SoC02 Uboreshaji wa huduma za afya unavyoweza kuchochea maendeleo ya taifa

Stories of Change - 2022 Competition

Davison03

New Member
Aug 23, 2022
4
1
UTANGULIZI
Huduma za afya ni jumla ya huduma za umma zinazotolewa ili kuboresha afya ya wananchi. Mfano wa huduma za afya ni pamoja na uboreshaji wa mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi katika vituo vya afya na hospitali,ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya, malipo bora kwa watumishi wa afya , utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kulindaa afya zao na pia kuhimiza wananchi juu ya kuimarisha afya zao kwa kufanya mazoezi ili kuweka miili Yao imara na hivyo kujikinga na maradhi mbalimbali.

UMUHIMU WA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NA MANUFAA YAKE KATIKA KULIJENGA TAIFA NA KUCHOCHEA MAENDELEO YA TAIFA
Huduma za afya ni chanzo cha ajira kwa taifa. Kama taifa litaamua kuboresha huduma za afya kwa kujenga vituo vingii vya afya na hospitali litakuwa limeweza kutatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana ,ambapo vijana wengi (wasomi na wasio wasomi) watapata ajira za kujenga majengo ya kutolea huduma za afya na hivyo kuweza kukidhi haja zao za maisha na hivyo kukuza uchumi wa mmjammoja na taifa kwa ujumla. Pia wataalamu wa afya ambao hawajapata Ajira wataajiriwa na hivyo kutatua tatizo la ajira kwa kiasi kikubwa na hivyo kuchochea maendeleo ya taifa la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Huduma bora za afya zitaweza kukuza biashara na shughuli za kiutalii nchini. Huduma bora za afya ikiwemo miundombinu bora ya utoaji wa huduma za afya na uwepo wa wataalamu wabobezia katika utoaji wa huduma za afya itawavutia wagonjwa we wengi kutoka nchi za nje (ndani ya Africa na nje ya Africa) kuweza kufuata huduma bora zitolewazo nchini kwetu Tanzania, na hivyo kupitia ujio wa wageni wengi kufika Tanzania tutakuwa tumetangaza utalii wa nchi kwa kiasi kikubwa na pia kukuza shughuli za kibiashara nchini. Na hivyo kukuza maendeleo ya taifa.

Huduma za afyaa kuweza kuongeza nguvuu kazi ya TAIFA katika kulijenga taifa. Taifa lililoendelea ,maendeleo hayo hujengwa na vijana wenye afya bora na nguvu, taifa imara haliwezi likajengwa na watu legelege, hivyo basi lazima tutambue kuwa kama tunataka kuimalisha uchumi wa taifa ,,lazma tuwekeze katika afya zetu ,ili kufanikisha shughuli za kiuchumi na ujenzi wa mikondo ya maendeleo ya taifa letu . Na hivyo kuweza kukuza uchumi na maendeleo ya taifa letu.

NINI KIFANYIKE ILI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI
Serikali lazima ihakikishe Kuna uwepo wa wataalamu wabobezi na maridadi katika kutoa huduma za afyaa. Hivyo serikali inapaswa kufanya yafuatayo;

Kutoa kipaumbele kwa vijana wanaosoma kozi za afya kama ,MD, DDS, PHYSIOTHERAPY, RADIOLOGY, MEDICAL LABORATORY, NURSING, PHARMACY NA ENVIRONMENT HEALTH SCIENCES. Kutokana na ghalama ya kozi hizi katika elimu ya juu vijana wengi wameshindwa kusoma kwa sababu ya maisha magumu na hivyo kushindwa kusoma na kuendelea na masomo serikali lazima itambue kwamba kutokana na kuwepo kwa badiliko kubwa la mtindo wa maisha hivyo magonjwa kama kiharusi(stroke), kisukali( diabetes mellitus), obesity(unene uliopita kiasi) arthritis ( maumivu ya jointi) nk.

