Ubobezi katika sheria wa Tulia Ackson ni upi?

Ubobezi katika sheria wa Tulia Ackson ni upi?

Ubobezi katika sheria wa Tulia Ackson ni upi?

8.jpg

Chanzo: CCM Blog: DK TULIA ACKSON NDIE NAIBU SPIKA WA BUNGE LA 11 LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Salaam,

Jana Tanzania iliweza kupata Naibu Spika wa Bunge la 11. Ni Tulia Ackson, aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali ya JMT, mjumbe wa Bunge Maalumu la kutunga Katiba, na Mhadhiri wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Pamoja na hizo nafasi ambazo alikuwa nazo awali, 'sifa' kubwa ambayo Tulia Ackson amekuwa akitajwa kuwa nayo ni ubobezi katika sheria.

Gazeti la Habari Leo limeandika, "Dk Tulia anakuwa Naibu Spika wa kwanza katika siku za karibuni, asiye Mbunge wa Jimbo, lakini akiwa amebobea katika sheria." Mawaziri- Majaliwa muadilifu, hana makuu

Likaendelea, "Alikuwa Mjumbe wa Bunge la Katiba na ni mtaalamu katika sheria za hifadhi za jamii, kazi, uhifadhi wanyamapori, udhamini, sheria ya usimamizi wa mirathi, ufadhili miradi na madini.
"http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/3727-mawaziri-majaliwa-muadilifu-hana-makuu

Na mengi ya kufafanana na sifa hiyo yamesemwa na watu hapa JF.

Sasa kwa minajili ya kutaka kufahamu ubobezi wake katika sheria (naomba kusema wazi kuwa mimi siyo mtaalamu wa sheria, na nilikuwa simfahamu Tulia Ackson. Ila napenda kujifunza nini watu walio wabobezi katika fani fulani wanafanya), nikaamua kufanya 'utafiti' kidogo. Lengo kuu la 'utafiti' huu usio rasmi ilikuwa ni kuangalia mchango wake kama Mhadhiri wa Sheria katika fani ya Sheria. Ninaposema mchango wake katika fani ya Sheria, ninamaanisha kuangalia machapisho yake katika majarida ya kitaifa na kimataifa katika fani ya Sheria. Katika akademia, ubobezi wa mtu utokana na nini alichochapisha, wapi alipochapisha (ikimaanisha viwango vya majarida husika katika fani), na watu wangapi wamesoma na kwa muhimu sana, kuyanukuu machapisho yake.

Ni rahisi sana kufahamu ubobezi wa mtu katika fani kwa sasa. Njia rahisi ni ya kutumia Google Scholar, kama injini ya kutafutia machapisho ya mtu fulani na kuangalia 'ubobezi' wake. Lakini, hii itategemeana kama mtu huyo ana akaunti katika Google Scholar. Kama hana, kuna vyanzo vingine maarufu kama, Researchgate na Academia.edu.

Kwa hiyo nilianza kwa kuandika jina "Tulia Ackson' katika Google Scholar, kwa bahati mbaya Tulia Ackson hana akaunti katika Google Scholar. Lakini machapisho yake yaliweza kujitokeza, ambapo niliweza kuona jumla ya machapisho 8 aliyoandika Tulia Ackson. Katika machapisho hayo 8, Google Scholar ilinionyesha idadi ya machapisho yaliyoweza kunukuu machapisho ya Tulia Ackson. Hapa chini naorodhesha machapisho hayo, na kuweka idadi ya nukuu za machapisho.

1. "Disability benefits and workers with HIV/AIDS: Coverage issues and challenges in the United Republic of Tanzania" - hili alichapisha katika jarida liitwalo International Social Security Review, mwaka 2008.
Linapatikana hapa: Disability benefits and workers with HIV/AIDS: Coverage issues and challenges in the United Republic of Tanzania - Ackson - 2008 - International Social Security Review - Wiley Online Library

Na toka mwaka huu, Google Scholar inaonyesha kuwa chapisho hili limenukuliwa mara moja tu. Na aliyelinukuu ni Abdallah Possi katika tasnifu yake ya shahada ya uzamivu mwaka 2014. Inapatikana hapa: www.opus4.kobv.de/opus4-fau/frontdoor/deliver/index/docId/5940/file/THESIS_Possi.pdf

2. "Justiciability of Socio-economic Rights in Tanzania" - hili amelichapisha katika jarida liitwalo, African Journal of International and Comparative Law, mwaka 2015. Linapatikana hapa: An Error Occurred Setting Your User Cookie

Mpaka natumia Google Scholar muda mfupi uliopita, chapisho hili lilikuwa halijanukuliwa.

