Asilimia 85 ya Wajawazito wanajifungulia katika vituo vya kutolea Huduma za Afya

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Wajawazito.jpeg
Moja ya kiashiria kikuu cha ubora wa Huduma za Afya ni kiwango cha wajawazito wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya ambapo kwa Mwaka 2023 kimeongeka kwa 85% kutoka 81% Mwaka 2022.

Waziri Ummy Mwalimu amesema hayo Januari 10, 2024 wakati akitoa taarifa ya hali ya utoaji huduma za Afya nchini kwa mwaka 2023 wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari uliofanyika kwenye ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es Salaam.

“Lengo la nchi ni kufikia asilimia 95 ya wanaojifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya ifikapo mwaka 2030,” amesema Waziri Ummy.

Amesema, Mwenendo huu wa utumiaji wa huduma unaendana na takwimu zinazosema vifo vitokanavyo na Uzazi vimepungua kwa asilimia 80 kutoka mwaka 2016 hadi 2022.
 
Back
Top Bottom