Uchaguzi 2010: Masilahi Ya Taifa Kwanza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi 2010: Masilahi Ya Taifa Kwanza!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Field Marshall ES, Nov 22, 2009.

 1. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Wakuu uchaguzi mkuu wa taifa uko kwenye kona, Mzee Mandela aliwahi kusema kwamba kwenye ishu muhimu za taifa kama hizi kuwa kimyaa au kuwa neutral ni dalili za kuwa coward.

  - Kwa wale tulio na influence ya namna moja au nyingine kwa taifa, ni vyema tukaweka wazi msimamo wetu kwa public kuhusu wagombea ambao tunaamini kwamba wanafaa katika kutusaidia taifa, nimekuwepo JF kwa muda mrefu sana sasa nikiwa na lengo moja tu, nalo ni siku moja kuliona taifa langu likiongozwa kwa kuheshimu sheria.

  - Kwa hiyo leo nitaanza rasmi kuwataja wagombea ninaona wanafa kwa masilahi ya taifa letu, na sababu.

  Respect.


  FMEs!
   
 2. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Prof. Ibrahimu Lipumba for 2010 presidency...wapinazni wote wamuunge mkono tafadhali..right person in a right time.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280

  nasuburi hao wagombea wako.
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,451
  Trophy Points: 280
  Hii itasaidia sana ili wagombea wapitishwe kwenye tanuru la moto la constructive cricitism huku tukichambua strength na weak points zao, siku ya siku, tunachagua kile tunachokijua, na sio kujikuta kwenye majuto kama tulivyo sasa.
   
 5. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #5
  Nov 22, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hatutaki Professor awe rais!Simpla man mwenye maadili!
   
 6. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #6
  Nov 22, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Nitafurahi sana Prof. Lipumba na Maalim Seif wasipokuwepo kwenye list ya wagombea, macho na masikio yetu yamewachoka!
   
 7. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Biblia inasema "kunakuwa na furaha sana mbinguni mwenye zambi mmoja akitubu " na kwa kweli leo hapa JF ni furaha kubwa sana mkerekwetwa unapofunguka macho na kuanza kuongelea masilahi ya taifa kuliko li chama lako.

  Karibu sana naona neema inakuja!
   
 8. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #8
  Nov 22, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Yaani Lipmba ataendelea kugombea tu? si atawaachia wengine sasa? Obama alisema kama unafanya vitu vilevile kwa namna ile ile usitegemee kupata matokeo tofauti.
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Nov 22, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,451
  Trophy Points: 280
  .

  This is not fair comments kukiita chama cha mtu li chama, hebu wafikirie wale wengine wote wenye vyao vyao kikiwepo cha kwako ulichomo kikitwa lichama.

  Tunapozungumzia maslahi ya taifa, ni over above party politics, sie wengine na mimi nikiwemo, tunaona bado hatuna hata chama kimoja cha kujiunga nacho lakini maslahi ya taifa tumo.
   
 10. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #10
  Nov 22, 2009
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,722
  Likes Received: 1,212
  Trophy Points: 280
  Kiongozi tu wa taifa, bila kujali anatoka wapi?
   
 11. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #11
  Nov 22, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Duh mbona wengi bado hatuchawachoka kila siku wanazidi kuwa makini zaidi it is time give them a chance...
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Nov 22, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu no offense lakini nadhani uswahilini tunatumia sana hiyo term ya lichama... ila sijui kama kuna maana nyingine

  Tukija kwenye mada, njia rahisi ni kuweka jedwali litakaloonyesha kila jimbo na potential candidates then tunakata kila wanapopungua... nadhani wiki hii pekee kuna vijana kama watano ndani ya chama tawala wameweka wazi nia zao na kuanza kushtua wakubwa majimboni

  au mnaonaje?
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Nov 22, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,451
  Trophy Points: 280
  Yes its good tukianza vyovyote, pia tuandae rules of the game to avoid character assasinations na to maintain their right to privacy wakati tukiwachambua ili tuwavue nguo na kuwatia aibu.
   