3. "Social Security Fragmentation in Tanzania: The Challenge of Governance" - hili aliliandika akiwa mwanafunzi wa shahada ya uzamivu pale Chuo Kikuu cha Cape Town, Afrika ya Kusini, mwaka 2008. Linapatikana hapa: http://www.idll.uct.ac.za/usr/idll/resources/monographs/IDL_monograph_2008-1.pdf

Aliliandika kama Monograph iliyotakana na tasnifu yake ya shahada ya uzamivu. Nalo toka mwaka huo, alijawahi kunukuliwa kwa mujibu ya Google Scholar.

4. "The role of the law of regional organisations in reforms of social protection systems: portability of social security benefits in the East African Community" - hili alichapisha kama sehemu ya kitabu kiitwacho, "Social Protection in Developing Countries: Reforming Systems" kilichoandikwa mwaka 2013. Kurasa za awali za kitabu hiki zinapitkana hapa: http://samples.sainsburysebooks.co.uk/9781136178511_sample_493868.pdf

Kwa mujibu wa Google Scholar, hili chapisho nalo halijaweza kunukuliwa na mtu yeyote.

5. ?Access to social services for non-citizens and the portability of social benefits in Tanzania? - hili nalo aliandika kama sehemu ya kitabu kiitwacho, "Access to Social Services for Non-citizens and the Portability of Social Benefits within the Southern African Development Community", kilichoandikwa mwaka 2011. Linapatikana hapa: https://www.uj.ac.za/EN/Faculties/l...uments/Access to social services.pdf#page=139

Kwa mara nyingine tena, Google Scholar inaonyesha kuwa andiko hili halijapata kunukukuliwa.

6. "Social Security Law and Policy reform in Tanzania with reflections on the South African Experience" - hili ndilo tasnifu ya shahada yake ya uzamivu aliyoipata pale UCT, mwaka 2007. Linapatikana hapa: https://open.uct.ac.za/handle/11427/4615

Nalo toka 2007, kwa mujibu wa Google Scholar, halijawahi kunukuliwa.

7. "Extension of social security coverage to the rural population in Tanzania: lessons from India and Iran" - hili alichapisha katika jarida liitwalo, Journal of African and International Law, mwaka 2009. Linapatikana hapa: AfricaBib | Extension of social security coverage to the rural population in Tanzania: lessons from India and Iran

Kwa mara nyingine, Google Scholar inaonyesha kwamba andiko hili halijawahi kunukuliwa.

8. "The New Employment and Labour Relations Law in Tanzania: An Analysis of Labour Legislation in Tanzania" - hili ameandika pamoja na B. Rutinwa na E. Kakula pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 2012. Lakini katika Google Scholar haitoi 'link' ya kuelekea andiko hili, wala ni wapi limechapishwa. Ingawa nalo halijawahi kunukuliwa.

Hivyo basi, katika maandiko yake hayo 8, Tulia Ackson, aliyekuwa Mhadhiri wa Sheria na anayesemwa kuwa mbobezi wa sheria, kaweza kunukuliwa mara 1 tu. Na aliyemnukuu ni mtanzania aliyekuwa akisoma shahada ya uzamivu katika sheria.

Sikuridhika sana na majibu ya Google Scholar. Nikaamua nihamishie utafutaji Researchgate, ambayo katika siku za hivi karibuni watu wengi katika akademia wameonekana kupenda kuwa na akaunti huko. Kule nilimpata Tulia Ackson na rekodi zake. Mwangalie hapa: https://www.researchgate.net/profile/Tulia_Ackson

Rekodi zake katika Researchgate zinaonyesha kuwa: ana jumla ya machapisho 8, ambayo kwa ujumla wake yamesomwa mara 33 (ilikuwa mara 32, ikaongezeka 1 baada ya mimi kufungua andiko lake moja) na kunukuliwa mara sifuri.

