Kigamboni: Wakazi wa Mtutu walia na ubovu wa barabara

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Baada ya Wakazi wa Mbutu, Mkwajuni Wilayani ya Kigamboni kufunga barabara kutokana na kero mbalimbali za miundombinu, @AyoTV_ imefika eneo la tukio na kuongea na Wakazi wa maeneo hayo ambao wamedai wanashindwa kupata huduma muhimu kutokana na changamoto hiyo.

Frank Nkunda ambaye ni Mkazi wa maeneo hayo amenukuliwa akisema “Sisi Wananchi kwa muda mrefu kero ambazo zinajitokeza hapa kuhusu barabara kutoka Mkwajuni hadi hapa ni Tsh. elfu 3, gari ndogo ndio hazipiti kabisa maisha yamekuwa magumu huduma nyingi zipo Mkwajuni ambapo ni shida kufika, kwahiyo leo kwa pamoja tukawasubiri Viongozi kuona nini kifanyike ndio tukawaambia tunafunga barabara ili kilio chetu kiweze kusikika”

Kwa upande wake, Ipuli Sagula Mkazi wa eneo hilo amesema “Nakumbuka juzi Mwanamke alijifungua kwa kukosa usafiri kwenda sehemu husika na Mimi mwenyewe Kijana wangu alivunjika mguu lakini yupo nyumbani maana Toyo ilishindwa kumfikisha sehemu husika tumejirabu kutumia uongozi kukubaliana kwa kutwa wamwage maji mara tatu”

Kwa upande wake Msaidizi wa Meneja wa TARURA Kigamboni, Edger Kimaro amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo “Ni kweli kuna hiyo changamoto tulifika pale na Polisi tumeiona lakini kimsingi Wananchi kuna information walikuwa hawajaziwasilisha ambapo kupitia Serikali ya Mtaa tukazungumza nao pamoja na Watu wa malori hivyo tukakubaliana na ngazi ya juu kurekebisha hiyo barabara”
 
Back
Top Bottom