Ubobezi katika sheria wa Tulia Ackson ni upi?

Ubobezi katika sheria wa Tulia Ackson ni upi?

mkuu Nzi elimu ulitoa kwenye uzi huu ni somo tosha!
 
Last edited by a moderator:
Ile mita 200 ambayo ilmchukua week nzima kutoa ufafanuzi

Pamoja kulazimisha mita 200 hazina uhalisia. Vituo vyote vya kupigia kura viko kwenye makazi ya watu. Sheria Ina madhumuni gani? Kwa nani? Haki inaonekana kutendeka?
 
Hebu ngoja tutumie mantiki kidogo. Haya, anadai kabobea kwenye kutafsiri kanuni za bunge, sheria za nchi na katiba. Huo ubobezi kaupataje? Keshawahi kufanya kazi bungeni na kupata tajiriba ya kiutendaji [practical experience]?

Ni wapi, lini, na kwa muda gani kawahi kutafsiri kanuni za bunge?

Jibu rahisi ni kwamba ameshiriki kutunga kanuni na sheria zote za bunge la katiba ambapo kimsingi halikua na tofauti kibwa ya kiutendaji na bunge la kawaida
 
Haya ni maswali magumu kupata majibu yake kwa nilichokiandika na kusikia video ya kujieleza kwake...hivyo kusema kwamba amebebwa ni sahihi kabisa...kwa sababu bado sijaona vigezo vya kumfanya apate hii hype inayotengenezwa..

Mkuu Nzi mwanzo nilidhani unania nzuri tu ya kisomi kutaka kujua ubobezi wa Dr Tulia kwa jicho la kisomi
Lakini sasa unaonyesha rangi zako, kumpinga kupata nafasi hiyo kwa kusema hakustahiki na amebebwa

Kuna hoja mbili hapa kuwa mbobezi na kubebwa!!!!

Kwanini kabebwa? Je hakustahiki nafasi hiyo kwasababu sio mbobezi?

Mkuu hukuwa na nia ya kuonyesha Dr Tulia sio mbobezi bali nia yako ilikua ni kumshusha na kuonyesha hastahili nafasi hiyo bali amebebwa kitu ambacho sio cha kweli

Nafasi ya naibu spika haina kigezo cha mbonezi kama ambavyo Magdalena sio mbobezi popote wala Makinda hakua mbobezi na wala Ndugai hakua mbobezi
 
Last edited by a moderator:
Nzi

unapoteza muda wako

article ndeefu kisa unataka kum dis mtu?

unafahamu journals ngapi dunia hii?

unafikiri waalimu wa UDSM ni vilaza? ulizia mkuu

suppose sio au hana elimu au hana ubobezi, unachotaka kusema nini hasa

Ni naibu spika, wewe haujawa, ni PhD holder wewe hauna,ni notable figure wewe ni NZI TU

Dah kweli jpm anakazi kubwa!
sijuwi kama unajijua kuwa nawewe ni jipu!
hii ni kutokana na comment yako!
pole mkuu.
 
Huyu dada hata lugha yake ya mwili inaonyesha kawekwa tu hapo.

Kuna kila dalili ya yeye kuwa na mtu au watu nyuma yake.

Sasa hebu jiulize...hivi kweli angeuweza uspika huyo?

Unajua kuna mambo mengine hayaingii kabisa akilini aisee.

Mkuu wakati mwingine mnapenda sana kuishi maisha ya kufikirika
Wewe kwaakili yako unaamini Dr Tulia amekua naibu spika by coincidence? Hata huko "Duniani" kwenyewe huwezi tu kupata nafasi fulani kwasababu katiba inasema, vetting is everything kwa manufaa ya wenye rungu!!!!!!

Kila system ina namna yake ya kufanya kuweka viongozi wake watendaji, sasa kama wewe hupendezwi nayo hayo ni matatizo yako binafsi
 
Mkuu wakati mwingine mnapenda sana kuishi maisha ya kufikirika

Oh really?

Wewe kwaakili yako unaamini Dr Tulia amekua naibu spika by coincidence?

Huyo hafai kabisa kuwa naibu spika. Wingi wa CCM tu ndo umembeba. Na kwa jinsi tu mambo yalivyo unfold inaonyesha wazi kuwa kuna mtu au watu wenye nguvu nyuma yake.