Sikuridhika sana. Nikasema, pengine yale majarida ambayo alichapisha maandiko yake ni ya viwango vya juu sana katika fani ya Sheria. Kwa maana katika ulimwengu wa akademia, wapi unachapisha maandiko yako ina nafasi kubwa sana ya kuonyesha 'ubobezi' katika fani. Unaweza kuwa na machapisho machache sana, lakini katika majarida ya viwango vya juu sana, na ukaonekana 'mbobezi' sana kupita yule aliye na machapisho mengi katika majarida ya viwango vya chini. Sasa katika 'utafiti' wangu huu, inaonyesha Tulia amekwishachapisha katika majarida haya: Journal of African and International Law, African Journal of International and Comparative Law, na International Social Security Review.

Nikaamua kwenda mbele zaidi kufuatilia kwa undani majarida hayo. Pengine nidokeze kidogo jambo hili: katika akademia ubora wa majarida utokana na kitu kinachoitwa 'impact factor', kwa tafsiri isiyo rasmi ni athari (katika taaluma sana sana) ya jarida katika fani husika. Na hii 'impact factor' utokana na wastani ambapo chapisho katika jarida hilo unukuliwa kwa mwaka. Kwa hiyo kama jarida lina 'impacts factor' ya 4, inamaanisha kwamba kwa wastani, machapisho katika jarida hilo unukuliwa mara 4 na machapisho mengine.

Sasa, jarida la Journal of African and International Law, tovuti yake ni hii: Law Journals: Submissions and Ranking, ingawa hii siyo tovuti rasmi, ila ni tovuti inayoonyesha 'link' kwenda kwenye tovuti ya jarida hilo. Kwa mshangao mkubwa, nimejaribu mara nyingi kufungua 'homepage' (http://aicil.or.tz/law-journal/) ya jarida hilo, na kushindwa mara zote. Anuani ya ofisi zake zinaonyesha zipo Songea, Tanzania, katika taasisi iitwayo, 'African Institute for Comparative and International Law'. Jarida halina 'impact factor' na kwa kweli inavyoonekana, ni jarida la viwango vya chini sana. Kwani hata katika Google Scholar, upatikanaji wa jarida hili, ni wa mashaka, ukitoa chapisho ambalo Tulia analo katika jarida hili.

African Journal of International and Comparative Law, jarida hili utolewa na 'Edinburgh University Press', Scotland. Ingawa nalo halina 'impact factor', lakini angalau linaonekana kuwa la kuaminika kiasi.

International Social Security Review, jarida hili uchapishwa na "International Social Security Association" kupitia Wiley Publishing. Ingawa nalo halina 'impact factor', lakini pia linaonyesha kuwa la kuaminika kiasi.

Kwa hiyo, pamoja na majarida hayo machache, Tulia hajaweza kuchapisha katika majarida yenye viwango vya juu katika fani ya sheria. Majarida ya viwango vya juu katika sheria ni yepi? Angalia hapa kupata list ya majarida ya fani ya sheria: http://about.jcr.incites.thomsonreuters.com/full-titles-2015.pdf

Kwa upande mwingine, kitu ambacho kinajidhiirisha katika rekodi yake ni kwamba, Tulia Ackson anaonyesha kuwa na 'utaalamu' katika sheria za hifadhi ya jamii. Na wala siyo mtaalamu wa sheria za uhifadhi wanyamapori, udhamini, sheria ya usimamizi wa mirathi, na ufadhili miradi na madini kama gazeti la Habari Leo linavyotaka kuniaminisha. Rekodi yake inaonyesha hivyo, wala siyo mimi ninayesema hivyo.

Kwa kifupi, 'utafiti' wangu usio rasmi umenifanya nijiulize maswali ya kile kinachoitwa ubobezi katika sheria wa Tulia Ackson. Labda kama kuna viashiria vingine (ambavyo mimi sivifahamu) katika ulimwengu wa akademia ambavyo umfanya mtu aitwe mbobezi katika fani yake. Lakini kama viashiria vinavyotumika kwa sasa: idadi ya machapisho, wapi yamechapishwa (hapa naongelea kuchapishwa katika majarida yenye viwango vinavyotambulika katika fani husika), na mara ngapi yamenukuliwa katika machapisho ya watu wengine, hakika bado sijaona ubobezi wa Tulia Ackson katika fani ya Sheria.

