Ndugu wana jamvi nikiwa kama mmoja wa wakazi wa kivule naomba mawazo yenu pengine ninyi mliwahi fanikiwa mlipokuwa na shida kama ya kwetu.
Ili kufika kivule njia kuu ni moja kupitia banana - kitunda - kivule, ni barabara yenye urefu wa takribani km 12hv
Kero kubwa tunayokabiliana sisi wakazi wa maeneo haya ni ubovu wa barabara ambao umepitiliza na hakuna kiongozi yoyote anayeonekana kujali licha ya kuwepo kwa hospitali kubwa iliyojengwa enzi za mwendazake na kupewa hadhi ya hospitali ya wilaya ila kwa hali ya barabara iliyopo kama mgonjwa akipakiwa kwenye ambulance kutokea kivule hadi amana ama muhimbili ni dhahiri hali yake itakuwa mbaya zaidi kwani kutokana na kuchekewa njiani na kurushwarushwa awapo ndani ya ambulance.
Barabara hii ipo katika ilani ya chama kuwekwa lami kwa ukamilifu ila hakuna dalili, hapo Kati alimfanya ziara mkuu wa mkoa Chalamila wakati akizungumzia ubovu wa barabara akasema wananchi tutulie tungetaka barabara safi tungejenga magomeni. Mbunge wetu haoneshi ushirikiano kwa wanakivule, diwani haonekani, mkurugenzi inawezekana anaungana na mkuu wa mkoa ki mtazamo.
Nina Imani ya kuwa humu kuna wabobezi wa mambo na kupitia jukwaa hili sauti hufika mbali.
Tunaomba ushauri nini tufanye kuilazimisha serekali yetu sikivu itukumbuke wakazi wa kivule?
Nawasiliaha.