Hata huko "Duniani" kwenyewe huwezi tu kupata nafasi fulani kwasababu katiba inasema, vetting is everything kwa manufaa ya wenye rungu!!!!!!

Kwani huyo dokta wako kapata unaibu spika kwa sababu katiba inasema? Katiba inasema nini?

Kila system ina namna yake ya kufanya kuweka viongozi wake watendaji, sasa kama wewe hupendezwi nayo hayo ni matatizo yako binafsi

Na wewe kama hupendezwi na kutopendezwa kwangu basi hilo ni tatizo lako na lako binafsi.
 
Siko sure but nimesikia inahusu Miss Tanzania
thats why nataka mtu alie sure atuletee majibu..

Nafahamu jambo moja kuwa kabla ya kuteuliwa mkuu wa wilaya moja kusini na baadae mkuu wa mkoa wa Dodoma,Dr Nchimbi alikuwa ni Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Historia pale UDSM!kwamba amebobea au hakubobea katika "Histroria ya Ulaya" au la sifahamu!
 
Jibu rahisi ni kwamba ameshiriki kutunga kanuni na sheria zote za bunge la katiba ambapo kimsingi halikua na tofauti kibwa ya kiutendaji na bunge la kawaida

Kushiriki kutunga sheria za bunge la katiba kunampa mtu sifa za kuwa "mbobezi"washeria na kanuni za bunge?
 
Waberoya ukifuata maana na maisha ya (jina) lako kwenye msaafu wa Biblia hao jamaa hawakuwa kama wewe unavyoonekana kupitia comment yako.

Ila umekurupuka kujibu na yawezekana ule msemo wa watz wavivu kusoma ulikuathiri, mtia mada ameongelea kitu tofauti na ulichoandika kujibu hoja.

Kwa jibu la platozoom linakufaa sana na nime_like KUBWA, badirika ndugu.

Post hii hapa #6
 
Last edited by a moderator:
kwa bandiko hili university of dar es salaam ina wakufunzi na inazalisha wataalam vilaza.
 
Hivi tukimchukua Dr.Tulia tukamlinganisha na Mh.Ndugai na mama Makinda mathalani, hivi hawa kwenye ubobezi wa sheria wapo sawa? Hivi hili neno kubobea nd'o linalotoa mtu roho kujaribu kufanya mjadala usioisha? Basi tufanye DrTulia ni msomi mzamivu wa sheria hajabobea kama ambavyo inaonekana Nzi,Nyani Ngabu and Co hilo linawatesa sana. Manake hata tujadili vipi habari haibadiliki nd'o naibu spika sasa yupo anakula bata sasa. Na si mbobezi.
 
Kabisa mkuu. Hiyo ndiyo practice....



Mkuu hawa watu wengine ni wa kuwashangaa tu....sasa unajiuliza mtu unaanzaje kuwalinganisha Lissu na Tulia kwa kutumia muktadha wa ubobezi wa kisheria kwenye akademia? Jambo la kuhuzunisha ni kwamba unaweza kukuta hawa wanaoongea hivi ndiyo washauri wa CCM..

Mimi nakushauri uachane na watu wa namna hii. Mada uliyoitoa imekaa kitaalamu zaidi na wale ambao hawana uzoefu na haya mambo wangeomba msaada wakasaidiwa.

Na hapa ndipo tunapodondoka kama taifa, kuchanganya mambo ya kitaalamu na porojo.
 
toa evidences kama mkuu Nzi alivokata ngebe za wadandiaji

Sikiliza ndugu, huu ni mjadala wa mambo ya taaluma. **** huna uelewa wa mambo hayo, soma na kuishia hapo.

Mimi sina tuhuma wala sababu yoyote dhidi ya Tundu Lisu na uwezo wake katika sheria akiwa Wakili wa mahakama kuu. Nimeshaona kazi zake na zimeniridhisha. Nzi alitaka kujiridhisha kama kweli Tulia ni mwanasheria mmbobezi tena kwenye mambo ya katiba na utawala/bunge. Amefanya kazi yake vizuri kwa sababu alikuwa na motives. Na kazi hii siyo ndogo kwani huwezi kuifanya kwa muda wa masaa kama unavyofikiria. Yet he did it in the highest standard and diligently.