Kwa hiyo, ningependa kuuliza, upo wapi huo ubobezi wa Tulia Ackson katika sheria kama inavyosemwa?

Hongera sana kwa uchunguzi ulioufanya. Sasa inawezekana Masaju ndo alishauri aingie bungeni ili awe anamsaidia. Lakini niseme tu kuwa na PhD kwenye fani yo yote haina maana mtu.ni mbobevu. How much one has published ndo inakaunti. Lakini pia ame-publish nini also matters. Labda ndo maana alishindwa kujibu swali la Silinde.
 
Nzi,

..kazi nzuri.

..huyu hajabobea ktk masuala ya sheria za bunge na katiba.

..kilichotokea hapa ni upendeleo wa waziwazi.
 
Last edited by a moderator:
Huyu hapa akijinadi bungeni.

Kumbe hata hotuba yake aliiandika na kuisoma.

She couldn't just flow off the top of her head?

Anasema kusoma ni haki yake kwa vile yeye ni mwanasheria na wanasheria huwa wanasoma!

Mweeeh!

I'm underwhelmed.

 
Last edited by a moderator:
mleta mada upo vizuri Sana kwa wasio elewa wataendelea kutoa misifa ya kijinga tu
 
Wanasema sheria ni msumeno , ikimaanisha majibu yote ni sawa (ndio na hapana) . usahihi wa jibu lako inategemea jinsi utakavyolitetea , sasa hapo ndipo ulipo ubobezi wa huyu mama anaweza kubadilisha kosa kuwa sahihi tujikumbushe bunge la katiba na kesi ya mita 200, huyu amewekwa kimkakati kabisa kubadilisha nyekundu kua njano . tutegemee mtifuano mkali vs lissu ila lisu atazidiwa maana mama kakalia kiti (kashika mpini)
 
Analysis nzuri sana na kwa kweli ingetakuwa wataalamu wetu wawekwe kwenye mizani ya namna hii.

Mtu ambaye hajawahi kuchapisha paper kwenye reputable journal na citations hana anasemekanaje kubobea katika eneo lake?

Ndiyo maana kitaaluma tumekufa!
 
Nimesikia kuna mtu anaitwa Rehema Nchimbi
hiyo PHD yake ni only in Tanzania
labda mkuu Nzi atufanyie uchunguzi wa huyu pia
Mambo gani sasa haya banaa....si uitaje tu.
Au Phd ya kudevelo rangi za ukili?
 
Wanasema sheria ni msumeno , ikimaanisha majibu yote ni sawa (ndio na hapana) . usahihi wa jibu lako inategemea jinsi utakavyolitetea , sasa hapo ndipo ulipo ubobezi wa huyu mama anaweza kubadilisha kosa kuwa sahihi tujikumbushe bunge la katiba na kesi ya mita 200, huyu amewekwa kimkakati kabisa kubadilisha nyekundu kua njano . tutegemee mtifuano mkali vs lissu ila lisu atazidiwa maana mama kakalia kiti (kashika mpini)

Naona polisi watakuwa wageni wa kudumu kwenye bunge la 11. Hatimaye litabaki kuwa caucus ya CCM. Time will tell.
 
Huyu hapa akijinadi bungeni.

Kumbe hata hotuba yake aliiandika na kuisoma.

She couldn't just flow off the top of her head?

Anasema kusoma ni haki yake kwa vile yeye ni mwanasheria na wanasheria huwa wanasoma!

Mweeeh!

I'm underwhelmed.



Mazee, asante kwa hii video. Napenda sana alichokisema kuanzia dakika ya 2.20 hadi 2.44. Amesema:

"...ninajiamini, nina uwezo na kazi ya naibu spika na spika ni kutafsiri kanuni za Bunge, sheria za nchi na pia katiba. Na mimi haya ndiyo maeneo ambayo nimebobea kikazi"

Amebobea kikazi kwenye kutafsiri kanuni za Bunge, sheria za nchi na katiba?!? Haya wanamwona huyu ni mbobezi katika maeneo hayo walete ushahidi. Maana kwenye utafiti huo usio rasmi, sijaona kubobea kwake.

Huyu bidada hajielewi kumbe! Hakika hii ni mbeleko. Angebaki kufundisha tu sheria au kuwa naibu mwanasheria mkuu...maana hapo Bunge kuaibika kwake is bound to happen. Na yeye ni mfano wa 'wabobezi' na 'wasomi' wajanja waliojaa Tanzania chini ya CCM.
 
