Uchaguzi 2010: Masilahi Ya Taifa Kwanza!

Uchaguzi 2010: Masilahi Ya Taifa Kwanza!

1. Salim had nothing to show.

2. Merit pekee ya Salim, ni muadilifu wa Nyerere type, he is a man of impecable integrity.

3. Mimi binafsi namuona kama too soft, ila akipata madaraka atapitia tanuru la aradite na kugeuka mgumu kama chuma cha pua.

4. Sifa nyingine ya huyu jamaa ana humulity ya ajabu, anauvumilivu wa hali ya juu na endurance isiyo mfano ya kuvumilia yote aliyozushiwa lakini amejinyamazia baada ya kujua who was behind,

5. Japo Salim is more of a diplomat than a statesman, ni afadhali kuliko uchafu uliopo.

- Mkuu Pasco, heshima mbele sana unasema hizi ndizo sifa za Dr. Salim aweze kupewa uongozi wa juu hasa urais? Au kuna zingine zaidi umeziacha?

- Ataweza kweli kupigana na ufisadi huu uliokithiri Tanzania?

Respect.

FMEs!
 
Na Tausi Mbowe, Urambo Tabora

SPIKA wa Jamhuri ya Muungano, Samuel Sitta amesema wakati wa malumbano umeisha na sasa ni wakati wa viogozi na wabunge kushirikiana na wananchi katika kuwaletea maendeleo kwa lengo la kupunguza umasikini katika kaya zao.

Spika Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki alisema hayo mjini hapa jana wakati wa hafla ya kuwakabidhi matreta aina ya 'power tiller' kwa ajili ya kilimo katika kata 12 za jimbo hilo yenye thamani ya zaidi ya Sh 100 milioni.

Akizungumza huku akishangiliwa na umati wa watu, Spika Sitta alisema kazi hiyo ni muhimu katika maisha ya wana Urambo kwa kuwa sasa wanachohitaji ni maendeleo na si suala lingine.

“Ndugu wana Urambo wenzangu tunaweza kila siku kuzungumza bila mafanikio, wananchi sasa wamechoka na wanachotaka kutoka kwa viongozi wao si maneno tu wanahitaji tuwape maendeleo ili waweze kujikwamua katika lindi la umasikini walionalo na si vinginevyo,”alisema Spika Sitta.

“Hivi wananchi hata kama tunaweza kujenga barabara, kuboresha miundombinu , lakini bila kipato ni kazi bure,”alisisitiza Spika Sitta huku akishangiliwa na umati huo.

Akizungumzaia kuhusu matrekta hayo, Sitta alisema matreta hayo yametolewa kwa ufadhili wa serikali ya Denmark na kwamba yatagaiwa kwa vikundi vya wanawake 38 ambapo vyenye kaya 800 zitakazonufaika kwa awamu ya kwanza ya mradi huo.

Akifafanua zaidi Sitta alisema, mara baada ya kumalizika kwa awamu ya kwanza, balozi wa Dermak atakuja kukagua mradi huo na endapo ataridhika serikali yake itatoa tena matrekta mengine kwa ajili ya awamu ya pili ambapo zaidi ya kaya 1,600 ikiwa ni mara dufu ya awamu ya kwanza zitanufaika.

“Kama tunavyojua sasa kipindi cha kilimo cha alizeti kimeisha, nimeagiza matrekta haya yatumike katika shughuli nyingine za maendeleo badala ya kusubiri kilimo cha alizeti na karanga pekee,” aliongeza.

Alisema matrekta hayo yana uwezo wa kufungwa pampu na pia yana uwezo wa kutumika katika kilimo cha umwagiliaji hivyo kusaidia mpango wa serikali wa kilimo kwanza kwa vitendo.

- Saafi sana, this is what I am talking about!

Respect.

FMEs!
 
Mkulu FMEs heshima mbele!
Nikweli tunahitaji kiongozi atakea piga vita Ufisadi. Lakini Mafisadi"Papa na Nyangumi"wanaoifilisi nchi yetu hawafiki hata kumi. Waliobaki wote ni vibaka Uchwara na wanafisadi nchi kwa sababu ya walio juu wanafisadi.
Raisi aliye very serious haitaji zaidi ya mwaka kuisafisha nchi na uozo wa Ufisadi uliopo!
Qualities nizionazo zinafaa kwa kiongozi ajaye
1:Muadilifu ka Mwl hapa nampa Salim Ahmed Salim
2:Mwenye vision na uwezo wa kusimamia maamuzi yake ka Paul Kagame.... Namuweka John Pombe Magufuli
3) A positive dictator ,raisi mtendaji na mwenye uchungu na nchi------- Still JPM
4)Mwenye uwezo wa kuifanya IKULU yetu kuwa maali patakatifu...........JPM
5)Kuizifanya bandari, reli na barabara zetu kuwa vipaumble vyetu kwa maendeleo, ukizingatia locality yetu katika East Africa--------------JPM
6) Kusimamia mapinduzi makubwa kwenye viwanda vyetu na kuacha porojo ya kilimo kwanza --------- Saalim Ahmed Salim
7)Mwenye uwezo wa kupiga vita UFISADI-------Samweli Sita,Harrison Mwakyembe, Dr Slaa ,Zito Kabwe, Anne Kilango etc etc.