Kwa hiyo, kama wewe unataka kujua habari za Tundu Lisu basi unaweza kunipa consultancy nikusaidie. Vinginevyo nina mambo mengine ya maana na yanayonilipa kwa kila muda wangu ninaotumia!
 
Last edited by a moderator:
68afde53fa17bc6c9ad649432ed3c76b.jpg
 
kuwa dr. si kigezo cha mtu kuwa mbobezi . kwa tuliofika university tunao ma- dr wengi tu vilaza kazi yao kutoa assignment kila siku na usumbufu usio na maana kwa wanachuo . ila kwa mtu ambaye hajafika chuo anaona phd kama kitu cha ajabu sana

YOU HAVE SAID IT WELL
.
Ongezea: Tunasumbuliwa na intellectual arrogance..ni ukweli usiopingika kua wakati kuna mataifa yanawasifu wasomi wao kwa Tija wanayoletea Taifa...mfano kuandika na kutekeleza mipango ya kiuchumi..sisi bado tuko kwenye kuabudu ma degree yasiyo na tija yanayofanya vijana watoke vyuoni wakiwa na mentality za white colar jobs..wakariri slides..wasio weza ku think out of the box....kuwa na phd...na kuwa productive ni two variables ambazo sometime hazina uhusiano!
 
Hio kesi ya mt 200, soma hukumu,tusiwasingizia majaji walifanya kazi yao kitaaluma, walichofanya serekali wanajua wenyewe,
 
kama mbobezi wa sheria ameshindwa swali moja, lini alijiunga na ccm akashindwa, ina maana hata akiulizwa lini alijiunga chuo kikuu atashindwa kujibu, ukweli akili za watu wengi zimedumaa wanauwezo wa kukariri lakini sio ukifikiri, Na kuhakikishia alichokaririshwa na ccm ndicho atakachofanya kwenye kiti cha spika.

Iq and level of education are two different things, knowledge can be easily attained by getting high quality education or pursuing degrees in school. on other hand, IQ is measured according to the actual capacity of the brain to process various types of information.
 
YOU HAVE SAID IT WELL
.
Ongezea: Tunasumbuliwa na intellectual arrogance..ni ukweli usiopingika kua wakati kuna mataifa yanawasifu wasomi wao kwa Tija wanayoletea Taifa...mfano kuandika na kutekeleza mipango ya kiuchumi..sisi bado tuko kwenye kuabudu ma degree yasiyo na tija yanayofanya vijana watoke vyuoni wakiwa na mentality za white colar jobs..wakariri slides..wasio weza ku think out of the box....kuwa na phd...na kuwa productive ni two variables ambazo sometime hazina uhusiano!

Kweli kabisa Mkuu. Kama nchi, tumeshindwa kabisa kuwapima wasomi wetu kwa utendaji na uzalishaji badala yake tunawapima kwa vyeti na GPAs. Tunashindwa kujua kuwa hivyo vipimo tunavyotumia havina tija kama haviwezi kubadilishwa na kuwa products. Ndiyo maana watu wanahangaika kutafuta vyeti hata kwa njia haramu!
 
Mkuu Nzi mwanzo nilidhani unania nzuri tu ya kisomi kutaka kujua ubobezi wa Dr Tulia kwa jicho la kisomi

Bwana Paulo, mbona hili nimelisema vizuri tu katika posts zangu zote? Wewe endelea kudhani tu, wakati jambo lipo wazi.

Lakini sasa unaonyesha rangi zako, kumpinga kupata nafasi hiyo kwa kusema hakustahiki na amebebwa

Ni kweli. Napinga upotoshwaji unaofanywa na watu wa CCM katika kumjengea Tulia taswira ya 'ubobezi' wa kisheria. Jambo ambalo kwa masikitiko makubwa Tulia mwenyewe 'amemezeshwa' na kusema kuwa yeye ni 'mbobezi' kikazi katika kutafsiri kanuni za Bunge, sheria za nchi na Katiba, kinyume na 'CV yake inavyoonesha. Nimeweka msisitizo kwenye neno kikazi, ili kuonyesha ni kwanini nimeamua kumchunguza kwenye engo ya akademia.

Kuna hoja mbili hapa kuwa mbobezi na kubebwa!!!!

