Katavi: Ubovu wa barabara katika Manispaa ya Mpanda, TARURA yanyooshewa kidole

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987

Ubovu wa barabara nyingi katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi umetajwa kuwa kero katika shughuli za kibinadamu hasa katika kipindi hiki cha masika ambapo barabara nyingi zinaendelea kuharibika na zingine kutelekezwa licha ya ahadi kutolewa na Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA).

Baraza la Madiwani Manispaa ya Mpanda limebainisha hayo na kuelezea kuwa barabara nyingi si rafiki katika shughuli za kimaisha ambapo wameilalamikia TARURA kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo katika kutengeneza na kukarabati barabara zilizopo katika manispaa hiyo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda, Haidari Sumry ameeleza kuwa amesikitishwa na uwajibikaji wa TARURA Mpanda.

Amesema barabara nyingi hazipitiki na hazileti taswira nzuri katika makao makuu ya mkoa wa Katavi huku akisisitiza TARURA kutanua wigo wa bajeti.

Joseph Hoza, Meneja wa TARURA amekiri kuwepo Kwa barabara nyingi ambazo si rafiki kwa watumiaji na vyombo vya usafiri, ambapo amewahakikishia madiwani kutengenezwa na kukarabatiwa barabara hizo kadri bajeti itakavyoruhusu.

Aidha, Hoza amesema Serikali inaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kufungua, kutengeneza na kukarabati barabara katika Manispaa ya Mpanda ambapo amesema kwa sasa bajeti haitoshelezi kukidhi mahitaji.
 
Huko Katavi ninachokumbuka ni Mahanga the great.... Poleni Sana mana jamaa alikuwaga mpambanaji na haigopi serikali
 
Back
Top Bottom