Nakamilisha kwa kupendekeza hivi;
Raisi : John Pombe Magufuli
Waziri Mkuu Salim Ahmed Salim
Waziri wa Mambo ya ndani .. DR Slaa ( regardless ya yeye kuwa mwana Chadema)
Waziri wa Nishati na Madini : Rutabanzibwa
Waziri wa Viwanda na Biashara: Reginald Mengi "msicheke jamani" creativity yake inahitajika hasa wakati uhuu wa Shirikisho la East Africa.
Mawasiliano na Uchukuzi : Mark Mwandosya.
Wizara nyingine wanaweza kupewa vijana waliopevuka kimaadili na wenye uchungu na nchi yao "so far waliopo kwenye baraza la mawaziri wa sasa wametuangusha vijana"
HAYO NI MAONI YANGU TU MKULU!
 
- Mkuu jaribu kuheshimu taifa, kama huna cha kuchangia kuhusu masilahi ya taifa basi waachie wanaoweza,

- Na ninaomba nikukumbushe wewe na wengine wote kwamba mimi ni mwanachama mkereketwa wa CCM, sijawahi kutokwua na msimamo wala kuwa neutral katika maisha yangu huku Duniani, ninaamini kwamba chama cha CCM hakina tatizo lolote, isipokuwa tuna viongozi wachache wabovu ambao demokrasia inahitaji tuwarekebishe ili waweze kurudi tena kwenye mstari.

- Now back to the ishu ni kwamba kwa mawazo na maoni yangu ufisadi, ndio hasa tatizo kubwa linaloliangamiza taifa letu, ninaamini kwamba tukiweza kuuthibiti ufisadi, yaani kuwashughulikia viongozi wezi wa mali za taifa, yaani za wananchi basi taifa letu litafanikiwa sana katika mbio zetu za kusonga mbele. Na the only way foward ni kukazania utawala unaoheshimu sheria kwanza kabla ya anything.

- Nafasi ya Rais kwa sasa ninaiacha wazi mpaka nitakapojua wanaoiwania kutoka vyama vyote ndio tutasema wazi msimamo wetu, ingawa for now tunaweza ku-speculate na kushauri pia nani anayefaa, lakini tutasema msimamo wetu kwa wagombea walioko kwenye nafasi tayari na wale walioonyesha nia ya kutaka kugombea.

- Na kila member hapa JF, anakaribishwa sana kutoa maoni yake kuhusu nani anatufaa kiuongozi katika taifa letu.

Respect.

FMEs!

safi sana
 
mie mpaka sasa sijui nani awe Rais Salim Ahmed Salim hawawezi kumpa nafasi hiyo 50/50

Lipumba hamna kitu -negative

Chadema hakuna rais - negative

mshangao!!
 
- Mkuu Pasco, heshima mbele sana unasema hizi ndizo sifa za Dr. Salim aweze kupewa uongozi wa juu hasa urais? Au kuna zingine zaidi umeziacha?

- Ataweza kweli kupigana na ufisadi huu uliokithiri Tanzania?

Respect.

FMEs!

Salim moto wa kuotea mbali! Mngelimpa tu hilo rungu muone ambavyo angeliibadilisha nchi hii kwa manufaa ya taifa. Salim MZALENDO wa hali ya juu. Salim is strict, Salim si mbabaishaji, Salim muadilifu, Salim ni kiongozi mzoefu wa kitaifa, kimataifa, na anakubalika. Salim hana 'njaa' wala tamaa ya kuwa tajiri anao uwezo wa kuishi kwa alichoweza kuchuma kwa jasho lake katika utumishi wake uliotukuka wa miaka nenda rudi nje ya nchi na akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri Mkuu mstaafu wa nchi yetu. Tungempa Salim urais ni wazi kabisa angeweka maslahi ya taifa Kwanza na si vinginevyo. Salim angeliweza sana kuvaa 'viatu vya Mwalimu' kwa mtindo wa kileo unaokwenda na wakati kwa sababu anaijua dunia na Tanzania vilivyo.

