naye kazi..ni type ya kina sumaye na mramba...na kauli zake zinazihirisha hivyo...zaidi ya yote anafaa aendelee kuwa mpayukaji huko upinzani kuliko kiongozi wa kitaifa lol
Tuendelee kumfukua zaidi kabla ya kufanya kosa kubwa sana kumuweka huyu jamaa hafai kabisaaaa!
 
Tumaini, yuo have to remember that you can not teach an old dog new tricks. unategemeya Prof. ana nini kipya cha ku2pa cc. for the last 15 yrs cjaona ki2 kipya kwake zaidi ya ngonjera za kila cku. Je 2nahitaji kiongozi bila uongozi au ungongozi bila kiongozi bora
Hujasema kitu hapa, zaidi ya streotype..jamaa anatoa options za kiongozi kila wakati anapopata fursa just take time to listen him..my assesment yeye ndiye anayefaa zaidi kuliko wengine wewe leta wa kwako tum-assess.
 
Tumain kuna post umesema "Lipumba is Obama like". Can you explain how Lipumba is Obama like? What comparisons did you make? Just curious.
Obama is intellectual and inteligent and so is Lipumba..OK
 
baadhi ya matatizo tuliyonayo ni
1. kutokujua haki zetu na namna gani ya kuzitetea
2. sheria nyingi zimewekwa kuwakandamiza raia (mf ukichelewesha bill ya umeme unapigwa faini lakini wao wakikukatia umeme? hakuna sheria ya kuwaadhibu tanesco nk)
3. kufikiria njia za mkato katika kutafuta maisha (hatuna long plans za maendeleo katika maisha) ndiyo chanzo kikubwa cha ufisadi/wizi kila ofisi/mahari
4. Bado tuna ndoto ya kufikiria kuwa kuna chama cha siasa kitatokea kitakacholeta maendeleo katika nchi yetu.
NK
NK
NK

ELIMU YA URAIA inahitajika kubadilisha ATITUDE za watu, wajue HAKI ZAO, WAZITETEE. nchi ikiwa na MSUKUMO Kutoka kwa WANANCHI kuna uwezekano mkubwa wa kufanikisha vile vitu vinavyoahidiwa na wanasiasa. Tumeona mifano mingi ambayo wananchi wameamka na kuweka msukumo na tumeona utekelezaji wake. Hii itapunguza tension ya kuhitaji viongozi bora ambao ni vigumu kuwapata. Na kama tusipowapata basi hao wabaya wasukumwe watekeleze kuringana na ahadi zao.
Je Jamiiforums inaweza ku support vipi elimu ya uraia
 
FMES hujajibu maswali yangu


FMES umesema vyema ni kwa maslahi ya taifa, ila pia wewe ni mkereketwa wa CCM. Unataka kutaja majina ya wana CCM wanaofaa kwa urais? au ''yeyote mwingine kwa maslahi ya taifa'?

Pili ukipropose majina ya wagombea, let say ndani ya CCM kama mwanaCCM mkereketwa unafikiri JK yuko tayari kuachia hii nafasi mwakani?

Kama hayuko tayari kuachia ngazi, lengo lako ni nini hapa?

Mwisho ni lini mtaweza kuwaondoa hao wanachama wabovu(kama usemavyo hili wengine wasafi kama wewe muendelee kushika nchi)? unaweza kuweka timeline? mmeshakaa madarani kwa miaka 40 sasa! how many more years are enough for you


Kama mkereketwa wa CCM na wanachama wengi namna hiyo, je unaweza kuniambia mwanachama wa CCM anayepingana na ufisadi kwa utashi wakwe mwenyewe na yuko tayari kufa kwa hilo.Maana hawa wapiganaji wenu walianza kelele baada ya wapinzani!
 
Field marshal,
Tatizo la Tanzania ni umaskini...hivi unafikiri umaskini umesababishwa na ufisadi tu? basi siyo kitu kingine? that will be wrong hypothesis to start with? kwanini wakati wa Mwalimu hakukuwa na ufisadi lakini mbona umaskini ulikuwa mbaya zaidi? mpaka kununua nyembe tunapanga foleni? tatizo ni uchumi na Prof. Lipumba ni right person for a job.