Yamekithili sana katika nchi yetu hivyo ipo haja ya serikali kuzidi kutoa kipaumbele katika kubolesha afya za wananchi na kuepuka wimbi kubwa la ukosefu wa wataalamu wa afya. Kwa kufanya ivoo tutakuwa tumeboresha huduma za afya kwa kiasi kikubwa.

Kujenga na kuweka mazingira mazuri ya kutolea huduma za afya. Serikali inapaswa kujenga miundombinu rafiki kwa watoa huduma na wagonjwaa kwa ujumla kuweza kupata huduma za afya kwa ufanisi wa hali ya juu ikiwemo kuongeza malipo kwa wahudumu wa afya na kujenga mazingira mazuri ya kuwapokea wagonjwa ili waweze kupokea huduma zao mapema na kwa ufanisi, ipo shida kubwa katika sekta za afya za kiserikali katika utoaji wa huduma za afya kwa mfano imekuwa ni desturi kwa watanzania kuamini kwamba sehemu ambayo wanaweza wakapata huduma bora za afya ni katika hospitali binafsi yaani PRIVATE HOSPITAL, na hii ni kwa sababu ubora wa huduma za afya katika hospitali binafsi ni mkubwa ukiringanisha na serikalini (Government hospital) kwa sababu ya malipo bora kwa wahudumu wa afya na ufanisi mkubwa katika utoaji wa huduma za afya.

Hivyo basi ipo haja ya serikali kuona namna ya kufanya ili kuboresha malipo ya wahudumu wa afya serikalini ili kuweza kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya katika hospitali za serikali ( Government hospitals).

Pia serikali inapaswa kutoa fursa kwa wanafunzi na wataalamu wa afya kufanya tafiti za magonjwa mbalimbali hasaa yasiyojulikana ili kupatiwa uvumbuzi . Hivyo basi serikali inatakiwa kutoa mtaji wa kufanyia tafiti hizo ili kuweza kupata uvumbuzi wa tiba ya magonjwa na maradhi mbalimbali ambayo bado hayajapatiwa uvumbuzi,

kwa kufanya ivyo tutakuwa tumezuia kwa kiasi kikubwa vifo vitokanavyo na maradhi hayo na hivyo pia kuvutia pia nchi za nje kufuata huduma bora nchini na hivyo kuweza kutangaza utalii na kukuza maendeleo ya taifa letu kwa ujumla. Kwa mfano ipo haja ya kuhimiza na kujenga mazingira kwa wanafunzi wa vyuo vya afya kama Muhimbili university of health and allied science (MUHAS) ,KCMC, CUHAS nk. Kuwawezesha wanafunzi hao kufanya tafiti mbalimbali zitakazoweza kuleta mabadiliko chanya katika utoaji wa huduma za afya nchini.

Kutoa fursa ya masomo ya kibingwa na kibobezi nje ya nchi ( hasa katika nchi zililokua katika sekta ya afya) ili kuweza kuongeza huduma za kibingwa katika hospitali zote nchini ( za wilaya,mikoa,kanda na rufaa) hii utaweza kuongeza ujuzi mkubwa katika utoaji wa afya na hivyo kupunguza au kufuta kabisa ghalama ya kusafirisha wagonjwaa kwenda kutibiwa nje ya nchi na hivyo kusababisha nchi kuwa na uchumi imara kwa kuepuka ghalama izoo.

MWISHO
Mapendekezo yangu kwa serikali juu ya utoaji wa huduma za afya nchini ni kwamba ipo haja ya serikali kuunda sera mpya itakayoweza kuipa kipaumbele sekta ya afya ili kuweza Kuboresha huduma za afya nchini kwa maendeleo ya taifa letu la Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Kama tulivoweza kuona hapo juu umuhimu wa uboreshaji wa huduma za afya unavyoweza kuleta mabadiliko makubwa na chanya katika kukuza na kuchochea maendeleo ya taifa letu.
 
Naombeni support yenu katika story yangu yenye kuleta mabadiliko chanya katika jamii zetu na maendeleo ya taifa kwa ujumla.🙏🙏🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom