Ubovu wa barabara Kisukulu Maji Chumvi - Segerea ni kero kubwa

YAANI NI KERO SANA HALAFU HICHO KIPANDE HAKIFIKI HATA KM 4, SIJUI NI NI TATIZO TUMEWAKOSEA NINI HASA WEE KIBONA?
 
YAANI NI KERO SANA HALAFU HICHO KIPANDE HAKIFIKI HATA KM 4, SIJUI NI NI TATIZO TUMEWAKOSEA NINI HASA WEE KIBONA?
Kibona ndo nani? au unamaanisha Mh.bona ambaye ndo mheshimiwa mbunge wetu wa jimbo la segerea?
 
YAANI NI KERO SANA HALAFU HICHO KIPANDE HAKIFIKI HATA KM 4, SIJUI NI NI TATIZO TUMEWAKOSEA NINI HASA WEE KIBONA?
Sio km 4 pale ni umbali wa km 1. Mie ndio maeneo yangu ya kukimbia mazoezi napita kuanzia Korogwe naenda mpk jeshini nakurudi na siku nyingine uwa napita hilo boda la vumbi naenda kugeuzia Segerea
 
Sio km 4 pale ni umbali wa km 1. Mie ndio maeneo yangu ya kukimbia mazoezi napita kuanzia Korogwe naenda mpk jeshini nakurudi na siku nyingine uwa napita hilo boda la vumbi naenda kugeuzia Segerea
Uyasemayo ni kweli kiongozi,hicho kipandeni kifupi sana ni suala la maamuzi(utashi wa kisiasa).
Ukiangalia umuhimu wa hii barabara,ilitakiwa hata kama si kuweka lami basi uhudumiwe kwa kuweka kifusi
ili kuwarahisishia raia wote wanaoitumia kupata riziki za kila siku.

Kuna mjumbe kasema barabara imebanwa sana,yaani watu wamejenga barabarani, ila ukweli ni kwamba ukiangalia hii barabara
na zile za mfano buguruni kwa mnyamani,na nyingine za mitaa kule temeke zilizorekebishwa huoni kama ufinyo wa barabara sio hoja.
Chukulia mfano sasa hivi ambapo pamoja na ubovu wake magari yanapishana makubwa kwa madogo,je si ikitengenezwa itakuwa bora zaidi.
 
Aisee ni kweli kabisa.ile njia ni mbaya sana kabisa. kimsing ni shortcut nzuri sana ya kwenda airport na ukonga kutokea ubungo ukitaka kukwepa folen ya Dampo,Buguruni,tazara Vingunguti na kipawa
 
Hiii barabara inakera sana, mbaya zaidi Mbunge wetu kazi kupigwa Katerero tu mpaka kutalikiwa. Yaaani kutoka maji chumvi hadi migombani unahisi gari lote limekuwa screpa kwa mashimo.
WanaSegerea tuna jambo letu 2025 ngoja mbunge aendeleze drama.
 
Hivi hakuna tunaloweza kulifanya kabla ya 2025?
Ndo maana kwenye uzi wangu nikamtaja VP Mh.Dr.Philip mpango,huyu alikuwa mwenzetu tukisali naye kigango cha Mazda pale, nikamtaja mh.Chongolo katibu mkuu wa ccm alikuwa mwanakisukulu mwenzetu,Leo Mungu amewainua hawawezi kutusaidia tukiwalilia?
na kimsingi ni maboss wa huyu mbunge ambaye haoni kama haya yanamhusu.
Hivi ni kweli wanakisukulu na watumiaji wote wa barabara hii kama short cut ya kuwahi uwanja wa ndege tunahitaji kusubiri 2025? kwenye box la kura?
 
Kiongozi wenye msemo huu hawana mbunge wa ccm,Kisukulu kuanzia wajumbe ,diwani mpaka mbunge ni ccm.
Kimsingi slogan ya mafiga matatu ilitendewa kazi lakini mateso kwa kwenda mbele.
Mwendazake alisema, wote kawabeba hakuna alieshinda uchaguzi, unategemea ufanisi? chadema hawapo sasa mpo wenyewe.
 
Ngoja nipitie kwa Dr Mangali hapa nimeze paracetamol,maana mpaka mwili unauma kwa mitikisiko ya hiyo barabara..
Pole sana mkuu,hukusoma taadhari niliyoitoa au ulipitia kujionea kwa macho yako mwenyewe๐Ÿ˜๐Ÿ˜
Wanakisukulu bado tunapiga moyo konde kwamba siku moja mamlaka husika zitatusikiliza na kulipatia suala hili ufumbuzi.
 
Mwendazake alisema, wote kawabeba hakuna alieshinda uchaguzi, unategemea ufanisi? chadema hawapo sasa mpo wenyewe.
Ni kweli tupo wenyewe,na ndo maana tunajaribu kupiga kelele ili watusikilize.
Chukulia mfano mnapokuwa kwenye daladala umesimama.ikitokea mtu akakukanyaga kwa bahati mbaya
na kwa kuwa haoni akaendelea kukanyaga mguu wako lazima umshtue ili ajue anakuumiza na mara atahamisha mguu wake.
Ni kweli mpo ndani ya daladala moja lakini aliyekanyagwa ni wewe na usiposema utaumizwa.
 
Dah,,kiongozi hii umetoa kali lakini umenisaidia,
sasa naanza kupata mwanga,ila nina swali kidogo,kwani serikali nayo inalogwa?
weeee! Jaribu kuembelea huko ujifunze kitu anzia kwenye hicho kiduka cha mbena uone..
Sirikali si ni watu bana??tena wanaenda chooni kushusha makubwa waliyo shiba vya wizi? Au unadhani ni nini??
 
weeee! Jaribu kuembelea huko ujifunze kitu anzia kwenye hicho kiduka cha mbena uone..
Sirikali si ni watu bana??tena wanaenda chooni kushusha makubwa waliyo shiba vya wizi? Au unadhani ni nini??
Funguka zaidi maana maana sijakupata vizuri point yako.
Kwani pale mbena si anapanga? au ni nyumbani kwake,na kama ni issue ya
ufinyu wa barabara,mbona buguruni kwa mnyamani kumetengenezwa na vichochoro vingi kule temeke
iweje kisukulu ndo ufinyu wa barabara uwe issue kubwa kiasi kwamba barabara haitengenezwi. Pia najaribu kuunganisha dots kati ya uchawi na ubovu wa barabara nashindwa kupata majibu ndo maana nakuomba ufunguke zaidi.
 
funguka!! funguka mpaja saa ngapi bana weee!!! jiongeze. Af punguza kunywa uji asubuhi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