It is very unfortunate kwamba ameamua kuwa hahitaji tena kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kugombea uongozi wowote nchini mwetu. Thanks to those 'uncouth' politicians na waandishi habari uchwala wasiojali maadili who frustrated him in a very big way. Katika mchakato wa kugombea urais walimchezea mchezo mchafu na wa kitoto. Mwenyezi Mungu bila shaka anawalipa/atawalipa wakingali hai kwa maovu waliyomtendea wakati ule.
 
- Mkuu Pasco, heshima mbele sana unasema hizi ndizo sifa za Dr. Salim aweze kupewa uongozi wa juu hasa urais? Au kuna zingine zaidi umeziacha?

- Ataweza kweli kupigana na ufisadi huu uliokithiri Tanzania?

Respect.

FMEs!

Amini nawaambieni, kama angelikuwa ni Salim, tusingefika hapa tulipofika, imebakiwa kuwa ingeli, kwa tulipo haipo, lazima tufike mahali tukubali the really true situation, tumemeze kidonge kichungu ili kutibu maradhi, vinginevyo ni piga ua garagaza, 2010 ni JK tena!.
 
- Mkuu Pasco, heshima mbele sana unasema hizi ndizo sifa za Dr. Salim aweze kupewa uongozi wa juu hasa urais? Au kuna zingine zaidi umeziacha?

- Ataweza kweli kupigana na ufisadi huu uliokithiri Tanzania?

Respect.

FMEs!

Hivi mkuu una allergy na jina la Dr Salim? Ina maana umahiri wako wote huu wa kuchambua mambo na madata kedekede unataka kusema kuwa hujui sifa za salimu kama kiongozi?

Nimefuatilia ule mjadala ulioanzisha kule kwengine dhidi yake ni wazi kuwa haukuwa na nia njema kwake Salim na wala watanzania. Unadai kuwalaumu mtandao kwa machafu waliyoyafanya wakati na wewe unarudia kuyaanzisha yaleyale.

Najaribu kujiulliza ni kwanini sasa. Inaelekea kuna watu ama makundi yanaogopa kuona kuwa Salim anakuwa karibu na JK kwa kuhofia kuhatarisha maslahi yao kisiasa.
 
..uzoefu wa Salim Salim ni ktk masuala ya diplomasia tu. katika nafasi zake zote za uongozi alizopata kushika hakuna hata moja inayohusiana/inayogusa moja kwa moja maisha ya mwananchi wa kawaida.

..uzoefu wake kama waziri mkuu na baadaye waziri wa ulinzi ni wa muda mfupi sana, na alitumikia hapo muda mrefu uliopita, kuweza kunishawishi kwamba anayafahamu na anaweza kuyakabili matatizo yanayoisibu nchi yetu leo hii.

..tunahitaji Raisi atakayesimamia mapinduzi ya KILIMO, VIWANDA,MIUNDO MBINU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA. tunahitaji Raisi ambaye yuko capable and comfortable dealing with the details and nuances za masuala niliyoyataja hapo juu.

..pia tunahitaji Raisi Mzalendo mwenye imani ktk uwezo na vipaji vya Watanzania. Raisi ambaye atahamasisha na kuimarisha wawekezaji wazalendo wa ndani.
 
FMES said:
- Ninasema Tanzania tunao watu ambao wakipewa nafasi wanaweza kuumaliza ufisadi in one month, I mean Mramba na Yona walipoenda Rumande kama Rais wetu angeshikilia pale pale na kukusanya na wengine wallahi huu mzizi wa ufsadi by now ungekua kalasi!

- Ninasema hivi regardless ya impact ya mjadala huu kwa taifa, atleast wananchi watasutwa na nafsi zao kila watakapopingana na mawazo yetu kuhusu nani anafaa na nani hafai kuhusu uongozi bora wa taifa letu, ndio maana leo ukiweza kufukua BCS na mwanzo wa JF, utagundua hakuna jipya yote tuliyasema mapema sana, sasa ni uamuzi wa wananchi kutusikiliza au kuwasikiliza mafisadi, lakini tutasema wazi viongozi wanaotufaa na wasiotufaa kwa masilahi ya taifa letu.

Respect.
FMES said:

FMES,

..Raisi hashughulikii ufisadi kwa namna ulivyoelekeza kwasababu amekosa pressure ya kutosha toka kwetu WANANCHI, na WABUNGE.