 14. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #14
  Nov 22, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu jaribu kuheshimu taifa, kama huna cha kuchangia kuhusu masilahi ya taifa basi waachie wanaoweza,

  - Na ninaomba nikukumbushe wewe na wengine wote kwamba mimi ni mwanachama mkereketwa wa CCM, sijawahi kutokwua na msimamo wala kuwa neutral katika maisha yangu huku Duniani, ninaamini kwamba chama cha CCM hakina tatizo lolote, isipokuwa tuna viongozi wachache wabovu ambao demokrasia inahitaji tuwarekebishe ili waweze kurudi tena kwenye mstari.

  - Now back to the ishu ni kwamba kwa mawazo na maoni yangu ufisadi, ndio hasa tatizo kubwa linaloliangamiza taifa letu, ninaamini kwamba tukiweza kuuthibiti ufisadi, yaani kuwashughulikia viongozi wezi wa mali za taifa, yaani za wananchi basi taifa letu litafanikiwa sana katika mbio zetu za kusonga mbele. Na the only way foward ni kukazania utawala unaoheshimu sheria kwanza kabla ya anything.

  - Nafasi ya Rais kwa sasa ninaiacha wazi mpaka nitakapojua wanaoiwania kutoka vyama vyote ndio tutasema wazi msimamo wetu, ingawa for now tunaweza ku-speculate na kushauri pia nani anayefaa, lakini tutasema msimamo wetu kwa wagombea walioko kwenye nafasi tayari na wale walioonyesha nia ya kutaka kugombea.

  - Na kila member hapa JF, anakaribishwa sana kutoa maoni yake kuhusu nani anatufaa kiuongozi katika taifa letu.

  Respect.


  FMEs!
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Nov 22, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  chukua tano kamili pasco, maana mada nzuri ya FMES inaweka ikaharibika bila ground rules!!
   
 16. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #16
  Nov 22, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sasa Pasco nifanyeje nianze kumpamba Lucifer eti kwa sababu tu anawafuasi?
   
 17. mponjoly

  mponjoly Member

  #17
  Nov 22, 2009
  Joined: Oct 4, 2009
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nafikiri ni wakati umefika upinzani ukapewa nafasi kuona kama wataweza kutupeleka mbele taifa hili angalau hatua tatu mbele na mbili nyuma!! tumekuwa na chama tawala cha sasa kwa muda na hamna makubwa zaidi yaliyofanyika!democrasia ni kuwa na vyama vingi na kama chama tawala chachemsha basi wangine wapewe nafasi, na kama nao wakichemsha nafasi apewe mwingine!
  swali ni kwamba ni mgomea gani wa chama pinzani ambaye ana visifa kidogo vya kuwa rais?
   
 18. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #18
  Nov 22, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nawaunga mkono wale wabunge wanaopinga vita ufisadi!
   
 19. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #19
  Nov 22, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Mkuu FMEs! heshima mbele kaka.

  Hii kitu nyekundu mkuu.....mimi nadhani hii kitu tungeiacha iwe open na tuwaachie wana JF wapendekeze ni nani na kwa sababu zipi..huwezi jua labda kuna watu watakaosukumwa na maoni ya watanzania na baadaye kuchuka form za kugombea.

  Mada safi sana hii, hongera kiongozi.

  Vipi Tingatinga atajaribu tena 2010 au basi tena?..

  MJ
   
 20. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #20
  Nov 22, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  FMES,
  Mimi nachukua msimamo tofauti kidogo na wako. Kwa kuwa umesema maslahi ya taifa nadhani itakuwa muhimu tuorodheshe kwanza matatizo tunayokabiliwa nayo kama taifa halafu ndio tuangalie katika matatizo haya ni vioingozi gani, waliopo au wanaodhaniwa, wanaweza kutusaidia kujikwamua nayo. Nimepoteza imani katika personalities.
  Mimi kwa kuanza tu nataja ufisadi na rushwa kama tatizo la kwanza. La pili ni ukosefu wa uzalendo na la tatu ni tamaa ya kujitajirisha haraka kwa migongo ya walala hoi.
  Tuendelee.
   
Loading...