Hakukuwa na umaskini wowote mbaya wakati wa Mwalimu. At least familia zote za mijini na vijijini zilikuwa zikiweza kula milo mitatu kwa siku damn it! Huwezi kulinganisha umaskini uliokuwepo wakati wa Mwalimu na umaskini huu wa leo! Umaskini wa awamu ya kwanza haukusababishwa na ubadhilifu na matumizi mabaya ya fedha za Serikali. In fact utawala wa awamu ya kwanza ulikuwa ukitafuta kila mbinu za kuwapunguzia wananchi makali ya umaskini waliokuwa nao kutokana na kukandamaizwa na Serikali za kikoloni ukianzia kwa Mjerumani na baadaye Muingereza. Kupanga foleni kununua nyembe kulikuwa ni kwa manufaa ya Taifa. Mwalimu alikuwa analifundisha taifa kujitegemea! Alitaka badala ya kuagiza hizo nyembe kutoka nchi za nje vifunguliwe viwanda na vitengeneze humuhumu nchini nyembe na bidhaa zingine za lazima zilizokuwa zikihitajika. Lakini, kwa umbumbumbu wetu tukaona hiyo ni karaha. Serikali ya Mwalimu ilitumia fedha za Umma kujenga shule, hospitali, zahanati, viwanda, Serikali ya Mwalimu haikununuua ma-BM wala mashangingi zilitumika gari za bei nafuu e.g. peugeot na landrovers ... naweza kuorodhesha mambo mengi ambayo yalikuwa yakifanywa na Serikali kwa makusudi kabisa ili kusaidia wananchi kuinua hali zao za maisha.

Tunataka kiongozi/viongozi ambao watauona umaskini wa kweli wa wananchi na umaskini huo uwakerekete na kuwauma hao viongozi. Hatutaki viongozi wanaoshabikia utajiri na kutetea ubadhilifu wakidai kwamba utajiri si dhambi. Utajiri ni dhambi kubwa kama unapatikana kwa kupandia migongo ya wananchi wenye dhiki.

Kwa kifupu, naunga mkono hoja ya FMEs kwamba Uchaguzi wa 2010, tutataka kiongozi anayejali maisha na maslahi ya wananchi.
 
Tunapojadili hoja, yatupasa pia tujue kuwa hoja nyingine zipo kufufisha harakati za kuleta mabadiliko ya kweli. Ni ukweli uliowazai kuwa huwezi kusema kuwa tujadili ubunge lkn tuanche nafasi ya urais hadi pale wagombea watakapojitokeza.

1. Kwanini isifanyike hivyo pia kwa ubunge, iwe ni hadi pale wabunge watakapojitokeza?

2. Kwanini mtu anapopendekezwa kugombe urais, ihojiwe kuwa amefanya nini kikubwa kwenye ufisadi na isiwe kuwa uongozi wake ukoje kulingwanishwa na rais anayepigana kurejea madarakani?

3. Kwanini kupendekeza watu kugombe ubunge, ikiwa na maana ya kuwaonyesha kuwa wao uwezo wao ni kuwa wabunge tu, na hawana uwezo wa kukisogelea kiti cha urais?

Mimi nadhani tunapigana tunajaribu tu kutwanga maji. Tatizo sio wabunge hata siku moja, tatizo ni mfumo, na kuibadilisha Tanzania sio kujipendekeza kuwataja watu wanaofaa kuwa wabunge badala ya kwenda pale penye tatizo. NAO NI URAIS WA NCHI. JK ameshindwa kujibainisha amesimama wapi katika maendeleo ya Tanzania, sasa makundi yakemkuwa makubwa hata watanzania hatujui mustakabili wetu, huku tunajidai kuwasukuma watu waende bungeni! watapitia wapi? Mkapa aliwahi kuwaambia wabunge watakaokataa miswaada yake watakutana naye Dodoma. Sasa hawa wote wanaojiita wapiganaji na wanaoitwa mafisadi wanajua watakutana na JK wapi?
 
Mnaonaje combination ya Asha-Rose Migiro na Samwel Sitta? Yeyote kati yao anaweza kuwa Rais na mwingine Waziri Mkuu. Ni watu ambao nimewafuatilia kwa muda mrefu na ninaamini wana uwezo mkubwa na uzalendo wa hali ya juu. Hawa wakiunda baraza la mawaziri lenye watu wachapakazi na wanaochukia ufisadi nchi itasonga mbele. Naomba kutoa hoja!
 