Hivi mkuu una allergy na jina la Dr Salim? Ina maana umahiri wako wote huu wa kuchambua mambo na madata kedekede unataka kusema kuwa hujui sifa za salimu kama kiongozi?

Nimefuatilia ule mjadala ulioanzisha kule kwengine dhidi yake ni wazi kuwa haukuwa na nia njema kwake Salim na wala watanzania. Unadai kuwalaumu mtandao kwa machafu waliyoyafanya wakati na wewe unarudia kuyaanzisha yaleyale.

Najaribu kujiulliza ni kwanini sasa. Inaelekea kuna watu ama makundi yanaogopa kuona kuwa Salim anakuwa karibu na JK kwa kuhofia kuhatarisha maslahi yao kisiasa.

- Mkuu hoja hujibiwa kwa hoja na sio viroja, halafu ninayoandika hapa Jf huwa ni yangu si ya kikundi chochote wala anything, sijui sifa za uongozi wa Salim, sizijui na ninakuwa mstaarabu sana kuuliza wanaozijua, ninajua tu akiwa Waziri Mkuu alienda kusini akakuta wananchi wamevaa magunia akawaletea mitumba,

- Kwa sifa alizokua nazo Salim enzi za Mwalimu, sikutegemea kwamba atashindwa kushika urais at this time and moment, meaning kwamba alikuwa akibebwa yeye mwenyewe hana ubavu, alipokuwa OAU ameajiri waarabu wa Oman tu, never mbongo hata mmoja, akiwa OAU mlinzi wake mmoja Mtanzania amekufa katika mazingara yenye utata sana, amesoma ukomandoo Cuba ambako alipelekwa na Babu this is all I know, sasa mkuu una tatizo nikiuliza wanaomjua vizuri waweke vitu vyake hapa wanaweka havijai mkononi sasa unataka nifanye nini mkuu nilazimishe hoja pasipo na hoja?

- Mkuu ninasema hivi sizijui sifa za uongozi wa Salim hapa Tanzania, sasa kama unazijua ziweke hapa ambazo zinaweza kumfanya akawa Rais tunayemtaka anayeweza kupigana na ufisadi, maana Salim hawezi fanya kazi yoyote chini ya Urais, sasa weka hoja hapa mkuu kama huna basi kaa pembeni uke elimu ya bure!

es!
 
1. Salim moto wa kuotea mbali! Mngelimpa tu hilo rungu muone ambavyo angeliibadilisha nchi hii kwa manufaa ya taifa.

2. Salim MZALENDO wa hali ya juu. Salim is strict, Salim si mbabaishaji, Salim muadilifu, Salim ni kiongozi mzoefu wa kitaifa, kimataifa, na anakubalika.

3. Salim hana 'njaa' wala tamaa ya kuwa tajiri anao uwezo wa kuishi kwa alichoweza kuchuma kwa jasho lake katika utumishi wake uliotukuka wa miaka nenda rudi nje ya nchi na akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri Mkuu mstaafu wa nchi yetu.

4. Tungempa Salim urais ni wazi kabisa angeweka maslahi ya taifa Kwanza na si vinginevyo. Salim angeliweza sana kuvaa 'viatu vya Mwalimu' kwa mtindo wa kileo unaokwenda na wakati kwa sababu anaijua dunia na Tanzania vilivyo.

- Mkuu ninakusikia sana kwamba hizi ndio sifa za Salim kuweza kuwa Rais effective, labda wananchi wengine nao wazione kwanza, au?

es!
 
FMES,

..Raisi hashughulikii ufisadi kwa namna ulivyoelekeza kwasababu amekosa pressure ya kutosha toka kwetu WANANCHI, na WABUNGE.

[/COLOR]
[/U]
FMES,
Rais hashughulikii mafisadi kama inavyopasa kwa sababu ya uswahiba wake pamoja nao.
 
Mkulu FMEs heshima mbele!
Nikweli tunahitaji kiongozi atakea piga vita Ufisadi. Lakini Mafisadi"Papa na Nyangumi"wanaoifilisi nchi yetu hawafiki hata kumi. Waliobaki wote ni vibaka Uchwara na wanafisadi nchi kwa sababu ya walio juu wanafisadi.
Raisi aliye very serious haitaji zaidi ya mwaka kuisafisha nchi na uozo wa Ufisadi uliopo!
Qualities nizionazo zinafaa kwa kiongozi ajaye
1:Muadilifu ka Mwl hapa nampa Salim Ahmed Salim
2:Mwenye vision na uwezo wa kusimamia maamuzi yake ka Paul Kagame.... Namuweka John Pombe Magufuli
3) A positive dictator ,raisi mtendaji na mwenye uchungu na nchi------- Still JPM
4)Mwenye uwezo wa kuifanya IKULU yetu kuwa maali patakatifu...........JPM
5)Kuizifanya bandari, reli na barabara zetu kuwa vipaumble vyetu kwa maendeleo, ukizingatia locality yetu katika East Africa--------------JPM
6) Kusimamia mapinduzi makubwa kwenye viwanda vyetu na kuacha porojo ya kilimo kwanza --------- Saalim Ahmed Salim
7)Mwenye uwezo wa kupiga vita UFISADI-------Samweli Sita,Harrison Mwakyembe, Dr Slaa ,Zito Kabwe, Anne Kilango etc etc.

