Mbunge Cherehani: Boresheni Huduma za Afya kwa Wazee

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

Mbunge Cherehani: Boresheni Huduma za Afya kwa Wazee

Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani amemuomba Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Ushetu Athuman Matindo kuboresha huduma kwa wazee ambao wanavitambulisho maalum kutoka ofisi ya serikali ya kijiji ili wapate huduma kwa wakati.

Amesema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Nsalaba Kata ya Chona Halmashauri ya Ushetu ambapo amesema amepokea malalamiko ya wazee katika kata hiyo kwamba wanachelewa kupata huduma katika vituo vya afya na Zahanati kutokana na kutokuwa na kadi ambazo hazijawafikia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Shinyanga ambae ni diwani wa kata hiyo Mabala Mlolwa amesema ,kutokana na changamoto ya ukubwa wa Halmashauri hiyo, ni vyema wazee watambuliwe kwa kutumia barua za wenyeviti wa vijiji wanapotoka.

Akijibu malalamiko hayo mganga mkuu wa Halmashauri hiyo Athuman Matindo amekiri kuwepo kwa changamoto hizo na kwamba anawaelekeza waganga wafawidhi wa vituo vyote vya afya na zahati kuhakikisha wanatoa huduma kwa kuwapa kipa umbele wazee katika madirisha yao.

Awali akizungumza kwenye mkutano huo mmoja wa wazee wa Kata ya Chona amesema, hawapati huduma katika vituo vya afya na zahati licha ya kuwa serikali imetenga dirisha la wazee kwa kigezo cha kukosa kadi ambazo zinatolewa na ustawi wa jamii ikiwa wameshindwa kugawa kadi hizo kwa wakati kutokana na ukubwa wa Halmashauri hiyo.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-03-12 at 01.14.49.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-12 at 01.14.49.jpeg
    36 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-03-12 at 01.14.50.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-12 at 01.14.50.jpeg
    71.4 KB · Views: 1
Back
Top Bottom