To be honest to my fellow country man and women,
Dr. Slaa hafai kuwa rais wa Tanzania kwasababu zifuatazo:-
1. Ni MUASI:-
a)Aliasi kanisa katoliki alipoacha u-padre akaja kwenye uraia kwakuwa tunajua kwamba kuwa padre unaapa kumtumikia Mungu milele..sasa mtu aliyemuasi mungu wake atashindwa kutuasi sisi kama taifa..no trust this guy whatsoever..
b) Aliasi CCM baada ya kutochaguliwa kwenye chama chake akakimbilia Chadema ambako ndipo alipo sasa..anaendeleza utaratibu wa kuasi nafikiri ni hulka yake..I don't trust this fellow...
2. Hatari ya kuvunja umoja wa kitaifa na Amani
a) Huyu bwana aliwahi kuwa katibu wa Wakatoliki je ameacha kutumikia kanisa? je hamuoni kwamba atakuwa bias sana kwa jamii ya kiislamu ya Tanzania? kwasababu ya historical backround sioni kama ana mvuta kwa pande zote za jamii zetu kwa hivyo ni hatari kwa umoja wetu..!!!
b) Kama katibu mkuu wa chadema hawana hata mwenyekiti wa kijiji huko zenj...na sioni kama kuna juhudi zozote za kufanya hivyo..damn nionavyo mimi hana interest na zenj kwasababu ya malezi ya kikanisa??does it make sense??? kuwa rais wa Jamhuri NO NO.
3. Ni Mbabe na Mjeuri..
Mimi namuona kama mtu ambaye hakuwezi kutengeneza relations na watu wanaofanya naye kazi..ni type ya kina sumaye na mramba...na kauli zake zinazihirisha hivyo...zaidi ya yote anafaa aendelee kuwa mpayukaji huko upinzani kuliko kiongozi wa kitaifa lol
Tuendelee kumfukua zaidi kabla ya kufanya kosa kubwa sana kumuweka huyu jamaa hafai kabisaaaa!

Kuna watu wana mielekeo ya tofauti pale inapokuja kuona kwamba ni nani anafaa kuwa rais,mathalan vigezo vyetu vinatofautiana kutokana na misimamo yetu mbalimbali dini ikiwa ni mojawapo.Uzuri hapa JF kama ilivyo kwenye jamii yetu,kuna watu wa tofauti na hao niliowamention...Ambao maslahi ya Taifa ni mbele kama ilivyoainishwa na mleta mada.

Pia kwangu binafsi naamini ushauri kutoka kwa aliye mpinzani wako ni wa kinyume,kwa mfano Masatu ambaye ni CCM aliposema kuwa Slaa hafai kuiwakilsha CHADEMA ama upinzani,utashangazwa sana kuwa yeye kama mpinzani wa CHADEMA ametumia vigezo gani ambavyo vina malengo ya kuwatakia mema wapinzani ama CHADEMA.

Vile vile na wewe kama mpinzani wa ukristo pamoja na CHADEMA sioni ni kwa vipi utachukizwa na hatua ya Padri kuachana na upadri ilhali hata ukristo wenyewe hauuamini,ni bora utafute vigezo vingine kwasababu huyo Mungu unayedai aliapa kumtumikia hata wewe haumuamini,so no double standards please kama wewe ni great thinker.

Na madai kwamba aliasi CCM na kwenda CHADEMA,je Lipumba aliasi nini?Kwanza si alikuwa mshauri wa Rais wa uchumi na uchumi uko wapi?N si ni juzi tu wamekubaliana sijui nini na CCM?

Mwisho uspende kujikesha kwa issue za kipuuzi,huwezi kumwita Slaa "Mropokaji" halafu unajichekesha,unamchekea nani wakati ni upuuzi kumwita mtu anayepigania maslahi ya Taifa "Mpayukaji?"
Humu ndani kuna great thinkers na pia very dangerous minds,wewe ni mwana CUF ambaye ni mpinzani na una guts za kusema list of shame speech ilikuwa ni upayukaji?
Ama kweli kuishi kwingi....
 
Back
Top Bottom