Last edited by a moderator:
Analysis nzuri sana na kwa kweli ingetakuwa wataalamu wetu wawekwe kwenye mizani ya namna hii.

Mtu ambaye hajawahi kuchapisha paper kwenye reputable journal na citations hana anasemekanaje kubobea katika eneo lake?

Ndiyo maana kitaaluma tumekufa!

Mkuu, haya ndiyo maajabu ya 'wasomi' na 'wabobezi' wetu Tanzania! Ujanja ujanja umekuwa mwingi mno. Nakumbuka nilikutana na Prof. mmoja wa kitanzania sehemu, akaniambia anawafahamu baadhi ya maprof wa kitanzania ambao wakienda Ulaya na Marekani uwa hawajitambulishi kama ni maprofesa. Bali ujitambulisha kama madaktari tu.Ujanja ujanja ambao unamfanya mtu afahamu kabisa 'titles' wanazozimiliki haziendani na 'madini' ambayo wanayo kichwani.
 
Nzi,

..kazi nzuri.

..huyu hajabobea ktk masuala ya sheria za bunge na katiba.

..kilichotokea hapa ni upendeleo wa waziwazi.

Mkuu, umemsikia kwenye video aliyoweka Nyani Ngabu.? Kasema yeye kabobea kwenye kutafsiri kanuni za bunge...
 
Muungano wa taaluma na siasa ni recipe ya hatari sana kwa nchi yetu.

Sikushangaa kusikia kuwa Dr Kigwangala anamalizia PhD
 

Mkuu nzi, kitendo tuu cha kusoma hadi chuo kikuu pekee, huyo ni msomi!, kufika tuu chuo kikuu sio issue sana unaweza kwenda kosomea sanaa, soshologia, lugha, etc, hata ukitoka na DIV 4 unaingia chuo kikuu!, lakini kujiunga chuo kikuu kusomea sheria miaka hiyo kabla digrii ya sheria kubinafshishwa, kujiunga UDSM kusoma sheria lazima uwe ni DIV 1 kali!.

Kusemea digrii ya pili ya uzamili ndiko mwanzo wa kubobea kwenyewe halafu kufanya shahada ya uzamivu, ndiko kubobea kwenyewe!, ila kitu ulichonisaidia, nilidhani amebobea kwenye administrative law au constitutional law ndio maana akautafuta usipika!, kumbe ni social security law!.

Asante.

Pasco

Pasco uwezo wako wa kuchambua Mambo nauona unaporomoka kwa kasi ya kimbunga. Hoja ni ubobevu wa Dr. Tulia kwenye sheria wewe unaleta story za matokeo ya form six. Wangapi walifail mitihani yao lakn leo ni watu makini kwenye fani zao. Refer professor muhongo ambaye inasemekana alifail darasa la saba zaidi ya mara tatu bt leo ndio miongoni mwa wataalam wabobevu wa geology duniani. Pole yako mkuu. Bt nikubaliane na wewe kuwa kwa kuwa na PhD tu tayari unakuwa na sifa ya kuwa mbobevu
 
Amebobea kikazi kwenye kutafsiri kanuni za Bunge, sheria za nchi na katiba?!?

Hebu ngoja tutumie mantiki kidogo. Haya, anadai kabobea kwenye kutafsiri kanuni za bunge, sheria za nchi na katiba. Huo ubobezi kaupataje? Keshawahi kufanya kazi bungeni na kupata tajiriba ya kiutendaji [practical experience]?

Ni wapi, lini, na kwa muda gani kawahi kutafsiri kanuni za bunge?
 
Hebu ngoja tutumie mantiki kidogo. Haya, anadai kabobea kwenye kutafsiri kanuni za bunge, sheria za nchi na katiba. Huo ubobezi kaupataje? Keshawahi kufanya kazi bungeni na kupata tajiriba ya kiutendaji [practical experience]?

Ni wapi, lini, na kwa muda gani kawahi kutafsiri kanuni za bunge?

Tanzania tuna namna yetu ya kutathmini utendaji wa kitaaluma ambao msingi wake mkuu ni uswahiba na chama na dola.

Vinginevyo sioni jinsi ya kuelezea mambo haya
 
Back
Top Bottom