Nakamilisha kwa kupendekeza hivi;
Raisi : John Pombe Magufuli
Waziri Mkuu Salim Ahmed Salim
Waziri wa Mambo ya ndani .. DR Slaa ( regardless ya yeye kuwa mwana Chadema)
Waziri wa Nishati na Madini : Rutabanzibwa
Waziri wa Viwanda na Biashara: Reginald Mengi "msicheke jamani" creativity yake inahitajika hasa wakati uhuu wa Shirikisho la East Africa.
Mawasiliano na Uchukuzi : Mark Mwandosya.
Wizara nyingine wanaweza kupewa vijana waliopevuka kimaadili na wenye uchungu na nchi yao "so far waliopo kwenye baraza la mawaziri wa sasa wametuangusha vijana"
HAYO NI MAONI YANGU TU MKULU!

- Mkuu ubarikiwe tunataka watu kama wewe wanaoweza kusimama na kuhesabiwa, lakini mkuu kweli Salim ni very senior halafu kua under very junior Magufuli? Imekaaje hiyo mkuu?

- Otherwise, ninaziheshimu sana choices zako Mwandosya, Dr. Slaa, Rutabanzibwa nafikiri wakati umefika wa huyu mkuu kupewa nafasi kuybwa kitaifa zaidi ya aliyonayo sasa!

Respect.

FMEs!
 
Matrekta yamekwenda...MAFUNDI wa kuyakarabati na kuyafanyia service wapo huko Urambo..??

- Mkuu Yebo yebo heshima mbele, kwanza wape wananchi matrekta halafu ya mafundi yatajiweka saawa yenyewe kutokana na mavuno ya kazi ya hayo hayo matrekta, sometimes tuwe positive jamani!

Respect.

FMEs!
 
FMES,

..Raisi hashughulikii ufisadi kwa namna ulivyoelekeza kwasababu amekosa pressure ya kutosha toka kwetu WANANCHI, na WABUNGE.

[/COLOR]
[/U]

- Hawashughulikii mafisadi kwa sababu kwanza ni marafiki zake wa karibu na pili hajapata sababu toka kwetu wananchi wa Tanzania.

es!
 
1. ..uzoefu wa Salim Salim ni ktk masuala ya diplomasia tu. katika nafasi zake zote za uongozi alizopata kushika hakuna hata moja inayohusiana/inayogusa moja kwa moja maisha ya mwananchi wa kawaida.

2. ..uzoefu wake kama waziri mkuu na baadaye waziri wa ulinzi ni wa muda mfupi sana, na alitumikia hapo muda mrefu uliopita, kuweza kunishawishi kwamba anayafahamu na anaweza kuyakabili matatizo yanayoisibu nchi yetu leo hii.

3. ..tunahitaji Raisi atakayesimamia mapinduzi ya KILIMO, VIWANDA,MIUNDO MBINU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA. tunahitaji Raisi ambaye yuko capable and comfortable dealing with the details and nuances za masuala niliyoyataja hapo juu.

4. ..pia tunahitaji Raisi Mzalendo mwenye imani ktk uwezo na vipaji vya Watanzania. Raisi ambaye atahamasisha na kuimarisha wawekezaji wazalendo wa ndani.

- Mkuu Joka, hii ni hukumu nzito sana na ndio kusimama kwenyewe huku ili kuhesabiwa, saafi sana zako ni hoja nzito sana na mimi binafsi ninazikubali sana kwamba wananchi wengi hatumjui Salim na hata wale wanaomjua wengi hawaridhiki na uwezo wake kuwa Rais.

- Lakini hii yako ni the strongest hukumu so far na imetulia sana. So far sio siri Magufuli na Dr. Slaa wanasimama juu sana na wananchi kuwakubali uwezo wao kiuongozi na hasa kupigana na vita vya mafisadi!

es!
 
Back
Top Bottom