Kulikuwa hakuna haja ya CCM kutengeneza hype juu ya bidada Tulia. Kwanini tu wasingesema huyu bidada ni msomi wa sheria tu. Lakini kwa kutaka kutuaminisha kuwa ni 'mbobezi', kwamba ni bora kuliko wengine, hapo ndipo mantiki yangu ya kusema kabebwa inapokuja. Hata ukitumia literal translation ya kubebwa, utapata mantiki yangu; yaani CCM kwa kutumia kigezo cha 'ubobezi' wakaamua kumbeba Tulia juu ya wengine. Hili ndilo ninalolipinga, kwani hana sifa hiyo ya ubobezi hata punje.

Kwanini kabebwa? Je hakustahiki nafasi hiyo kwasababu sio mbobezi?

Hakustahili kupata nafasi kama kigezo ambacho CCM walikitumia ni ubobezi kwenye sheria.

Mkuu hukuwa na nia ya kuonyesha Dr Tulia sio mbobezi bali nia yako ilikua ni kumshusha na kuonyesha hastahili nafasi hiyo bali amebebwa kitu ambacho sio cha kweli

Narudia tena kusema, kwa kuwa CCM wanataka kutuaminisha kuwa Tulia Ackson ni mbobezi katika fani ya sheria, in fact, hata bidada mwenyewe kasema alipokuwa akijieleza Bungeni, na kwa vile nimeonyesha Tulia hana ubobezi wowote katika fani ya sheria ki-akademia (kikazi kama alivyosema mwenyewe), basi hitimisho ni rahisi tu Bwana Paulo, kabebwa. Hili wala huhitaji kuumiza kichwa kulifikia.

Kama siyo kweli kabebwa kwa kutumia kigezo cha ubobezi, basi jibu swali langu. Maana hadi sasa unakwenda na kurudi, lakini hujajibu swali langu la msingi: upo wapi huo ubobezi wa Tulia Ackson katika sheria kama inavyosemwa? Jibu hili ni kuni-prove wrong kwa kuonyesha kuwa halistahili kupata nafasi kwa kigezo cha ubobezi katika taaluma ya sheria. It is that simple Paul.

Nafasi ya naibu spika haina kigezo cha mbonezi kama ambavyo Magdalena sio mbobezi popote wala Makinda hakua mbobezi na wala Ndugai hakua mbobezi

Hili nakubaliana nawe. Lakini tafadhali usitake kuchanganya mambo. Hapa ninachoongelea ni ubobezi wa Tulia katika taaluma ya sheria, kama alivyosema yeye (kwamba ni mbobezi kikazi kwa miaka 14) na kama wanavyosema watu wa CCM. Kama alivyosema mkuu Dark City, usichanganye ubobezi wa mwanataaluma na practitioner. Haya ni maeneo mawili tofauti. Kwa sababu tukienda kwa vigezo vya ubobezi kwenye practice, Tulia hawezi kushindana hata na Sakaya, Makinda wala Ndugai. Wapo miles ahead of her.

Kuhusu vigezo vya nafasi ya Naibu Spika: ukiangalia kifungu cha 85 (vifungu vidogo vya 1 na 2) cha Katiba yetu, utaona kabisa zaidi ya kusema kuwa NS atachaguliwa miongoni mwa wabunge, na hatopaswa kuwa waziri, naibu waziri au mtu mwingine mwenye madaraka yoyote kama itakavyotajwa na sheria za Bunge, hakuna vigezo vingine zaidi ya hivi. Hivyo basi, hii inadhiirisha ni jinsi gani CCM wasivyofahamu hata Katiba ya nchi hii. Kulikuwa hakuna haja ya kutengeneza hype juu ya 'ubobezi' na upekee wa Tulia Ackson katika sheria ili ku-justify ugombeaji wake wa nafasi ya NS. Lakini kwa sababu ya mbeleko, utengenezwaji wa hype ulikuwa haepukiki. Nilichofanya ni kupinga upotoshaji huo na kuonyesha kuwa bidada Tulia siyo mbobezi katika sheria kama anavyodai na CCM wanavyotuaminisha. Nimetumia tu uhuru wangu kutenganisha ukweli na uongo; ili ukweli ubaki kuwa ukweli, na uongo uendelee kuwa uongo.

Sasa jibu swali langu: upo wapi huo ubobezi wa Tulia Ackson katika sheria kama inavyosemwa?
 
Back
Top Bottom